Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amezitaka Maabara Nchini kuhakikisha zinafuata misingi na kanuni sahihi katika kuzingatia ubora na ufanyaji.
Akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Shinyanga, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla aliweza kukagua Maabara ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu ambapo alibaini mambo mbalimbali yakifanywa bila kuzingatia taratibu sahihi za Mabara huku akiagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanarekebisha mapungufu hayo katika Maabara hiyo.
Miongoni mwa mambo ambayo alikuta katika Maabara hiyo ni pamoja na kutokuwa na taratibu za kiutendaji hasa kwa wafanyakazi wenyewe wa Maabara ambao walishindwa kuzingatia vigezo na msharti ambayo taratibu za Maabara zinahitaji.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua Maabara hiyo ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu. |
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo namna ya Maabara inavyotakiwa iwe na taratibu zake. |
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na wafanyakazi wa Hospitali hiyo ya Kishapu |
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na wafanyakazi wa Hospitali hiyo ya Kishapu |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.