ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 3, 2015

Friday, January 2, 2015

RAIS JK AMTEUA DK.MIGHANDA KUWA MWENYEKITI BODI YA WAKURUGENZI TANESCO

Tanesco.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dk. Mighanda Manyahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Kwa taarifa iliyotolewa leo na kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini ilisema ,kufuatia uteuzi huo,Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewateua Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO .
Wajumbe wa bodi walioteuliwa ni Kissa Vivian Kilindu,Juma Mkobya,Dk.Haji Semboja, Shabaan Kayungilo, Dk.Mtesigwa Maingu, Bodi Mhegi, Felix Kabodya pamoja na Dk.Nyamajeje Weggoro.
Taarifa hiyo ilisema bodi hiyo imeanza kazi Januari 1 na itaishia Februari 31 Mwaka 2017.

MASHALI NA DULLAH MBABE NGOMA DROO


Na Michael Machellah.
MPAMBANO  wa ngumi za kirafiki kati ya Thomasi Mashali kutoka Manzese jijini Dar es Salaam na Abdalah Pazi kutoka Mwananyamala limetoka sare (Technical draw-dt) baada ya Thomas Mashali kuvuja damu nyingi toka juu ya jicho la kushoto alilopasuliwa kwa konde zito na mpinzani wake Abdala Pazi(Dullah Mbabe) mwishoni mwa raundi ya pili.

Raundi ya tatu mwanzoni Mashali alishambuliwa zaidi kiasi cha kukosa muelekeo ambapo pia damu zilizidi kutoka kushoto kwa jicho lake ndipo mwamuzi wa mpambano, Hakwe Mtulya alisimamisha mpambano kwa matibabu na baada ya Daktari kufanya uchunguzi wa kina ikadhihirika Mashali hawezi kuendelea na pambano hilo kwani damu zilikuwa zinatoka zaidi eneo la jeraha.

Kwa hatua hiyo mpambano ulikuwa ni droo kwa mujibu wa sharia za ngumi (Proffesional Boxing) kuwa mpambano unaoshia chini ya roundi ya nne ukiwa haujakamilika kwa ajali hiyo ni droo(Technical draw-dt).

Kabla ya matokeo hayo kutangazwa mashabiki wa ngome ya mashali walianzisha fujo iliyopelekea kuharibu viti,meza na watu kuumizwa ovyo ililazimika matokeo ktotangazwa na Katibu Mkuu wa Ngumi za kulipwa Tanzania(Tanzania Proffessional Boxing), Ibrahim Kamwe(Big Right) aliyathibitisha haya yote.

Mpambano wa Thomasi Mashali na Abdalah Pazi ulikuwa ni wa kirafiki wa  round inane(8), kutafuta kadi  unaowawezesha kugombania  Ubingwa ulifanyika juzi tarehe 1,1,2015 katika Ukumbi wa Manzese France Corner jijini Dar es Salaam.

BOB HAISA ASITISHA RASMI UTARATIBU WA KUACHIA WIMBO MPYA KILA MWEZI

"Wapendwa mashabiki na wadau wa Muziki ninapenda kuwataarifu kwamba ule utaratibu  tuliokua tukiendeleanao wa kuachia wimbo mpya kila mwezi tumeusitisha rasmi ukiwa na nafanikio lukuki, Sina zaidi ya shukrani kwa mungu na wote waliofanikisha zoezi hili lililotimiza mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu lianze, 

HERI YA MWAKA MPYA KWA KILA MMOJA
Asanteni sana".Bob Haisa yes

MWANZA YAANZA KWA KISHINDO TAIFA CUP 2015 WANAWAKE

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Jamal Malinzi akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa Michuano ya Kitaifa ya Soka kwa wanawake ijulikanayo kama Proin Promotions Women Taifa Cup 2015 iliyozinduliwa jana katikadimba la CCMKirumba Mwanza.   
Mwanza Queens (blue) walishuka dimbani kupepetana na Mara Queens (red), ambapo hadi mwisho Mwanza mchezo ulishuhudiwa kwa Mwanza kuibuka na ushindi mnono 6-1.
Mwenyekiti wa Kamati ya soka la wanawake TFF Blass Kiondo akizungumza mipango na mikakati iliyopo katikakukuza na kuinua soka la wanawake nchini.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Jamal Malinzi akikagua timu wenyeji Mwanza Queens katika ufunguzi wa Michuano ya Kitaifa ya Soka kwa wanawake ijulikanayo kama Proin Promotions Women Taifa Cup 2015 iliyozinduliwa jana katika dimba la CCMKirumba Mwanza.  
Rais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Jamal Malinzi akikagua timu ya Mara Queens katika ufunguzi wa Michuano ya Kitaifa ya Soka kwa wanawake ijulikanayo kama Proin Promotions Women Taifa Cup 2015 iliyozinduliwa jana katika dimba la CCMKirumba Mwanza.  
Mwanza Queens.
Mara Queens.
Mwanza wanapata kona. 
Wakiwa na mazoezi ya kutosha kupitia kambi ya muda mrefu waliyoweka Mwanza Queens waliinyanyasa ngome ya Mara Queens katika mchezo wa ufunguzi wa Proin Promotions Women Taifa Cup 2015, na kuondoka na ushindi wa bao 6-0.
Mashambulizi.
Dakika 80 za mchezo zinamalizika katika dimba la CCM Kirumba, Mwanza Queen wakiondoka na ushindi 6-0 dhidi ya Mara Queens.
ALBERT G. SENGO: MWANZA
MICHUANO ya kitaifa ya Soka la Wanawake Tanzania ijulikanayo kama Taifa Cup hatimaye imezinduliwa hii leo dimba la CCM Kirumba, Mwanza Queens wakishusha kichapo cha fungulia mwaka kwa kuibamiza Mara Queens bao 6-1. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA 

HALMASHAURI YA SITISHA MKATABA WA KAMPUNI YA SENSON YA UKUSANYAJI USHURU WA MABANGO PIA YAIDAI SH MILIONI 102 KUIBULUTA MAHAKAMANI


NA PETER FABIAN, MWANZA. 
HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza imesitisha mkataba na Wakala wa ukusanyaji ushuru wa Mabango Kampuni ya Senson Ltd katika maeneo yote ilikokuwa ikikusanya fedha jijini hapa. 

Akizungumza na MTANZANIA juzi Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Jiji hilo, Halifa Hida, alieleza kuwa uamuzi huo wa kusitishwa kwa Wakala huyo wa Kampuni ya Senson Ltd aliyekuwa ameshinda zabuni ya ukusanyaji ushuru wa mabango katika maeneo yote ya Halmashauri unaanza kutekelezwa Januari Mosi mwaka huu wa 2015.

 Mkurugenzi Hida alifafanua kuwa Wakala huyo wa ukusanyaji ushuru alitakiwa kukusanya ushuru wa Sh milioni 56,400,000/= kila mwezi ikiwa ni mkataba alioingia na Jiji hilo baada ya kushinda zabuni iliyokuwa imetangazwa, lakini ameshindwa kufikia malengo ya kiasi alichotakiwa kukusanya na imekuwa ikikusanya fedha kiasi cha chini ya Sh miilioni 30 kwa kila mwezi kinyume na mkataba.

 Hida alifafanua kuwa kutokana Kampuni hiyo kuonekana kukusanya chini ya kiwango na kushindwa kuwasilisha fedha alichokubali kwenye mkataba wakati aliposhinda zabuni, Halmashauli inamdai kiasi cha Sh milioni 102,000,000/= ambazo ni ushuru wa mwezi Julai hadi Agosti mwaka 2014.

 “Tumesitisha mkataba wa Wakala huyu, lakini tumemwandikia barua ya kumtaka alipe fedha kiasi cha Sh milioni 102,000,000/= zikiwa ni makusanyo ya ushuru na malimbikizo kwa miezi miwili ambayo alikusanya na kuwasilisha kiasi kidogo kinyume na mkataba ,”alisema. 

Mkurugenzi alifafanua kuwa tayari hatua ya utekelezaji huo umetakiwa kuanza tangu jana Januari mosi mwaka huu wa 2015 na taarifa zimetolewa katika kikao cha Kamati ya fedha chini ya Mwenyekiti wake Meya wa Jiji, Stanslaus Mabula (CCM) ambaye ni Diwani wa Kata ya Mkolani na Bodi ya zabuni ya Halmashauri hiyo. 

“Tunazo taratibu, kanuni na sheria za Halmashauri ya Jiji katika kuingia mikataba na utekelezwaji wake iwapo Wakala wa Kampuni husika iliyoingia mkataba ameshindwa kufikia malengo atakuwa amevunja mkataba na hapo tunageukia sheria inasema nini basi tunaitekeleza kwa kumtaka alipe akishindwa tunamfikisha Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria,”alisisitiza. 

Hida amewatahadhalisha wananchi wa Jiji kutolipia ushuru wa mabango kwa Wakala huyo Kampuni ya Senson Ltd, kwani tayari amesitishiwa uhalali wa ukusanyaji ushuru na kuwataka wananchi kulipia ushuru huo katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji ili kuepuka kupoteza fedha zao ili kuepuka kulipia tena. 

Mkurugenzi Hida, ametoa wito kwa wananchi kulipa ushuru wa mabango na kodi mbalimbali kwa Mawakala walio na sifa na ambao bado wana mikataba ya ukusanyaji na Halmashauri kwa wakati ili kuepuka kulipa na kupigwa faini kutokana na kushindwa kufanya hiyo kwa wakati ili kutekeleza kauli mbiu ya “lipa ushuru kwa maendeleo ya Jiji”.

Thursday, January 1, 2015

MKESHA WA KUKARIBISHA MWAKA MPYA UWANJA WA CCM KIRUMBA WATAKIWA KUENDELEA KULIOMBEA TAIFA.

Happy New Year from Google!
NA PETER FABIAN, MWANZA

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo ameonya baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa wanaohamasisha vurugu na uchochezi unaopelekea uvunjifu wa amani. 

Akizungumza kwenye mkesha wa kuliombea taifa uliofanyika katika uwanja wa michezo wa CCM Kirumba jana jijini hapa, RC Mulongo alisema kuwa wananchi hawana budi kuendelea kuliombea taifa bila kujali itikadi za madhehebu ya dini zao na itikadi za kisiasa chini ya mfumo wa vyama vingi. 

“Wananchi msikubaliane na baadhi ya watu wachache wakiwemo viongozi wa kisiasa wanaotuhamasisha katika misingi ya vurugu, uchochezi na hata tuanze kubaguana kwa madhehebu ya dini zetu, rangi na makabila jambo ambalo tukiruhusu litatuingiza katika taifa lenye vurugu na machafuko na kusababisha amani iliyopo itoweke,”alisema. 

Mulongo alisema kuwa kutokana na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwana kukumbwa na changamoto mbalimbali za ulinzi na kupelekea imani za kishirikina kuchukua nafasi na kusababisha mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinisimu) kujitokeza. 

“Serikali ya Mkoa itachukua hatua ya kukomesha imani hizo potofu na kuwakamata wanaofanya vitendo hivyo vya mauaji kwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria pia wananchi mwendelee kuliombea taifa ikiwemo watu wa aina hiyo ili kusaidia taifa kuendelea kuwa na amani na utulivu,”alisisitiza. 

RC Mulongo alitumia mkesha huo kuwakumbusha wananchi tukio la kutoloshwa kwa mtoto ambaye anaulemavu wa ngozi (Albino) lililotokea hivi karibuni wilayani Kwimba ambapo uchunguzi wa awali umebaini ndugu wa karibu kuhusika na tukio hilo. 

“Tuendelee kumuombea pia mtoto huyo ili apatikane akiwa hai wakati ambapo serikali na Jeshi la Polisi likiendelea kuwatafuta watu waliomwiba kutokana na shindikizo za imani za kishirikina kutawala baadhi ya miyo za watu, lakini wananchi watupatie taarifa za siri zitakazowezesha kumpata mtoto huyo na watu wanaeendesha vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wetu,”alisisitiza. 

Awali Askofu Charles Sekelwa kwa niaba ya maaskofu na wachungaji wa madhehebu ya makanisa mbalimbali yaliyopo jijini Mwanza yaliyoandaa mkesha huo wa kuliombea taifa na Mkoa wa Mwanza , alisema wataendelea kumlilia “Mungu” ili kudumisha amani ya taifa iliyopo.

 Askofu Sekelwa alisema kuwa hali ya taifa ilivyo inajulikana kutokana na baadhi ya maeneo kukumbwa na vurugu na kusababisha kuashiria kwa machafuko na uvunjifu wa amani kutokana na kukumbwa na changamoto hizo ni vyema kuendelea kuliombea taifa kwa nguvu zote. 

“Tushirikiane kuliombea taifa hasa mwaka huu ambapo taifa litakuwa katika upigaji kura za maoni juu ya kupata Katiba mpya na uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ili kuendelea kuwa na utulivu na amani, jambo ambalo linatakiwa kupewa kipaumbele na kila mwananchi,”alisema. 

Wito ni watanzania wote kuendelea kuliombea taifa na viongozi wa serikali ni kuhakikisha changamoto mbalimbali zilizopo katika kuwapatia huduma na maendeleo wananchi zinafanyiwa kazi haraka ikiwemo kuzisikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi badala ya kuzisikiliza kisha kutozitekeleza kwa wakati jambo linalowatia hofo na mashaka wananchi.

MWANZA YAUKARIBISHA MWAKA 2015 KWA STYLE HII....!!

Ni bendi mpya ya vijana tupu iliyo na maskani yake hivi sasa jijini Mwanza The Mambaz aka Jembe ni Jembe Band aka JJ-Band walikamua ile kisawasawa na kuzikonga nyoyo za mashabiki walioibuka kuuaga mwaka 2014 kuukaribisha mwaka mpya 2015 ndani ya Jembe Beach Mwanza Tanzania.
Friendz wa ukweli waliibuka Jembe Beach kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka mpya 2015.
Hapa lilipigwa charanga likawachanganya mashabiki hawa.
Selfie na JJ Band aka The Mambaz
Hatariiiii...
Ng'adu kwa ng'adu...
Break dance.
Full Light @Jembe palipendeza kwa maandali ya kipekee
Meza ya wastaarabu.
Flowerz
Meza hii ilikuwa na shangwe 'hATAri'
Hapa alikalishwa mtu....!!
KamuaaaaAAA...!! Kushoto ni CEO wa Jembe ni Jembe Dakitari Mkare.
Blue thing..!!
JJ Band kwa area...
New style imeingia mjini katika kuserebuka na hapa ikitambulishwa na Jembe team.
'Sugua mpaka itakate'
Baada ya makamuzi ya bendi kumalizika Jembe Djz walikamua mpaka jua likaonekana.