ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 24, 2018

LIVE: WASAFI FESTIVAL 2018 KUTOKA MTWARA


Kwa mara ya kwanza #Mapinduzi ya Burudani Wasafi Festival2018 Katika Uwanja wa #Nangwanda Sijaona Mkoani #Mtwara

WANANCHI NA WADAU WA MAENDELEO WAHAMASISHA KUCHANGIA MFUKO WA UDHAMINI WA UKIMWI.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani  Dodoma  Bw. Jabir  Shekimweri akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa  Udhamini wa UKIMWI  Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha  wananchi,  wanafunzi  na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI  (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akizungumzia mambo yatakayofanyika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ikiwemo wiki ya maonesho itakayoenda sambamba na kuanzishwa kwa jiji cha vijana ndani ya uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambapo vijana watajifunza masuala mbalimbali ikiwemo Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Upimaji wa Virusi vya UKIMWI, Ushauri nasaha, upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama shinikizo la damu na kisukari .
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI  (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI  (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa  Udhamini wa UKIMWI  Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha  wananchi,  wanafunzi  na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI  (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng  akizungumzia hali ya UKIMWI Duniani ambapo alibainisha kuwa takribani watu milioni 37 wameambukizwa virusi hivyo, hayo yamejiri leo  wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa  Udhamini wa UKIMWI  Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha  wananchi,  wanafunzi  na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani  Dodoma  Bw. Jabir  Shekimweri  (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wananchi walioshiriki katika wa hafla ya kuhamasisha na  kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa  Udhamini wa UKIMWI  Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha  wananchi,  wanafunzi  na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
Kikosi cha Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikiongoza matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha  wananchi,  wanafunzi  na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI kwa lengo la kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa  Udhamini wa UKIMWI  Tanzania (ATF).
Sehemu ya washiriki wa  matembezi ya hisani yaliyolenga kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya Mfuko wa  Udhamini wa UKIMWI  Tanzania (ATF) , matembezi hayo ya  hisani yamefanyika Jijini Dodoma.
 Mmoja wa wasanii walioshiriki katika hafla ya uchangiaji  fedha kwa ajili ya Mfuko wa  Udhamini wa UKIMWI  Tanzania (ATF) , Bi. Hadhara Charles akionesha umahiri wake katika kumiliki mpira wa miguu wakati wa hafla hiyo iliyotanguliwa na matembezi  ya  hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia UKIMWI na Madawa ya Kulevya Mhe. Oscar Mukasa  ambaye ni Mbunge wa Biharamulo akizungumzia faida za wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia mfuko  wa  Udhamini wa UKIMWI  Tanzania leo Jiji Dodoma wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangia mfuko huo, hafla hiyo ilitanguliwa na matembezi  ya  hisani.
Msanii wa Jijini Dodoma Bi. Judith Jenaro akiimba wimbo wa kuhamasisha wananchi kujitokeza kupima virusi vya UKIMWI ili watambue hali zao ili waweze kuchukua  hatua stahiki.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa  Mkoani  Dodoma  Bw. Jabir  Shekimweri  (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu wanafunzi walioshiriki katika hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa  Udhamini wa UKIMWI  Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha  wananchi,  wanafunzi  na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia UKIMWI na Madawa ya Kulevya Mhe. Oscar Mukasa (Kushoto)  ambaye ni Mbunge wa Biharamulo akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI  (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng   mara baada ya hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa  Udhamini wa UKIMWI  Tanzania (ATF).
(Picha zote na MAELEZO na TACAIDS)

SERIKALI YATEUA MAGEREZA KUMI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS JPM


NaibuWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa tofali linalotengenezwa  na  wafungwaikiwa  ni  mpango wa  uongozi  wa  gereza  la  Kwamngumi  kukabiliana  na  changamoto  ya  makazi kwa  askari, Kulia  ni  Mkuu  wa  Gereza  hilo,Christopher Mwenda, lililopo   Wilayani  Korogwe, mkoani  Tanga.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa nyumba iliyojengwa   na matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamngumi lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga.Kushoto ni  Mkuu wa Gereza hilo, Christopher  Mwenda.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia tofali ambazo zimetengenezwa na wafungwa wa Gereza la Kwamngumi, ambazo hutumika kujengea nyumba za askari ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji na kilimo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa Kaunda suti), na ujumbe alioongozana nao wakipita mbele ya nyumba  iliyojengwa kwa kutumia matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamgumi lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Magereza kumi yateuliwa kutekeleza agizo la Rais Magufuli
Na Mwandishi Wetu.

Serikali imeteua jumla ya magereza kumi nchini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Magufuli la kulitaka Jeshi la Magereza litumie rasilimali watu ya wafungwa kuzalisha mazao kwa ajili ya biashara na chakula badala ya serikali kuingia gharama ya kulisha wafungwa.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa agizo hilo katika Gereza la Kwamngumi wilayani Korogwe ,mkoani Tanga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema utekelezaji huo unaenda sambamba na uteuzi wa magereza kumi ya kilimo nchini na akiweka wazi uwapo wa mpango maalumu wa kutathmini na kupima mpango mkakati huo kwa kila gereza.

Aliyataja magereza hayo kuwa ni Songwe(Mbeya),Kitai(Ruvuma),Ludewa(Njombe), Mollo (Rukwa), Kitengule (Kagera) ambayo yameteuliwa kulima mahindi, mengine ni Idete na Kiberege (Morogoro) yaliyoteuliwa kulima mpunga huku Kitete (Rukwa), Kitengule (Kagera) na Gereza la Arusha yakiteuliwa kulima maharagae

“Tunahitaji matumizi sahihi ya rasilimali watu na ardhi tuliyonayo katika magereza yetu itumike ipasavyo kwa shughuli za uzalishaji ili tuweze kutekeleza amri ya Mheshimiwa Rais, huku lengo la wizara kupitia jeshi la magereza ni kuweza kuwekekeza fedha kwa kulitumia shirika la uzalishaji mali lililopo ndani ya jeshi hilo na ikiwezekana hapo baadae tuweze kutafuta wateja watakaonunua mazao yatakayozalishwa katika mashamba hayo,” alisema Masauni.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Gereza la Kwangumi, Christopher Mwenda, alisema wao kama uongozi wa gereza hilo wamejipanga vizuri katika utekelezaji wa aguzo hilo huku akiiomba wizara kuongeza vifaa vya kilimo ili waweze kuzalisha kwa kiwango kikubwa zaidi.

WAZIRI MWAKYEMBE AITAKA SIDO KUONYESHA WELEDI KWA KUSAIDIA WAJASIRIAMALI.


 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) akilitaka shirika la SIDO kuwasaidia wajasiriamali wa mkoa wa Tabora kutengeneza mashine za kisasa zitakazowasaidia kukausha bidhaa zao za chakula kisasa na kuziongezea thamani alipokuwa akifunga Jukwaa la Fursa za  Biashara na Uwekezaji  ambalo limefanyika  mkoani hapo kwa siku tatu leo,kulia ni Waziri wa Viwanda  Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri.
 Waziri wa Viwanda  Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda (kulia) akizitaka taasisi zilizipo chini ya wizara yake kujipanga kukutana na uongozi wa mkoa wa Tabora kwa ajili ya kushauriana namna ya kufanikisha maadhimio ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  leo wakati kufunga jukwaa hilo mkoani hapo,kushoto ni  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe.
 Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe.Magreth Sitta akitoa shukrani kwa uongozi wa Mkoa wa Tabora kwa niaba ya wabunge wenzake kufanikisha  Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  wakati wa ufungaji wa Jukwaa hilo liloendeshwa mkoani hapo kwa siku tatu.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi akiiomba serikali  kutafuta Mwekezaji atakaye  uendeleza na kuuboresha uwanja wa Michezo wa Ali Hassan Mwinyi uliyopo Tabora Mjini na kuwasaidia leo wakati wa kufungwa kwa Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoa hapo.
 Kaimu Mhariri Mtendaji Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN)  Bibi.Tuma Abbdalah akipongeza mwitiko wa wakazi wa Tabora katika kushiriki Jukwaa la fursa za Biasharana Uwekezaji  na hamasa ya maendeleo waliyoonyesha wakati wa kufungwa kwake leo mkoa hapo.
Mkuu wa Mkoa waTabora Mhe.Aggrey Mwanri akimweleza Mwenyekiti wa Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji namna Mkoa huo umejipanga kuleta mabadiliko baada ya kumalizika kwa Jukwaa hilo mkoani  leo wakati wa kufungaji   Jukwaa hilo.



Na Anitha Jonas – WHUSM
24/11/2018
TABORA
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe ameitaka taasisi ya SIDO nchini kuonyesha weledi wake kwa kuwa tengenezea  wajasiriamali wa Mkoa wa Tabora kifaa chenye Teknolojia rahisi ya kukaushia bidhaa zao za chakula ili kuziongezea ubora.

Mheshimiwa Mwakyembe ameyasema hayo leo Mkoani Tabora alipokuwa   akifunga Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji lililokuwa likifanyika Mkoani hapo kwa siku tatu  kwa lengo la kutangaza fursa za biashara na uwekezaji za mkoa huo pamoja na kuwajengea uwezo wajasiriamali  wa kuboresha bidhaa zao pamoja na kuona umuhimu wa rasimisha bidhaa hizo kwa ajili ya kuongeza wigo wa biashara na kipato.

“Naupongeza uongozi wa Mkoa huu kwa hatua waliyochukua kufikia maadhimio ya kugawana majukumu ya kuendeleza sekta  ya viwanda kimkakati  kwa kuhakikisha kila wilaya inawajibika kuleta maendeleo kwa wananchi wake pamoja na Halmashauri ya Mji wa Tabora kutekeleza utengaji wa eneo la uwekezaji  kwa ajili ya maendeleo ya viwanda hakika jukwaa hili limesaidia kutia chachu ya mafanikio katika mkoa huu,”alisema Mhe.Mwakyembe.

Naye Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda aliwasihii waandaaji wa Jukwaa hilo ambao ni Kampuni ya Magazeti Tanzania (TSN) kuhakikisha wanatembelea Mikoa yote nchini na baada ya hapo kushuka katika ngazi ya Wilaya kama alivyoagiza Mhe.Waziri Mkuu Kassim Majiliwa katika ufunguzi wa Jukwaa hilo.

“Kwa kuzingatia manufaa ya Jukwaa hili nimeziagiza  taasisi zilizopo chini ya Wizara yangu kujipanga na kuja hapa Tabora na kuzungumza na  viongozi wa Mkoa huu pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu ili kufanikisha maadhimio ya Jukwaa hili kwa manufaa ya taifa,”alisema Mhe.Kakunda.

Kwa upande Kaimu Mhariri Mtendaji (TSN) Bibi.Tuma Abdallah aliupongeza uongozi wa Mkoa huo pamoja na kuwashukuru Mawaziri waliyoshiriki Jukwaa hilo kwa uwepo kwani uwepo wao umesaidia kufanikisha jukwaa hilo na kulifanya kuwa la kihistoria kwa mikakati iliyowekwa ili kufanikisha utekelezaji wa maadhimio yake.

“Katika Jukwaa hili la nane  tangu tumeanza  uendeshwaji wa Jukwaa hili nimejifunza kuwa Tabora ina hari ya hali ya juu ya kupata maendeleo kwa namna walivyojikita katika mijadala na hoja mbalimbali wanazo ziibua hii yote inaonyesha kiu kubwa ya wananchi wa Mkoa huu kutaka kupata maendeleo”alisema Bibi.Tuma.

Pamoja na hayo nae Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri alisisitiza kuwa uongozi wa mkoa hautakubali  ujio wa Jukwaa hilo kutowaletea manufaa kwani kwa maadhimio ya jukwaa hilo  wamejipanga vizuri kuhakikisha  kila Wilaya inatekeza mradi ambao utaleta manufaa kwa wananchi wake kwa kutelekeza  hilo Wilaya ya Urambo itajenga  Kiwanda cha Tumbaku,Wilaya ya Kaliua itaandaa ranchi pamoja  kiwanda cha alizeti na karanga halikadhalika uuzaji wa mazao ya misitu kwa kuzingatia sheria,Wilaya ya Uyui itasimamia masoko ya Kilimo na Mifugo na Wilaya ya Nzega kuanzisha Kiwanda cha uchakataji wa Nyama na Ngozi pamoja na kuanzisha ranchi pamoja na Wilaya ya Igunga kutekeleza kilimo cha Mpunga.

ONYO KWA MADEREVA WANAOJIHUSISHA NA USAFIRISHAJI DAWA ZA KULEVYA.



NJOMBE/GSENGOtV

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limetoa Onyo Kwa Madereva Mjini Makambako Kuacha Kujihusisha na Usafirishaji wa Dawa za Kulevya na Badala Yake Wasaidie Kuripoti Viashiria Vya Dawa Hizo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Renatha Mzinga Ametoa Kauli Hiyo Wakati Akifunga Mafunzo ya Udereva Yaliyokuwa Yakiendeshwa Mjini Makambako Chini ya Chuo Cha  Future World Driving School Cha Jijini Dar es Salaam Mafunzo Ambayo Yamekuwa Yakitolewa Katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Njombe.

TAARIFA ZAIDI NA AMIRI KILAGALILA

MAAFISA ARDHI WATATU WASIMAMISHWA KAZI ARUSHA.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewasimamisha kazi watumishi watatu wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya Jiji la Arusha  kwa tuhuma  ya kushirikiana na matapeli wa viwanja katika jiji hilo.

Aidha, Lukuvi ameagiza maofisa hao waliosimamishwa kazi kutokanyaga katika eneo la ofisi za Jiji mpaka hapo uchunguzi utakapofanyika na maamuzi dhidi ya tuhuma zao yatakapotolewa.

Lukuvi alichukua uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Jiji la Arusha jana kufuatia kuwepo tuhuma nyingi  za matapeli ya viwanja kushirikiana na baadhi ya maofisa wa ardhi wasiokuwa waaminifu kufanya utapeli kwa wamiliki halali wa viwanja.

Maafisa  ardhi waliosimamishwa kwa tuhuma hizo za kushirikiana na matapeli kudhulumu viwanja kwa wamiliki halali katika jiji la Arusha ni Elizabeth Mollel, Lassen Mjema na Zawadi Mtafikikolo.

Mbali na kusimamishwa kazi kwa watumishi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliagiza maafisa Ardhi wa Jiji la Arusha kuhakikisha matapeli wote wa viwanja wanaoshirikiana na watumishi hao wasipatiwe huduma katika masuala yoyote ya ardhi kufuatia  kuonekana kujihusisha na mipango ya utapeli wa viwanja kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa sekta ya ardhi katika  jiji la Arusha.

Katika ziara yake hiyo ya kushtukiza pamoja na kuelezwa na Afisa Ardhi Mteule wa Jiji la Arusha Dicley Nyato uwepo wa watumishi wawili Lassen na Zawadi huku Elizabeth akiwa katika likizo ya uzazi, watumishi hao walipotea ghafla ofisini bila taarifa mara baada ya kuelezwa wanahitajika kwa waziri na hata pale walipopigiwa simu za mkononi  hazikupatikana.

Kwa mujibu wa Lukuvi, watumishi hao wa sekta ya ardhi katika jiji la Arusha wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na matapeli wa viwanja katika jiji hilo jambo linalotia mashaka utendaji wao wa kazi na kubainisha kuwa  maafisa hao wamekuwa na tabia ya kufuatilia kesi zilizopo katika Mabaraza ya Ardhi kwa nia ya kuwasaidia  matapeli.

Kufuatia kadhia hiyo, Lukuvi ameagiza kuanzia sasa hati zote za wito wa Mahakama nchini kusainiwa na Afisa Ardhi Mteule au Msajili wa Hati ama Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Kanda na Mwanasheria wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi lazima afahamishwe uwepo wa kesi husika.

“Kuanzia sasa summons zote zipokelewe na Maafisa Ardhi Wateule, Makamishna au Wasajili wa Hati wa Kanda na watumishi wengine wasipokee wala kujihusisha” alisema Lukuvi

Lukuvi alisema matapeli wa viwanja wamekuwa wakifungua kesi  katika Mabaraza ya Ardhi dhidi ya wamiliki halali na wakati mwingine matapeli hao hawawafahamu hata wamiliki  lengo lao likiwa kuwakatisha tamaa pale kesi inapochukua muda mrefu hasa ikizingatiwa baadhi ya wamiliki hawana uwezo wa kuweka mawakili na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kupoteza haki zao.

Alisema, tabia hiyo haiwezi kuvumiliwa na kusisitiza kuwa mtandao wote wa matapeli wa viwanja katika jiji la Arusha ataukomesha kama alivyofanya katika jiji la Dar es Salaam ambalo huko nyuma lilishamiri sana kwa tabia hiyo ili kusaidia haki za wanyonge.

Kwa upande wake Afisa Ardhi Mteule wa Jiji la Arusha Dicley Nyato alimueleza waziri Lukuvi kuwa wamekuwa wakisumbuliwa sana na matapeli wa viwanja katika jiji hilo na wakati mwingine matapeli hao huwashitaki lengo likiwa kujipatia viwanja kwa njia ya udanganyifu na kuviuza.

Lukuvi alifanya ziara hiyo ya kushtukiza katika ofisi za jiji Arusha akitokea wilayani Babati mkoa wa Manyara ambako huko aliweza kutoa faraja iliyopotea kwa muda mrefu kwa wananchi wa vijiji vya Singu na Endasago  kwa kuamuru kubaki katika maeneo yao kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa takriban miaka hamsini kati ya wana kijiji na wamiliki wa mashamba ambao ni kampuni za Agric Tanzania Ltd na  Endasago Co Ltd.

MBUNGE WA KWIMBA HAONI HASARA KUMEGA SEHEMU YA MSHAHARA WAKE KUKARABATI BARABARA ZA JIMBO LAKE



NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Moja kati ya changamoto zinazorudisha nyuma maendeleo ya wananchi kwa vijiji vingi nchini Tanzania ni ubovu wa miundombinu ya barabara.


Pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya 5 yenye kasi, bado barabara nyingi za maeneo hayo zinapitika kwa shida na hata kusababisha baadhi ya vyombo vya usafiri kukongoroka au kuharibika kabisa na nyakati nyingine hasa kipindi cha masika barabara hizo kutopitika kabisa kiasi kinachosababisha baadhi ya watoa huduma za usafiri na usafirishaji kulazimika kutoza nauli mara 5 au 10 zaidi ya tofauti ukilinganisha na gharama ya kusafiria umbali huo huo maeneo ya mijini (kwenye barabara za lami).

Gharama kubwa za usafiri na usafirishaji siyo tu inachangia kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi kiuchumi na biashara, bali pia yanafifisha juhudi za Serikali kupambana na umasikini kwa wananchi kwani imekuwa ikichangia baadhi ya vifo vya akinamama, watoto na wagonjwa ambao wangehitaji rufaa au huduma katika hospitali kubwa zilizoko mijini lakini wameshindwa kutokana na kushindwa kumudu gharama usafiri.

Kutokana na changamoto hizo za ubovu wa barabara kwa vijiji vya jimbo la Kwimba mkoani Mwanza, Mhe.SHANIF MANSOOR, ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, amefanya ziara ya kukagua kujionea hatua zilizofikiwa za ukarabati wa barabara zilizo kwenye mradi. 

Mbunge huyo, amekagua barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita 6, inayotoka kijiji cha Mwashigi kata ya Nyamilama kuelekea kata ya Mwakilyambiti ambayo amesema  ikikamilika itachochea maendeleo na urahisishaji wa utoaji huduma kwani inaunganisha vijiji mbalimbali vya jimbo la Kwimba.

Aidha mbunge huyo wa vitendo, amesema amehamasika kuikarabati barabara hiyo kutokana na adha ya muda mrefu aliyoiona kwa wapiga kura wake sanjari na kutimiza ahadi aliyoitoa kipindi cha uchaguzi. "Itambulike kwamba ukarabati huu fedha zake si za mfuko wa jimbo bali ni kutoka kwenye mshahara wangu, najitolea kwa moyo wa dhati kwa kuwa nami ni mwananchi wa hapa na ninaogopa kuulizwa juu ya ahadi yangu niliyoitoa" Alisema MANSOOR. 

Friday, November 23, 2018

LUGOLA - ASKARI ATAKAYESHIKWA NDEVU NA JAMBAZI KUKIONA





GSENGOtV
Ziara ya Waziri Kangi Lugola jijini hapa imekuja mara baada ya tukio kubwa la kusisimua lililotokea hivi karibuni baada ya jeshi la polisi mkoani Mwanza kufanikiwa kuanza kuvunja mtandao wa majambazi  ambapo mara baada ya kuzuka majibizano ya silaha za moto kwa zaidi ya muda wa dakika 45, polisi walifanikiwa kuwauwa zaidi ya majambazi 7 wanaosadikika kuhusishwa na matukio kadhaa ya uhalifu Kanda ya Ziwa. 
Akizungumza na maofisa wa polisi na baadhi ya askari wa vikosi vyote vya polisi jijini hapa leo Ijumaa Novemba 23,2018 katika viwanja vya polisi Mabatini, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema askari wote walioshiriki katika mapambano na kufanikisha zoezi hilo lililotokea Novemba 15, 2018 jijini Mwanza watapandishwa vyeo.
"Kwenye sheria yetu ya Jeshi la polisi na polisi wasaidizi sura ya 322, ukienda kwenye makosa ya kinidhamu ya askari, Ni kosa kwa askari kuwa mwoga, 'askari hupaswi kukimbia tukio' lazima ukabiloane nalo" Naomba nikuhakikishie Kamanda Shanna, kwa wale vijana wote waliofanya kazi kubwa kwenye tukio la juzi kukabiliana na majambazi, mimi kama Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi kwa amri ya Serikali tutawapa zawadi ya kuwapandisha vyeo" 
Lugola ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wananchi kuwa wapo salama na kuwatumia salamu wanaofanya uhalifu kwamba bora wajisalimishe na kuacha mara moja vitendo hivyo vinginevyo watashughulikiwa popote watakapokuwa hata kama ni mapangoni maana Serikali ina mkono mrefu.
Awali, Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana amesema mkoa huo upo shwari licha ya kuwapo matukio kadhaa ya wahalifu lakini wamekuwa wakiwadhibiti kabla ya kutekeleza azma yao.

MWAKYEMBE HATOWAACHA WALIOPUUZA USHIRIKA WA JUKWAA LA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI


 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza umuhimu wa viongozi wa Juu katika Taasisi za Viwanda na Biashara kushiriki Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora leo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa mada,wa kwanza kulia ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda na wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Bw.Habbi Mkwizu.
 Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda akitoa maelekezo ya kila mkoa kutenga eneo la uwekezaji ambalo litawekewa miundombinu yote muhimu kama Maji,Umeme,Barabara na Huduma za kijamii ili kuweka mazingira rafiki ya kuvutia wawekezaji,leo wakati wa uwasilishaji mada katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Viwanda leo linaloendea Mkoani Tabora.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akisisitiza suala la Wakurugenzi wa Halmashauri kusaini makubaliano na ofisi yake mara baada ya hitimisho la Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora leo katika kikao cha uwasilishwaji wa madambalimbali.
 Mkurugenzi Mkuu wa Export Processing Zones Authority (EPZA) Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akionyesha Jezi ya Michezo inayotengenezwa hapa nchini na kuuzwa nje ya nchi na moja ya Kiwanda kilichopo Morogoro kinachosimamiwa na EPZA ambapo alipokuwa akiwasilisha mada ya namna ya kuvutia wawekezaji nchini kutoka nje katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora leo.
 Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe.Gift Msuya akichangia mada wakati wa uwasilishaji wa mada mbalimbali uliyokuwa ukifanyika leo katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora.
Mkurugenzi Mkuu wa Export Processing Zones Authority (EPZA) Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora andiko la EPZA linaloonyesha namna ya kujenga mazingira uwekezaji bora na kutafuta masoko ya kimataifa kwa bidhaa utakazozalisha leo katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora.



Na Anitha  Jonas – WHUSM
23/11/2018
Tabora.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watendaji wakuu wa taasisi zinazohusika na Uwekezaji na Biashara nchini kutopuuzia ushiriki akatika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji inaloratibiwa na Kampuni ya Magazeti  Serikali (TSN).

Mheshimiwa  Mwakyembe ametoa tamko hilo leo Mjini Tabora alipokuwa  akiendesha mijadala inayotokana na uwasilishwaji wa maandiko mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloratibiwa na TSN na kusisitiza kuwa kwa viongozi wa taasisi ambazo zimepuuzia ushiriki  nitatoa yao taarifa kwa Waziri Mkuu.

“Watendaji  wakuu wa Taasisi za Uwekezaji  hili Jukwaa siyo la kulichukulia mzaha kwa sasa tunataka kujenga nchi ya Viwanda na kuboresha mazingira yetu ya uwekezaji nyinyi ndiyo wakutoa taarifa rasmi kwa  watanzania na wajasiriamali wengi nchini hawana uwelewa mzuri wa kuendesha shughuli zao kisasa na utaratibu wa kurasimisha biashara zao, hivyo ili tupige hatua ni lazma tuboreshe mazingira ya ndani ya nchi yetu kwa kuwaeleza wajasiriamali wetu fursa zilizopo na namna ya kuzifikia,” alisema Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika Jukwaa hilo Waziri Mwakyembe aliuagiza uongozi  wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kuanzia Jukwaa  lijalo litakalo andaliwa na TSN nao kushiriki kikamilifu bega kwa bega ili kuongeza tija katika kufanikisha azma ya nchi kufikia uchumi wa Viwanda na Uchumi wa Kati kwa kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo  Mikoani ili kuvutia wawekezaji  mbalimbali.

Naye Waziri wa Biashara Viwanda na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda  alisisitiza kuwa kwa Taasisi ya SIDO na TBS Wakurugenzi wake kushindwa kufika ua kuelekeza kiongozi yoyote wa juu kumwakilisha na badala yake kumpa Afisa wa ngazi ya chini basi ni lazma atawajibika kujieleza kwa barua kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

“Sasa ifike mahali tuache masihara katika masuala ya kujenga taifa  katika Jukwaa hili tumeona Watendaji wa Wakuu mbalimbali wa Taasisi wamewasilisha maandiko yao na kueleza mipango madhubuti wanayotekeleza na fursa zilizopo na ni utaratibu gani unaweza kutumika kufanikisha mazingira mazuri ya biashara na ukuaji wa viwanda,” Mhe.Kakunda.

Pamoja na hayo Mhe.Kakunda amewataka Wakuu wote wa Mikoa  kujipanga na kutenga maeneo ya uwekezaji ambayo yatahakikishwa yanawekewa miundo mbinu  yote muhimu  kama Maji,Umeme,Barabara na Huduma za kijamii ambazo zitasaidia kuvutia wawekezaji.

Hata hivyo Waziri huyo wa Viwanda Biashara na Uwekezaji aliendelea kusisitiza kuwa kwa viwanda vilivyokuwa vimepewa wawekezaji na wawekezaji hao kushindwa kuviendeleza serikali haitakubali viwanda hivyo kuwa magofu bali itavichukua na kutafuta wawekezaji wengine watakao viendeleza.

Halikadhalika nae Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri  alisisitiza kuwa kwa upande wa Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoa huo mara baada ya kufungwa kwa Jukwaa hilo watasaini makubaliano katika yao na Mkuu wa Mkoa ya namna wataenda  kutekeleza miradi mitatu kwa halmashauri zao kufuatia elimu waliyoipata katika jukwaa hilo na kwa Mkurugenzi atakayeshindwa kutekeleza hilo hatosita kumchukulia hatua kali sababu hatoshi kwa Mkoa wa Tabora unaoangazia maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa sasa.

MKUTANO WA MAKAMANDA WA VIWANJA VYA NDEGE NA MIKOA PAMOJA NA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE (TAA)

 KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA (CGF) THOBIAS ANDENGENYE AKIZUNGUMZA NA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIWANJA VYA NDEGE WA JESHI HILO KATIKA MKUTANO ULIOANDALIWA NA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA) MAPEMA LEO HII KATIKA UKUMBI WA (TCAA) UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM.

MKURUGENZI WA RASILIMALI WATU NA UTAWALA BW. LAWRENCE THOBIAS KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA AKIWASILISHA MADA KATIKA MKUTANO WA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIWANJA VYA NDEGE WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA, ULIOFANYIKA LEO TEREHE 23.11.2018 KATIKA UKUMBI WA TCAA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM.

MKAGUZI WA VIWANJA VYA NDEGE KUTOKA MAMLAKA YA ANGA BW. BURHAN HAJJI MAJALIWA AKITOLEA UFAFANUZI UKAGUZI UNAOFANYWA NA MAAFISA USALAMA KATIKA VIWANJA VYA NDEGE , LEO KATIKA MKUTANO WA UONGOZI WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA NA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIWANJA VYA NDEGE WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KATIKA UKUMBI WA TCAA UKONGA JIJINI DAE ES SALAAM.

KAMISHANA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA (CGF) THOBIAS ANDENGENYE AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MWAKILISHI WA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA) BW. LAWRENCE THOBIAS PAMOJA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LEO KATIKA VIWANJA VYA TCAA UKONGA JIJINI DAR ES SASALAAM.

SERIKALI KUJENGA VITUO VYA POLISI 65 KATIKAWILAYA MPYA

Naibu   Waziri   wa Mambo  ya   Ndani   ya   Nchi,   Mhandisi   Hamad   Masauni,akiwaongoza   Wajumbe   wa   Kamati   ya   Ulinzi   na   Usalama   ya   Wilaya   yaKilindi   kuingia   Kituo   cha   Polisi   cha   Songe, ikiwa   ni ziara   ya   kikazi   yaNaibu   Waziri   kukagua   shughuli   za   ulinzi   na   usalama   wilayani   Kilindimkoani Tanga .Picha  na  Wizara  ya Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi 
Naibu   Waziri   wa Mambo   ya   Ndani   ya   Nchi,   Mhandisi   Hamad   Masauni,akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha   Wajumbe   wa   Kamati   yaUlinzi  na  Usalama  ya  Wilaya  ya Kilindi  ikiwa  ni ziara  ya  kikazi  ya  NaibuWaziri   kukagua   shughuli   za   ulinzi   na   usalama   wilayani   Kilindi   mkoaniTanga  .  Kushoto ni  Mkuu wa Wilaya  ya  Kilindi,  Sauda  Mtondoo  na  Kulia  niKatibu  Tawala  wa  Wilaya  hiyo,  Warda  Abeid. Picha na Wizara ya Mambo yaNdani  ya  Nchi
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda  Mtondoo   akizungumza  katika  kikao  chandani kilichohusisha  Wajumbe  wa  Kamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya  Wilayaya Kilindi  ikiwa  ni ziara  ya  kikazi  ya  Naibu  Waziri  wa  Mambo ya Ndani yaNchi,   Mhandisi   Hamad   Masauni   (katikati)   kukagua     shughuli     za     ulinzi     nausalama  wilayani  Kilindi  mkoani Tanga . Kulia ni  Katibu  Tawala  wa  Wilayahiyo, Warda  Abeid. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani  ya  Nchi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi , EdwardBukombe,  akizungumza  katika   kikao   cha  ndani  kilichohusisha    Wajumbe    waKamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya  Wilaya  ya Kilindi  ikiwa  ni ziara  ya  kikaziya   Naibu   Waziri   wa   Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani, ) kukagua   shughuli   za  ulinzi   na  usalama  wilayani   Kilindimkoani Tanga . Picha  na  Wizara  ya Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi


Serikali imedhamiria kujenga Vituo vya Polisi 65 katika wilaya mbalimbali nchiniikiwa ni juhudi za kukabiliana   na uchakavu na upungufu wa vituo vya polisinchini.

Hayo   yamesemwa   na   Naibu   Waziri   wa   Mambo   ya   Ndani   ya   Nchi,   MhandisiHamad Masauni   baada ya kutembelea na   kukagua  Kituo cha Polisi cha   Songeambacho ndio kituo kikuu katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga

Alisema Serikali inatambua changamoto za vituo vya polisi ikiwemo uchakavu,udogo   wa   majengo   katika   vituo   mbalimbali   nchini   na   iko   katika   mpango   wakujenga vituo vya polisi 65 ili kuwepo na ulinzi thabiti wa raia na mali zao.

“Serikali   inatambua   changamoto   ya   vituo  vya   polisi  hasa   katika  wilaya   mpyanchini, ikiwepo uchakavu wa majengo, kwahiyo uko mkakati maalumu wa kujengavituo vya polisi 65 nchi nzima ili kuweza kukabiliana na matukio ya kiuhalifu,lengo la serikali ni kuhakikisha raia wake na mali zao zinakua salama na matukioya kiuhalifu yanapungua na kutoweka kabisa,” alisema Masauni

Alisema Serikali pia inakaribisha nguvu za wananchi na wadau mbalimbali ambaowako tayari kusaidia ujenzi wa vituo vya polisi huku akipongeza baadhi ya maeneonchini  ambako   vituo  vya  polisi  vimejengwa   kwa  ushirikiano  wa  michango   yawananchi na serikali.

Awali akitoa taarifa ya Ulinzi na Usalama  ya Wilaya ya Kilindi, Mkuu wa Wilayaya  Kilindi   na  Mwenyekiti   wa  Kamati   ya   Ulinzi   na  Usalama,   Sauda  Mtondooalisema hali ya uhalifu kuanzia kipindi cha Januari hadi Oktoba 2018 ilikua yawastani huku kukiripotiwa upungufu wa makosa kwa asilimia 9.8 kati ya mwaka2018 na 2017.

“Kwa mujibu wa takwimu za uhalifu kulikuwa na jumla ya makosa makubwa yajinai 163 ndani ya mwaka huu yaliyoripotiwa kwa kulinganisha na makosa 179yaliyoripotiwa ndani ya mwaka 2017, ukiwepo upungufu wa makosa 16 katikavipindi hivyo viwili,” alisema Sauda

Akizungumza   wakati   wa   ziara   hiyo,   Mbunge   wa   Kilindi,   Omari   Kibuaalimshukuru  Naibu Waziri kwa kufika jimboni hapo kujionea hali halisi ya kituohicho kikuu cha wilaya  baada  ya  kumuomba  kufanya  hivyo wakati wa kikaocha bunge kilichomalizika hivi karibuni

WATALII TANZANIA WATOLEWA HOFU.


Siku chache baada ya Benki kuu ya Tanzania kutoa ufafanuzi juu ya oparesheni ya ukaguzi wa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni jijini Arusha , Wizara ya Mali asili na Utalii imejitokeza na kusema zoezi hilo halijaathiri shughuli za Kitalii

Naibu waziri wa maliasili na Utalii Constatine Kanyasu ameyasema hayo wakati lipotembelea taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kwenye mkutano wake na wafanyakazi wa shirika la hifadhi za taifa(TANAPA) jijini Arusha na kusema watalii wanaendelea kupata huduma kwani zoezi hilo ni la kawaida na limelenga maslahi ya nchi.

Mara baada ya Mazungumzo hayo Naibu Waziri akiwa nje ya Ukumbi wa Mamlaka hiyo , amezungumza na Wanahabari kisha kugusia suala la oparesheni iliyofanywa na Benki Kuu hivi karibu Jijini hapa.Ameeleza kuwa zoezi hilo lililovishirikisha vyombo vya dola na halijaathiri uchumi katika sekta ya fedha za kigeni hasa kwa upande wa utalii kwa kuwa ni zoezi hilo la mara moja kuwahusisha wanajeshi ambao wanawajibu wa kulinda rasilimali za nchi yao.

'' Wanajeshi hawawezi kuathiri uchumi wa nchi hasa sekta ya utalii kwakuwa wanawajibu wa kulinda rasilimali zetu‘’alisema Kanyasu .Akiongelea suala la migogoro ya Ardhi na mipaka kwa baadhi ya mipaka amesema wizara yake imejipanga kukomesha changamoto hiyo ambayo imekuwa ikitumia fedha nyingi bila kupatiwa ufumbuzi.


Aidha amesema migogoro baina ya Hifadhi na Wananchi,Naibu waziri anasema hakuna mtu ama taasisi inayonufaidika na Migogro hiyo na imekuwa ikichochewa na makundi machache na tayari serikali imekwisha anza kuchukua hatua.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Jumla ya Vijiji mia tatu tisini na mbili vitanufaika na zoezi la upimaji wa matumizi bora ya ardhi lenye lengo la Kupunguza

Migogoro ambapo tumepanga billion 2.5 kwa miradi midogo midogo kuweza kuweka nguvu kwa wananchi kuondoa misuguano isiyo na lazima ambayo inaathiri kiasi kikubwa shughuli za uhifadhi.