Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza umuhimu wa viongozi wa Juu katika Taasisi za Viwanda na Biashara kushiriki Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora leo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa mada,wa kwanza kulia ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda na wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TSN Bw.Habbi Mkwizu.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda akitoa maelekezo ya kila mkoa kutenga eneo la uwekezaji ambalo litawekewa miundombinu yote muhimu kama Maji,Umeme,Barabara na Huduma za kijamii ili kuweka mazingira rafiki ya kuvutia wawekezaji,leo wakati wa uwasilishaji mada katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Viwanda leo linaloendea Mkoani Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akisisitiza suala la Wakurugenzi wa Halmashauri kusaini makubaliano na ofisi yake mara baada ya hitimisho la Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora leo katika kikao cha uwasilishwaji wa madambalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa Export Processing Zones Authority (EPZA) Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia akionyesha Jezi ya Michezo inayotengenezwa hapa nchini na kuuzwa nje ya nchi na moja ya Kiwanda kilichopo Morogoro kinachosimamiwa na EPZA ambapo alipokuwa akiwasilisha mada ya namna ya kuvutia wawekezaji nchini kutoka nje katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora leo.
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe.Gift Msuya akichangia mada wakati wa uwasilishaji wa mada mbalimbali uliyokuwa ukifanyika leo katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora.
Mkurugenzi
Mkuu wa Export Processing Zones Authority (EPZA) Kanali Mstaafu Joseph
Simbakalia akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora andiko la EPZA linaloonyesha
namna ya kujenga mazingira uwekezaji bora na kutafuta masoko ya kimataifa kwa
bidhaa utakazozalisha leo katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloendelea Mkoani Tabora.
Na Anitha Jonas – WHUSM
23/11/2018
Tabora.
Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watendaji
wakuu wa taasisi zinazohusika na Uwekezaji na Biashara nchini kutopuuzia
ushiriki akatika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji inaloratibiwa na Kampuni
ya Magazeti Serikali (TSN).
Mheshimiwa Mwakyembe ametoa tamko hilo leo Mjini Tabora
alipokuwa akiendesha mijadala inayotokana
na uwasilishwaji wa maandiko mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa katika Jukwaa
la Fursa za Biashara na Uwekezaji linaloratibiwa na TSN na kusisitiza kuwa kwa
viongozi wa taasisi ambazo zimepuuzia ushiriki
nitatoa yao taarifa kwa Waziri Mkuu.
“Watendaji wakuu wa Taasisi za Uwekezaji hili Jukwaa siyo la kulichukulia mzaha kwa
sasa tunataka kujenga nchi ya Viwanda na kuboresha mazingira yetu ya uwekezaji
nyinyi ndiyo wakutoa taarifa rasmi kwa
watanzania na wajasiriamali wengi nchini hawana uwelewa mzuri wa
kuendesha shughuli zao kisasa na utaratibu wa kurasimisha biashara zao, hivyo ili
tupige hatua ni lazma tuboreshe mazingira ya ndani ya nchi yetu kwa kuwaeleza
wajasiriamali wetu fursa zilizopo na namna ya kuzifikia,” alisema
Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza
katika Jukwaa hilo Waziri Mwakyembe aliuagiza uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)
kuanzia Jukwaa lijalo litakalo andaliwa
na TSN nao kushiriki kikamilifu bega kwa bega ili kuongeza tija katika kufanikisha
azma ya nchi kufikia uchumi wa Viwanda na Uchumi wa Kati kwa kutangaza fursa za
uwekezaji zilizopo Mikoani ili kuvutia
wawekezaji mbalimbali.
Naye Waziri wa
Biashara Viwanda na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda alisisitiza kuwa kwa Taasisi ya SIDO na TBS
Wakurugenzi wake kushindwa kufika ua kuelekeza kiongozi yoyote wa juu
kumwakilisha na badala yake kumpa Afisa wa ngazi ya chini basi ni lazma
atawajibika kujieleza kwa barua kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kwa kushindwa
kutekeleza majukumu yake.
“Sasa ifike mahali
tuache masihara katika masuala ya kujenga taifa
katika Jukwaa hili tumeona Watendaji wa Wakuu mbalimbali wa Taasisi
wamewasilisha maandiko yao na kueleza mipango madhubuti wanayotekeleza na fursa
zilizopo na ni utaratibu gani unaweza kutumika kufanikisha mazingira mazuri ya
biashara na ukuaji wa viwanda,” Mhe.Kakunda.
Pamoja na hayo
Mhe.Kakunda amewataka Wakuu wote wa Mikoa
kujipanga na kutenga maeneo ya uwekezaji ambayo yatahakikishwa
yanawekewa miundo mbinu yote muhimu kama Maji,Umeme,Barabara na Huduma za kijamii
ambazo zitasaidia kuvutia wawekezaji.
Hata hivyo Waziri
huyo wa Viwanda Biashara na Uwekezaji aliendelea kusisitiza kuwa kwa viwanda
vilivyokuwa vimepewa wawekezaji na wawekezaji hao kushindwa kuviendeleza
serikali haitakubali viwanda hivyo kuwa magofu bali itavichukua na kutafuta
wawekezaji wengine watakao viendeleza.
Halikadhalika nae
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri alisisitiza kuwa kwa upande wa Wakurugenzi wa
Halmashauri Mkoa huo mara baada ya kufungwa kwa Jukwaa hilo watasaini
makubaliano katika yao na Mkuu wa Mkoa ya namna wataenda kutekeleza miradi mitatu kwa halmashauri zao
kufuatia elimu waliyoipata katika jukwaa hilo na kwa Mkurugenzi atakayeshindwa
kutekeleza hilo hatosita kumchukulia hatua kali sababu hatoshi kwa Mkoa wa
Tabora unaoangazia maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa sasa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.