Saturday, September 11, 2010
BANGO
NI USIKU WA LEO MABINTI 31 KUKUTANISHWA KATIKA KILELE CHA KUMTAFUTA VODACOM MISS TANZANIA 2010. YUKO WAPI KATI YA HAWA PICHANI?
* Date of the event – September 11, 2010
* Venue of the event – Mlimani city Conference Hall, DSM
* Time of the event – From 7pm sharp onwards
* Tickets selling points – Vodashop Ohio street, Miss Tanzania offices at Mkwepu street, Steers at City Centre, Best Bite Namanga, Rose Garden Bar Mikocheni, Photo Points at Benjamin Mkapa Building City Centre and Mayfair Plaza Mikocheni,
* List of entertainment – Wahu from Kenya, AY, THT group (Barbana, Linah & Mataruma), The Tanzanite band, Chege and Temba.
Saturday, September 11, 2010
HABARI
Friday, September 10, 2010
HABARI
Kasisi wa Kimarekani ambaye amezua lalama kali duniani kufuatia mpango wake wakuchoma Koran tukufu hapo Kesho Septemba 11 amesema mpango wake utategemea kutekelezwa kwa masharti anayotaka yafanywe.
Saa chache zilizopita, Mchungaji Terry Jones alitangaza kufutilia mbali mpango wake wa kuchoma moto nakala za Koran tukufu
Hii ilikuwa baada ya kudai kwamba alikuwa amefikia makubaliano na viongozi wa kiislamu.Alidai walikubaliana kubadili sehemu ya kujenga kituo cha kiislamu, mjini New York, ili naye mchungaji huyo afutilie mbali uamuzi wake wa kuchoma moto nakala za kitabu cha Koran.
Jones aliandamana na Imam wa eneo lake akitoa tangazo hilo.
"Raia wa Marekani hawataki msikiti pale na bila shaka waislamu hawataki sisi tuchome Koran. Imam amekubali kuhamisha mpango wa kujenga kituo cha utamaduni cha kiislamu, katika eneo ambako mashambulio yalifanyika"Alisema Jones.
Hata hivyo si wazi kama makubaliano yamefikiwa. Msemaji wa kundi linalohusika na ujenzi wa kituo hicho amesema kuwa hakuna mpango wowote wa kuhamisha kituo hicho na msikiti.
Bw Jones anadai kuwa viongozi hao wa kiislamu walimhadaa.
Huenda kile mchungaji Jones anachosema ni makubaliano, ni mazungumzo tu kwamba yeye na Imam wa New York, Faizal Rauf, ambaye ndiye msimamizi wa mradi huo watakutana jumamosi kujadili, hali ambayo bado ni ya utata kuhusu ujenzi wa kituo hicho.
Awali, katika mohojiano na kituo cha televisheni cha ABC, rais Obama alitaja mpango wa mchungaji huyo kama mchezo wa kuigiza.
"Kama anasikiliza natumaini anaelewa kwamba kile anachopendekeza kukifanya, ni kinyuma kabisa na maadili yetu kama wamarekani. Kwamba nchi hii ilijengwa kwa misingi ya uhuru wa kuabudu na kuvumiliana kwa dini. "alionya Obama.
Kitendo cha mchungaji huyo kutaka kuchoma moto kitabu cha Koran kimeshutumiwa vikali kote duniani.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
Thursday, September 09, 2010
HABARI
Wednesday, September 08, 2010
HABARI
Mamia ya wafungwa wametoroka jela moja iliyo eneo la kati la Nigeria baada ya genge lenye silaha kuvamia gereza.
Wakuu wa Nigeria wanadai kuwa kundi lenye msimamo mkali wa Kiislamu, Boko Haram ndilo lililohusika na shambulio hilo.
Imethibitishwa kuwa watu wanne waliuawa na wengine sita kujeruhiwa.
Polisi sasa wanasaka baina ya watu mia saba na mia nane katika Jimbo la Bauchi.
Wahalifu hao wenye silaha walivamia jela na kuingia kila chumba wakiwaachilia huru wafungwa kabla ya kulichoma moto jengo zima la gereza.
Wakuu hao wanasema taarifa za kijasusi zinaonyesha kuwa kundi la Boko Haram lenye msimamo mkali unaopinga elimu ya magharibi na sayansi ndilo lililohusika.
Takriban wafuasi 100 wa kundi hilo walikuwa ndani ya jela hiyo wakisubiri hukumu kutokana na ghasia za mwaka jana dhidi ya polisi na serikali ya Nigeria.
Wakati huo zaidi ya watu 800 waliuawa na kiongozi wa kundi hilo Mohammed Yousef akauawa kwa risasi baada ya kuizingira nyumba yake.
Lakini katika siku za hivi karibuni kundi hilo limejigamba kuwa na kiongozi mpya na kwamba lina mipango ya kujiimarisha kwa silaha.
Kuna khofu kwamba kundi hilo linatumia mbinu mpya na ujanja na huenda limehusika katika 'mawaji baridi' ambamo maofisa kadhaa wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye silaha wakitoroka kwa kutumia kasi ya pikipiki.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
Wednesday, September 08, 2010
huzuni
HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE NA ZA KUTHIBITIKA KABISA, ZINARIPORI KWAMBA MKURUGENZI MSAIDIZI WA BENDI YA MUZIKI WA DANSI YA DIAMOND MUSICA, PERFECT KAGISA 'P. DIDDY' (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA.
P. DIDDY AMBAYE ALIKUWA NI MCHUMBA WA MTANGAZAJI MAARUFU WA TBC1,MAIMATHA JESSE AMEPATWA NA MAUTI HAYO LEO HII WAKATIKA AKIWA KATIKA MATEMBEZI YAKE YA KILA SIKU BAADA YA KUANGUKA GHAFLA KATIKA BARABARA YA LUMUMBA, MNAZI MMOJA, JIJINI DAR ES SALAAM
MWILI WA MAREHEMU UMEPELEKWA KATIKA HOSPITAL YA TAIFA YA MUHIMBILI KWA UCHUNGUZI ZAIDI.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN
KWA HISANI YA MICHUZI JR.
Tuesday, September 07, 2010
BANGO
BAADA YA KIMYA CHA MUDA MREFU NA WATU KUPATWA NA GONJWA JIPYA UBUNA (UPUNGUFU WA BURUDANI NAFSINI), ILE CLUB YAKO IMERUDI TENA NA SAFARI HII NI ZAIDI.
FUNDI AKINAKSHI SEHEMU ZA KUTA NDANI YA UKUMBI WA STONE CLUB ROCK CITY AMBAPO UFUNGUZI RASMI KUFANYIKA EID MOSI, DJ MWALIKWA DJ PQ KULIGENGESHA.
MBALI NA KUWA NA MWONEKANO WA UTOFAUTI NA ULE ULIOZOEA, STONE CLUB KWA SASA ITAKUWA NA SOUND YA UKWELI, LIGHTS ZIMEFUNGWA MPYA, ZILE ZA ZAMANI TUPA KULEE, DANCE FLOW TAMU, KAUNTA KONA ZOTE TANO, SMOKING CHAMBER, WASH ROOM ZA KISASA, AIR CONDITION NA.....
NIMEVAMIA TU! KAZI IKIKAMILIKA UTAUFAIDI MWONEKANO.
Monday, September 06, 2010
MWANZA