Polisi akiwa ameubeba mwili wa mtoto aliyeuawa. |
Polisi wakishirikiana kupakia miili ya marehemu hao kwaajili ya kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi. |
Watu watatu wa familia moja wameuawa kikatili usiku wa kuamkia jana na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi katika kijiji cha Ihila B, Kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana hapa Mkoani Mwanza.
Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kwamba watu hao ambao ni Jonus Elius (44) ambae ni baba wa familia, Lucia Jonus (35) ambae ni mama wa familia pamoja na Eliud Jonus (1) ambae ni mtoto wa familia hiyo wameuawa kikatili kufuatia baba wa familia hiyo kuchinjwa shingoni na kitu kinachosadikiwa kuwa na ncha kali huku mama na mtoto wakisadikiwa kunyongwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni waya.
Uchunguzi wa awali unaeleza kwamba kulikuwa na mgeni ambae alifika katika familia hiyo ndani ya siku nne kwa ajili ya shughuli ya kufyatua tofali za ujezi wa nyumba ya familia hiyo, ambae anasadikiwa kutenda tukio hilo kwa kuwa baada ya mauaji hayo ametoweka katika familia hiyo.
Akiwa katika eneo la tukio Mkuu wa makosa ya upepelezi Mkoa wa Mwanza RCO Joseph Konyo ameeleza kwamba mauaji hayo yanasadikika kutekelezwa kati ya majira ya saa nane hadi saa kumi usiku wa kuamkia leo.
Aidha RCO Konyo amesema kwamba bado uchunguzi zaidi juu ya mauaji hayo unaendelea na taarifa zaidi zitatolewa na msemaji wa jeshi la polisi Mkoa wa wa Mwanza ambae ni RPC pindi upelelezi utakapokamilika ambapo amewataka wananchi kutoa ushirikiano wao ili kuweza kufanikisha upelelezi huo mapema.
Kufuatia mauaji hayo ya kusikitisha ambayo yanasadikika kutekelezwa huku sababu zikiwa bado ni kitendawili, wananchi na majirani wa eneo hilo la tukio wameeleza kusikitishwa kwao na matukio ya aina hiyo ambayo wametoa rai kwa jeshi la polisi kuhakikisha likamilisha upelelezi wake mapema na kuhakikisha kwamba wahusika wote wanafikishwa katika vyombo vya dola.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.