ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 8, 2019

HIVI .... KIBONDE ALIKUWA KATIKA HALI GANI KWENYE MSIBA WA RUGE?



WANANCHI mkoa wa Mwanza wamekuwa watu wa awali kuuaga mwili wa aliyekuwa  mtangazaji maarufu nchini Tanzania, mshereheshaji wa dhifa mbalimbali Ephraim Kibonde aliyefariki dunia jana wakati akipatiwa huduma za matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda jijini Dar es salaam kwaajili ya taratibu nyingine za mazishi.

Kibonde amefariki dunia alfajiri ya siku ya Alhamisi ya tarehe 7 mwezi Machi 2019 katika hospitali ya Rufaa ya Bugando, baada ya kuzidiwa ghafla akiwa mjini Bukoba ambako alikwenda kuhudhuria mazishi ya Ruge Mutahaba, na kusafiri hadi mkoani Mwanza ili kupatiwa matibabu zaidi lakini baadaye umauti ukamkuta.

Akiwa mjini Bukoba kwenye mazishi ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media  naye akiongoza kama Mc, hakuna aliyedhani kuwa saa 48 mara baada ya tukio hilo naye angetoweka.

Jeh kuna chochote ambacho kwa jicho la kibinadamu kuna yeyote angeweza kubaini? Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula anasimulia ya kwake aliyoyaona.......

WANAHABARI MWANZA WAGUSWA NA MSIBA WA KIBONDE



SHUKRANI 

Ndugu waandishi wa habari wa Mwanza, tunawashukuru sana  kwa kujitokeza kwenu  tangia asubuhi hadi jioni kwenye  tamati ya kuusindikiza mwili wa  Mwandishi mwenzetu Ephraim Kibonde 

Tulijumuika sote kwa umoja wetu km waandishi wa Mwanza, hili ni jambo la kujivunia sana. Pia taasisi zetu za kihabari UKWAMA, UTPC, MPC na OJADACT zilifanya kazi kubwa ya kutuunganisha pamoja bila kujali itikadi zetu.

Tulipata nafasi ya kumuaga na kumsindikiza mwenzetu, hakika tumetimiza wajibu wetu.

Tunawashukuru sana 

 Edwin Soko 

Thursday, March 7, 2019

Uzinduzi wa jukwaa la NAWEZA wafana Jijini Mwanza

Kaimu Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Esther Mariki akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa jukwaa la mawasiliano ya afya kwa watu wazima liitwalo NAWEZA lililo chini ya mradi wa USAID TULONGE AFYA. Uzinduzi huo ulifanyika jana Machi 06, 2019 Jijini Mwanza, lengo likiwa ni kuhamasisha utekelezaji wa afya mbalimbali ili kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto chini ya miaka mitano.
BMG Habari
Kaimu Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Esther Mariki akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa jukwaa la Naweza.
Kaimu Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Esther Mariki akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Kaimu Katibu Tawala mkoani Mwanza, Emily Kasagara akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Ukumbusho wa picha na viongozi mbalimbali.
Tazama BMG Online TV hapa chini

Tuesday, March 5, 2019

MRISHO MPOTO AMLIZA MAKONDA, RIDHIWAN, MONGELLA, STEVE NYERERE, ADEN RAGE NA MAMA HUYU


BAADA ya kupasa sauti zaidi ya mara tatu akiliita jina la mja mwendazake Ruge Mutahaba, huku wengi wakihisi huenda kwa sauti yake hiyo marehemu angeweza kunyanyuka akiwa hai, akilia kwa uchungu mwanamuziki Mrisho Mpoto, ananena maneno haya.....

"Unasema tusilie, Umetuambia tusilie, Nani anaweza kuzuia machozi yasitiririke katika viwanja hivi Ruge? Naniiiiiiiiiiiiiii anyooshe mkono, anyanyue kidole aseme tusilie"


"Ikiwa Mungu ameweza kupokea maombi yetu ya kusimamisha mvua ili leo tukulilie, Tukushangilie kwa machozi, nauliza ni nani atakayemudu kututuliza...............?" 

Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba umezikwa kishujaa nyumbani kwao katika kijiji cha Kiziru Kata ya Karabagaine Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera huku mamia ya watu wakiwemo viongozi wa serikali wakishiriki mazishi hayo. 

Zoezi la kuzika mwili wa Ruge lilianza kwa Ibada ya mazishi ambayo iliongonzwa na Katibu wa Parokia ya Itahwa, Anatory Kyatwa huku nyimbo za maombolezo za kiswahili na za kabila la kihaya zikipamba tukio la mazishi.

Sunday, March 3, 2019

KWA NINI MAREHEMU RUGE ANAPATA HESHIMA KUBWA KIASI HIKI?



"Marafiki zangu hasa wa nje wamekuwa wakiniuliza ni nani huyo anaye tikisa kwa habari za msiba wake na hata kupata mapokezi mazito kiasi hicho, huku vyombo vya habari vikisitisha taratibu zake za kawaida na kumuomboleza?" ilikuwa ni sehemu ya maelezo ya yake mwanahabari Abdalah Majura aliyepata nafasi kuzungumza na Jembe Fm + GsengoTv wakati akimuelezea marehemu Ruge Mutahaba kwenye mapokezi Uwanja wa Ndege wa mjini Bukoba.

Inatosha kumuenzi Ruge Mutahaba kwa kuyaishi mambo yote aliyoyaamini na kuhimiza ... kama kijana ambaye Mwenyezi Mungu alimjaalia vipawa vingi lakini kubwa kuliko yote ni kuishi ndani ya mioyo ya watu.