WANANCHI mkoa wa Mwanza wamekuwa watu wa awali kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji maarufu nchini Tanzania, mshereheshaji wa dhifa mbalimbali Ephraim Kibonde aliyefariki dunia jana wakati akipatiwa huduma za matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda jijini Dar es salaam kwaajili ya taratibu nyingine za mazishi.
Kibonde amefariki dunia alfajiri ya siku ya Alhamisi ya tarehe 7 mwezi Machi 2019 katika hospitali ya Rufaa ya Bugando, baada ya kuzidiwa ghafla akiwa mjini Bukoba ambako alikwenda kuhudhuria mazishi ya Ruge Mutahaba, na kusafiri hadi mkoani Mwanza ili kupatiwa matibabu zaidi lakini baadaye umauti ukamkuta.
Akiwa mjini Bukoba kwenye mazishi ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media naye akiongoza kama Mc, hakuna aliyedhani kuwa saa 48 mara baada ya tukio hilo naye angetoweka.
Jeh kuna chochote ambacho kwa jicho la kibinadamu kuna yeyote angeweza kubaini? Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula anasimulia ya kwake aliyoyaona.......
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.