ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 24, 2015

TOTO YASHINDA NYUMBANI1-0 DHIDI YA POLISI MARA

WAKATI timu ya Mwadui Fc ya mjini Shinyanga ikilazimishwa sare tasa nyumbani kwa Kanembwa Fc pale mkoani Kigoma kunako uwanja wa CCM Kirumba Mwanza mchezo mwingine wa Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara uliowakutanisha Toto Africana dhidi ya Polisi Mara umeishuhudia timu hiyo ya Mtaa wa Kishamapanda (Toto Africans) ikiibuka kifua mbele na kuzidi kujiweka pazuri mara baada ya kuondoka na pointi zote tatu muhimu kwa kuifunga Polisi Mara bao 1-0. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA

HAYA NDIO MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI YALIYOTANGAZWA NA RAIS KIKWETE JIONI HII

Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri,Ikulu Jijini Dar es Salaam.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ametangaza mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri,ambalo Ameliapisha jioni hii Ikulu,Jijini Dar es Salaam.

Akitangaza uteuzi huo muda mchache kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue amesema uteuzi huo unahusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa Sospeter Muhongo.

Profesa Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieachishwa kazi kutokana na kuhusika kwake katika sakata la akaunyti ya Tegeta Escrow.

Kwa upande wa Profesa Muhongo aliachia ngazi mwenyewe mapema leo,  kwa kile alichotaja kuipisha Serikali iendelee kuwatumikia Wananchi badala ya kuendelea na malumbano ya Escrow.

Katika mabadiliko hayo,sura mpya za manaibu mawaziri zimeingia na baadhi ya mawaziri wamehamishwa wizara.

Akitangaza Mabadiliko hayo,Balozi Sefue aliwataja mawaziri hao kama ifuatavyo.

MAWAZIRI

1. Mh. George Simbachawene - Waziri wa Nishati na Madini
2. Mh. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mahusiano na Uratibu)
3.Mh. Christopher Chiza - Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
4. Mh. Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
5.Mh. William Lukuvi - Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
6.Mh. Steven Wasira - Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
7.Mh. Samwel Sitta -Waziri wa Uchukuzi
8.Mh. Jenista Muhagama - Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge

MANAIBU WAZIRI
1. Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais - Muungano
2. Mh. Angela Kairuki -  Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
3. Mh. Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4. Mh. Anna Kilango - Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5 . Mh. Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini

HATIMAYE WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA MUHONGO AJIUZURU

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akitangaza kujiuzulu mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 
WAZIRI wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo ameamua kujiuzulu nafasi yake. 

Profesa Muhongo ametangaza hatua hiyo leo asubuni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habarimakao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
Akitangaza kujiunzulu mbele ya waandishi wa habari mapema leo Jumamosi Januari 24, 2015 makao makuu ya wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam Waziri wanishati na Madini, Profesa sospeter Muhongo, ametangaza kujiuzulu kutoka wadhifa huo mapema leo Jumamosi Januari 24, 2015.

Waziri huyo mtaalamu wa miamba, amejiuzulu kufuatia shinikizo la mudamrefu la kumtaka afanye hivyo au awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya bunge lililopita, lililoiagiza Serikali kuchukua hatua dhidi ya viongozi wote na watendaji waliohusika na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow iliyobainisha kiasi cha fedha bilioni 302 kuchotwa BOT zilipokuwa zikihifadhiwa.

Mwishoni mwa mwaka jana, 2014, Bunge la Tanzania lilitoka na maazimio ya kutaka kuwajibishwa kwa mawaziri Profesa Sospeter Muhongo, Profesa Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema, kutokana na sakata la uchotaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu (BoT) kwa kutaka mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao. Mbali na hao, yumo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)..

Profesa Muhongo anakuwa ni kigogo wa nne kufuata mkumbo baada ya Waziri Profesa Anna Tibaijuka kufukuzwa nafasi yake na Rais, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema kujiuzulu mwenyewe, huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akisimamishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuvunjwa.


Katika hotuba ya mwisho ya Rais Jakaya Kikwete, siku alipotengua uwaziri wa Profesa Anna Tibaijuka alisema amemeweka kiporo Profesa sospeter Muhongo wakati uchunguzi zaidi wa kashfa hiyo ukifanywa.Taarifa zaidi ni hapo baadaye..

Friday, January 23, 2015

KAMA UKO MWANZA HIZI HAPA NAFASI ZA KAZI


Kuanzia kesho utaziona taarifa hizi na sifa husika kwa uzuri zaidi katika bango hapo juu ya Blogu. 

Kwa yeyote mwenye sifa tajwa hapo juu, tuma vielelezo vyako yaani CV ukiambatanisha na Certificates zako husika kupitia Email:- sales@kambasinvestiments.com 
Kabla ya tarehe 05/02/2015.
Aksante 
Naomba kuwasilisha.

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE YA SEKONDARI KITETO MANYARA

Wanafunzi wa shule ya sekondari kiteto wakionyesha vitabu baada ya kukabithiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mradi wake wa Airtel shule yetu wenye lengo la kuchangia katika sekta ya elimu nchini.

Na Mwandishi wetu

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imepiga jeki jitihada za serikali za kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule ya sekondari ya Kiteto iliyopo mkoani Manyara.

Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 1.5 unahusisha vitabu vya fizikia, hisabati, baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo katika shuleni hiyo.

Akipokea msaada huo Diwani wa kata ya Central wilayani Kiteto Mh Yahya Masumbuko, amesema shule nyingi wilayani hapo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitabu vya masomo ya sayansi licha ya kwamba kuna uhaba pia wa walimu wa masomo hayo.

“Ni kweli kwamba uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujifunza kwa ufasaha masomo ya Sayansi wilayani Kiteto hali inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu ya sayansi wilayani hapa”. Alisema Mh Masumbuko.

“Uhaba wa vitabu ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi pia ni kikwazo kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa wanafunzi wetu hapa wilayani” aliongeza Mh Masumbuko.

Aidha Diwani huyo ameishukuru kampuni ya simu ya Airtel  kwa kuona umuhimu wa kuboresha masomo ya sayansi ambayo  ufaulu wake umekuwa mdogo hali ambayo inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.

“Msaada huu utaongeza hamasa kwa wanafunzi wetu kujifunza masomo ya sayansi hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kuona umuhimu wa kusaidia shule hii na hasa vitabu vya sayansi” alieleza Mh Masumbuko.

“Sisi wa Kiteto tunaendelea na jitihada za kuhakikisha wanafunzi wetu wanajifunza masomo hayo na ndio maana hata mgao wa walimu tulioupata tumeuelekeza katika ufundishaji wa masomo ya Sayansi. Alimalizia Mh Masumbuko. 

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kiteto wameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuwawezesha kupata vitabu vitakavyowasaidia katika masomo yao.

Msaada huo wa vitabu vya masomo ya hisabati,kemia,fizikia na Bailojia utasaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye shule hiyo ya wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Airtel shule yetu ni mpango endelevu uliodumu kwa takribani miaka 10 iliyopita mpaka sasa zaidi ya shule za sekondari 1300 nchini zimeidika na msaada wa vitabu chini ya mradi huu. Tutaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha sekta ya elimu na kutoa kipaombele kwenye masomo ya sayansi ili kuwa na wanasayansi wengi nchi ambao kwa sasa ni changamoto katika shule nyingi na nchi kwa ujumla alisema Meneja mauzo wa Airtel kanda ya kati Bwana  Hendrick Bruno

SKYLIGHT BAND YAIBUA KIFAA KIPYA MITHILI YA KASUKU SI MWINGINE NI ASHURA KITENGE, NJOO LEO UMSHUHUDIE THAI VILLAGE

DSC_0014
Mratibu wa Skylight Band, Lubea akimkaribisha mdau wa bendi hiyo Miryam Kamaliza shot ya Tequila wakati wa show iliyobamba wakazi wa Dar Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki.
DSC_0017
Mratibu wa Skylight Band, Lubea akimimina kinywaji cha Tequila kwa Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village.
DSC_0018
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akipiga kilaji cha Tequila kupasha mwili joto kabla ya kupanda jukwaani, kinywaji hicho ni maalum kwa mashabiki wa bendi hiyo pindi wanapoingia kwenye kizingiti cha ukumbi huo wa Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0019
Msanii wa Skylight Band Joniko Music (katikati), akifungua dimba la burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo huku akipewa sapoti na Aneth Kushaba AK 47 pamoja na Sam Mapenzi (kulia) wakati show zao za kila Ijumaa ndani ukumbi wa Thai Village Masaki, jijini Dar.
DSC_0115
Aaaah Komando Kipensi weeeeeee... si mwingine ni Le Manager her self Aneth Kushaba AK 47 mutoto ya Kisukuma akifanya yake jukwaani Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar......Tukutane baadae pale kati....Full MAU-KODAK kuwa huru kuomba picha na washikaji zako mdau wetu.
DSC_0034
Murembo mupya binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni, Ashura Kitenge akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita huku akipewa sapoti na Rapa mkongwe Joniko Flower pamoja na Aneth Kushaba AK47.
DSC_0126
Mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga kwa raha zao.
DSC_0053
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 a.k.a #KomandoKipensi akiwa kwenye hisia kali wakati akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0068
Daudi Tumba akifanya yake jukwaani kuhakikisha mashabiki wa Skylight Band wanapata ladha nzuri ya muziki wa Live ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita.
DSC_0072
Majembe ya Skylight Band yakijimwaga na sebene jukwaani kwenye show za bendi hiyo zinazofanyika kila Ijumaa ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0120
Mashabiki wa Skylight Band wakijiachia kwa raha zao ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar.
DSC_0088
Vijana wa Skylight Band wakitimua vumbi jukwaani wakiongozwa na Sony Masamba.
DSC_0141
Twende kazi.... Sony Masamba akilisongesha na vijana wenzake.
DSC_0098
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower (kushoto) akichana mistari huku wenzake wakitimua vumbi jukwaani.
DSC_0109
Sam Mapenzi asali ya warembo akiwa kenye hisia kali alipokuwa akiwapa haki yao mashabiki wa Skylight Band na nyimbo za kisasa zikiwemo Naija Flava, Reggae na zingine kibao....jamaa ni mkali asiyekubali ni mchawi...!
DSC_0131
Mashabiki wa Skylight Band wakijinafasi kwa raha zao.
DSC_0105
Rais wa #Wanamanyoya Sultan Gijegije (kulia) akipata ukodak na wanamanyoya Joshua Ndege (katikati) pamoja na mdau.
DSC_0082
Sura mpya ndani ya Skylight Band yenye sauti mithili ya ndege Kasuka si mwingine ni Ashura Kitenge akishow love na Joshua Ngoje back stage.
DSC_0083
Kisura mwingine wa Skylight Band anayefamika kwa jina la Baby (kulia) akipata ukodak na shosti yake back stage.
DSC_0106
Wadau nambari One wa Skylight Band wakishow love na Ukodak.
DSC_0154
#TeamWadananda wakishow love na mdau.
DSC_0159
Rapa wa Skylight Band Sony Masamba akishow love na wadau wa bendi hiyo baada ya kuhitimisha show ya Ijumaa iliyobamba ndani ya kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar. Tukutane baadae.

Thursday, January 22, 2015

TAIFA STARS V/S AMAVUBI NGOMA DROO 1-1 CCM KIRUMBA MWANZA.

Nahodha wa Taifa Stars Simon Msuva (kushoto) akibadilishana bendera na nahodha wa timuya taifa la Rwanda 'Amavubi' Haruna Niyonzima (kulia) kabla ya mpambano wa kirafiki uwanja wa CCM Kirumba Mwanza. Hadi mwisho wa mchezo timu zinatoka sare ya kufungana bao 1-1.

KUSIKIA KILICHOJIRI BOFYA PLAY
Kikosi cha Taifa Stars 'Maboresho' kilichoshuka leo dimba la CCM Kirumba kukiputa na Amavubi.
Timu ya taifa la Rwanda aka 'Amavubi'
Rais wa TFF Malinzi (wa tano toka kushoto) akiwa na safu ya wakuu meza kuu wakati wimbo wa taifa la Rwanda ukipigwa.
Rwanda.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa MWAUWASA Anthony Sanga akipata utambulisho toka kwa nahodha wa Taifa Stars Simon Msuva (kulia) ambaye hapa akimtambulisha golikipa wa Stars Manyika Peter.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa MWAUWASA Anthony Sanga akipata utambulisho toka kwa nahodha wa Rwanda Haruna Niyonzima (kulia) ambaye hapa akimtambulisha golikipa wa Amavubi Oliver Kwizera.
Nahodha wa Stars Simon Msuva (kushoto) akiukokota mpira kulia mwa uwanja kuelekea goli la Rwanda mbele ya Mugeraneza Batist ambaye ndiyo mfungaji wa bao la Rwanda katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki ulio katika Kalenda ya FIFA ukifanyika dimba la CCM Kirumba Mwanza. Hadi mwisho Tanzania na Rwanda zinatoka sare ya 1-1.  
Simon Msuva akihaha winga ya kushoto kuelekea lango la Amavubi Rwanda nyuma yake ni beki namba mbili Baysenga Emiry (15) na kwa umakini golikipa wa Rwanda Oliver Kwizera (18) akifuatilia mwenendo wa ulinzi. 
Hili ndili goli la kuongoza la Rwanda likifungwa kwa kichwa dakika ya 9 ya mchezo na Mugeraneza Batist, golikipa kupitia mpira wa kona, naye golikipa wa Stars Manyika akiwa ametoka kuuokoa mpira huo alirudi golini kinyumenyume akiushuhudia ukitikisa nyavu zake .
Mpira unazama kimiani ....Rwanda inapata bao la kuongoza.......
Kutoka kushoto ni Sibomana Patrick (Rwanda), katikati ni Shiza Rama (Tanzania), Mugeraneza Batist, Bigirimana Issa na Ismail Nshatyamagara wote wa Rwanda.
Patashika langoni mwa Rwanda toka winga ya kushoto.
Aaaah mzigo wa Selfie..... Kutoka kushoto ni G.Sengo, Haruna Niyonzima na Ladilaus Mbogo wa Toto Africans ya Mwanza.
Tanzania:- Peter Manyika, Miraj Adam, Gabriel Michael, AndrewVicent, Joram Mgeveke, Salim Mbonde, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Kevin Friday/Rashid mandawa dk70, Simon Msuva na ShizaRamadhani/Salum Telela dk 45.

Rwanda:- Oliver Kwizera, Emery Bayisenga, Ismail Nshyutamagara, Maxime sekamana/Yanick Mukunzi dk75, Michael Rusheshangonga, Jean Baptiste Mugiraneza, Haruna Niyonzima, Issa Bigiramana/Andrew Buteera dk61, Betrand Iradukunda/Justin Mico dk90, PatrickSibomana na Janvier Mutuima.

JIJI HATARINI KUSHINDWA KUTEKELEZA MRADI WA TSCP WA ZAIDI BL 3.7 WA UBORESHAJI DAMPO LA BUHONGWA.

NA PETER FABIAN, MWANZA. 

HALMASHAURI YA JIJI la Mwanza hatarini kushindwa kutekeleza mradi wa Tanzania Stragic Cites Projecty (TSCP) chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia wa zaidi ya Sh. Bilioni 3.7 wa uboreshaji wa Dampo la taka eneo la Kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana jijini hapa.

Hatari hiyo inatokana na kuwepo mkanganyiko uliojitokeza hivi karibuni wakati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, alipofanya ziara ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi, kukagua miradi na kujitambulisha kwao katika Wilaya ya Nyamagana, ambapo akiwa Kata ya Buhongwa wananchi walitaka kujua lini watalipwa fidia ya maeneo yao wanayotakiwa kuachia Jiji.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa Mulongo aliambatana na Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM), Mkurugenzi wa Jiji hilo, Halifa Hida baadhi ya wajumbe wa Kamati za ulinzi na usalama Mkoa na Wilaya hiyo, wataalamu wa Jiji, Mameneja wa Tanesco, Tanroad, Mkurugenzi wa MWAUWASA na viongozi wa CCM Wilaya ya Nyamagana.

Baada ya kero hiyo ya fidia kuelezwa na wananchi, RC Mulongo alimtaka Afisa wa Idara ya Mipango miji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Deo Kalemenzi, kujibu hoja hiyo ambayo ilionekana kushangiliwa na wananchi waliokuwa wamefurika kumsikiliza katika viwanja vya shule ya msingi ya Buhongwa.

Kalemenzi akijibu hoja hiyo, alifafanua kuwa katika eneo hilo la dampo la Buhongwa kulifanyika utafiti wa kina na Jiji ili kutekeleza mradi wa TSCP kwa mwaka huu wa fedha wa 2015/2016, kufanya uthamini wa ardhi katika maeneo yasiyo ya makazi yanayozunguka eneo hilo la dampo Buhongwa. “Uthamini uliofanyika katika maeneo hayo ulizingatia taratibu, kanuni na sheria ya Mipango miji na ukadiriaji thamani chini ya kifungu Na 179 cha sheria ya Ardhi Na 4 ya mwaka 1999 sura ya 133, pia kuzingatia bei ya soko ambapo kila Hekri 1 ikilipwa kiasi cha Sh. Milioni 3 katika maeneo ambayo siyo ya makazi ikiwa ni mashamba,”alisema.

Kufatia majibu hayo ya kitaalamu zaidi, RC Mulongo aliagiza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kuacha kulipa fidia ndogo na kuutaka kulipa fidia ya kiwango cha Sh milioni 12 kwa Hekri 1 kwa wananchi wato ambao maeneo yao yataguswa na kupitiwa na mradi huo wa TSCP.

 Hatua ambayo Jiji limedai kuwa halitaweza kutekeleza mradi huo wa TSCP kutokana na kiwango hicho kuwa kikubwa na kutofuata taratibu, kanuni na sheria ya Mipango miji iliyopo ikiwa ni pamoja na bei ya soko ukizingatia pia kuwa eneo hilo siyo la makazi bali la dampo la kuhifadhi taka kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji na Manspaa ya Ilemela.

“Tusipotekeleza mradi huu kutokana na mkanganyiko huu Halmashauri ya Jiji itakosa fedha iliyokuwa ipate zaidi ya Sh. 3,711,165,142.67/= bilioni, pia mtambo wa kuchakata taka zote zinapelekwa dampo hilo, magari ya kuzolea taka, vifaa vya kuhifadhia taka kabla ya kuchukuliwa kupelekwa dampo na vifaa vya kufanyia usafi maeneo yote ya Jiji hili,”alisema Afisa Afya wa Jiji Danifrod Kamenya.

Naye Mkurugenzi wa Jiji, Halifa Hida, alisema kuwa watamwelewesha zaidi RC Mulongo kutokana na agizo lake hilo kuwa pengine amechanganya bei ya viwanja vya makazi na maeneo yanayochukuliwa kwa ajili ya shughuli za taasisi za Afya, Elimu na Uwekezaji ili kunusuru hali iliyopo sasa kwa wananchi wa maeneo hayo ili kuwezesha utekelezaji wa mradi huo mkubwa.

UTIWAJI SAINI MKATABA WA KUJENGA TENA UMOJA NA KUKIUNGANISHA UPYA CHAMA TWALA CHA SUDAN KUSINI CHA SUDA


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akikaribisha viongozi na wajumbe katika mkutano huo
 Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo akisoma muhtasari wa mazungumzo hayo


 Sehemu ya ukumbi wa mkutano huo

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza utiaji wa saini wa  Mhe. Salva Kiir Mayardit  Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD). 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.

 Rais Yoweri Museveni wa Uganda akiongea
 Dkt. Riek Machar akiongea 
 Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiongea
 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kulia) na Bw. Bw. Deng Alor Kuol  wakifurahia wakati  Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (wa pili kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
 Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini
 Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Kikwete na Bw. Dkt Kuol wakipiga makofi wakati  Rais Salva Kiir Mayardit  wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny wakipeana mikono kwa furaha baada ya kutia saini mkatana wa  makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusin

 Naibu Rais wa Afrika ya Kusini Mhe Cyril Ramaphosa akiongea na kupongeza hatua iliyofikiwa
 Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
 Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
 Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
 Wajumbe wa kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO)


 Sehemu ya wajumbe wa kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO)
 Kila mtu alisimama kumshangilia Rais Kikwete
 Wajumbe wa  kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD)
 Furaha kwa kila mtu
 Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mwezeshaji wa mazungumzo akisoma dondoo za makubaliano
 Meza kuu katika picha ya pamoja na kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG)
Picha ya pamoja na kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO)
 Picha na Sekretareti ya mazungumzo hayo
 Rais Kikwete na Mzee Malecela wakipongezana baada ya kufanikisha mazungumzo na hatimaye makubaliano ya viongozi wa SPLM
 Rais Kikwete akishukuru vikundi vya ngoma za utamaduni vilivyokuwapo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kumsindikiza  baada ya mkutano wa mafanikio

MKATABA wa kujenga tena umoja na kukiunganisha upya Chama Tawala cha Sudan Kusini cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM) ulitiwa saini usiku wa jana, Jumatano, Januari 21, 2015, katika sherehe ya kufana iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Ngurdoto, Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha.
Mkataba huo unaojulikana kama Agreement on the Re-unification of Sudan People’s Liberation Movement umepongezwa kuwa ni hatua muhimu katika kulitoa taifa changa la Sudan Kusini katika hali ya machafuko, vita vya wenyewe kwa wenyewe, kutoelewana na kutoaminiana, mambo ambayo yameligubika taifa hilo tokea mwishoni mwa 2013 wakati kutokuelewana kulipozuka ndani ya SPLM na hatimaye katika Serikali ya nchi hiyo.
Viongozi waliotia saini ni Mheshimiwa Salva Kiir Mayardit, Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD).
Sherehe hiyo ilishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho kimesimamia mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo. Rais Kikwete pia ndiye mdhamini mkuu wa Mkataba huo.
Wengine walioshuhudia tukio hilo muhimu ni Rais wa Uganda, Mheshimiwa Jenerali Yoweri Kaguta Museveni; Rais Uhuru Muigai Kenyatta wa Kenya; Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo na Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mwezeshaji wa mazungumzo.
Mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo yalianza mwishoni mwa mwaka jana baada ya Rais Kikwete na Chama cha CCM kuombwa na Rais Kiir Mayardit kukubali chama hicho tawala cha Tanzania kutumia uzoefu na ujuzi wake wa miaka mingi wa uongozi na siasa kujaribu kuleta suluhu ndani ya SPLM.
Mazungumzo hayo ya kutafuta suluhu ambayo yamefanyika kwa awamu mbili, ya kwanza yakiwa yamefanyika Oktoba mwaka jana na pili yakiwa yameanza mwanzoni mwa mwezi huu, Januari 2015,  yameongeza thamani kwenye mazungumzo mengine yanayofanyika Addis Ababa, Ethiopia chini ya usimamizi wa taasisi ya IGAD na yanayojadili jinsi ya kurejesha amani nchini humo.
Viongozi wa SPLM wanaamini kuwa kwa sababu mgogoro wa kisiasa nchini mwao ulianzia ndani ya chama hicho na kwa sababu SPLM ndicho chombo pekee ambacho kinawaunganisha wananchi wote wa Sudan Kusini, basi busara inaelekeza kuwa suluhu ianze kutafutwa ndani ya chama hicho.
Mkataba wa jana, kimsingi, unalenga kuweka mazingira ya kujenga utulivu, maelewano, amani na umoja wa kudumu ndani ya chama hicho na nchini humo kwa kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mambo ya msingi yaliyokubaliwa kuhusu shughuli za siasa, uongozi na oganisheni ya chama hicho yanafanyika bila kukawia.
Mkataba huo pia unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinabuni na kutekeleza sera za kuondokana na ukabila, makundi yenye mitazamo finyu na mwenendo wa kijeshi katika siasa za Sudan Kusini.
Aidha, Mkataba huo unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinafanya mageuzi ya kuanza kujenga utamaduni wa kuvumiliana na ujenzi wa misingi ya demokrasia.
Mkataba huo pia unataka watu wote ambao walishiriki katika mauaji na umwagaji damu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wasiruhusiwe kugombea wala kushika nafasi ya uongozi wa umma ndani ya chama hicho.
Pia viongozi wote wa Sudan Kusini wanatakiwa, chini ya Mkataba huo, kuwaomba radhi wananchi wa nchi hiyo ya Sudan Kusini kwa kuruhusu nchi hiyo kuingia katika machafuko ya umwagaji damu mkubwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
22 Januari,2015