ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 1, 2012

PARTY LA DJ FETTY LILIVYOKUWA MWANZA


Dj Fetty wa XXL na Clouds Fm usiku wa kuamkia leo kakutana na part la bazdei yake akiwa Sukuma Land (Mwanza) hapa akikata keki ndani ya hoteli Mornach Hotel and Pavilion.

Friends wakishow love na m-bazdeiwa.

Mbwiga akiserebuka na Fetty....

Special time ni Mbwiga, Imma na Mebb.

Papaa Hando mzee wa shika hapa acha hapa (kushoto) alikwea pipa hadi Rock City kwaajili ya SaPraIzi''' akiwa na sie.

Hapa - Babra Hassan, hapa Platnum, pale C Pwaa pale G. Sengo

Ze card.....

Fishi finga 

Kitu cha kijani.
Upooo...

Furahia utamu wake..


Aaaam....

Shika hapa acha hapa.....

Furahia utamu wake

aaaaaM

Kakaaaaaa...

to Mr Mebb..

To my brother 

SERENGETI FIESTA MUSOMA 2012 HII HAPA.....!!!

Bofya hiyo video uone jinsi palivyokuwa hapatoshi ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lilipokuwa linaunguruma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoriki, akiwajibika mbele ya mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Ngosha the Swagadon, akiwaimbisha mashabiki (hawapo pichani) wake waliokuwa wamefurika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
 Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
 Wasanii wa Filamu Steve Nyerere (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana kuonesha uwezo wa kuzungusha mauno yao katika tamasha la Sererengeti Fiesta 2012, lililofanyika kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma. 
 Sehemu ya umati uliyofurika viwanjani hapo ukifuatilia kwa makini makamuzi ya wasanii hao wa Filamu, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
 Msanii mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma. 
 Kati ya mashabiki waliyoshindwa kujizuia katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012, wakizungusha nyonga zao kama inavyoonekana kwenye viwanja vya Karume mjini Musoma. 
 Ray na Steve Nyerere (wa kwanza kutoka kushoto), wakishindana kusakata sebene kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Ray akipagawa na jukwaa huku makelele yakiwa yametawala kila kona uwanjani hapo.
Rais wa masharobaro Bongo, Bob Junior (katikati), akisongesha burudani za Serengeti Fiesta 2012, na Wanenguaji wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Profesa Jay akionesha uwezo wake wa kukamua jukwaani kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Ommy Dimpoz akipagawisha mashabiki wake ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma, katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Mwasiti akiwa amepakatwa na mmoja wa mashabiki zake kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma huku akiyamwaga mauno ya kiuchokozi chokozi.
Mmoja wa wasanii waliyoibuka kidedea katika mchakato wa Serengeti Super Nyota 2012, akidhihirisha uwezo wake wa kuimba ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Dimpoz na wanenguaji wake, wakiwajibika kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya viwanja vya Karume mjini Musoma.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Rachel (kushoto), akionyesha uwezo wake katika uwanja wa Karume mjini Musoma, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 na wanenguaji wake.
Rachel akikamua kwenye uwanja vya Karume mjini Musoma ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Chege,Temba na Bi Cheka wakiwajibika jukwaani kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma.
Mashabiki wa kizungu wakipagawa na burudani ya Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini msoma.
Baadhi ya sehemu ya umati wa mashabiki waliozama ndani ya viwanja hivyo wakishuhudia burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Msanii wa michano ya Bongo Fleva, Nay wa Mitego akipagawisha jukwaani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Mmoja wa Ma'DJ wa Clouds TV, PQ akisababisha burudani ya Serengeti Fiesta 2012 mjini Musoma.
Mashabiki wa burudani za Serengeti Fiesta 2012, wakiwa wamefurika uwanjani hapo tayari kwa kushuhudia burudani mbalimbali.

MZEE YUSSUF AFUNGUA KAMPUNI YA USAMBAZAJI WA KAZI ZAKE



Meneja Mauzo wa Kampuni ya  Usambazaji ya MY CollectionMUSSA MSUBA akiwa katika duka la mauzo ya kazi za Jahazi
MSANII WA MZIKI WA TAARABU,MZEE YUSUFU KUSHOTO AKIANGALIA MOJA YA KAZI YAKE ILIYOKUWA FEKI ZILIZOKAMATWA NA WASANII WENYEWE KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTANTAINMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM
DVD ZA JAHAZI
MUSSA MSUBA

Na Mwandishi Wetu

MSANII wa mziki wa Taarabu nchini Mzee Yussuf ameamua kufungua kampuni yake ya usambazaji ijulikanayo kama MY Collection kwa ajili ya kusambaza kazi zake

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Mussa Msuba amesema wameamua kufungua duka kwa ajili ya kuuza CD NA DVD za bendi ya Jahazi inayongozwa na Mzee Yussuf duka hilo lililopo makutano ya barabara ya likoma na Muhonda

linalojihusisha na huzwaji wa DVD za taarabu kwa jumla na rejareja kwa ajili ya kuwaweka karibu wapenzi wake ili waweze kupata burudani kupitia nyimbo zao kwa kuwaburudisha wakiwa majumbani

Msuba amesema kuwa Mzee yusufu yupo mbioni kutoa albamu yake ya mduara itakayokuwa hivi karibuni ambayo ni yake binafsi mbali na hilo bendi hiyo itatoa video yake ya Live za albamu zake zote za Two in One,Kazi ya Mungu, Nakula ka Naksh Naksh,tupendane,Daktari wa Mapenzi

Ambazo zitakuwa madukani kwa ajili ya kuwapa wapenzi wao burudani wakiwa majumbani mwao

Nae Mzee Yussuf aliongeza kwa kusema ameanzisha Kampuni yake binafsi baada ya kuona kwamba kazi zake nyingi zimekuwa zikichakachuliwa kutokana na kuwepo kwa wizi wa kazi za Sanaa

Kampuni yake imekuwa ikisambaza kazi zake kwa ajili ya kuogopa kuibiwa kutokana na wimbi wa kazi za wasanii nchini

Duka lililopo mtaa wa Muhonda na Likoma kwa ajili ya CD za Jahazi pekee  mbali na duka hilo mzee Yusufu anamiliki Duka lingine la Nguo lililopo Magomeni Mapipa kwa ajili ya kujiongezea kipato chake mbali na bendi yake

Bendi ya Jahazi mpaka sasa imekwisha toa albam nane ambazo zipo madukani zinauzwa kwa ajili ya watu wotekupata burudani wakiwa majumbani mwao

Kwa sasa bendi hiyo ipo mbioni kuachia albamu yake ya tisa ambayo aijapewa jina inatarajiwa kuzinduliwa mwezo October kwa ajili ya kutoa burudani kwa wapenzi wao na kuwataka mashabiki wao kuja kuangalia na kusikiliza nyimbo mpya popote pale wanapotoa burudani zao katika kumbi mbalimbali za jijini Dar es salaam


DUKA LA MZEE YUSSUF LILILOPO KATIKA MAKUTANO YA MTAA YA LIKOMA NA MUHONDA LINALOSAMBAZA KAZI ZA BENDI YA JAHAZI


-- 

Friday, August 31, 2012

SERENGETI FIESTA MWANZA ZIMEBEKI SIKU MBILI TU!!

Serengeti Fiesta 2012 imefika hadi kwa akina mama hawa wanaoziboresha barabara zetu jijini Mwanza kwa Usafi hapa ilibidi wachukuwe flash na mchuma wetu.

Mbwiga akitiririka na wana hapa ni pande za Tanganyika bus stand.

Dj fetty na wadau Tanganyika bus stand.

Mafundi wa Clouds fm na Tv Meboo na Daudi kazini.

Tanganyika bus stand.

Umia ujae....

Mchuma sehemu ya parking na Mornach Hotel ambao ni moja kati ya wadhamini wetu.