ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 30, 2022

SERIKALI YATOA MWONGOZO KWA WANAFUNZI WANAOJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023...HAKUNA UHAMISHO WA KUTWA KWENDA BWENI, PIA HAKUNA CHAGUO LA PILI

 


DODOMA. Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Riziki Shemdoe amesema hakutakua na uhamisho wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule za kutwa kuhamia bweni.

Shemdoe ametoa agizo hilo Desemba 29, 2022 Dodoma katika kikao kazi cha kufanya tathmini ya usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini kwa mwaka 2022 kwa Maafisa Elimu wa Mikoa.


Amesema, tangu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe.Angellah Kairuki atoe taarifa ya kuwapangia shule wanafunzi wa kidato Cha kwanza mwaka 2023, Desemba 14, 2022 Ofisi ya Rais-TAMISEMI imekuwa ikipokea maombi kutoka kwa wazazi ama walezi ya kuomba watoto wao kuhamia kwenye shule za bweni kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ugonjwa au matamanio ya wazazi au watoto.

Kutokana na hali hiyo, Profesa Shemdoe amesema hakutakuwa na uhamisho wa wanafunzi waliochaguliwa shule za kutwa kwenda kwenye shule za bweni kwani upangaji wa wanafunzi umefuata vigezo na taratibu zilizowekwa.

"OR-TAMISEMI inasisitiza kuwa hakuna uhamisho kutoka shule ya kutwa kwenda bweni kwasababu wale waliopangiwa bweni wamekidhi vigezo vya kuchaguliwa katika shule hizo."

" Na kwa wanafunzi wenye changamoto za kimazingira, mfano amehama makazi ya awali wawasilishe changamoto hizo kwa Makatibu Tawala wa Mkoa ili zitatuliwe, maana upangaji wa wanafunzi kwenye shule umezingatia ukaribu wa shule na makazi ya wanafunzi hivyo endapo wamehama awali kunaweza kutokea changamoto ya umbali.

Profesa Shemdoe amesema kupangiwa shule kwa wanafunzi kumezingatia viwango vya ufaulu, ushindani pamoja ukaribu wa shule na makazi.

Aidha, idadi ya wanafunzi waliopangiwa kwenye shule za bweni imezingatia viwango vya juu vya ufaulu na nafasi zilizokuwepo katika shule hizo ili kuepusha msongamano kwa wanafunzi darasani na mahali pakulala.

Endapo zitatokea nafasi za bweni zitakazohitajika kujazwa hapo baadae, maombi yatakayokuwa yamefikishwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI makao makuu yatachambuliwa na kamati maalum ambayo itaangalia sifa za walioomba kuhamishiwa huko.

Aidha, Prof. Shemdoe ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanaripoti shuleni kwa wakati na kwamba hakutakua na chaguo la pili la mwanafunzi.

" Kwa mwaka huu hakutakuwa na chaguo la pili la wanafunzi kwasababu fedha zilizotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu zimetosha kuboresha miundombinu ya kuwachukua watoto wetu wote kwa intake(mkupuo) mmoja ."

" Tangu Rais aingie madarakani ameshatoa fedha zilizowezesha kujenga zaidi ya vyumba vya madarasa 20,000 ndani ya miaka miwili hatua ambayo imewaondolea adha watoto kwa kuanza masono kwa pamoja huku wazazi wakiwa hawajachangishwa kitu."

TAKWIMU ZA MCHEZAJI ALIYENASWA NA LIVERPOOL.

 

CODY GAKPO 

✍️Cody Gakpo amefunga mabao 21 na kutoa pasi za mabao 25 katika michezo 41 ya Eredivisie tangu ulipoanza msimu uliopita, ndiye mchezaji pekee katika zile ligi 10 bora barani ulaya, aliyefunga mabao 20+ na pasi za mabao 20+ tangu ulipoanza msimu wa 2021-22 hadi sasa.

✍️Cody Gakpo ndiye mchezaji pekee msimu huu aliyehusika katika mabao 30 ya mashindano yote katika zile ligi 10 bora barani ulaya.

Takwimu zake katika mashindano yote msimu huu.

Michezo 24

Mabao 13

Pasi za mabao 17


✋Moto utawaka katika ep

WANAHABARI MWANZA WATWAA TUZO.

 


TAASISI ya ADLG imetoa tuzo mbili kwa waandishi wa habari George Binagi @gbpazo kutoka BMG Online @bmghabari pamoja na Nashon Kennedy kutoka Daily News ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika uandishi wa habari za Utawala Bora.


Tuzo hizo zimekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya Magu, Salum Kalli kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Adam Malima kwenye halfa ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza iliyofanyika Usiku wa Disemba 29, 2022.

BRAZIL YAANZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO, PELE KUZIKWA SANTOS.


Uwanja ambao nguli wa soka wa Brazil Pelé alicheza baadhi ya mechi bora zaidi za maisha yake pia utaruhusu watu kutoa salamu zao za mwisho siku ya Jumatatu na Jumanne.


Santos, klabu ambayo Pelé alicheza huko Brazil, ilisema katika taarifa kwamba umma utaweza kutoa heshima zao za mwisho kwenye Uwanja wa Vila Belmiro, nje ya Sao Paulo. Pelé, ambaye jina lake kamili lilikuwa Edson Arantes do Nascimento, alifariki Alhamisi baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu. Alikuwa na miaka 82.


Santos ilisema jeneza lililombeba bingwa huyo mara tatu wa Kombe la Dunia litaondoka katika hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo mapema Jumatatu asubuhi na litawekwa katikati ya uwanja.


Mazishi yatafanyika kwenye Ukumbusho wa Necrópole Ecumênica, kaburi la wima huko Santos. Familia pekee ndiyo itahudhuria. Pelé ana nyumba huko Santos, ambako aliishi zaidi wakati wa uhai wake.

Serikali ya Brazil ilitangaza siku tatu za maombolezo.

Anasifiwa kwa kufunga mabao 1,281 katika rekodi ya dunia katika mechi 1,363 katika kipindi cha miaka 21 ya maisha yake, yakiwemo mabao 77 katika mechi 92 za nchi yake.


Mchezaji pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, akinyakua taji hilo mnamo 1958, 1962 na 1970, Pele alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Karne wa Fifa mnamo  2000.


Alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo na kibofu katika miaka ya hivi karibuni.


Pele alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye utumbo wake mnamo Septemba 2021 katika Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo, baada ya uvimbe huo kugunduliwa katika vipimo vya kawaida.


Alirejeshwa hospitalini mwishoni mwa Novemba 2022.

MTANGAZAJI MAHIRI WA TELEVISHENI CATHERINE KASAVULI AMEFARIKI.

 

 

MTANGAZAJI mashuhuri Catherine Kasavuli ameaga dunia. Kasavuli amefariki akiwa na umri wa miaka 60 katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta. Kasavuli alikuwa akiuguzwa ugonjwa saratani tangu Oktoba 26 mwaka huu. Kifo chake kilithibitishwa na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha KBC Samuel Maina

ALAT MWANZA KUCHUKUWA HATUA KWA WATUMISHI WANAOHUSIKA NA VITENDO VYA UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA.

 NA ALBERT G.SENGO/SENGEREMA MWANZA

Katibu tawala wa mkoa wa mwanza ELIKANA BALANDYA amezitaka halmashauri za wilaya, manispaa na Jiji Mkoani Mwanza kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha za maendeleo ili kuwezesha miradi inayotekelezwa kuwa na tija kwa wananchi. Akizungumza katika mkutano wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini (ALAT) Mkoa wa Mwanza BALANDYA pia amewaasa viongozi na watendaji wa halmashauri kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaohusika na vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma.

Tuesday, December 27, 2022

TAZAMA WANAODAIWA KUMZIKA MTOTO AKIWA HAI WALIVYOPANDISHWA KIZIMBANI.

 MWANZA. Watu watatu akiwemo Mkazi wa kijiji cha Mahaha wilayani Magu mkoani Mwanza, Zawadi Msagaja (20) wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kike mwenye umri wa miezi sita kwa kumzika shambani akiwa hai ili wapate mali.

Wengine katika kesi hiyo ya mauaji namba 7/2022 ambao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza na kusomewa shtaka la mauaji ya mtoto huyo ni dada yake Zawadi, Elizabeth Kaswa na mmewe, Mussa Mazuri ambaye ni mganga wa kienyeji.