ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 2, 2016

MWANAMUZIKI NATALIE COLE AFARIKI DUNIA

 Albamu yake ya Unforgettable ilishinda tuzo sita za Grammy Natalie Cole, mwanamuziki nyota kutoka Marekani aliyeimba nyimbo maarufu kama vile Unforgettable , amefariki akiwa na umri wa miaka 65. 

Aiimba wimbo huo akishirikiana na babake Nat "King" Cole. 

Mwanamuziki huyo aliyeshinda tuzo za Grammy alifariki akitibiwa katika hospitali moja mjini Los Angeles, Alhamisi usiku. Alikuwa amefutilia mbali tamasha kadha, ikiwemo ya mkesha wa Mwaka Mpya. 

Cole alipata umaarufu kama mwimbaji wa R&B kwa nyimbo kama vile This Will Be na Inseparable. Mtetezi wa haki za kiraia wa Marekani Kasisi Jesse Jackson alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutuma salamu za rambirambi. 

Mwanamuziki huyo aliwahi kutatizwa na matumizi ya dawa za kulevya na ugonjwa wa hepatitis awali, na alibadilishwa figo mwaka 2009. 

Cole aliwahi kutatizwa na uraibu wa dawa za kulevya

Ufanisi wake kimuziki ulitokana na albamu ya Unforgettable... With Love aliyoichomoa 1991 ambayo aliitumia kutoa heshima kwa babae marehemu, akifanya upya nyimbo maarufu za babake kama vile That Sunday That Summer, Too Young na Mona Lisa. Albamu hiyo ilishinda tuzo sita za Grammy, zikiwemo tuzo za albamu bora ya mwaka, na wimbo bora wa mwaka. CHANZO BBC SWAHILI.

MAZOEZI YA KITAIFA YA BONANZA LA MATEMBEZI YA WANAMICHEZO WA ZANZIBARUWANJA WA AMANI ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki katika Matembezi ya Bonaza la Wanamichezo wa Zanzibar akiongoza matembezi hayo yalioazia katika viwanja vya Matumbnaku Miembeni na kumalizia katika viwanja vya Amaan Zanzibar kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi Shariff Khamis Raiswa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Mwenyekiti wa Umoja Mazoezi Zidi , Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Bihindi Hamad, Waziri wa Kilimo na Mali Asili Mhe Sira Ubwa Mwaboya na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Ayoub Mohammed Mahmoud.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipokea matembezi ya Wanamichezo mbalimbali walioshiriki matembezi hayo ya Kitaifa ya Bonaza la Michezo Zanzibar yaliowashirikisha Wanamichezo kutoka Ungua Pemba na Dar es Salaam wakiingia katika viwanja vya Amaan kumalizia matembezi hayo na kumalizia katika viwanja vya Amaan Zanzibar kwa ajili ya mazoezi ya viungo.





























UTENDAJI WA WAANDISHI WA HABARI MWAKA 2015

Kutana na mwenyekiti wa waandishi wa habari wanaoandika habari za masuala ya madawa ya kulevya mkoani Mwanza Edwin Soko, pamoja na mwandishi wa kituo cha redio ya Chuo cha SAUT Martin Mnyoni wakikuhabarisha kuhusu utendaji wa waandishi wa habari mwaka 2015.

Vipi utendaji wa vyombo vya habari.

Ufanisi wa mitandao ya kijamii unatathimini gani kwa mwaka 2015 - 2016?

IRENTE VIEW POINT LUSHOTO TANGA, MOJA YA KIVUTIO AMBACHO WATU WENGI HAWAJAKITAMBUA.

Hapa ndipo kileleni na Mwonekano wa Irente 
 Hii ni Miamba mikubwa iliyopo Irente na moja ya kivutio kikubwa katika eneo hili kwa upande kwa Kushoto.
Eneo hili wakazi wa Irente wanaliita Pango ambapo watu wengi wanapenda kupigia picha
Hii ni njia ya kuelekea Pangoni 
Ukiwa Juu ndani ya Pango utaona hivi 
Mmoja wa walinzi akiandika akiwakatia risiti wageni mbalimbali waliotembelea eneo hilo.
 Mmoja wa wandishi wa Blogs za Mikoa Fredy Tony akiwa amefika kujionea eneo hilo.

Watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kukalili kuwa wanapoambiwa kwenda kufanya utalii basi mawazo yanahamia katika hifadhi za taifa au Fukwe za Bahari, wakati kuna utalii wa kupanda milima,utalii wa uwindaji utalii wa picha, utalii wa kiutamaduni,Utalii wa Ikolojia,utalii wa fukwe,Michezo ya kwenye maji, utalii wa mali kale,utalii wa mikutano,utalii wa matibabu,utalii wa mashambani na utalii wa jiji.

Irente View Point inapatikana katika kijiji cha Irente kilichopo wilayani lushoto mkoani Tanga, eneo hili liligunduliwa na wazee wa kale ambao walikuwa wakifika hapo kwa ajili ya kuomba na kufanya matambiko na wengine walikuwa wakifika katika eneo hilo kwaajili ya kufanya ibada hasa wakati wa sikukuu za Christmas

Eneo hili lina urefu wa Mita 1500 kutoka usawa wa Bahari , ukiwa juu unaweza kuona maeneo mbalimbali vizuri bila usumbufu wowote, pia watalii wengi wamekuwa wakifika eneo hilo kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri, kuona Mandhari nzuri hasa wakati wa asubuhi na jioni.

Jinsi ya kufikia ikiwa unatokea upande wowote, fika hadi Mombo, panda daladala Tsh 3,000 mpaka Lushoto mjini baada ya hapo unaweza panda Boda boda Tsh 3,000 au ukachukua Tax Tsh 10,000 , kiingilio ni Tsh 2,000. 

(Imeandaliwa na Fredy A. Njeje 0765056399)


LEO NI BIRTHDAY YA DR. JEMBE

4 sure you have been inspirational to all of us.. Si juhudi zako pekee, moyo wa upambanaji, usikivu pamoja na utii bali pia msimamo wa ujasiri ulionao katika kuhakikisha safari ya vijana wenzako katika kusaka mafanikio inasonga... Hakika Kamanda WEWE NI JEMBE✔Happy birthday Big Boss @jembenijembe @jembenijembe @jembenijembe @jembenijembe ikiwa leo ni 2/January 2⃣0⃣1⃣6⃣