ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 12, 2011

AMANI NA UTULIVU WAREJEA GHAFLA MKOANI MBEYA NA SHUGHULI KUENDELEA KAMA KAWAIDA KUANZIA LEO, MMTU MMOJA AFARIKI KATIKA VURUGU ZA SIKU 2.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama katika jengo la kitega uchumi la OTTU lililopo stendi ya magari madogo ya abiria(daladala), mara baada ya Mbunge Mbilinyi kuhutubia wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama mwenye shati la miraba ya samawati(Katikati) katika picha ya pamoja kabla ya Mheshimiwa Mbunge Joseph Mbilinyi Kuhutubia.

Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha na utatuliwe kisayansi badala ya kisiasa na pia amewapongeza machinga kwa utulivu waliouonesha bila kupora bidhaa madukani.

Halaiki ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu wa maeneo ya kufanyia biashara ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.

Wananchi wakirudi makwao kwa furaha baada ya mgogoro uliodumu kwa siku mbili kumalizika, baada ya hotuba ya Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi.

Picha zote na:
http://www.mbeyayetublog.blogspot.com/

TABORA YAKUMBWA NA UHABA WA MAFUTA IKIWA LEO NI SIKU YA NNE TATIZO LAWA KUBWA

Uhaba wa mafuta katika mkoa wa Tabora na Hivi ndivyo hali ilivyo katika pita pita za Latest news Tz na kujionea mstari mrefu watu wakisubiri kupata huduma ya mafuta. Hali hii ilianza kama siku nne zilizopita na kila siku kituo kimoja kinatoa huduma hiyo.

Picha na :
www.latestnewstz.blogspot.com

Friday, November 11, 2011

VURUGU ZA LEO WAMACHINGA SOKO LA MWANJELWA

Watu Mbali Mbali wakiwa wanakimbia ili kujiokoa na Hatari katika eneo hilo.

Wamachinga wakiwa Tayali kwa ajili ya Kupambana na FFU wakati wa tukio hilo

Baadhi ya wananchi wakiwa wameokoka katika eneo hilo


Wamachinga Mbali mbali wakikimbia katika eneo la tukio wakati wa machafuko hayo yamepamba moto

Polisi wakijalibu Kuzuia Ghasia katika eneo hilo na kufukuza Wamachinga.
Picha zote na:
http://www.latestnewstz.blogspot.com/

KOZI YA WALIMU WA NGUMI YASOGEZWA MBELE.

BOXING FEDERATION OF TANZANIA (BFT)
SLP 15558
DAR ES SALAAM
6/11/2011.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI;
YAH; KUSOGEZWA MBELE KWA TAREHE YA KUFANYIKA KWA KOZI YA WALIMU WA MCHEZO WA NGUMI ZA RIDHAA SASA YATAFANYIKA TAREHE 17/11/2011 KIBAHA PWANI.

Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) kwa kushirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) wamelazimika kusogeza tarehe ya kufanyika kozi ya kimataifa ya walimu 30 wa kufundisha mchezo wa ngumi.Sasa itafanyika kuanzia tarehe
17-25/11/2011 Kibaha Pwani.

Awali kozi hiyo ilikuwa ifanyike kuanzia kuanzia tarehe 12-18/11/2011 Kibaha Pwani.
Sababu ya kusogezwa kwa kozi hiyo,imetokana na mkufunzi mkuu wa kozi hiyo,ambaye ameteuliwa na Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) Ndg Azzedin Aggoune kutoka Algeria,kuomba kozi hiyo isogezwe mbele kutokana na yeye kupata dharula nchini kwao na kushindwa kufika hapa nchini kama ilivyokuwa imepangwa.

Awali mkufunzi huyo ilikuwa awasili hapa nchini tarehe 11/11/2011,kutokana na dharula iliyompata sasa atawasili hapa nchini tarehe 16/11/2011.

Aidha kwa sasa makocha hao watalazimika kuhudhuria mashindano ya Kova Cup yatakayoanza kufanyika tarehe 14/11/2011 PR Stadium Hotel.zamani Imasco Centre.

Makore Mashaga
KATIBU MKUU BFT.
Mob; 0713588818.
Email;mashagam@yahoo.com

JUMUIYA YA AFRIKA YANG'ARA KATIKA WORLD TRADE MARKET UINGEREZA

Ilikuwa ni siku ya jumuiya ya Afrika mashariki ambayo hufanyika kila mwaka katika maonyesha ya WTM nchini Uingereza. Kwa kawaida sherehe hizi hufanyika katika banda la nchi ambayo ni Mwenyekiti wa Afrika Mashariki, kwa hiyo mwaka huu tafrija hii ilifanywa kwenye banda la ndugu zetu wa Kiburundi. Waziri wa Utalii na Mali asili Mh Ezakiel Mahige na Naibu Balozi Chabaka wakipokea zawadi ya mpira.

Mchezaji maarufu wa kimataifa kutoka nchini Ghana Asamoah Gyan alipotembelea Banda la Tanzania.

Waheshimiwa Ephraim Kamuntu, Najib Balala na Victorie Ndikumana.

Bw Meena. Bw Issa. Mh A. Jihad Naibu Balozi Chabaka, Jonathan.

Frank, Bw Issa na Bi Jestina.

Mwenyekiti wa bodi ya utalii ya Uganda akiwa na Bw William Byeruhanga.

Asamoah na wapenzi wake kutoka Tanzania.

Mh Jihad akiwa na wafanyakazi wa Bodi ya utalii ya Zanzibar

Thursday, November 10, 2011

Wednesday, November 9, 2011

KAMPENI YA CHANJO KITAIFA 12-15 NOV 2011

SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara yake ya Afya na Ustawi wa Jamii inao mkakati kabambe wa kutokomeza ugonjwa wa SURUA na POLIO kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5.

Wizara itaendesha kampeni ya kuwapatia chanjo watoto wote wenye umri kuanzia miezi 0-59 nchi nzima. Pia katika zoezi hili itatolewa Matone ya VITAMINI A na DAWA ZA MINYOO

Rais Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuzindua kampeni hiyo ya kitaifa ambayo uzinduzi wake utafanyika mkoani Arusha Novemba 12, mwaka huu na JK ambaye ni balozi wa chanjo kimataifa, atashiriki kutoa chanjo.


<-Ngozi ya mtoto anayeelekea kupona surua.

Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Tito Jeremiah Mahinya, ametoa rai kwa vyombo mbalimbali vya habari nchini kusaidia kufikisha ujumbe kwa jamii kwa kutoa matangazo, kuendesha vipindi vyenye kuelimisha na kuhamasisha jamii ili walengwa ambao ni ni watoto wadogo wapate haki yao ya msingi katika kulinda afya zao.

Zoezi hilo litakuwa kwa watoto wenye miezi 0 hadi miaka 4 na miezi 11, litafanyika katika vituo 124 katika kata zote za halmashauri ya jiji la Mwanza, kuanzia tarehe 12-15 November, 2011, Wazazi wawapeleke watoto wao kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja kamili jioni kwenye vituo vya chanjo.

CHANJO NI HAKI YA MSINGI YA MTOTO.

PSPF YAPEWA TUZO KWA KUTOA MIKOPO YA NYUMBA KWA WASTAAFU

Waziri wa Kazi na Ajira Bi. Gaudensia Kabaka akimkabidhi kaimu Mkurugenzi wa PSPF .Bw.Adam Mayingu tuzo ya kutambua juhudi za PSPF katika kutoa mkopo wa nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafu wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana.

Mkurugenzi wa PSPF. Bw.Adam Mayingu akitoa maelezo kwa waziri wa kazi na Ajira Bi. Gaudensia Kabaka juu ya miradi inayofanywa na mfuko huo.

Wafanyakazi wa PSPF wakifurahia tuzo waliyoivuna wakati wa ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya hifadhi ya jamii iliyoanza katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam jana tuzo hiyo ni kwa kutambua juhudi za mfuko huo katika kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake wanaokaribia kustaafu.

Waziri wa Kazi na Ajira Bi.. Gaudensia Kabaka akijaza fomu ya uhakiki wa wastaafu wakati alipotembelea banda la PSPF katika maonesho ya Wiki ya hifadhi ya Jamii Mnazi Mmoja Dar es salaam jana Kabaka ni mmoja wapo wa wastaafu wa PSPF na kushoto ni Ofisa wa Fedha Mwandamizi Bw. Victor Luvena.

'Jamani eeh! tulizo vuna ndiyo hizi...!!' (picha na Mpigapicha wetu)

RUNCH YA REO INAKAMATIKA HIVI NA KITU BALIMI

Wajameni kAlAnChI kArEwO kAtAmU!!!!!

MIAKA 50 YA UHURU SHULE YA MSINGI NYAMAGANA YAZIDI KUSHUKA CHINI KIMAENDELEO

Ni moja kati ya shule kongwe jijini Mwanza iliyokuwa ikisifika kuwa na mazingira mazuri, vyumba vya madarasa, madawati, ufundishaji mzuri na vitabu vya kufundishia, wafanyabiashara watz wenye asili ya kiasia na wazawa wenye uwezo walikuwa wakileta watoto wao kusoma hapa....lakini leo ukiitembelea mmmmmmh...

Kwa uchunguzi wa haraka nilioufanya, baadhi ya madarasa shuleni hapa, hii leo hayana hata sakafu, hali ambayo inawalazimu wanafunzi kukaa kwenye vumbi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa walimu katika ufundishaji wao.


Pamoja na kwamba ni shule ambayo iko katikati ya jiji la Mwanza baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wanakalia mawe na matofali, hali ambayo imekuwa ikichangia kuporomoka kwa kiwango cha elimu.

Vyoo ndiyo kabisaaaa 'chokesti' Pamoja na kwamba matatizo haya ni la muda mrefu, lakini viongozi hasa wanasiasa wanatoa ahadi tu wasizozitekelezeka, ni mfanyabiashara mmoja tu aitwaye Aritaf Mansoor aka Dogo kwa pesa zake ndiye aliye ameamua kujenga madarasa mengine shuleni hapo.

Mlio soma hapa enzi za Mwalimu mupooo? Jeh! mwayaona haya?

Tuesday, November 8, 2011

ZA MWIZI 39 ANASWA NA UMEME AKIIBA MAFUTA YA TRANSFOMA

Mtu mmoja ambaye hajatambulika jina lake amenaswa na umeme wa transfoma usiku wa kuamkia leo katika eneo la Hospitali ya Bugando jijini Mwanza na kufariki dunia papo hapo.

Taarifa za uchunguzi zinamtaja mtu huyo ambaye inasemekana kuwa alikuwa katika mchakato wa kuiba mafuta ya transfoma hilo, wakati akifanya hujuma hiyo alipigwa shoti na kunasa mara baada ya kuegemea bila kujua moja ya nyaya zilizokuwa na umeme.


Mafundi wa umeme kutoka Tanesco wakipanda kuunasua mwili wa jamaa huyo.

Kutokana wizi huo baadhi ya maeneo ya jiji la Mwanza hususani eneo la Hospitali ya Bugando na maeneo yake ya jirani yamekosa umeme usiku mzima hadi leo na baadhi ya shughuli kusimama kwa kukosa nishati ya umeme.

Asubuhi ya leo mashuhuda kutoka sehemu mbalimbali walimiminika kwenye tukio hilo la kutisha na kuona hatua kwa hatua za ushushaji wa mwili wa mwizi huyo wa mafuta ya transfoma.

TANESCO kupitia kitengo chake cha usalama, kimekuwa kikifuatilia kwa ukaribu hali hiyo, ili kupambana na wizi huo na licha ya kuwakamata baadhi ya wahalifu ambao baadhi yao walifikishwa mahakamani na kesi zao bado zinaendelea kusikilizwa kwenye mahakama mbalimbali hapa nchini bado wizi unafumuka kwa kasi tena ya ajabu chanzo kikuu kikitajwa kuwa ongezeko la mahitaji.

Kila kukicha TANESCO imekuwa ikingia gharama katika kununulia vifaa vilivyoibwa badala ya kuendeleza maendeleo ya miradi ya umeme nchini.

Mwili wa mtu huyo ukipelekwa kuhifadhiwa hospitali ya Rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Meneja wa TANESCO mkoa wa Mwanza bw. Makoye Nyerere amesema kuwa Shirika lake pekee halitaweza kulikabiliana na tatizo hilo, hivyo jamii inatakiwa itambue kuwa tatizo hilo ni kubwa linahitaji ushirikiano wa pamoja, kuanzia wananchi, viongozi pamoja na serikali yenyewe.

"Ni muhimu basi, mtu yeyote anayejua juu ya wizi huo, atoe taarifa ya siri, ili kunusuru mamilioni ya fedha kutumika kurekebisha badala ya kuendeleza miundombinu ya umeme na kuletea watu maendeleo" alisema Makoye.

SHEREHE ZA SIKU YA KUZALIWA MWANZAILISHI WA DINI YA SIKH GURU NANAK

Maelfu ya wafuasi wa dini ya Sikh walijitokeza siku ya Jumapili tarehe 6 Novemba 2011 katika mjini wa Southall, Middlesex UK ili kusherekea siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa dini yao Guru Nanak aliezaliwa mwaka 1469 nchini Pakistani.Waumini wa dini ya Sikh wakiazimisha siku hii..

Halaiki ya kubwa ya waumini wa dini ya Sikh wakisherekea

Wadau wakiwa kazini kutayarisha chakula.

Hata watoto nao walikuja kusaidia kutayarisha chakula

Wakati wa kupata mapocho pocho.

chakula kilikuwa bure kwa kila mtu

Frank wa Urban Pulse ni mmoja wa mashuhuda hapa akiwa katikati ya mitaa ya Southall kushuhudia sherehe hii.

Muasisi wa Dini ya Sikh Guru Nanak.

Inatajwa kuwa wakati akiwa na umri wa miaka 30 alipotea kwa hali ya miujiza kwa mda wa siku tatu. Alipo rejea alianza kuhubiri, kufundisha na kuandika dini ya Sikh wakati maisha yake yote. Pia Guru Nanak alisafiri dunia nzima kuitangaza na kujadili dini hii kwa waumini wengine kama waislamu pamoja na Hindus

Kwa Miaka zaidi 550 wafuasi wa dini hii wamekua na desturi hii ya kusherekea siku moja kabla ya kuzaliwa kwake Guru Nanak kwa kuandaa maandamano haya makubwa ya Sherehe hii ambayo hufanyika India pamoja na baadhi ya sehemu za nchi ya Uingereza. Kwa kawaida sherehe hizi huongozwa na wafuasi wakuu watano wanaojulikana kama ''Panj Piare'' wakiambatana waimbaji, wanamuziki na timu ya wacheza upanga (Martial Arts) kuelekea hekaluni kwao ''Gurdwara'' Sri Guru Singh Sabha, hapa Southall hekalu lao ndio kubwa kuliko yote katika bara la ulaya.

Sherehe hizi huanza mapema asubuhi kwa kuimba, kuomba kwa pamoja. Baadae chakula cha kitamaduni kinachojulikana kama ''Langar'' hutolewa bure kwa kila mtu.

Maandamano ya Southall yanaitwa Nagar Kirtan,

CHANZO NA URBAN PULSE CREATIVE.

LEO NI SIKU YA KUZALIWA ANORD KAYANDA

LEO ni siku ya kuzaliwa mshkaji wa karibu sana na blogu hii my brother toka Clouds Fm wa kipindi cha Jahazi.

Blogu hii inakutakia kila la kheri kwenye siku yako hii muhimu ikisemaaaaaaaaaaaaaaaa:-

Usiiangalie JANA kwa HASIRA wala KESHO kwa UOGA bali itazame LEO kwa HEKIMA na BUSARA huku ukimtanguliza MUNGU kwa kila JAMBO!!!

HAPPY BIRTHDAY BRO.

Monday, November 7, 2011

PSPF YAKABIDHI MSAADA KWA KIKUNDI CHA WALEMAVU CHANG'OMBE

Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma PSPF, Bi.Fatma Elhady (kushoto) akimkabidhi msaada wa hundi ya shilingi milioni 1.5, Bi.Dominion Apiyo wa Kikundi cha Walemavu cha Little cha Chang'ombe wilayani Temeke, Dar es Salaam jana(.Picha na mpigapicha wetu)