Kwa uchunguzi wa haraka nilioufanya, baadhi ya madarasa shuleni hapa, hii leo hayana hata sakafu, hali ambayo inawalazimu wanafunzi kukaa kwenye vumbi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa walimu katika ufundishaji wao.
Pamoja na kwamba ni shule ambayo iko katikati ya jiji la Mwanza baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wanakalia mawe na matofali, hali ambayo imekuwa ikichangia kuporomoka kwa kiwango cha elimu.
Vyoo ndiyo kabisaaaa 'chokesti' Pamoja na kwamba matatizo haya ni la muda mrefu, lakini viongozi hasa wanasiasa wanatoa ahadi tu wasizozitekelezeka, ni mfanyabiashara mmoja tu aitwaye Aritaf Mansoor aka Dogo kwa pesa zake ndiye aliye ameamua kujenga madarasa mengine shuleni hapo.
Mlio soma hapa enzi za Mwalimu mupooo? Jeh! mwayaona haya?
Tupe maoni yako
Duh!Hali inatisha na kusikitisha..Kama Nyamagana ipo hivi vipi shule za Ibitabagumba au kome mchangani zitakuwaje?
ReplyDeleteHongera sana G sengo kwa kutuletea Taswira za jiji la mwanza sio kila siku watu wanaweka picha za majengo ya NSSF PPF.
Nilibahati kusoma hapo darasa la sita la saba.Hakika hali inasikitisha sana sana..Something should be done..
Tunaomba utuwekee na picha za Nyanza.
ReplyDeleteAisee Nyamagana ndio imekuwa hivi!!am shocked nilikuwa napicha nyingine kabisa kuhusu hii shule. Nimetoka Mza muda mrefu sana na hali ya shule hii imenishtua mnoo. Wakati mwingine nadhani sie wenyewe wana Mza tunatakiwa kulipa fadhila kwa kusaidia vitu kama hivi. Binafsi nafikiria kipi cha kusaidia Mungu akipenda soon nakuja Mza
ReplyDeleteHata walimu huwa haangali usfi.mwalimu kwake
ReplyDeleteanashindwa kupasafiha loe ijeiwe shule Loooo....
panatisha kama hali ndiyo hii.