Taarifa za uchunguzi zinamtaja mtu huyo ambaye inasemekana kuwa alikuwa katika mchakato wa kuiba mafuta ya transfoma hilo, wakati akifanya hujuma hiyo alipigwa shoti na kunasa mara baada ya kuegemea bila kujua moja ya nyaya zilizokuwa na umeme.
Mafundi wa umeme kutoka Tanesco wakipanda kuunasua mwili wa jamaa huyo.
Kutokana wizi huo baadhi ya maeneo ya jiji la Mwanza hususani eneo la Hospitali ya Bugando na maeneo yake ya jirani yamekosa umeme usiku mzima hadi leo na baadhi ya shughuli kusimama kwa kukosa nishati ya umeme.
Asubuhi ya leo mashuhuda kutoka sehemu mbalimbali walimiminika kwenye tukio hilo la kutisha na kuona hatua kwa hatua za ushushaji wa mwili wa mwizi huyo wa mafuta ya transfoma.
TANESCO kupitia kitengo chake cha usalama, kimekuwa kikifuatilia kwa ukaribu hali hiyo, ili kupambana na wizi huo na licha ya kuwakamata baadhi ya wahalifu ambao baadhi yao walifikishwa mahakamani na kesi zao bado zinaendelea kusikilizwa kwenye mahakama mbalimbali hapa nchini bado wizi unafumuka kwa kasi tena ya ajabu chanzo kikuu kikitajwa kuwa ongezeko la mahitaji.
Kila kukicha TANESCO imekuwa ikingia gharama katika kununulia vifaa vilivyoibwa badala ya kuendeleza maendeleo ya miradi ya umeme nchini.
Mwili wa mtu huyo ukipelekwa kuhifadhiwa hospitali ya Rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Meneja wa TANESCO mkoa wa Mwanza bw. Makoye Nyerere amesema kuwa Shirika lake pekee halitaweza kulikabiliana na tatizo hilo, hivyo jamii inatakiwa itambue kuwa tatizo hilo ni kubwa linahitaji ushirikiano wa pamoja, kuanzia wananchi, viongozi pamoja na serikali yenyewe.
"Ni muhimu basi, mtu yeyote anayejua juu ya wizi huo, atoe taarifa ya siri, ili kunusuru mamilioni ya fedha kutumika kurekebisha badala ya kuendeleza miundombinu ya umeme na kuletea watu maendeleo" alisema Makoye.
Tupe maoni yako
Bado wengine.... za mwizi huwa hazichelewi
ReplyDelete