....Uongozi wa Jembe Media Group kupitia kipindi chake #SportsRipoti kinachoruka hewani kila siku saa #3hadi4usiku, tofauti na siku ya IJUMAA tu ambapo huruka saa #2hadi3usiku kwa heshima kubwa tunaungana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mhe. John Mongella kuitakia kila la kheri timu ya nyumbani #AllianceSportsAcademy kupata ushindi hatimaye Tukutane #VPL "Tulianza na Mungu, Tunamaliza na Mungu" Amen @juma_ayo @elikanamathias @danyajr_219 @moseswilliamtz @gsengo @jembenijembe #Masamaki @loveess_lovie
Msanii Radio wa nchini Uganda ambaye alifariki Februari 1, amezikwa leo kijijini kwao Nakawuka nchini Uganda, na kuhdhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali za nchi hiyo na wasanii wa nchi jirani.
Hapo jana Ijumaa ya Februari 2, wananchi wa Uganda na mashabiki wa muziki walipata fursa ya kufanya ibada ya mwisho ya kumuombea marehemu kanisani, na kisha baadaye mwili wake kupelekwa kwenye uwanja wa michezo wa Airstip, ambapo walikesha nao huku kukipigwa show ya nguvu kutoka kwa wasanii mbali mbali wa nchini Uganda.
Kabla ya mazishi hayo kuliibuka mvutano mkubwa wa nguo ya kuvalishwa marehemu, huku Lilian Mbabazi ambaye ni mama wa watoto wake wawili ambaye mwenyewe alimtambulisha kama mke wake akitaka marehemu azikwe na suti aliyovaa kwenye tamasha la 'Nakudata' ambayo ndio ngoma iliyompa umaarufu na kumfanya atoboe kwenye game, na mwanamke wake mzungu ambaye amezaa naye mtoto mmoja akisema marehemu alitaka akifa azikwe na nguo za jeshi kwani alipenda kuitwa mwanajeshi, na hatimaye akavalishwa gwanda za jeshi.
Asubuhi ya leo mwili huo ulipelekwa kijijni kwao Nakawuka na kuwekwa kwenye makazi yake ya milele, ambapo kwenye tukio hilo watu walionekana kuwa wengi na baadhi wakizimia.
Miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi hayo ni msanii na mbunge Jaguar wa Kenya, wasanii mbali mbali wa Uganda na viongozi wa serikali.
YANGA SC imejivuta kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Lipuli Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 31 baada ya kucheza mechi 16, ikipanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, sasa ikiwazidi kwa pointi Azam FC ambao wanacheza mechi yao ya 16 usiku dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Yanga pia imepunguza pengo la pointi inazozidiwa na vinara, Simba SC hadi kubaki tano – lakini Wekundu wa Msimbazi nao watacheza mechi yao ya 16 kesho dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Erick Onoka aliyesaidiwa na Geoffrey Kihwilio na Janeth Balama, Yanga ilipata bao moja kila kipindi.
Na mabao hayo yalikuja baada ya Yanga kupata pigo dakika ya 17 kufuatia kipa wake wa kwanza Mcameroon, Youthe Rostand kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na chipukizi, Ramadhan Awam Kabwili.
Kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Papy Kabamba Tshishimbi alifunga bao la kwanza dakika ya 19 kwa kichwa akimalizia mpira uliotemwa na kipa Agathon Anthony Mkwando baada ya kichwa cha kuparaza cha winga Emmanuel Martin kufuatia kona ya kiungo Pius Charles Buswita
Kipindi cha pili, Yanga ya kocha Mzambia, George Lwandamina ilirudi na mchezo mzuri na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Buswita dakika ya 55, aliyempiga chenga kipa Mkwando baada ya pasi nzuri mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa kutokea pembeni kulia na kufunga bao zuri.
Yanga ilijitahidi kuendelea kusaka mabao zaidi, lakini Lipuli walikuwa imara na kumaliza mchezo kwa kipigo cha mabao 2-0.
Lipuli FC; Agathon Mkwando, Stephen Mganga, Ally Mtoni, Martin Kazila, Joseph Owino, Novaty Lufunga, Seif Karihe/Tola Mangonela dk69, Mussa Nampaka/Zawadi Mawiya dk71, Adam Salamba, Malimi Busungu na Jamal Mnyate/Jerome Lembele dk78.
Yanga SC; Youthe Rostand/Ramadhani Kabwili dk17, Hassan Kessy, Gardiel Michael, Kelvin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Papy Kabamba Tshishimbi, Emmanuel Martin, Raphael Daudi/Raphael Daudi dk86, Obrey Chirwa, Pius Buswita na Geoffrey Mwashiuya/Maka Edward dk81.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwa ameongozana na baadhi ya wakuu wa idara wa halmashauri ya mji wa Geita pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya ya Geita kwenye mradi wa vijana na wanawake uliopo magogo .
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akipokewa na katibu tawala wa wilaya ya Geita,Thomas Dimme wakati alipowasili kwenye mradi wa vijana na wanawake wa magogo.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ,akipokea taarifa ya uchunguzi ambao umefanyika juu ya mradi wa vijana na wanawake kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikagua baadhi ya vifaa ambavyo vilikuwa kwenye sehemu ya chakula(Kantine).
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ,akiwa kwenye kalakana ya uchomeleaji wakati alipofika kujionea vifaa vilivyopo kwenye mradi huo.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akipokea maelezo ya mashine ya kuchomelea kutoka kwa mmoja kati ya wahusika kwenye kamati ya uchunguzi.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikagua mashine ya kufyatulia matofali ya kisasa.
Na,Joel Maduka,Geita
Serikali Mkoani Geita imeeleza kusikitishwa na uendeshwaji wa
miradi ya mgodi wa dhahabu wa Geita, (GGM) kwa kutozingatia sheria ya
ushirikishaji kwa Halmashauri zilizopo mkoani humo na kushindwa kujulikana kwa
gharama za miradi ya jamii inayotekelezwa na mgodi huo.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku
chache baada ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kukabidhi mradi wa Maendeleo ya uchumi kwa
Vijana na Wanawake ulipo Mtaa wa Magogo Kata ya Bombambili Halmashauri ya Mji
wa Geita.
Hali hiyo ilimlazimu Mkuu wa mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert
Luhumbi kuzulu kwenye mradi wa vijana na wanawake uliopo
kata ya Bomba mbili ,mtaa wa magogo kwa lengo la kujiridhisha baadhi ya vifaa
ambavyo vilitakiwa kuwepo kwenye mradi huo na hata hivyo amebaini kuwepo kwa
udanganyifu mkubwa kwenye vifaa ambavyo vilitakiwa kuwepo kwenye mradi huo.
Luhumbi alisema
baadhi ya watumishi kutoka serikalini
na baadhi yao kutoka GGM wameendelea kushirikiana kwa pamoja
kuhujumu miradi mingi ambayo
imekuwa ikilenga kuleta chachu ya maendeleo kwa wakazi wa Geita ambao
wamezungukwa na Mgodi huo na kufuatia hatua hiyo ameagiza uchunguzi wa kina
ufanyike ili kuwabaini wale wote ambao wameshiriki kuchakachua fedha za miradi
hiyo.
“Sasa katika miradi yote ishirini na sita (26) ambayo imekwenda
yote ina matatizo na ajabu mwaka huu
niliambiwa kuna fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya CSR ya mwaka huu nilikagua
baadhi ya miradi kuna mradi mmoja nilikuta ni wa bilioni moja nukta sita
lakini mimi siwezi kuficha hata tukitumia fedha vibaya kidogo tunaweza kutumia
milioni mia tatu (300) lakini bilioni moja
nukta tatu inapotea na watu kutoka ofisi
zetu walikwenda mgodini wakaa na kuweka mkataba wakurugenzi hawakuwepo mkuu wa wilaya afahamu baadae
tunaambiwa fedha ipo tayari kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo nimesema sisi
kama mkoa hatubariki miradi hiyo
kabisa”Alisema Luhumbi.
Hata hivyo kutokana na kuonekana upungufu kwenye miradi ya jamii
Mhandisi Luhumbi amewakataa maafisa mahusiano ya jamii wa mgodi wa GGM kutokana
na kushindwa kufanya shughuli zao kwa
weledi kwenye maeneo waliyopangiwa na mgodi huo.
Na pia ameviagiza vyombo vyote vya sheria kuhakikisha wanaingia
kwa undani zaidi na kufanya uchunguzi wa kutosha na ndani ya wiki moja endapo
kuna mtumishi wa serikali atakayebainika
kuhujumu basi sheria ichukuliwe dhidi yake ikiwa ni pamoja na kumwajibisha.
Afisa sheria wa Mkoa huo Bi Sarah Mwangole alisema mradi wa
Magogo ambao umekabidhiwa hivi karibuni umefanyika bila ya makubaliano baina ya
Halmashauri na mgodi wa GGM hivyo pia wameshauri vyombo vya sheria kuingilia na
kufanya uchunguzi na kwamba hadi sasa ofisini kwao hawajapata nyaraka zozote za
mradi huo licha ya kuzihitaji.
Mtandao huu umezungumza
na Msimamizi wa
kitengo cha mahusiano kwenye mgodi wa GGM Bw Joseph
Mangilima ambaye alisema mengi ya mambo
yaliyozungumziwa hawezi kuyazungumzia yeye kwa kuwa hayahusiani na kitengo
chake moja kwa moja na kwamba kazi iliyompeleka kwenye mradi huo ni kupeleka
funguo za majengo baada ya kusikia mkuu wa mkoa anautembelea mradi huo.
MBUNGE
wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamud Mgimwa amemwokoa mtoto wa kike
ambaye ni mlemavu wa viungo kwa kumpeleka shule baada ya wazazi wake
kushindwa gharama za masomo.
Mtoto
huyo Rosemary Lutego ambaye ana umri wa miaka 15 alichaguliwa kujiunga
na kidato cha kwanza katika shule yawasichana Iringa lakini alishindwa
gharama za masomo na matumizi shuleni baada ya wazazi wake kukimbia
jukumu la kumpeleka shule.
Mbunge
Mgimwa baada ya kugundua changamoto inayomkabili binti huyo licha ya
kufaulu na kushindwa kujiunga na wenzake kuanza masomo ya kidato cha
kwanza ndipo alipoamua kumsomesha katika shule maalum ya Wasichana
Iringa ambayo ni mchanganyiko.
Mwanafunzi
huyo alijulikana kama yuko nyumbani baada ya ziara ya kikazi aliyofanya
mbunge Mahamud Mgimwa katika kata mbalimbali na kubaini uwepo wa
mwanafunzi ambaye alikosa vifaa mbalimbali vya shule na kuamua kuchukua
jukumu la kumsomesha hadi anamaliza shule.
Mara
baada ya kupata taarifa za mwanafunzi huyo,Mgimwa alizungumza na wazazi
na walimu katika shule ya Msingi Ikweha na kuwataka uongozi wa kijiji
cha Ikweha kuwatafuta wazazi hao na kuwapeleka katika vyombo vya sheria
huku akichukua jukumu la kumnunulia vifaa vyote vinavyohitajika shuleni
hapo.
Aidha
aliwataka wazazi wote ambayo wana tabia ya kuwazuia watoto waliofaulu
kujitokeza haraka kabla ya msako kuanza popote pale katika jimbo la
Mufundi Kaskazini ambapo wawapeleke shule kutokana na sasa hakuna ada
wala mchango katika shule za serikali.
Aidha
aliwataka wazazi kuacha tabia ya kuwafundisha watoto wao tabia ya
kujifelisha katika mitihani ili waweza kuolewa wakati uwezo wa kufaulu
upo kwa mtoto husika.
Akizungumza
mara baada ya kupata msaada huo mtoto Rosemary Lutego alisema kuwa
ndoto yake ya kupata elimu na kuweza kuja kuwasaidia wazazi wakeimeanza
kupata mwanga kwani alidhani ndoto zake zimeishia darasa la saba.
alimshukuru
sana mbunge Mgimwa msaada huo mkubwa wa kufanikisha masomo yake kwani
itakuwa mfano mkubwa wa wazazi wengine ambayo hawataki mtoto wa kike
aende shule.
Aliongeza
kuwa wazazi wake walimwambia kuwa wanaenda kutafuta fedha za kununulia
vifaa lakini hadi sasa hawakuweza kufanikisha hali iliyomlazimu abaki
nyumbani wakati wanafunzi wengine wakiendelea na masomo.
"Namshukuru
sana mbunge kwa kusikia na kuamua kugharamia masomo yangu ya sekondari
nitahakikisha nasoma kwa bidii licha ya ulemavu wangu ili kuweza
kuikomboa familia yangu katika umaskini." alisema
Mwenyekiti wa Muda wa Asasi ya kiraia ya Legal Services Facilities (LSF) Dkt. Benson Bani , akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia ya LSF Bw. Kees Groenendijk akitoa mada yake ambapo alizungumzia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelezea malengo, mambo mbalimbali yaliyofanyika kwa mwaka 2017 pamoja na mwelekeo kwa mwaka 2018, wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Meneja Miradi wa LSF Bw.Ramadhani masele akielezea kiundani juu ya utendaji , mrejesho na nini kifanyike wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Baadhi ya wakurugenzi na wajumbe wa Bodi za ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria wakitoa maoni mbalimbali wakati wa warsha hiyo
Afisa ufuatiliaji na tathimini kutoka LSF Bi. Saada Mkangwa akitoa ufafanuzi juu ya ukusanywaji wa taarifa za wanufaika wa ruzuku.
Mkurugenzi wa miradi wa LSF Bi. Scholastica Julla akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Makundi mbalimbali ya ya wakurugenzi pamoja na wajumbe wa bodi za wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria wakijadili mambo mbalimbali na namna watakavyofanya kazi na LSF kwa mwaka 2018.
Wawakilishi katika makundi wakitoa mrejesho wa kile ambacho walikuwa wamekijadili wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria, ambapo wote walionesha kuwa watafanya kazi zao kwa weredi zaidi kwa mwaka 2018
Meneja wa ufuatiliaji na matokeo kutoka LSF Bw. Said Chitung akielezea mambo mbalimbali pamoja na malengo ya LSF kufikia 2021 wakati wa warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria.
Wakurugenzi na wajumbe wa bodi wakati wakiendelea kufuatilia mambo mbalimbali ya warsha ya wadau wanaotoa huduma ya msaada wa kisheria iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ambapo amesisitiza viongozi kusimamia Kanuni na taratibu juu ya usimamizi wa madini, leo 3 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Kamati ya
ulinzi na usalama Wilaya ya Kahama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Fadhil
Nkulu wakisikiliza maelekezo mbalimbali kutoka kwa Naibu Waziri wa Madini Mhe
Doto Mashaka Biteko alipozuru Wilayani humo kwa ziara ya kikazi, Leo Februari 2018.
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza wakati wa kikao cha kazi na Uongozi wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga aakiwa katika ziara ya kikazi, leo 3 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Shinyanga
"Sheria mpya ya madini ya mwaka 2017 inataka kurudisha
uchumi wa madini kuwa uchumi fungamanishi kwa sekta nyingine, Hatuwezi kuwa na
Mgodi ndani ya nchi ambao ajira zote zinapelekwa nje ya nchi kupitia huduma
mbalimbali, unaweza kuagiza bidhaa za kila aina kutoka nje ya nchi lakini
huwezi kuagiza ajira za wananchi wako zitoke nje kuja ndani, kamwe
haiwezekani"
Ni Kauli ya Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko leo 3
Februari 2018 wakati akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya Kahama Mkoani
Shinyanga ambapo amesisitiza zaidi viongozi wa serikali katika maeneo yao
kusimamia Kanuni na taratibu juu ya usimamizi wa madini.
Mhe Biteko alikaririwa akisema kuwa usimamizi madhubuti wa
sheria na taratibu zilizowekwa ni sehemu imara na makini itakayowanufaisha
watanzania ambapo watakuwa wamemuunga mkono kwa vitendo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ambaye amejidhatiti kwa
mtazamo wa kuwanufaisha watanzania kupitia rasilimali zao.
Kanuni
ya madini ya mwaka 2018 imeelekeza kuwa mgodi wowote unapoanza asilimia 100% za
watoa huduma za chakula wanapaswa kuwa watu wa wananchi wa Tanzania, Pia huduma
za ulinzi kwa asilimia 100% zinapaswa kutolewa na kampuni za ndani. Hivyo
wataalamu wa sekta ya madini ni lazima kusimamia Kanuni hizo kwa usahihi.
Mhe Biteko aliongeza kuwa kampuni ya kigeni inaweza kufanya
huduma hizo lakini ni lazima iingie ubia na wananchi wa Tanzania na kanuni hizi
serikali imeziweka kwa makusudi kabisa ikiwa na mtazamo wa kuwanufaisha
wananchi kupitia rasilimali zao.
Mhe Biteko alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho
kimeingia mkataba na wananchi katika kuwatumikia kwa usimamizi madhubuti
kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 hivyo viongozi wa CCM wanapaswa
kusimamia vyema serikali ili kuongeza tija katika utendaji.
Sambamba na CCM kusimamia vyema serikali pia Naibu Waziri huyo
wa Madini amewataka watendaji wote wa serikali kuwa na umoja katika utendaji
wao kwa usimamizi madhubuti wa rasilimali madini huku akitoa onyo Kali kwa
watendaji wa serikali, Viongozi, vyama vya siasa na wananchi kujihusisha na
rushwa kwani kufanya hivyo ni kuzififisha juhudi za serikali ya awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Magufuli ya kuwainua wananchi wanyonge ili kila mtanzania
aweze kunufaika na rasilimali zilizopo.
"Ndugu zangu ni aibu mno dhahabu na madini yetu mengine
kuchimbwa nchini lakini yanajenga nchi nyingine, Uhakika wa barabara bado
hatuna katika maeneo mengi, maji bado hatuna, sekta ya afya haijaimarika,
Zahanati zina shida lakini pia Karibu kila maeneo hatujajidhatiti kwa asilimia
100% Kwa hiyo Mhe Dc naomba sana msicheke na mtu yeyote anayecheza na
rasilimali zetu This Must be a Serious business, Mimi najua we have the same
spirit lazima tufanye kazi kwa weledi.
Aidha, Naibu Waziri huyo wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko
amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Fadhil Nkulu sambamba na Mbunge wa
Jimbo la Msalala Mhe Ezekiel Maige kwa jukumu kubwa la utendaji wao katika
kuimarisha juhudi na ufanyaji kazi uliotukuka katika sekta ya madini kwa
maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla huku akisisitiza kuwa kila kiongozi
atapimwa kwa matokeo ya utendaji kazi wake na si kwa cheo chake.
" Waheshimiwa Viongozi, Mhe. Rais na wanatanzania
watatupima kwa matokeo si kwa nafasi na vyeo vyetu" alisisitiza Mheshimiwa
Biteko wakati akihitimisha hotuba yake kwa uongozi wa serikali wilayani Kahama.
NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV. TAREHE 01.02.2018
MBUNGE wa Jimbo la Kwimba mkoani Mwanza, Shanif Mansoor, amesema asilimia 80 ya vijiji jimboni hapa vipo mbioni kupata umeme.
Amesema miradi hiyo ya umeme wa Rea Vijijini, itapatikana kwa kipindi cha kuanzia sasa hadi kufikia mwaka 2020, ili kuwasaidia wananchi kupata maendeleo.
Mansoor aliyasema hayo juzi katika ziara yake ya kikazi jimboni hapa, na kwamba anahitaji kuwasaidia wananchi kupata maendeleo ya kisekta.
"Napenda kusema kazi tumeshaanza. Mwaka huu kuna mradi mkubwa sana wa umeme wa Rea Vijijini. Baadhi ya maeneo umeme haujafika....lakini tutapata umeme hadi Mwakilyambiti.
"Kwa hiyo apambana kuhakikisha asilimia 80 ya vijiji vya Jimbo la Kwimba vinapata umeme wa Rea, ifikapo mwaka 2020," alisema Mbunge huyowa Jimbo la Kwimba na kuongeza:
“Naomba sana ushirikiano wenu wananchi, ili tuijenge Kwimba na taifa kwa ujumla katika maendeleo ya kweli.”
Katika hatua nyingine, Mansoor aligawa majembe ya kilimo 18,000 yenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 200, ambapo karibu kila kaya itanufaika na vifaa hivyo.
Alisema lengo la kuwawezesha wananchi vifaa hivyo vya kilimo, ni kuwawezesha kuzalisha mazao ya chakula na biashara.
Alisema kuwa, licha ya kuahidi kutoa vifaa hivyo kwa wananchi lakini pia amelenga kuinua uchumi wa kila mwananchi kupitia kilimo, ndani ya Jimbo la Kwimba.
"Staki mpate tabu wakati mbunge wenu nipo. Halmashauri yetu ya wilaya nayo nimeipatia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara, katika Shule ya Sekondari Bujiku Sakila.”
Aliipongeza pia Serikali kwa kujenga mradi wa maji jimboni Kwimba, unaogharimu zaidi ya sh. Milioni 576.
Kwa mujibu wa mh.Mansoor, mradi huo tayari umeshakamilika kwa kiwango cha asilimia 80, ambapo umelenga kupunguza kama si kuondoa kabisa adha ya maji katika jimbo la kwimba.
“Mimi mwenyewe nataka kila kijiji kiwe na mradi wa maji safi na salama ya kunywa kutoka ziwa victoria,umeme na miundombinu rafiki pamoja na kutengeneza barabara za mitaa ya miji inayoendelea katika jimbo la kwimba.
“Nimechimba mabwawa na visima zaidi ya 35 vya maji kwa nguvu zangu. Lengo langu ni kuwasaidia wananchi walioniamini na kunipa kura za kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa 2015,” alisema Mansoor.
Wakati huo huo, Mansoor amewakatia bima za afya viongozi wote wa Halmashauri za Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kwimba.
Alisema kuwakatia kwake bima viongozi hao ni lengo la kutaka kuwasaidia, katika changamoto za masuala ya afya, hivyo anahitaji kuona jamii inatekeleza vema majukumu yake.
Mbunge wa Jimbo la Kwimba mkoani Mwanza, Shanif Mansoor akigawa majembe kwa kikundi cha akinamama waliofika kwenye kusanyiko lake, ambapo pia alipata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi.
Jembe ni mali.
Mimi ni jembe.
Mansoor aligawa majembe ya kilimo 18,000 yenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 200, ambapo karibu kila kaya itanufaika na vifaa hivyo.
Karibu kila kaya itanufaika na vifaa hivyo vya kilimo.
Mkutano wa ndani na wanachama wa CCM.
Mansoor alikutana na wananchi wa jimbo lake kupokea ushauri na pia kuwasilisha mipango mikakati kwa hatua zijazo.
Mada Iliyowasilishwa na Bwana Joseph M. Mapunda, Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Maudhui ya TCRA, Katika Warsha ya Wahariri na Watengenezaji wa Vipindi vya
Redio na Televisheni, Mwanza ,Februari01, 2018.
Utangulizi
Nchi yetu imejaliwakuwa na rasilimali nyingi za kuiwezesha kupata maendeleomakubwa katika nyanja zote za uchumi,
hudumaza jamii, utamaduni, habari na
michezo bila kusahau suala zima la demokrasia (siasa). Kuna fursa nyingi za
kuliwezesha Taifa kupata maendeleo ya haraka ikiwa rasilimali zilizopo zitatumika
kikamilifuna kwa umakini mkubwa.
Kwa upande wa sekta ya habari na utangazaji, sera na sheria
zilizopo zimetoanafasi na uhuru mkubwa
kwa sekta ya umma(Serikali) na sekta binafsi kumiliki na kuendesha vyombo vya
habari na utangazaji kwa lengo kuu la kuvifanya viwechachu ya kuhamasishawananchi na wadau wengine ndani na nje ya
nchi yetu kushiriki kikamilifu katika kutekeleza mipango ya maendeleo kwa faida
ya vyombo vyenyewe, wananchi na Taifa kwa ujumla.
Ukuaji wa Sekta ya
Habari na Utangazaji
Vyombo vingi vya habari na utangazaji vimeanzishwa hapa
nchini tangu miaka ya 1990 wakati mfumo wa uchumi ulipoanza kushirikisha rasmi
Sekta binafsi tofauti na huko nyuma ambapo shughuli zote kuu za uchumi na kijamiizilikuwa zikimilikiwa na kuendeshwa na
Serikali.
Utaratibu huo pia ulihusisha masuala ya kisiasa ambapo nchi
ilikuwa ikitawaliwakatika misingi ya
demokrasia ya Chama kimoja cha siasa (one Party democracy).
Idadi ya Vyombo vya Habari na Utangazaji
Hadi sasa kuna vituo 32 vya
televisheni; vituo 155 vya redio na idadi kubwa ya mitandao ya kijamii. Hali
kadhalika kuna magazeti na majarida 432 yaliyosajiliwa kisheria. Vyombo vingi
zaidi vya habari na utangazaji vinaendelea kusajiliwa na hivyo kutoa fursa
nyingi za uwekezaji na ajira katika Sekta hii muhimu ambayo baadhi ya watu
wamezoea kuiita Mhimili wa Nne (Fourth Estate). Zaidi ya asilimia tisini na tisa
(99 per cent) ya vyombo vilivyopo vinamilikiwa na Sekta binafsi.
Utajiri huu mkubwa wa idadi ya
vyombo vya habari na utangazaji ni ushahidi tosha kuwa sekta hii ni nyenzomuhimu na ya kutegemewa katika kuwapa habari,
kuwaelimishana pia kuwahamashisha wananchi kushiriki
kikamilifu na kwa uelewa mkubwa katika kuibua na kutekeleza mipango ya maendeleo
ya nchi yetu.
Kwa vile zaidi ya asilimia sabini
na tano (75 per cent) ya Watanzania wanaishi vijijini wakishughulika na
kilimo---ambacho ni uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa--- ni wazi kuwa vyombo vya
habari na utangazaji vina wajibu mkubwa wa kuelekeza nguvu na rasilimali zake
huko ili kutangaza mafanikio, matarajio na changamoto za kilimo, ufugaji, afya,
maji, elimu, utamaduni na michezo pamoja na mambo mengine mengi ya msingi.
Hali Ipoje?
Pamoja na idadi hiyo kubwa ya
vyombo vya habari na utangazaji, sehemu kubwa ya makala na habari zinazorushwa
na vyombo hivi zinahusu matukio na shughuli za mijini ambako kuna wananchi
wachache. Hali hii inamaanishakuwa
juhudi na matukio ya watu wengi waishio vijijini na wilayani hupewa nafasi
kidogo sana katika matangazo ya vyombo vyetu.
Natoa rai kwa wamiliki na watendaji
wakuu wa vyombo vyote vya habari na utangazaji kuonyesha uzalendo usioyumba
(unshakable patriotism) ili kuhakikisha kuna kuwa na uwiano mzuri/sawia wa
habari na matukio ya mijini na zile za vijijini ili kutoa fursa na hamasa kubwa
kwa wananchi wote kujuzwa juu ya mambo muhimu yanayoendelea nchini na hivyo
kuwawezesha kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza mipango mbali mbali ya
maendeleo.
Kuelekea Uchumi wa Kati
Serikali imedhamiriakuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati ( middle income economy) ifikapo
mwaka 2020. Mkazo hapa umewekwa katika kujenga na kuimarisha Sekta ya
Viwanda kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa bidhaaza viwandani hasa zile zinazotokana na
malighafi za kilimo na ufugaji na shughuli nyingine nyingi za kiuchumi kuanzia ngazi ya kijiji
hadi Taifa. Mkakati huu pia unahusu ufufuaji wa viwanda vilivyokufa na vile
ambavyo ujenzi wake haujakamilika. Mafanikio ya juhudi hizi yatawezesha
kupatikana ajira nyingi, ongezeko la uzalishaji mali, mapato ya Serikali na maslahi ya wananchi kwa
ujumla.
Vyombo vya habari na utangazaji
vina nafasi kubwa ya kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuielewa dhana nzima ya uchumi wa viwanda na jinsi
wanavyoweza kushiriki katika utekelezaji wa azma hii ya Serikali kwa vitendo.
Twende Vipi?
Uchumi wa viwanda ni dhana pana
sana. Inahusisha sekta zote za uchumi na jamii (production and service
sectors). Sekta zote hizi zinaingiliana na kushabihiana katika mfumo wake wa
utendaji. Naomba tuangalie kwa muhtasari baadhi ya sekta na jinsi gani vyombo
vya habarina utangazaji vinaweza kuchukua
nafasi yake katika kurusha matangazo yenye kuendana na dhana ya viwanda nchini.
Kilimo
Hii nisekta kiongozi katika uchumi wa Taifa letu na
itaendelea kushika nafasi hiyo kwa miaka mingi ijayo. Kwa kuzingatia hilo, ni
vema wakulima na wafugaji wakaelimishwa mbinu za kilimo cha kisasa ili
kuzalisha mazao bora yenye kukidhi mahitaji ya ndani ya nchi na ziada kwa ajili
ya soko la nje.
Matangazo yazingatie kuwaelimisha
wananchi juu ya misingi bora ya kilimo na ufugaji hasaupatikanaji kwa wakati wa
pembejeo na zana nyingine muhimu za uzalishaji na pia jinsi ya kuyafikia masoko
kirahisi ili bidhaa zitakazo zalishwa zisiozee mashambani.
Elimu zaidi pia itolewe na
kutiliwa mkazo kuhusu uanzanzishwaji wa viwanda vinavyotegemea mazao ya kilimo
katika ngazi ya vijiji ili kuyaongezea thamani. Mkakati huu utawahakikishia
wananchi ajira nyingi, mapato makubwa, afya bora na huduma muhimu za kijamii.
Kupitia viwanda, wananchi
wataweza kula vyakula safi na salama vilivyosindikwa hapa nchini. Hali hii
itatuondoleatatizo sugu la kula vyakula
vibovu na hatarishi kutoka nje ya nchi.
Wengi wetu hapa tumewahi kusikia uvumi kupitia mitandao ya kijamii na
kwingineko kuwa soko letu limevamiwa na mchele wa plastiki, samaki wa plastiki,
mayai bandia ya kuku, maziwa, nyama, na bidhaa nyinginezisizokuwa na viwango vinavyokubalika kiafya.
Hali kadhalika, Watanzania wengi
huvaa nguo na viatu vya mitumba wakati tuna pamba na ngozi nyingi zinazoweza
kuzalisha bidhaa bora. Suala la viwanda vidogo vidogo vilivyoanzishwa na
wananchi wenyewe katika ngazi ya vijiji na wilaya litiliwe mkazo.
Wananchi waelezwe na kuelemishwa
ipasavyo kuhusu masuala haya muhimu na jinsi ya kuyakabili ili kutuwezesha kujitegemea,
kulinda afya zetu na kujijengea miili imara na akili timamu.
Elimu ni Kila Kitu
Wote tunafahamu umuhimu wa elimu
katika uchumi na ustawi wa jamii. Shule na vyuo vyetu katika ngazi zote
vihamasishwena viwezeshwe kutoa
wahitimu au wataalam wa fani mbali mbali watakaowezakulisaidia Taifa kwa vitendo kuleta maendeleo
na mapinduzi katika maisha yao.
Vyombo wa habari na utangazaji
vijikite katika kurusha matangazo yanayolengamaendeleo na kuhakikisha watu wote, hasa maskini, wanaondokana na hofu
ya njaa na shida nyingine nyingi za daima ili kufikia kiwango cha maisha
yanayomstahilibinadamu.
Kwa mfano, akina mama huko
vijijini na baadhi ya miji yetu wakipunguziwa mzigo wa kujitwika mitungi na
ndoo za maji kilometa nyingi wanaweza kupata fursaza kujihusisha kikamilifu katika uzalishaji
mali kwa upeo na ufanisi mkubwa. Tutilie mkazo dhana ya watu kujiletea
maendeleo yao wenyewe.
Kupitia tafiti mbali mbali vyombo
vya utangazaji vinaweza kuandaamakala
na vipindi maalum vitakavyoonyesha au kuelekezamambo yanayowezekana kufanywana
jinsi yanavyoweza kufanyika. Ni dhahiri kuwa watu wenye elimu na ujuzi wanaweza
tu kuwa na manufaa kama watachanganyika na kushirikiana kwa dhati na jamii
inayowazunguka. Haya yote yanaweza kutendekaikiwa moyo wa uzalendo utajengeka na kuimarishwa ndani ya vyombo vya
habari na utangazaji.
Afya na Ustawi wa Jamii
Hii ni dondoo yenye uzito mkubwa katika utekelezaji wa
mipango ya maendeleo. Tunahitaji kuwa na watu wenye siha nzuri na ya kutegemewa
katika shughuli nzito na muhimu za
maendeleo. Ili tuweze kupatamaendeleo
ya kweli na ya haraka inabidisuala la
afya litiliwe mkazo maalumna vyombo vya
habari na utangazaji. Jukumu la msingi hapa ni kuandaa na kurusha vipindi na
makala zenye kuelimisha watu kuhusu namna ya kuzuia na kujikinga na maradhi,
kutunza mazingira, kula vyakula vyenye kujenga mwili, kunywa maji safi na
salamana kuondokana na unywaji wa pombe zilizotengenezwa bila kuzingatia
masharti na viwango vinavyokubalika kiafya.
Uzoefu unaonyesha kuwa makala na taarifa
nyingi zinazorushwa zinahusu matukio ya
magonjwa ya mlipuko na majanga mengine ya kiafya na ya kijamii. Tuandike na
tutangaze habari zinazowahamisisha na kuwashawishi watukuishi vizuri kwa kuzingatia masharti na
matakwa ya afya bora.
Watu wengi wamezoea au
wanalazimika kula vyakula vya mitaani katika mazingira machafu. Juhudi za dhati zifanyike kuwahimiza mamalise
na babalishe kupika vyakula bora na ambavyo vimeandiliwa kwenye mazingira bora
na kupakuliwa kwenye vyombo vinavyokubalika kiafya.
Siku hizi Watanzania wenzetu wengi
wanasumbuliwa na magonjwa yasiyotibika kama saratani, ambayo kwa kiwango
kikubwa chanzo chake ni kula vyakula visivyokuwa na viwango sahihi. Shughuli za
taasisi kama Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Vyakula na Madawa
Tanzania (TFDA) zipewe kipaumbele katika matangazo ili mchango wao uweze kuwa
wa manufaa zaidi kwa wananchi na ustawi wa jamii.
Vile vile, elimu ya kina itolewe
kuhusu faida zinazotokana na kula vyakula vya asili (fresh foods) kama vile
mboga zilizolimwakatika mazingira safi
na salama, matunda, nafaka za mafuta kama karanga, ufuta, alizeti, nazi na
vingine vingi. Kwa bahati nzuri bidhaa hizi zote zinazalishwa kwa uwingi hapa
nchini kwa bei ambazo watu wengi wanaweza kuzimudu. Tujihadhari na bidhaa
zilizosindikwakutumia madawa/chemikali
ili kuepuka athari za kiafya.
Utamaduni, Muziki na Burudani
Sektahii pia ina mchango mkubwa sana katika
maendeleo ya nchi yetu. Vituo vya utangazaji viandae na kurusha vipindi
vinavyohamasishaukuaji na uendelezaji wa
muziki na burudani zenyemaudhui ya yanayoendana
nautamaduni wetu wa Kitanzania. Pamoja na kuwepo umuhimu wa kurusha muziki na
ngoma kutoka nje ya nchi ni vema busara ikatumika kuchagua maudhui yenye
kulenga uendelezaji na udumishaji wa mila na desturi zaKitanzania.
Ngoja niwashirikishe kitu kimoja hapa. Siku chache zilizopita
nilipigiwa simu na mtu mmoja ambaye alinidokeza kuwa alikiona kipindi cha muziki katika kituo kimoja cha televisheni
cha Dar es Salaam ambacho kilirusha wimbo wenye maudhui ya kulidhalilisha Taifa
letu. Sehemu ya wimbo husika una maudhui yanayosomeka “…..Bongo kubaya twende zetu
Ulaya; Bongo maisha mabaya, Ulaya kuna raha tele…..”.Je, kwa maudhui kama haya
tunaitendea haki nchi yetu?
Tuijengee heshima nchi yetu kwa kurusha vipindi vyenye
maudhui ya kizalendo na yale yanayohamasisha sifa nzuri na umoja na mshikamano
wa Taifa letu.
Amani na Utlivu
Nchi yetu imejizolea sifa nyingi sana duniani kama mahali
penye amani, usalama na utulivu. Sifa hii imetujengea heshima namazingira
mazuri kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Sekta yetu ya utalii na sekta za
uwekezaji zimevutia wageni wengi kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza katika uchumi
wetu kutokana na sifa nzuri za Watanzania. Kwa kuzingatia ukweli huo, vyombo
vyetu vinapaswa kuendelea kutangaza kwa nguvu zote taswira ya Tanzania yenye
amani, utulivu na usalama.
Jukumu hili lichukuliwe kwa uzito mkubwa hasa
tukizingatiakuwa tabia ya wageni kwa
maana ya watalii na wawekezaji ni kwenda mahali ambapo usalama wao na wa mali zao unalindwa kama mboni za
jicho lako!
Kutangaza kwa ushabiki
vitendo vya uhalifu na matamshi ya kisiasa yanayoashiria uvunjifu wa amani yana
athari kubwa sana katika juhudi zetu za maendeleo. Tuwahakikishie wageni wetu
kuwa Tanzania ni nchi tulivu, inazingatia utawala wa kisheria na pia inaendesha
mambo yake kwa uwazi na inazingatia kwa dhati suala zima la haki za binadamu.
Dondoo yetu kubwa iwe kutangaza habari zenye maslahi kwa Taifa kiuchumi,
kisiasa na kijamii.
HITIMISHO
Tanzania ni nchi yetu nzuri sana.
Ina watu wapole na
wakarimu. Majirani zetu na watu wengine duniani wanaimezea mate. Tuna haki na wajibu kuilinda,
kuiheshimu na kuienzi kwa uzalendo wa hali ya juu ili tuweze kuijengea
mazingiria imara ya maendeleo katika nyanja zote.
Dhamana tuliyopewa ya kulitumikia Taifa hili kupitia vyombo
vya habari na utangazaji tuiheshimu na tuitumie vizuri kwa maslahi ya Taifa na
ya wananchi wote. Nawatakia mafanikio katika kazi zenu. Mungu awalinde na
awaongoze daima.
Arusha Yasimama Kwenye Maombi: Miaka 63 ya Uhuru
-
Viongozi wa dini ,mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda na wananchi
wakiendelea na maombi katika matembezi ya kuombea mkoa wa Arusha na
maathimisho ya mi...