NA ALBERT G.SENGO/DODOMA
Kutana na Mhandisi Imelda Salum ambaye ni Mkurugenzi wa TCRA Kanda ya Ziwa akizungumza juu ya wajibu wa vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu 2025. Mhandisi Imelda ameyasema hayo akiwa katika Mkutano wa siku mbili wa wadau wa habari na TCRA, mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ukishirikisha Vituo vya utangazaji, waandaaji na wasambazaji wa maudhui mtandaoni, wauzaji wa vifaa vya utangazaji na wadau wote wa sekta ya utangazaji ukiongozwa na kauli mbiu 'Wajibu wa vyombo vya utangazaji kuelekea uchaguzi mkuu 2025'.Saturday, February 15, 2025
Thursday, February 13, 2025
PROF. KABUDI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI TANZANIA... AKERWA NA WANAO 'BANANGA' KISWAHILI


Katika hatua nyingine, alizungumzia kauli mbiu ya Mkutano huo, 'Wajibu wa Vyombo vya Utangazaji kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025', na kuwasihi waandishi wa habari kutumia taaluma zao kusimamia haki na usawa katika kuhabarisha umma, huku wakizingatia weledi, sheria, na kanuni za utangazaji.
Alisisitiza pia waandishi wa habari kuepuka habari za kugushi, hasa kwa kuzingatia mabadiliko ya kiteknolojia katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, ili kuepuka kupotosha umma au kuleta taharuki.
Prof. Kabudi ametoa pongezi kwa waandishi wa habari kwa juhudi zao za kuhabarisha umma kuhusu taarifa mbalimbali za serikali, ikiwa ni pamoja na Mkutano Mkuu wa Nishati uliohudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali, uliofanyika jijini Dar es Salaam, na akawasihi waendelee kuelimisha wananchi kuhusu jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwani hiyo ni ajenda ya kitaifa.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Saida Muki, amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kuwa makini na matumizi ya Teknolojia ya Akili Bandia (AI) wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ili wasiwasilishe maudhui yanayoweza kupotosha umma.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Grayson Msigwa, amewashauri waandishi wa habari kuwa, kupitia Mkutano huu, wanapaswa kuzingatia weledi katika taaluma yao hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kulinda usalama wa taifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Bakari, amesema mkutano huu umeandaliwa ili kujadili masuala muhimu yanayohusu sekta ya habari na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokikabili sekta hiyo.
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, Dkt. Bakari amewasihi waandishi wa habari kutumia taaluma zao vizuri, kuhabarisha umma kuhusu hatua zote za uchaguzi hadi siku ya kupiga kura.
Baadhi ya waandishi wa habari wameelezea kuridhishwa na hatua ambazo serikali imekuwa ikichukua katika kuimarisha sekta ya habari.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo mhe Palamagamba Aidan Mwaluko Kabudi amezungumza na kuweka msisitizo ambao amesema kuwa matumizi mabaya ya Utangazaji na utoaji wa habari ambazo zisizo na Ueledi zinavyoleta Athari kubwa katika Dunia na Kuleta mifarakano
BARAZA LA MADIWANI KIBAHA MJI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 57.5 KWA MWAKA 2025 /2026
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Akisoma taarifa katika kikao cha baraza maalumu kwa ajili ya kupitisha mapendekezo ya mpango huo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mji Karimu Mtambo amesema kwamba kwa upande wa mapato ya ndani halmashauri imekisia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 11.640 ikiwa ni ongezeko la asilimia 29 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana ambayo ilikuwa ni shilingi bilioni 8.
Aidha amesema kwamba katika bajeti hiyo fedha ndani itakwenda kutekeleza miradi ikiwemo uboreshaji wa danpo la misugusugu, ununuzi wa gari la taka, ujenzi wa sehemu ya biashara,pamoja na kituo cha utoaji wa huduma katika kata za tumbi,maili moja, Kongowe,Mkuza pamoja na Tangini ikiwa pamoja na kujenga miundombinu ya biashara za machinga, sambamba na ujenzi kituo cha mafuta na karakana na ununuzi wa gari kwa ajili ya shughuli za ardhi.
Pia amebainisha kwamba kupitia bajeti hiyo kwa upande wa elimu msingi jumla ya vyumba vya madarasa 25, matundu ya vyoo 47,vitajengwa, ukarabati wa maadarasa saba, shule 1, pamja ana ujenzi wa shule mpya tatu na utengenezaji wa madawati 500 utafanyika.
Makamu huyo amesema kwa upande wa elimu sekondari ujenzi wa shule mpya 1,vyumba vya maadarasa 5,Bweni moja,na Bwalo 1 la chakula utafanyika pamoja na umaliziaji wa nyumba moja ya walimu,maabara, 4 na ofisi 2 za walimu sambamba na utengenezaji wa viti na meza vipatavyo 466.
Akizungumzia kuhusiana na upande wa afya amesema kwamba ujenzi wa kituo kimoja, cha afya na majengo matano ya zahanati,yatafanyika,ukamilishaji wa wodi 1 ya kituo cha afya na vyumba tatu za watumishi utafanyika ikiwa pamoja na ukarabati wa kituo kimoja cha afya.
Kwa uapnde wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mji Mussa Ndomba amesema kwamba katika bajeti hiyo wametenga kiasi cha shilingi milioni 60 kwa ajili ya kuboresha huduma za miundombinu ya maji katika baadhi ya kata kwa lengo la kuweza kuwaondolea changamoto ya maji wananchi.
Pia amesema kwamba Halmashauri ya Kibaha mjini katika bajeti hiyo wametenga kiasi cha shilingi milioni 30 katika kata zote 14 kwa ajili ya kuweza kuboresha miundombinu ya barabara ili ziweze kupitika kwa urahisi katika kipindi chote.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe. Silvestry Koka amepongeza mpango wa bajeti hiyo na kuimiza kuhakikisha kwamba fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo zisimamiwe vizuri kwa ajili ya kuleta chachu ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.
Koka ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuweza kuweka mipango ya kuibua vyanzo vipya vyaa mapato amabvyo vitakwenda kusaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza mapato ya ndani na kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa wananchi wa maeneo mbali mbali katika miradi ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, pamoja na huduma ya maji.
TAMASHA LA KIPEKEE LA UTAMADUNI LITAKALOWATAJIRISHA MTOTO WAKO LAJA.
NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Mwanza mpewe nini hili hapa laja huyu hapa Benard James akifunguka zaidi yaliyomo.WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA UONGOZI WA KISIASA
RC BALOZI BATILDA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAHIMIZE WAUMINI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Na Oscar Assenga,Tanga
WAKURUGENZI WA UFUATILIAJI NA TATHMINI NGAZI YA WIZARA WAKUTANA KUPITIA TAARIFA YA UTENDAJI WA SERIKALI
![]() |
Na Mwandishi wetu - Iringa.
Wakurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini ngazi ya wizara wamekutana leo tarehe 12 Februari 2025 katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa lengo la kupitia Taarifa ya Utendaji wa Serikali (Government Performance Report kwa Mwaka wa Fedha 2023/24).
Kikao kazi cha wakurugenzi hao kimeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na kuhudhuriwa na Wakurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini na Maafisa kutoka katika Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini ndani ya wizara.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. James Henry Kilabuko, Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Sakina Mwinyimkuu amesema, jukumu la Ufuatiliaji na Tathmini ni muhimu katika kuboresha utendaji wa serikali kwa ujumla hivyo Serikali imeendelea kutoa msukumo na kuboresha Miundo na Mifumo kwa kuandaa Miongozo ya Ufuatiliaji na Tathmini Ili kuimarisha U&T ndani ya Serikali.
“Dhumuni kubwa ni kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji huduma bora kwa wananchi hivyo wataalam wa Vitengo mnapaswa kusimamia na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyoainishwa katika mipango ya serikali” amebainisha Bi. Sakina
Aidha, Bi. Sakina amewaasa wataalam kutofanya kazi kwa mazoea, uoga au kutojiamini, kwani kwa kufanya hivyo serikali haitafikia malengo na kupunguza umuhimu wa kuanzisha Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini. Hivyo ni vema kuifanya ufuatiliaji na tathmini kuwa nyenzo ya msingi ya kusaidia utendaji wa taasisi, sekta na nchi kwa ujumla.
Kikao kazi hicho pamoja na mafunzo ya namna ya matumizi ya Miongozo ya Ufuatiliaji na Tathmini (U&T) katika taasisi za serikali iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kitafanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 12 hadi 13 februari 2025.
Kikao kazi kikiendelea. |
![]() |
Wednesday, February 12, 2025
CBE YATEKELEZA MAONI YA BUNGE KWA VITENDO YAJA NA MPANGO HUU......
NA ALBERT GSENGO/MWANZA
Linapokuja suala la Mitaala na Sera ya Elimu nchini, watanzania wengi hukumbuka fikra na michango yenye tija inayotafsiri uhalisia iliyotolewa Bungeni na Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kibera Kishimba kisha ikachangiwa na waheshimiwa wabunge wengine wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwenye moja ya mahojiano yake yaliyozua maswali mengi na mingi mijadala, Mhe. Kishimba alihoji 'Kwanini vijana wengi wanaomaliza mafunzo ya ufundi wanapoingia kwenye ajira wanakutwa si mafundi?' Hii ikitasfiri kwamba vyuo vingi nchini vimejikita katika utoaji wa mafunzo kwa nadharia na si kwa vitendo. Jeh vyuo vyetu hapa nchini vinakabiliana vipi na changamoto hiyo? Dr. Robert Golan Mashenene ni Mkurugenzi wa Chuo Cha elimu ya Biashara, CBE tawi la Mwanza anakuja na majibu ya yote hayo... MENGINE YALIYOWASILISHWA BUNGENI. "Elimu yetu tumeirithi kutoka Uingereza. Uingereza kama una watoto wanne wanaangalia mshahara wako unaweza kutunza watoto wangapi. Kama un unaweza kutunza watoto wawili hawa wengine wawili Serikali inakusaidia. Sisi huku Tanzania hakuna kitu kama hicho." - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Tunaweza kupeleka mabadiriko Kijijini lakini wananchi wasipokee kama tulivyopeleka kwasababu suala la umasikini hatuliangalii" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Muda wa kufunga shule umetuathiri sana Kijijini kwa sababu ni utaratibu ambao umetoka Ulaya kwamba wakati wa baridi wakoloni walikuwa wanafunga shule na sisi tukarithi kulekule. Muda wa Masika kama tutafunga shule itawasaidia Wazazi kuwa na wanafunzi wao kwenye shughuli za kilimo" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Mtoto afundishwe Elimu ya kujitegemea ya kiuchumi. Uchumi darasa la kwanza. Kinachompeleka mtu kwenda kujiajiri ni faida anayoipata kule. Kinachomfanya Mtoto apende kazi ya kujiajiri na kujitegemea ni faida anayoipata kule" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Kwenye vitabu vyetu tueleze kwamba nikilima Mahindi matano ni sawa na kilo moja ya Mahindi ambayo ni Shilingi 1000 kwa bei ya leo na ndoo moja ya Maji inaweza kumwagilia Mahindi labda 50. Huyu mtoto kichwani anakuwa na akili akiwa bado darasa la kwanza" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Utamzuiaje rushwa mtu kama wewe unamkataza kuelewa namna ya kutafuta hela? Atakapojua namna ya kumwagilia Mahindi wakati wa kiangazi atajua ugumu wa hela, kwahiyo hawezi kununua chocolate ataitunza pesa. Ukikataa atakwenda ataingia kwenye rushwa maana rushwa ndiyo njia rahisi. Lakini kama atakuwa amefundishwa itatusaidia sana darasa la kwanza" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Kwa sisi Mikoa ya Shinyanga na Mwanza, Pamba asilimia 80 hailimwi na wazee wenye familia maana ni kama kazi ya ziada (Extras) ni kama kilaba (Part time). Ifundishwe shuleni, ieleze faida na bei, isije ikasema labda watoto wataharibika" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini