ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 12, 2025

CBE YATEKELEZA MAONI YA BUNGE KWA VITENDO YAJA NA MPANGO HUU......

 NA ALBERT GSENGO/MWANZA

Linapokuja suala la Mitaala na Sera ya Elimu nchini, watanzania wengi hukumbuka fikra na michango yenye tija inayotafsiri uhalisia iliyotolewa Bungeni na Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kibera Kishimba kisha ikachangiwa na waheshimiwa wabunge wengine wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwenye moja ya mahojiano yake yaliyozua maswali mengi na mingi mijadala, Mhe. Kishimba alihoji 'Kwanini vijana wengi wanaomaliza mafunzo ya ufundi wanapoingia kwenye ajira wanakutwa si mafundi?' Hii ikitasfiri kwamba vyuo vingi nchini vimejikita katika utoaji wa mafunzo kwa nadharia na si kwa vitendo. Jeh vyuo vyetu hapa nchini vinakabiliana vipi na changamoto hiyo? Dr. Robert Golan Mashenene ni Mkurugenzi wa Chuo Cha elimu ya Biashara, CBE tawi la Mwanza anakuja na majibu ya yote hayo... MENGINE YALIYOWASILISHWA BUNGENI. "Elimu yetu tumeirithi kutoka Uingereza. Uingereza kama una watoto wanne wanaangalia mshahara wako unaweza kutunza watoto wangapi. Kama un unaweza kutunza watoto wawili hawa wengine wawili Serikali inakusaidia. Sisi huku Tanzania hakuna kitu kama hicho." - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Tunaweza kupeleka mabadiriko Kijijini lakini wananchi wasipokee kama tulivyopeleka kwasababu suala la umasikini hatuliangalii" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Muda wa kufunga shule umetuathiri sana Kijijini kwa sababu ni utaratibu ambao umetoka Ulaya kwamba wakati wa baridi wakoloni walikuwa wanafunga shule na sisi tukarithi kulekule. Muda wa Masika kama tutafunga shule itawasaidia Wazazi kuwa na wanafunzi wao kwenye shughuli za kilimo" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Mtoto afundishwe Elimu ya kujitegemea ya kiuchumi. Uchumi darasa la kwanza. Kinachompeleka mtu kwenda kujiajiri ni faida anayoipata kule. Kinachomfanya Mtoto apende kazi ya kujiajiri na kujitegemea ni faida anayoipata kule" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Kwenye vitabu vyetu tueleze kwamba nikilima Mahindi matano ni sawa na kilo moja ya Mahindi ambayo ni Shilingi 1000 kwa bei ya leo na ndoo moja ya Maji inaweza kumwagilia Mahindi labda 50. Huyu mtoto kichwani anakuwa na akili akiwa bado darasa la kwanza" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Utamzuiaje rushwa mtu kama wewe unamkataza kuelewa namna ya kutafuta hela? Atakapojua namna ya kumwagilia Mahindi wakati wa kiangazi atajua ugumu wa hela, kwahiyo hawezi kununua chocolate ataitunza pesa. Ukikataa atakwenda ataingia kwenye rushwa maana rushwa ndiyo njia rahisi. Lakini kama atakuwa amefundishwa itatusaidia sana darasa la kwanza" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini "Kwa sisi Mikoa ya Shinyanga na Mwanza, Pamba asilimia 80 hailimwi na wazee wenye familia maana ni kama kazi ya ziada (Extras) ni kama kilaba (Part time). Ifundishwe shuleni, ieleze faida na bei, isije ikasema labda watoto wataharibika" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.