ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 14, 2017

KENYA YATAHADHARISHA JUU YA UWEZEKANO WA KUFANYIKAMASHAMBULIZI YA KIGAIDI.


Vyombo vya usalama vya Kenya vimetahadharisha juu ya uwezekano wa kufanyika mashambulizi ya kigaidi nchini humo. 
George Kinoti Msemaji wa Polisi ya Kenya alisema jana usiku kuwa tayari kumesambazwa taarifa kwamba magaidi tisa wanafanya kila linalowezekana kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

Magaidi wamekuwa wakifanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya serikali huko Kenya baada ya kupata pigo mbele wanajeshi wa Kenya. Kundi la kigaidi la al Shabab lenye makao yake Somalia limekuwa likifanya mashambulizi na hujuma mbalimbali katika ardhi ya Kenya; jambo linalowatia wasiwasi viongozi wa serikali ya Kenya.

Shambulio dhidi ya basi la abiria lililofanywa na al Shabab huko Kenya mwaka jana
Aidha wiki iliyopita wanamgambo 15 wa kundi la kigaidi la al Shabab waliuawa katika mapigano na wanajeshi wa Kenya katika eneo la Gedo kusini mwa Somalia. eneo hilo ni eneo la mpaka wa pamoja kati ya nchi mbili hizo.

WAKRISTO WAADHIMISHA IJUMAA KUU LEO.

Dar es Salaam. Ijumaa Kuu huadhimishwa siku moja kabla ya Sikukuu ya Pasaka (kufufuka kwa Yesu),  hivyo leo Wakristo dunia wanaadhimisha siku hiyo.

Pasaka huadhimishwa ikiwa ni kumbukumbu ya mateso ya Yesu, huku viongozi wa dini wakihimiza upendo, msamaha na utu wema.

Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Raymond Saba amesema Ijumaa Kuu ni siku muhimu ambayo waumini wa kanisa hilo wanakumbuka fumbo la ukombozi kupitia mateso ya Yesu Kristo.

Amesema Pasaka inaonyesha jinsi Mungu alivyo na upendo uliomuwezesha kumtoa mwanaye mpendwa Yesu Kristo kuteswa kwa kupigwa, kubebeshwa msalaba, kuvalishwa taji la miba na kutobolewa na mkuki hadi kufa ili kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi .

“Hivyo hakuna Pasaka bila Ijumaa Kuu kwa kuwa hapo ndipo tuliona kilele cha upendo wa Mungu kwa wanadamu, sisi,” amesema

Thursday, April 13, 2017

RAIS MUGABE ABADILISHA DIZAINI YA NYWELE ZAKE.

 Mtindo mpya wa Rais Mugabe akiwa amenyoa nywele

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kwa mara ya kwanza amepigwa picha akiwa amenyoa nyele zake wakati alipohudhuria mazishi ya mwanajeshi wa zamani.

Wengi wanaamini ni mara ya kwanza Mugabe kunyoa nywele zake na hata masharubu.

Picha zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii zimevutia maoni kutoka kwa raia wa Zimbabwe
Baadhi wamesema kuwa mtindo alionyoa umechangia aonekane kijana.

Lakini hata hivyo wengine wanasema kuwa wameshangaa kuwa nia yake ni ipi.

Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila akiwa na kipara.
Labda kubadilisha mtindo wa ni jambo limenza kuiwa na viongozi wa nchi. Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila pia naye alipigwa picha akiwa na mtindo mpya wa nyele nyingi kichwani alipohudhuria wabunge wiki iliyopita.

Rais Kabila akiwa na nywele nyingi

SIJAFA, NINA NGUVU KAMA KIJANA WA MIAKA 20 - DK. MZINDAKAYA.

Dar es Salaam. Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Dk Chris Mzindakaya amesikitishwa na watu wanaovumisha taarifa kuwa amefariki na kuwaita ni wapumbavu.

Akizungumza leo akiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, (JKCI), Mzindakaya amesema afya imeimarika zaidi na ataruhusiwa kuondoka hospitalini hapo wakati wowote.

 Usiku wa kuamkia leo mtandao ya kijamii ilikuwa ikisambaza taarifa potofu za kifo chake.

Baada ya uvumi huo,Dk Mzindakaya alitoa kauli hiyo leo huku akiwahakikishia waandishi kuwa baada ya matibabu, madaktari wamemweleza Afya yake imeimarika mfano wa kijana wa miaka 20.

WATANZANIA 8 WALIOKABILIWA NA KESI YA UJASUSI, WAACHILIWA MALAWI.

WATANZANIA wanane waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ujasusi, nchini Malawi wameachiwa huru jana na sasa wapo njiani kurejea nchini Tanzania .

Hukumu ya kesi yao ilitolewa jana jioni tarehe 12 mwezi Aprili mwaka huu,Watanzania hao waliokuwa wanashikiliwa katika Gereza Kuu la Mzuzu nchini Malawi kwa tuhuma za kuingia kinyume cha sheria katika mgodi wa urani uliopo eneo liitwalo Kayerekera.

Serikali ya Tanzania ilikataa kwamba Watanzania hao walitumwa na serikali ili kufanya shughuli za kijasusi katika mgodi huo wa urani. Tanzania iliongeza kwamba watu hao walikuwa ni wafanyakazi wa Taasisi ya misaada ya Caritas iliyo chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Songea mkoani Ruvuma.

Wakili aliyekuwa anaisimamia kesi hiyo ,Flaviana Charles ameiambia BBC kuwa watu hao kwa sasa wako huru pamoja na kuwa wamepitia katika magumu mengi na ya kukatisha tamaa lakini kila kitu kilikuwa wazi na upande wa walalamikaji hawakuwa na ushaidi wa kutosha wa kuwafunga kwa kuwa watanzania hao waliingia nchini humo kihalali kuanzia mpakani na walikuwa na mualiko na wakati wanawakamata walikuwa hawajafika mgodini bado maana walikamatwa wakiwa wanatoka hotelini hivyo hawakufika mgodini au kuhoji mtu yeyote hivyo shutuma zao zilikuwa zenye mashaka sana.

Je,kuna fidia ambayo wamelipwa baada ya kuwekwa kizuzini tangu mwezi desemba mwaka jana?
Wakili Flaviana amesema kuwa kuna ujanja ambao mahakama imeutumia ili kukwepa fidia kwa kudai kuwa ambayo wameshatumikia kifungo kwa kipindi hicho chote watuhumiwa hao walipokuwa kizuizini hivyo kwa sasa wako huru.

BBC imezungumza pia na baadhi ya watu hao waliokuwa wanatuhumiwa,,wanasema wana furaha sana maana walikuwa wameenda Malawi kwa matarajio ya kukaaa siku 3 lakini sasa wamejikuta wamekaa zaidi ya miezi mitatu,bila kujua kinachoendelea katika familia zao pamoja na shughuli zao za kila siku

wamesema walikuwa wakiteseka bila sababu ilhali nia yao kwenda Malawi ilikuwa njema kabisa .
Watanzania hao nane,wanashukuru sana serikali yao ya Tanzania haswa kwa balozi kufika kuwaona.

Wednesday, April 12, 2017

GOLIKIPA WA MBAO FC APONZWA NA SIMBA.

Uongozi wa Mbao FC umebaini utovu wa nidhamu ulikithiri katika kikosi chao wakati wa mchezo dhidi ya Simba uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwanzoni mwa juma hili.

Afisa habari wa Mbao FC Crinstant Malinzi amesema baada ya kikao cha viongozi kilichoketi jana, wamebaini suala hilo na tayari wameanza kuchukua hatua za kinidhamu kwa kumsimamisha mlinda mlango wao Erick Ngwegwe.


“Kweli kikao kilichofanyika jana na leo kimefikia mwafaka wa kumsimamisha mchezaji golikipa wetu aliyedaka kwenye mechi dhidi ya Simba Erick Ngwegwe kwa muda usiojulikana kwa kile kinachoashiria kwa namna moja au nyingine kuwa ni upangaji wa matokeo ili kupisha uchunguzi wa kamati zinazohusika na mambo hayo na kutuletea taarifa kamili kws ajili ya kufanya maamuzi. Kwa hiyo kwa sasa Ngwegwe ameondolewa kambini wakati timu inajiandaa na mechi dhidi ya Tanzania Prisons siku ya Jumapili,” amesema Malinzi wakati akithibitisha kusimamishwa kwa Ngwegwe.


“Mwenyewe anasema ni makosa ya kimchezo, lakini kwa dondoo za awali tulizozipata tumeona kuna viashiria vya utovu wa nidhamu wa makusudi uliopelekea matokeo kuwa vile. Kwa hiyo kwakua tunaendelea na uchunguzi, tumeamua tumuondoe kabisa kambini ili tusiharibu uchunguzi wakati bado tunaendelea na maandalizi ya meche zetu.”

 
Tuhuma hizi zomemuangukia golikipa pekeake hakuna mchezaji mwingine tuliyembaini hadi sasa kutokana na uchunguzi wa awali tulioufanya. Ikithibitika rungu zito litamuangukia kutoka katika klabu ya Mbao lakini kama hatakuwa na hatia basi atarejeshwa kwenye klabu hapo baadae.”
“Kuna rushwa za aina nyingi, kuna kuipendelea timu bila kupewa chochote wala kushawishiwa lakini inawezekana mchezaji akawa na mapenzi na timu fulani na anataka ipate matokeo mazuri. Unapocheza na hizi timu zinakua na mambo mengi sana zinakua kama zimeuteka mpira wa Tanzania.”


“Hatujamfukuza tumemsimamisha kupisha uchunguzi ili tuweze kubaini nini kilifanyika, baada ya hapo tutatoa ripoti yetu.”


Ngwegwe anatuhumiwa kuifungisha timu yake (Mbao FC) wakati ikicheza na Simba na kupoteza kwa kufungwa magoli 3-2. Mbao FC ilifunga magoli yake mawili kipindi cha kwanza na iliongoza hadi dakika 82 na Simba kuanza kurudisha.


Golikipa huyo mrefu anahusishwa na kuchukua kitu kidogo ili kuipa Simba ushindi. Goli linalolalamikiwa zaidi ni lile ambalo alushindwa kuudhibiti mpira na kusababisha mshambuliaji wa Simba Frederick Blagnon kufunga kwa urahisi.

BAADHI YA MATUKIO YALIYOJIRI KATIKA UZINDUZI WA RELI YA KISASA PUGU JIJINI DAR ES SALAAM


Sehemu ya hotuba ya Rais Magufuli kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa  wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa Pugu jijini Dar es Salaam.
 
Kauli ya Rais Magufuli kuhusu ufisadi nchini, kuzuia usafirishaji wa mchanga wa dhahabu, suala la kulinda amani ya nchi, na uchapakazi kwa kila mtu, kazi kwanza siasa baadae.

VIDEO ZA MAGOLI YOTE YA JUVENTUS Vs BARCELONA 3-0 UEFA 2017.


Barcelona imechabangwa magoli matatu kwa sufuri na Juventus katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.

Paulo Dybala alifunga magoli mawili katika dakika ya 7 na ya 22. Bao la tatu lilifungwa na Giorgio Chiellini katika dakika ya 55.

Barcelona walicheza kufa na kupona kujaribu kupata japo bao moja la ugenini lakini hawakuweza kufua dafu.

BUNGE:- MALIPO YA FIDIA KWA WAKAZI WA KATOMA GEITA.

Ni lini mgodi wa GGM utawalipa fidia wakazi wa Katoma Geita? 

Hapa naibu waziri nishati na madini anatoa ufafanuzi.

TANZANIA YA VIWANDA: BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO KUSAIDIA AZMA YA SERIKALI

 Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB. 

Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB.

 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto) akimuangalia Mkuu wa Huduma za Kisheria wa TADB, Bibi Neema Christina John (Katikati) wakati akiendelea na zoezi la ugongaji wa mihuri Mikataba ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.

Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano (Kushoto) akibadilishana Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia).

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB.
 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (Katikati) akizungumza na Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kulia). Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto).

TANZANIA YA VIWANDA: BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO KUSAIDIA AZMA YA SERIKALI
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kusaidia azma ya serikali katika kujenga Tanzania ya viwanda kwa kusaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda nchini kwa kutoa mikopo nafuu kwa wakulima nchini.

Azma hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila wakati wa utiaji saini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na Benki hiyo katika hafla iliyofanyika Ofini kwa Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.
Bibi Kurwijila amesema kwamba TADB itakeleza kwa vitendo juhudi za Serikali za Kujenga Uchumi wa Viwanda kwa kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo, mifugo, samaki na misitu ili kuongeza tija ya kilimo hivyo kutoa malighafi kwa viwanda nchini.

Benki imepitia upya mpango mkakati wake katika kutoa mikopo ili kuwezesha kufikia wakopaji wengi zaidi ili kuweza kufikia lengo la kuleta maendeleo katika sekta ya kilimo hasa katika kuongeza tija ya kilimo hivyo kutoa malighafi kwa viwanda nchini,” alisema Bibi Kurwijila.

Bibi Kurwijila ameongeza kuwa katika kuchagiza malengo hayo, TADB imejpanga katika Kushirikiana na wadau mbalimbali kufanya upembuzi wa miradi ya Maendeleo ya Kilimo na Umwagiliaji nchi nzima ili kubaini mahitaji halisi ya fedha na pia kusaidi kupanga maeneo ya vipaumbele ili kuanza kutoa mikopo hasa kwa utaratibu mahsusi. 

Ametaja malengo mengine ya kimkakati ya TADB ni pamoja na kuboresha huduma kwa kuanzisha mazao maalum ya huduma za kibenki kwa wakulima wadogowadogo kulingana na mnyororo husika wa thamani na pia kuanza huduma za Zaidi kupitia taasisi za fedha zilizopo (wholesale lending and Refinancing) ili kufikia wakulima wengi zaidi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa mpaka sasa Benki imefanikiwa kukopesha jumla ya shilling bilioni 6.5 kwa vikundi 20 vyenye jumla ya wakulima 2575.

Bw. Assenga ameongeza kuwa Benki imeweza kuvijengea uwezo vikundi 336 vya wakulima wadogowadogo vyenye jumla wa wanachama 44,400 katika mikoa ya Iringa, Morogoro na Tanga.
“Kupitia mafunzo hayo TADB imewezesha jumla ya vikundi 19 kutimiza masharti na maandalizi ya msingi ya kuweza kukopa; Vikundi vingine vilivyobaki vinaendelea kupatiwa mafunzo ili viweze kufikia hali ya kuweza kukopesheka,” ameongeza. 

Kwa mujibu wa Bw. Assenga, TADB imeweza kuinua idadi ya wakulima watumiao mabenki na vyombo vya fedha wapatao 2,359 ambao kati yao wanawake ni 863 sawa na asilimia 36.6 ya wanufaika.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano alisema taasisi za umma zina wajibu wa kuisaidia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali ili kuleta maendeleo endelevu nchini.

STAR WA SA ALIYEKUWA NA TATTIZO LA KUKUA HARAKA Ontlametse Phalatse AFARIKI DUNIA.

 STAR wa nchini Afrika Kusini aliyekuwa akipendwa kutokana na kuwa mwenye furaha licha ya tatizo la kukua haraka alilokuwa nalo, Ontlametse Phalatse amefariki dunia.

Amefariki jana usiku kwenye hospitali ya Dr George Mukhari Academic huko Ga-Rankuwa, Pretoria. Phalatse aliyekuwa na miaka 18, alikuwa mmoja kati ya wasichana wawili tu nchini humo wenye tatizo hilo nadra liitwalo Progeria.
Awali madaktari wake walitabiri kuwa angekuwa hadi akifikisha miaka 14 tu. Mwezi uliopita Rais Jacob Zuma alitimiza ndoto ya msichana huyo kuonana naye.

Taarifa ya familia yake imesema: It is with great sadness to inform you of the passing of our first lady, Ontlametse Ntlami Phalatse. Our hearts are filled with pain and sadness but Ontlametse — as we know her — would want us to carry on with her courageous spirit.”

Alikuwa maarufu sana Instagram ambako alikuwa na followers 63.6k.

MSANII IZZO BUSINESS ATUMBUIZA KWENYE ONYESHO LA COCA-COLA NDANI YA MKOA WA MBEYA

 
Msani Izzo Business akiwa kwenye jukwaa la Coca-Cola kutoa burudani kwa wakazi wa Mbeya. Burudani hiyo ilitolewa katika uwanja wa Nzovwe, mjini Mbeya.

MAGAZETI YA LEO:- WABUNGE CCM WAJILIPUA, RIPOTIYA BENKI KUU YA DUNIA YAIPAISHA TZ, ARSENAL RASMI MTAA WA 6, BARCA HOI.


Ripoti ya benki kuu ya dunia yaipaisha Tanzania, Wabunge CCM wajilipua, TAKUKURU yakabidhi ripoti kwa rais Magufuli,  Barca hoi.
 
Mtikisiko Bungeni, Sakata la dawa za kulevya: Marekani yaweka hadharani Mtanzania alivyozisambaza, Arsenal rasmi mtaa wa 6. Habarika na dondoo hizi za magazeti ya leo hapa.

JARIBIO LA MGOMO WA WALIMU NEEMA KWA 25

NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza

HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza, imewalipa Walimu 25 waastafu stahiki zao Kabla ya   msululu wa kundi hilo kujazana kwenye ofisi za Mkurugenzi  Kiomoni Kibamba kufuatia maandamano yaliyokuwa yamepangwa  kupiga kambi wakidai malipo yao.

Akizungumza na waandishi  wa habari jana Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Nyamagana, Sibora Kisheri  amesema baada ya maazimio ya kikao chao na kuwasilisha taarifa kwa mwajiri wao na kuanza  kuchukuliwa  hatua  za haraka jambo ambalo limewafanya kusitisha mpango wa kuandamana na  kuweka kambi katika ofisi za mkurugenzi wa jiji hilo ili kulipwa stahiki zao.

Walimu hao   walikuwa wamejindaa kuweka  kambi isiyo na kikomo huku wakisisitiza kutoogopa kupigwa mabomu na polisi hadi watakapolipwa stahiki zao baada ya kufikia maamuzi yaliyoamuliwa hivi karibuni kwenye hafla ya kuwaaga Walimu 25 na kuwapatia zawadi ya  mabati 20 na Sh 20,000 kama nauli ambapo walilalamikia kitendo cha mwajiri wao kushindwa kuwalipa stahiki zao kwa muda muafaka jambo ambalo linaloendelea kuchochea maisha kuwa  magumu.

“Mpaka sasa walimu wastaafu 25, wameitwa na mkurugenzi na kulipwa nauli zao, pia walimu waliokuwa wamehamishwa vituo kati ya  mwaka 2016 hadi Machi mwaka huu wameanza kulipwa na taarifa nilizopewa  ni kwamba wamelipwa walimu 30 na zoezi linaendelea”amesema Kisheri.

Amesema  zoezi hilo linakwenda sambamba na walimu  waliokwenda likizo na kushindwa kulipwa ambapo deni lilifikia Sh milioni 205.75, na kwamba  wameanza kulipwa , huku  walimu wastaafu  Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wamekujasha chukua majina ya wastaafu ili kuingizwa katika malipo ya kila mwezi kulingana na asilimia ya mshahara wao.

“Kwa hatua zilizochukuliwa na mwajiri pamoja na PSPS wameona hakuna haja tena ya kuendelea na mpango waliokuwa wameazimia kwa lengo la kulipwa stahiki zao ambapo aliiomba Serikali kuacha  tabia ya kutotekeleza wajibu wao mpaka  shinikizo la watumishi”amesema Kisheri.
 Amesema  imekuwa mazoea kwa serikali kutekeleza madai ya walimu pale wanapotangaza mgogoro  huku akihoji wapi fedha zilipotoka na kuanza kuwalipa  wakati awali Mkurugenzi wa jiji hilo, Kibamba alidai hana fedha.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake wastaafu, Eliamin Msangi, ameeleza  hivi sasa waastafu wamekuwa wakiona jambo la  kustaafu ni kama janga kwao kutokana na kile waajiri wao hushindwa kutekeleza licha ya   kuwa hatua hiyo ni muhimu  kwani kipindi hicho ni cha kupumzika na kubaki mshauri kwa wafanyakazi waliobaki kwenye utumishi.

“Unapostaafu tu mshahara unakoma mara moja, leo tunapozungumza hapa baadhi yetu tumekuwa kero kwenye nyumba za walimu tunaambiwa tuondoke ili mwalimu mwingine aingie, sisi wastaafu wa mwaka jana tumeathiriwa sana na zoezi la uhakiki wa  vyeti na  watumishi hewa kwani hesabu zetu zimepigwa kwa madaraja ya chini” amesema Msangi.

Tuesday, April 11, 2017

*MASHABIKI WA SIMBA WASHUTUMIWA KWA UHARIBIFU UWANJA WA CCM KIRUMBA MECHI DHIDI YA MBAO FC TAREHE 10.04.2017*

*TAARIFA YA UHARIBIFU WA UWANJA WA CCM KIRUMBA KWENYE MECHI YA MBAO FC VS SIMBA SC TAREHE 10.04.2017*

Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba, kupitia Meneja wa Uwanja Ndg *Steven E. Shija* unapenda kutoa taarifa za uharibifu wa Uwanja.

Mechi iliyochezwa Tarehe 10.04.2017, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kati ya Mbao Fc Vs Simba Sc umesababisha uharibifu Mkubwa kwenye Maeneo ya kuingilia Wachezaji, Waamuzi na Geti Namba 4 ambapo walikuwa wamekaa Mashabiki wa Simba

Uharibifu huo umetokana na Mashabiki wa Timu ya Simba Sc kupanda Juu ya maeneo ya Kivuli yaliyojengwa kwenye maeneo yaliyotajwa ( Vyumba vya Kubadirishia Nguo kwa wachezaji, Waamuzi na Geti namba Nne), uharibifu huo umepelekea kushindwa kufunga Milango ya Mbele ambapo ni hatari kwa usalama wa maeneo hayo muhimu

Hivyo uongozi wa Uwanja umeishazitaarifu Mamlaka husika ili zichukue hatua kwa Wanaohusika ili kuhakikisha eneo hilo linatengenezwa mapema kabla ya Mechi ya Toto African Vs Simba Sc Tarehe 15.04.2017


*Imetolewa:-*
*Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba - Mwanza*
*11.04.2017*

MLIPUKO WASABABISHA KUAHIRISHWA MCHEZO WA BORUSSIA DORTMUND Vs MONACO.

Mchezo kati ya Borussia Dortmund's kupata timu zitakazoingia robo fainali ya UEFA Champions dhidi ya AS Monaco umeahirishwa baada ya mlipuko kutokea been at the home side's team bus has seen BVB defender Marc Bartra taken to hospital with injuries. ​Bild report that the incident occurred just 10km from the club's stadium, and the club have since confirmed on Twitter that the game will be postponed until Wednesday at 18:45 local time (17:45UK)

Mchezo huu wa  Borussia Dortmund dhidi ya Monaco ambao umeahirishwa baada ya basi ya Dortmund kushambuliwa utapangwa tena kufuata ratiba ya UEFA. Ingawa mchezo wa marudiano ni wiki ijayo kama kawa.

MAKAMPUNI YA SIMU YAUNGANA KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA

Meneja wa Airtel Money kutoka kampuni ya Airtel Tanzania Moses Alphonce akitoa elimu kwa mmoja wa watumiaji wamitandano ya simu kwa namna Makampuni ya simu za mikononi nchini yameungana kwa kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha kwenda mitandao yeyeto nchini kwa kiwango cha gharama ile ile.

Makampuni ya simu za mikononi nchini yameungana kwa kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha kwenda mitandao yeyeto nchini kwa kiwango cha gharama ile ile. 

Kwenye muungano huo ambao unaitwa Taifa Moja, makampuni matatu makubwa ya kutoa huduma za simu za mkononi ya Tigo Tanzania, Airtel Tanzania na Zantel, wateja wanaweza kutuma pesa na kupokea kutoka kwenye moja ya mitandao hiyo kwa gharama zile zile.

 Hapo awali, kutuma pesa au kupokea pesa kutoka mtandao tofauti mteja alikuwa akipokea ujumbe mfupi ambao ilikuwa ni lazima apeleke kwa wakala wa mtandao ambao amepokea fedha kutoka na ilikuwa izizidi siku saba tofauti na hapo fedha hiyo ilikuwa inarudi kwa aliyetuma. 

Kwa huduma hii, mteja anapaswa kuchangia huduma ya kutuma pesa kutoka kwa menu ya kawaida, halafu anachangua kutuma pesa kwenda mitando mingine. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kutembelea watumiaji wa huduma za kutuma na kupokea pesa, Meneja wa Airtel Money kutoka kampuni ya Airtel Tanzania Moses Alphonce alisema kupitia muungano wa Taifa Moja wameweza kuwafanya wateja wapate njia rahisi ya kutuma na kupokea fedha.

Tunajua hapo zamani kuna baadhi ya wateja walikuwa wanapata wakati mgumu linapokuja suala la kutuma na kupokea fedha. Ilikuwa aidha upokee fedha kwa ujumbe mfupi au uwe na laini ya simu zaidi ya moja. Ukipokea fedha kwa ujumbe na kwa bahati mbaya ukaufuta ilikuwa inamaanisha fedha imepotea, alisema Alphonce. 

Lakini vile vile si kila mtu anayepokea fedha kupitia simu ya mkononi anahitataji kutoa. Wengine wanataka kulipia huduma mbali mbali kupitia huduma ya simu kama kulipia maji, kununua umeme au matumizi mengineyo. Kwa huduma hii mpya ya Taifa Moja imekuwa ni njia rahisi kwa wateja wetu, aliongeza Alphonce 

Kupitia huduma hii ya kutuma pesa na kupokea kutoka mitandao yeyote itachangia kuongeza idadi ya watu wanaotumia huduma za kutuma na kupokea fedha kwa kutumia simu za mkononi na pia kuongeza faida kwa makampuni ya simu. 

Hii ni mara ya kwanza Tanzania kwa makampuni ya simu kuungana pamoja kwa huduma ya pamoja. Hata hivyo, Taifa Moja sio huduma au mtandao mpya mbali ni njia ambayo imepewa promosheni hii ya kutuma na kupokea fedha kutoka mtandao wowote. 

Kwa upande wake, Mkuu wa usambazaji mkoa wa Dar es Salaam kutoka kampuni ya Tigo Tanzania Lloyd Kaaya. alisema ni furaha kwao kuona kwamba wateja wa simu za mkononi kwa sasa hivi anaweza kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao wowote kwa gharama zile zile. Hii inaamanisha matumizi wa kutuma pesa yataongeza na yatakuwa na manufaa kwa upande wetu, alisema Kaaya.