NA ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza
HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza, imewalipa Walimu 25 waastafu
stahiki zao Kabla ya msululu wa kundi hilo kujazana kwenye ofisi za
Mkurugenzi Kiomoni Kibamba kufuatia
maandamano yaliyokuwa yamepangwa kupiga
kambi wakidai malipo yao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu
Tanzania (CWT) Wilaya ya Nyamagana, Sibora Kisheri amesema baada ya maazimio ya kikao chao na kuwasilisha
taarifa kwa mwajiri wao na kuanza kuchukuliwa hatua za haraka jambo ambalo limewafanya kusitisha
mpango wa kuandamana na kuweka kambi
katika ofisi za mkurugenzi wa jiji hilo ili kulipwa stahiki zao.
Walimu hao walikuwa wamejindaa kuweka kambi isiyo na kikomo huku wakisisitiza
kutoogopa kupigwa mabomu na polisi hadi watakapolipwa stahiki zao baada ya
kufikia maamuzi yaliyoamuliwa hivi karibuni kwenye hafla ya kuwaaga Walimu 25
na kuwapatia zawadi ya mabati 20 na Sh
20,000 kama nauli ambapo walilalamikia kitendo cha mwajiri wao kushindwa
kuwalipa stahiki zao kwa muda muafaka jambo ambalo linaloendelea kuchochea
maisha kuwa magumu.
“Mpaka sasa walimu
wastaafu 25, wameitwa na mkurugenzi na kulipwa nauli zao, pia walimu waliokuwa
wamehamishwa vituo kati ya mwaka 2016
hadi Machi mwaka huu wameanza kulipwa na taarifa nilizopewa ni kwamba wamelipwa walimu 30 na zoezi
linaendelea”amesema Kisheri.
Amesema
zoezi hilo linakwenda
sambamba na walimu waliokwenda likizo na
kushindwa kulipwa ambapo deni lilifikia Sh milioni 205.75, na kwamba
wameanza kulipwa , huku walimu wastaafu Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma
(PSPF) wamekujasha chukua majina ya wastaafu ili kuingizwa katika malipo
ya
kila mwezi kulingana na asilimia ya mshahara wao.
“Kwa
hatua zilizochukuliwa na mwajiri pamoja na PSPS wameona
hakuna haja tena ya kuendelea na mpango waliokuwa wameazimia kwa lengo
la
kulipwa stahiki zao ambapo aliiomba Serikali kuacha tabia ya
kutotekeleza wajibu wao mpaka shinikizo la watumishi”amesema Kisheri.
Amesema imekuwa mazoea kwa serikali kutekeleza madai
ya walimu pale wanapotangaza mgogoro
huku akihoji wapi fedha zilipotoka na kuanza kuwalipa wakati awali Mkurugenzi wa jiji hilo, Kibamba
alidai hana fedha.
Akizungumza
kwa niaba ya walimu wenzake wastaafu, Eliamin
Msangi, ameeleza hivi sasa waastafu wamekuwa
wakiona jambo la kustaafu ni kama janga
kwao kutokana na kile waajiri wao hushindwa kutekeleza licha ya kuwa
hatua hiyo ni muhimu kwani kipindi hicho ni cha kupumzika na
kubaki mshauri kwa wafanyakazi waliobaki kwenye utumishi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.