ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 5, 2011

ZANTEL'S EPIC NATION CONCERT MWANZA

Bob Jurnior.

Roma

P Unity toka Kenya.

Fid Q

Suma Lee Hakunaga.

NYANI MZEE ATUNUKIWA NONDO......!!

Mtangazaji wa Clouds Fm 88.4 katika kipindi cha Power Breakfast (wa pili kulia) akichangia furaha pamoja na wapiganaji wenzake mara baada ya kupata nondoz ya Mass Communication kutoka katika chuo cha Tumaini, Dar es Salaam. Mahafari yalifanyika ijumaa Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA INJILI KUFANYIKA JIJINI MWANZA JUMAPILI HII

Kutoka kushoto ni Humphrey Maziba ambaye ni mratibu wa tamasha hilo, Mwimbaji muziki wa injili John lissu na Adolph Nzwala wa HHC Radio Mwanza.
TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA INJILI LINALOJULIKANA KAMA YEHOVA YU HAI PRAISE AND WORSHIP TOUR, LINATARAJI KUFANYIKA KESHO JUMAPILI KATIKA UKUMBI WA GOLD CREST HOTEL JIJINI MWANZA

TAMASHA HILO LENYE KUSHIRIKISHA VIJANA WA RIKA MBALIMBALI NA VIPAJI TOFAUTI SAFARI HII LINAKUJA LIKIWA NA NIA YA KUWAAMSHA VIJANA WAIMBAJI WA MUZIKI WA KUMTUKUZA MUNGU KUTUMIA VIPAJI VYAO KUISAIDIA NCHI KATIKA HARAKATI ZA UTOAJI ELIMU MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA KUIASA JAMII KUACHANA NA MADAWA YA KULEVYA, ELIMU YA UKIMWI NA NAMNA YA KUISHI KWA PAMOJA..WAIMBAJI MBALIMBALI KUTUMBUIZA KWENYE TAMASHA HILO LA KUMSHUKURU MUNGU KWA MIAKA 50 YA UHURU NA KWA AJILI YA MIAKA MINGINE 50 IJAYO, LITAKALOONGOZWA NA MWIMBAJI MAHIRI MUZIKI WA INJILI NCHINI TANZANIA JOHN LISU, WENGINE WAKIWA NI HUIMA BAND, REVIVAL GOSPEL NA HOSSANA PRAISE AND WORSHIP TEAM AMBAO WOTE WATAIMBA LIVE.

KIINGILIO NI SHILINGI 10,OOO/= TU
NTOTE MNAKARIBISHWA

Friday, November 4, 2011

MAFUNZO YA TACAIDS KWA WAANDAAJI NA WATANGAZAJI YAMALIZIKA LEO MWANZA

Watoa mada Glory Mziray na Richard Ngaiza wakifuatilia hatua ya mwisho ya mafunzo hayo ya siku mbili inayohusu Kubainisha changamoto zinazo ikabili sekta ya upashaji habari kwa vipindi vya elimu ya Ukimwi kwa redio, kwenye semina hiyo inayotolewa na TACAIDS.

Kwa siku ya leo washiriki walijigawa kwa makundi kulingana na mikoa kukusanya changamoto zao na kuzipima ambapo baadaye waliziwasilisha zikiwa na either utatuzi au ushauri. Pichani washiriki kutoka mkoani Shinyanga.

Washiriki wa redio mbalimbali za kijamii kutoka jiji linalokuwa kwa kasi, uchumi wake ukiendeshwa na biashara kubwa ya samaki na spidi kali ya ongezeko la watu Mwanza, Uzoefu unaonyesha kuwa mwingiliano wa watu kutoka sehemu na sehemu ni chanzo cha ongezeko la maambukizi ya ukimwi.

Mara ni miongoni mwa mikoa yenye makabila mengi nchini Tanzania, mila inachukuwa nafasi kwenye maisha ya wakazi wa maeneo hayo na kuegemewa na wengi, takwimu zinaonyesha kuwa baadhi ya mila zilizopo zinahusika katika kuchangia maambukizi.

Mkoani Kagera ambako inasemekana kwa upande wa Tz ndipo ulipoanzia, takwimu zinaonyesha ugonjwa huo unazidi kupungua kiasi cha asilimia 3.4 lakini kuna tabia na mienendo inayoonyesha kuwa hali ya baadaye itakuwa mbaya iwapo hatua za dhati hazitochukuliwa.

Kwa mwingiliano wa kibiashara na wakimbizi mipakani mwa nchi nako hali si shwari maambukizi ni ya kasi watu wakiamini hadithi za mitaani zaidi kutokana na uhaba wa elimu stahiki kuhusu Ukwimwi, by washiriki toka Radio Ekwizera.

Uwasilishaji pia ulikuwa na kipengere cha Je! Tunapimaje Mwitikio wa wasikilizaji aka Je! Tunasikilizwa na Tutatambuaje kama vipindi vya ukimwi virushwavyo na kituo husika vinasikilizwa na vinamanufaa kwa jamii??

Produser maarufu hapa nchini Duke, alikuwa bize katika meza yake akikusanya sauti ya yote yaliyokuwa yakijiri kwenye mafunzo hayo toka Tume ya kuthibiti ukimwi nchini (TACAIDS) chini ya usimamizi thabiti wa Kampuni ya Masoko AGENCIES (T)Ltd.

BREAKING NEWS: MAJAMBAZI WATANO WENYE SILAHA WAUAWA KATIKATI YA JIJI LA MWANZA

Mafisa wa jeshi la polisi katika tukio.
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kuwaua majambazi watano waliokuwa na silaha hatari za moto wakiwa katika harakati za kufanya uporaji kwenye moja ya maduka ya vifaa vya ujenzi yaliyopo mtaa wa Nyerere jijini Mwanza.Mtaa wa Liberty
Tukio hilo lilitokea Leo majira ya saa 3:30 asubuhi, katika duka la uuzaji wa vifaa vya ujenzi la mfanyabiashara mtanzania mwenye asili ya kiasia aliyejulikana kwa jina moja tu la Mukesh.

Majambazi hayo yaliyokuwa na silaha yalipovamia duka hilo na kukuta kiasi kidogo cha fedha cha shilingi elfu sitini ikiwa ni tofauti na matarajio yao (kukuta kiasi kikubwa cha fedha), yalishikwa na taharuki na kuanza mabishano kiasi cha kutoa mwanya kwa jeshi la polisi kuzunguka eneo la tukio na kuanza mapambano.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Liberatus Barow amesema kuwa mapambano hayo ya silaha yaliyodumu kwa muda wa dakika kumi jeshi lake limefanikiwa kuwauwa majambazi wote watano huku ikiripotiwa kuwa hakuna mwananchi yeyote aliyepoteza maisha.
Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la tukio.
Taarifa zinasema kuwa majambazi mawili kati ya matano yaliyouawa yamejulikana mmoja akiwa raia wa Burundi na mwingine akijulikana kwa jina la Maulid Said raia wa Tanzania.

Maulid Said ambaye ni jambazi sugu anahusishwa na matukio mbalimbali kanda ya ziwa likiwemo lile la mwaka 2009 lililotokea mtaa wa Liberty na kisha baadaye Nyegezi katika gesti ya Pambazuko ambapo jambazi hilo lilimpa majeraha ya risasi Koplo Shahban na kutokomea kusikojulikana.

MANUNUZI MBALIMBALI KUFANYIKA KATIKA SWAHILI FASHION WEEK 2011

Kama utapenda kununua au kuuza kitu chochote kutoka Swahili Fashion Week, unaweza kufanya hivyo kupitia eneo la manunuzi wakati na baada ya maonesho,

KWAHIYO KAMA UTAPENDA KUPATA NAFASI YA KUUZA VITU WAKATI WA MAONESHO YA SWAHILI FASHION WEEK TAFADHALI HIFADHI NA TENGENEZA ENEO LAKO SASA.

Kwa maelezo zaidi piga kwa:
Hamis K Omary
0719252628
0787747918

MDAU ABEL NGAIZA, KUSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUMKUMBUKA MAMA YAKE MPENDWA

Abel Ngaiza.

Hi G. Sengo! ' hope ur doing fine all with ur family, I would like to announce my birthday in your blog.

Name: Abel P. Ngaiza
Birth date: 05.11.19..? so nina miongo kadhaaa babuu.
The birthday party will go through with fifteen years (15)memorial since our lovely mother Mama GEORGIA KOKUSIMA NGAIZA passed away.

Anakumbukwa na watoto wake wapendwa Abel (mie), Paul, Pamela, Penina, Prisca na Hadia Saif, pamoja na wajukuu zake wapendwa Jane ,Carlos, Collin's, Carllen,Clara & Hope.
May God rest you in peace mom!


Finger crossed!!
Best regards,
Abel Ngaiza

Thursday, November 3, 2011

BONDIA ALLAN KAMOTE KUMVAA MKENYA J.PILI

Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania , Yasin Abdallah , amesema novemba 6 mwaka huu bondia machachali kutoka Tanga Allan Kamote atapambana na bondia Fredrick Nyakesa kutoka kenya katika mpambano wa kimataifa wa kirafiki utakaofanyika katika ukumbi wa Ridoch mkoa wa Tanga na mabondia hawo watapambana katika pambano la raundi 8 la uzito wa kilogram 61.2 light weigth yasin alisema kutakua na mapambano ya utangulizi mengine yatakayowakutanisha mabondia kutoka tanga na Dar es salaam

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

"Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi" alisema Super D

WAANDAAJI WA VIPINDI NA WATANGAZAJI WA REDIO ZA KIJAMII KANDA YA ZIWA WAKABIDHIWA NYENZO NA TACAIDS KUIELIMISHA JAMII KUHUSU UKIMWI

Washiriki mafunzo.
Mafunzo ya kujengewa uwezo kwa watangazaji na waandaaji wa vipindi vya redio za kijamii yaliyoandaliwa na TACAIDS kupitia Kampuni ya Agencies (T)ltd, kwa Kanda ya Ziwa yamefanyika leo katika hotel ya Victoria Palace jijini Mwanza na kuhudhuriwa na washiriki wa vituo mbalimbali. "Ngono za wapenzi wengi na ngono za biashara zinazidi kubarikiwa na jamii kwa kupewa majina mengi mazuri kama kuhalalishwa, kama Shuga Dadi, Shuga Mami, Kibustani...." Glory Mziray:-public Relations Officer TACAIDS.

"Redio za jamii zikitumika vyema zina nguvu kufanikisha vita dhidi ya maambukizi ya Ukimwi" Richard Ngaiza:- Communication and Media Expert, Lecturer in New Media Technologies (Tumaini university Dar es Salaam College)

Washiriki wa mafunzo hayo yaliyoanza leo na kutarajiwa kumalizika kesho, wa kwanza kabisa kushoto ni Ester Tindos Kusekwa toka Living Water Fm Mwanza.

Washiriki Emanuel Chibasa wa Victoria Fm, John D. Mponeja Victoria Fm na Ally Mwafrika wa Kahama Fm.

"Ubunifu na Lugha kwa mtayarishaji na mtangazaji ni muhimu katika ufikishaji wa ujumbe na elimu kuhusu suala zima la kujilinda na kupambana na maambukizi ya Ukimwi" Richard Ngaiza.

Ndani ya mafunzo kushoto ni Maganga J. Gwesanga(Living Water Fm), Caroryne Mwaipungu (HHC Alive Fm) na Helen (Living Water Fm).

Edwin Sokwe, Cecilia Ndabigize na wengine...
Matumizi ya Kondom:
ACording to the 2007/8 THMIS: Among women who reported having higher risk sex in the past 12 months, 43% used condom during the last act

Among men who reported having higher risk sex in the past 12 months, 53% used a condom during the last act

This levels were higher amon younger respondents Of the men ages 15-49 who paid for sex in the past 12 mont, 60% used a condom.

SANGARA WACHANGA 900 WAKAMATWA WAKITINGA KIWANDANI

Kikosi cha doria cha Idara ya Uvuvi mkoani Mwanza, kimekamata zaidi ya samaki wachanga 900 aina ya Sangara kwenye gati la kufikishia samaki katika kKiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha Vicfish kilichojengwa kandokando ya ufukwe wa Ziwa Victoria jijini Mwanza.

Samaki hao ambao uzito wao haukufahamika mara moja wamekamatwa muda mfupi nbaada ya boti ya wakala anayesambazia kiwanda hicho samaki kutia nanga kwenye gati hilo.

Mkuu wa Kikosi cha Doria cha Idara ya Uvuvi mkoani Mwanza, Juma Makongoro pamoja naye Bwana Lukanga ambaye ni Mkuu wa Maabara ya Ubora wa Samaki iliyopo Nyegezi wamethibitisha kukamatwa kwa samaki hao wachanga kwenye gati la kufikishia samaki kiwandani hapo ambapo wanaaminika kuwa walikuwa ni kwaajili ya kuchakatwa.

Lukanga amesema kuwa samaki hao wamekamatwa kutokana na taarifa kutoka kwa raia wema kwamba kulikuwa na boti ambayo ilikuwa ikitoka kwenye moja wapo ya visiwa vilivyopo katika Ziwa Victoria kwa upande wa Tanzania ambayo ilikuwa imebeba shehena ya sangara wachanga kwa ajili ya kwenda kuwauza katika Kiwanda cha Vicfish jijini Mwanza usiku.

Taratibu zinafanyika ili kupata kibali kutoka mahakamani kwa ajili ya kugawa samaki hao kwa baadhi ya shule au taasisi zingine ambazo zinahitaji msaada wa chakula kwa vile samaki hao hawana madhara kiafya na kwamba hatua nyingine kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

Nyavu haramu chanzo cha uvuvi samaki wasio na viwango.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Vickfish, Murtaza Alloo, amethibitisha samaki hao kukamatwa lakini amesema samaki hao bado walikuwa ni mali ya wakala kwa vile walikuwa hawajapokelewa kiwandani.

Uchunguzi unaonyesha kuwa kwa kipindi ch miaka mitatu iliyapita viwanda vya kusindika minofi ya samaki vilivyoko eneo la Kanda ya Ziwa vimekabiliwa na uhaba wa samaki , hali ambayo imesababisha viwanda mbalimbali kupunguza wafanyakazi.

Samaki wasio ruhusiwa ni wale walio chini ya ukubwa wa sentimita 50.

Wednesday, November 2, 2011

VODACOM YATUA RASMI MWANDOYA, WANANCHI WASEMA NI ZAIDI YA MAWASILIANO

Mara baada ya blogu hii sambamba na kituo cha Clouds Fm, Chanel Ten pamoja na magazeti mbalimbali nchini kuripoti juu ya kadhia inayosababishwa na mawasiliano duni wanayoipata wananchi vijiji vya Mwandoya makao makuu ya jimbo la Kisesa wilayani Meatu, ikisababisha wananchi hao kutafutana shati kwa shati, wakilazimika kusafiri umbali wa kilometa kadhaa kusaka huduma za utumaji na upokeaji fedha au zile za kibenki.

Mtandao wa simu za mkononi Vodacom tayari umekwisha tinga eneo hilo, hivyo kuanzia sasa wananchi wake wanawasiliana bila tabu na ndugu na jamaa zao toka meneo mbalimbali nchini na hata nje ya nchi.
Yu mmoja wa wananchi wa Mwandoya wanaoamini kuwa Vodacom inapotua mahali ni zaidi ya mawasiliano kwani inauwezo wa kutatua hata suala lao la kibenki. Kupitia huduma ya M-PESA, wanapokuwa mbali itarahisisha suala la kuwatumia pesa za matumizi wazazi, ada ya shule kwa wanafunzi hata kuhifadhi pesa zao mara baada ya mauzo kwa zao lao kuu la pamba, nao wafanyabiashara kuagiza bidhaa mijini hasa ukizingatia kuwa hakuna benki iliyojitokeza kutoa huduma kijijini hapo watapata fursa kuagiza mizigo na kutuma fedha pasina kusafiri.

Katibu wa CCM wilaya ya Maswa Omary Kalolo (kushoto) naye alikuwepo katika eneo la tukio kutoa sapoti kwa tukio zima la uzinduzi wa mawasiliano ya Vodacom lililofanywa na Mh. Luhaga Mpina Mbunge wa jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu (mwenye suti nyeusi katika).

Moja ya changamoto zinazoikabili wilaya ya meatu ni upatikanaji wa nishati ya umeme.

Hata hivyo zaidi ya bilioni 1.6 zimetengwa kupitia bajeti ya serikali kuipatia umeme wilaya ya Meatu na vijiji vyake ambapo mpaka sasa miundombinu ya nguzo imekwisha simikwa huku mradi ukitegemewa kukamilika rasmi mwezi desemba 2011 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete anategemewa kuzindua mradi huo.

BREAKING NEWZ: POLISI WALIPUSHA MABOMU KUTAWANYA WAANDAMANAJI KESI YA KUCHOMA KURAN MWANZA.

>Katika hali isiyotarajiwa, ghafla mazingira ya mahakama ya mwanzo iliyoko karibu na ofisi za idara ya maji safi na maji taka jijini Mwanza, eneo la Kemondo na maeneo ya Ghandh hall, Polisi wamelazimika kulipua mabomu ya machozi majira ya saa nne asubuhi ili kuwatawanya waandamanaji waliofurika kwa wingi nje ya mahakama ya Wilaya ya Nyamagana wakifanya vurugu kushinikiza maamuzi yafanyike dhidi ya watuhumiwa wa kesi hiyo….

Hali tete ilianza kwa waandamanaji hao kufanya vurugu kwa madai ya kutaka waliopewa dhamana wasipewe dhamana, huku wengine wakisema hawataondoka mahakamani hapo pale tu watakapo kabidhiwa watuhumiwa hao...

Mzozo wa waandamanaji na askari wa jeshi la polisi.

Makundi ya watu nje ya mahakama.

Hali si shwari..

Hali tete nje ya mahakama polisi wakiendelea kurusha mabomu ya machozi.

Hali Mara baada ya dakika 30.Toka angani eneo la mahakama ya wilaya Nyamagana.
Asubuhi ya leo jumla ya watuhumiwa wanne wanadaiwa kushirikiana kuchoma Korani, wamefikishwa mahakamani hapa kujibu mashtaka dhidi yao katika kesi inayotajwa kuahirishwa zaidi ya mara nne sasa kutokana na kuhofia usalama wa watuhumiwa.

Watuhumiwa wanaohusishwa na kesi hiyo ni waumini wa Kanisa la Tanzania Assembly of God (TAG) ni Tumaini Jumanne (30) ambaye ni mwalimu wa Biblia, Petro Mashauri (29) mfanyabiashara, Dickson Magai (30) mfanyabiashara na mwanamke pekee, Kalista Mlomo ambaye ni mkulima.

Wakikabiliwa na mashitaka matano ambayo ni kula njama, kufanya kusanyiko lisilo halali, kuingia kwa jinai nyumbani kwa Husna Hamis na kuharibu mali, pamoja na lile linalozungumzwa zaidi la kudhalilisha dini kwa kuchoma moto kitabu cha Korani Tukufu.


Vurugu hizo zimesababisha barabara kadhaa kufungwa kwa muda kwaajili ya usalama wa mahabusu wengine na kuruhusu kesi nyingine kuendelea kusikilizwa mahakamani hapo.

Si biashara tena bali msaada kukosha macho kwa maji ya kahawa.

Askari wa jeshi la polisi wakifanya doria eneo la mahakama.

Kutokana na hatua ya kufunga barabara watu wamelazimika kutembea kwa miguu nao polisi wakipiga marufuku kusanyiko la aina yoyote kwenye eneo husika.

LIVE NDANI YA CHANEL TEN

Ni Kundi jipya linaloitwa BABATAN likiwa na maana ya 'Shikamana baada ya kukandamizwa' (cheki na kamusi ya kiswahili), kundi likiwa na wasanii idadi kubwa ya wale waliopigwa stopu' wakiunda kundi la awali la FUTUHI.

Kutoka kushoto ni Mansoor Jalaludin (kamera man), Lwiza Rwechungura aka Kafuku Kaulananga, Mwashum Ismail aka Brandy Muswaili, Hashim Abeid aka Itagata na Robinson Daudi aka Mchele Chubu Mwanashidondofilo, nyuma wanaonekana John Mlinga aka Babu Mkombe na Ibrahim Mussa aka Chicochengambili.


Sasa mavijana haya yenye vipaji full balaa, baada ya kimya kirefu sasa yatakwenda kuonekana ndani ya kituo cha Televisheni nchini Chanel Ten kila ijumaa.

USKOSE UHONDO;

Tuesday, November 1, 2011

MPINA::KIWANDA CHA KUCHAMBUA PAMBA KUJENGWA MAKAO MAKUU YA JIMBO LA KISESA.


Mbunge wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu Mh.Luhaga Joelson Mpina (CCM) mwishoni mwa wiki amefanya mkutano wa hadhara kijiji cha Mwandoya ambako ndiko makao makuu ya Jimbo, lengo kuu likiwa kuainisha na kubainisha mikakati ya maendeleo iliyopo na inayotarajiwa kufanyika jimboni humo.

Kwa mujibu wa Mpina Tayari jimbo la Kisesa limepata mwekezaji wa kujenga kiwanda cha kuchambua pamba ambacho ujenzi wake utaanza rasmi pindi umeme utakapoingia Mwandoya mnamo mwezi desemba mwaka huu.

Faida zinazotajwa kupatikana pindi kiwanda hicho kitakapojengwa na kuanza kufanya kazi ni pamoja na vijana wa jimbo la Kisesa kupata ajira, wakulima watapata fursa ya kuuza pamba yao kwa bei nzuri zaidi kwani wanunuzi wengi hupunguza bei ya zao hilo kwa kisingizio cha gharama za usafirishaji kwenda kwenye vinu vya kuchambua pamba.

Burudani nayo haikukauka hapa ni kwaya ya Mwandoya ikitumbuiza.

Raha ilipozidi kiongozi wa kundi aliimba begani mwa mwananchi.

Kijiji hiki cha Mwandoya kinaonekana kukuwa kwa kasi katika suala zima la maendeleo kutokana na juhudi za dhati za mbunge Joelson Mpina sambamba na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wananchi wa jimbo lake kwani ndani ya kipindi cha miaka miwili kupitia changizi mbalimbali tayari wamefanikiwa kujenga Zahanati moja pamoja na nyumba nane za walimu wa shule zinazozunguka eneo hilo.

Wazee wa wakimsikiliza mbunge wao.

Kwa lengo la kukuza vipaji vya soka Mh. Joelson Mpina, alikabidhi jezi seti moja moja kwa timu za Mwandoya Shooting na Maskani Football Club.

Kakaaaa nawe upo-po hapa....!!!