Mtandao wa simu za mkononi Vodacom tayari umekwisha tinga eneo hilo, hivyo kuanzia sasa wananchi wake wanawasiliana bila tabu na ndugu na jamaa zao toka meneo mbalimbali nchini na hata nje ya nchi. Yu mmoja wa wananchi wa Mwandoya wanaoamini kuwa Vodacom inapotua mahali ni zaidi ya mawasiliano kwani inauwezo wa kutatua hata suala lao la kibenki. Kupitia huduma ya M-PESA, wanapokuwa mbali itarahisisha suala la kuwatumia pesa za matumizi wazazi, ada ya shule kwa wanafunzi hata kuhifadhi pesa zao mara baada ya mauzo kwa zao lao kuu la pamba, nao wafanyabiashara kuagiza bidhaa mijini hasa ukizingatia kuwa hakuna benki iliyojitokeza kutoa huduma kijijini hapo watapata fursa kuagiza mizigo na kutuma fedha pasina kusafiri.
Katibu wa CCM wilaya ya Maswa Omary Kalolo (kushoto) naye alikuwepo katika eneo la tukio kutoa sapoti kwa tukio zima la uzinduzi wa mawasiliano ya Vodacom lililofanywa na Mh. Luhaga Mpina Mbunge wa jimbo la Kisesa wilaya ya Meatu (mwenye suti nyeusi katika).
Moja ya changamoto zinazoikabili wilaya ya meatu ni upatikanaji wa nishati ya umeme.
Hata hivyo zaidi ya bilioni 1.6 zimetengwa kupitia bajeti ya serikali kuipatia umeme wilaya ya Meatu na vijiji vyake ambapo mpaka sasa miundombinu ya nguzo imekwisha simikwa huku mradi ukitegemewa kukamilika rasmi mwezi desemba 2011 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete anategemewa kuzindua mradi huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.