ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 17, 2025

SERIKALI YATAKA TAMISA ISIMAMIE KWA UADILIFU SHUGHULI ZA SEKTA YA MADINI ILI KUWANUFAISHA WAZAWA

WhatsApp%20Image%202025-05-16%20at%201.12.46%20PM%20(1)

Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Masoko ya Chama cha Wasambazaji wa Huduma katika Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA), Dkt. Sebastian Ndege akifafanua jambo wakati wa kongamano la TAMISA lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Mei 16, 2025.

WhatsApp%20Image%202025-05-16%20at%201.12.44%20PM%20(2)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eng. Yahya Samamba akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mei 16, 2025 katika uzinduzi wa Kamati ya Masoko na Mawasiliano ya TAMISA.
WhatsApp%20Image%202025-05-16%20at%201.12.45%20PM
Katibu wa TAMISA, Dkt. Theresia Numbi akizungumza katika uzinduzi wa Kamati ya Masoko na Mawasiliano ya TAMISA lililofanyika jijini Dar es Salaam leo Mei 16, 2025.

SERIKALI  kupitia Wizara ya Madini imeitaka  Chama cha Wasambazaji wa Huduma katika Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA) kusimamia kwa weledi na uadilifu shughuli zote za sekta ya madini nchini ili kuhakikisha rasilimali hizo zinawanufaisha Watanzania, hususan wazawa.

Hayo ameyasemaleo Mei 16, 2025,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eng. Yahya Samamba wakati akizungumza katika uzinduzi wa Kamati ya Masoko na Mawasiliano ya TAMISA, alisema kuwa Tanzania kwa sasa ina zaidi ya masoko 40 na vituo zaidi ya 100 vya kuuzia madini, jambo linaloonesha mafanikio makubwa ya sekta hiyo.

Eng. Samamba alisisitiza kuwa mafanikio haya yatakuwa na tija endapo TAMISA itasimamia ipasavyo shughuli zinazofanywa na wazawa, sambamba na kutekeleza maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Madini ya kuhakikisha uchimbaji na usambazaji wa madini unaleta faida kwa taifa.

 “Tunapokusanya kodi pamoja na tozo zisizo za kikodi, hiyo ni hatua nzuri, lakini tukiweka nguvu zote katika ukusanyaji wa kodi bila kusimamia vizuri shughuli nzima ya sekta hii, manufaa halisi tutayaona baadaye tu baada ya Mwenyezi Mungu kutuwezesha kuwa na madini haya,” alisema Eng. Samamba.

Aidha, alieleza kuwa mabadiliko ya sheria na kanuni za sekta ya madini lazima yalenge kuwawezesha na kuwanufaisha wazawa, kwa kutoa ajira, mafunzo na kutumia teknolojia ya kisasa ili kuinua uwezo wa Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye uchumi wa madini.

Amewataka TAMISA na wadau wake kuhakikisha wanazingatia masuala ya Local Content, ajira kwa vijana, pamoja na usimamizi wa teknolojia kwa maendeleo ya nchi.

 “Serikali imedhamiria kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia sekta hii, na hilo litawezekana tu ikiwa sheria zitasimamiwa ipasavyo,” aliongeza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAMISA, Peter Kumalilwa, alisema wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa wazawa kuhusu kupewa kazi na kushindwa kuzifanya kwa viwango stahiki, hali inayochangia ukosefu wa uaminifu na migogoro katika sekta hiyo.

 “Tumejipanga kufanya tathmini ya kina ili kuongeza uaminifu na kupunguza migogoro,” alisema Kumalilwa.

Aliitaka serikali kutekeleza ahadi ya kuishirikisha TAMISA moja kwa moja kwenye zabuni za serikali, kama ilivyoahidiwa katika kikao cha Mei 1, 2025, jijini Dodoma.

 “Ushirikishwaji huu utasaidia wanachama wetu kujiandaa mapema na kuchukua hatua stahiki ili kushiriki kikamilifu katika zabuni hizo,” aliongeza.

Aidha, alitaja changamoto ya wageni kupewa kazi ambazo kisheria ni za wazawa, akiiomba serikali kuingilia kati na kuhakikisha ushirikiano kati ya wageni na wazawa unazingatia sheria za Local Content ili kulinda maslahi ya wazawa na kuleta tija kwa taifa.
WhatsApp%20Image%202025-05-16%20at%201.12.44%20PM
Katibu wa TAMISA, Dkt. Theresia Numbi, alieleza kuwa kuanzishwa kwa kamati maalum ya mawasiliano na masoko ni hatua ya kimkakati katika kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi.

Alisema TAMISA ni matokeo ya kikao kati ya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, na wadau wa sekta ya madini kilichofanyika Januari 2024, ambapo ilielekezwa kuanzishwa kwa chombo kitakachowaunganisha watoa huduma na wamiliki wa leseni nchini.

 “Kuwepo kwa jukwaa la pamoja kutasaidia kuwashirikisha Watanzania katika sekta ya madini na kuhakikisha kipaumbele kinatolewa kwa bidhaa na huduma za wazawa,” alisema Dkt. Numbi.

Aliongeza kuwa usimamizi wa sheria na ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta hiyo umechochea fursa nyingi ikiwemo ajira, mafunzo, utafiti, uhamishaji wa teknolojia na manunuzi ya bidhaa zinazozalishwa nchini.

“Niwataarifu Watanzania mliopo hapa kuwa fursa za kwenye migodi ni kwa ajili yetu sote Watanzania,” alisisitiza.
WhatsApp%20Image%202025-05-16%20at%201.12.43%20PM
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Sekta Binafsi, Raphael Maganga, alisema kuwa uzinduzi wa kamati hiyo una lengo la kuhakikisha sekta binafsi inakuwa na ushawishi mkubwa katika uchumi wa Tanzania kupitia madini.

“Tunataka sera zetu ziwezeshe sekta binafsi kufikia malengo. Lengo letu ni kuhakikisha sekta ya madini inazalisha mabilionea wa kutosha nchini,” alisema Maganga.

Mkutano huo umeonyesha dhamira ya serikali na wadau wa sekta ya madini kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha sekta hiyo inachangia kwa kiwango kikubwa katika maendeleo ya taifa kwa kuwezesha wazawa kushiriki kikamilifu.
WhatsApp%20Image%202025-05-16%20at%201.12.43%20PM%20(1)

WhatsApp%20Image%202025-05-16%20at%201.12.43%20PM%20(2)

WhatsApp%20Image%202025-05-16%20at%201.12.47%20PM

WhatsApp%20Image%202025-05-16%20at%201.12.47%20PM%20(1)
Matukio mbalimbali wakati wa kongamano la TAMISA lililofanyika leo Mei 16, 2025 jijini Dar es Salaam.
WhatsApp%20Image%202025-05-16%20at%201.12.44%20PM%20(1)
Picha ya pamoja.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Masoko na Mawasiliano iliyozinduliwa leo, Dkt. Sebastian Ndege amesema, kutokana na Tanzania kuwa na aina mbalimbali za madini na kampuni za nje na ndani ya nchi kuwekeza, ni wakati wa watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa madini.

Amesema, wanafahamu kuwa wanayo haki ya kushiriki katika kutoa huduma lakini pia wanao wajibu wa kuhakikisha wanatoa huduma sahihi kwa wakati sahihi na weledi. “Sisi kama TAMISA kazi yetu itakuwa ni kusimamia wanachama wetu kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa weledi na kuhakikisha kuwa tunafuata maadili ya utoaji huduma ili tuweze kuaminika na hili tutalisimamia kwa nguvu zetu zote,” amesema Dkt Ndege.

RAIS SAMIA AWATAKA WATANZANIA KUWA WAZALENDO KUCHANGAMKIA HAKI YAO YA MSINGI YA KUJIANDIKISHA.

Na Janeth Raphael MichuziTv - Chamwino Dodoma

RAIS wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameboresha taarifa zake za mpiga kura katika Kijiji Chamwino Ikulu, huku akiwataka watanzania kuwa wazalendo kwa kuchangamkia haki yao ya msingi ya kujiandikisha.

Uboreshaji wa taarifa za mpiga kura awamu ya pili ulianza Mei 16,2025 ambapo jana Rais Samia alihakiki taarifa zake katika kitongoji cha Sokoine Kijiji cha Chamwino Ikulu.

Rais Samia alifika saa 8.20 mchana na moja kwa moja alielekea katika kituo cha kupiga kura ambapo alitumia dakika 10.

Mara baada ya kumaliza kujiandikisha,Rais Samia alipata nafasi ya kuzungumza na Wananchi waliojitokeza ambapo alidai ametumia nafasi yake ya kikatiba kujiandikisha katika kituo cha Chamwino Ikulu.

"Nimeona nijiunge nanyi kama mnavyojua mimi ni mkazi wa Chamwino huko nyuma nimepiga kura sehemu nyingi.Nimekuja kurekebisha taarifa zangu huko nyuma nilikuwa nikijiandikisha na kupiga kura Zanzibar mwaka huu inabidi nipige hapa Makao Makuu ya Nchi na Serikali,"alisema Rais Samia.

Aidha,Rais Samia amesisitizia wananchi kujitokeza kupiga kura kwani huo ni mzunguko wa pili na wasipofanya hivyo watakuwa wamepoteza haki yao ya msingi.

"Niwaombe tuje tupige kura huu ni mzunguko wa pili tukikosa huko mbele huwezi kurudia ili turudishe Serikali.Nitumie fursa hii kuwashukuru nawaomba waiteni ambao hawajaja waje,"alisema Rais Samia.

"Kazi inachangamoto wastahimili wale wanakuja kujiandikisha waendelee kadi zimepungua subiri.Nataka niwahakikishie kwa mipango mizuri kila mwenye haki ya kuandikishwa ataandikishwa,"alisema Rais Samia.

Rais Samia alisema : "Kutokujitokeza ni kukataa haki ya kikatiba suala unajiuliza ww ni mzalendo wa aina gani?

Nenda kapige kura wewe ukitaaa wenzako wataenda kumweka wanaomtaka suala kubwa hapa ni uzalendo hii ni fursa kubwa ni vyema kila mtanzania ajitokeze atumie nafasi hii,"alisema Rais Samia.

Kwa upande wake Afisa Mwandikishaji kutoka Majimbo ya Chamwino na Mvumi,Godfrey Mnyamale alisema wananchi wamejitokeza kwa wingi kujiandikisha ambapo amedai malengo ni kuwaandikisha wananchi 280,000.

Alisema zoezi hilo ni Maalimu kwa wale ambao waliokosa nafasi ya kujiandikisha awamu ya kwanza,pamoja na wale ambao wanataka jkubotesha taarifa pamoja na wale waliokosa sifa.

"Kama alivyosema Mheshimiwa Rais,niwaombe wananchi wa Majimbo haya ya Chamwino na Mvumi kutumia fursa hii,"alisema Mnyamale.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo tarehe 17 Mei, 2025 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino mkoani Dodoma ambapo pia aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari hilo.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionyesha kadi yake ya mpiga kura mara baada ya kushiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo tarehe 17 Mei, 2025 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino mkoani Dodoma.

Dkt. MPANGO AZINDUA SHULE YA SEKONDARI YA MFANO YA BENKI YA CRDB, BENKI HIYO IKITIMIZA MIAKA 30

 

Arusha 16 Mei 2025 - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, amezindua rasmi Shule ya Sekondari ya Mfano ya Benki ya CRDB, itayojengwa katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya Benki ya CRDB.

Shule hiyo ya kisasa ni matokeo ya dhamira ya Benki hiyo ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwekeza kwenye elimu bora kwa watoto wa Kitanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shule hiyo uliofanyika katika seimna ya wanahisa wa Benki ya CRDB kuelekea Mkutano Mkuu, Dkt. Mpango aliipongeza Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kijamii, hususan sekta ya elimu.
“Nawapongeza kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa sekta binafsi. Mmekuwa mstari wa mbele sio tu kwenye huduma za kifedha bali pia katika kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii,” alisema Dkt. Mpango huku akiipongeza benki hiyo pia kwa kutimiza miaka 30 tokea kuanzishwa kwake mwaka 1996.


Akizungumza katika semina hiyo ya wanahisa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1996, Benki ya CRDB imeendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo kwa Taifa kwa kutoa huduma za kifedha zenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Shule ya Sekondari ya Mfano ya Benki ya CRDB ina uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 600 na imejengwa kwa viwango vya kisasa ikiwa na madarasa ya kisasa 16, maabara 4, maktaba 1 chumba cha TEHAMA 1, ofisi za walimu na wafanyakazi 11, vyoo 53, miundombinu rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, pamoja na maeneo rafiki ya michezo. Mradi huu unatarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 5.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela, alisema shule hiyo ni zawadi ya Benki kwa Watanzania katika kuadhimisha miaka 30 ya mafanikio ya benki hiyo. “Tulipojiuliza ni zawadi gani ya kipekee tungeweza kuwapa Watanzania katika kutimiza miaka 30, tulikubaliana kwamba elimu ni urithi wenye nguvu kuliko wote. Shule hii ni ushahidi wa dhamira yetu ya kuwekeza katika kizazi kijacho,” alisema Nsekela.
Nsekela aliongeza kuwa shule hiyo ni sehemu ya mpango mpana wa Benki ya CRDB wa kurudisha kwa jamii katika nyanja za ya elimu, afya, mazingira na uwezeshaji wanawake kupitia CRDB Bank Foundation. “Tunaamini kuwa maendeleo endelevu hayawezi kufikiwa bila uwekezaji wa makusudi katika elimu. Kupitia shule hii, tunaweka msingi wa taifa lenye maarifa, maadili na ushindani wa kimataifa,” alibainisha.
Akitoa salamu zake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb), aliishukuru Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini. “Kwa niaba ya Serikali na Wizara ya Elimu, naishukuru sana Benki ya CRDB kwa maono na uamuzi huu wa kujenga shule ya kisasa kwa ajili ya watoto wa Kitanzania. Huu ni mfano hai wa jinsi sekta binafsi inavyoweza kushirikiana na Serikali katika kujenga musatakabali bora kwa watoto na vijana wetu.”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB Bank Foundation, Martin Warioba, alisema shule hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya CRDB kuboresha mazingira ya elimu nchini na kufungua fursa kwa watoto wa Kitanzania. “Mbali na kujenga shule hii ya mfano, tumejipanga pia kuanzisha mpango wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kwa kushirikiana na Wizara ya elimu.”

Uzinduzi wa shule hiyo unachukuliwa kama alama ya mafanikio ya miaka 30 ya Benki ya CRDB, na uthibitisho wa maono yake ya kujenga taifa lenye misingi imara ya elimu, usawa na maendeleo endelevu. “Tunajivunia kuona uwekezaji wetu ukiendelea kuzaa faida zaidi katika jamii,” alisema mmoja ya Wanahisa waliohudhuria semina hiyo.
Wanahisa wa Benki ya CRDB watafanya Mkutano Mkuu wa 30 kesho ambapo ajenda mbalimbali zinatarajiwa kujadiliwa ikiwamo kuidhinisha pendekezo la bodi ya wakurugenzi la gawio la shilingi 65 kwa hisa ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 kulinganisha na gawio la shilingi 50 kwa hisa lililotolewa kwa mwaka 2023.


BARAZA LA MADIWANI KASULU LIMEMCHANGIA MILIONI 1 RAIS DKT SAMIA KWA AJILI YA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA TENA URAIS.

 

Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu limemshukuru na kumpongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa ambapo wamechangia kiasi cha  shilingi 1,000,000  kwa ajili  ya kuchukua fomu ya kugombea Urais kwa Mhe.Rais na shilingi 577,000 kwa ajili ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini,Mhe.Vuma Olle  kuchukua fomu ya kugombea ubunge
Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu limemshukuru na kumpongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa ambapo wamechangia kiasi cha  shilingi 1,000,000  kwa ajili  ya kuchukua fomu ya kugombea Urais kwa Mhe.Rais na shilingi 577,000 kwa ajili ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini,Mhe.Vuma Olle  kuchukua fomu ya kugombea ubunge
Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu limemshukuru na kumpongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa ambapo wamechangia kiasi cha  shilingi 1,000,000  kwa ajili  ya kuchukua fomu ya kugombea Urais kwa Mhe.Rais na shilingi 577,000 kwa ajili ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini,Mhe.Vuma Olle  kuchukua fomu ya kugombea ubunge



Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu limemshukuru na kumpongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa ambapo wamechangia kiasi cha  shilingi 1,000,000  kwa ajili  ya kuchukua fomu ya kugombea Urais kwa Mhe.Rais na shilingi 577,000 kwa ajili ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini,Mhe.Vuma Olle  kuchukua fomu ya kugombea ubunge


 Na Fredy Mgunda,Kigoma.

Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu limemshukuru na kumpongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa  na nzuri aliyoifanya ya kuleta fedha nyingi za utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika halmshaur hiyo.

Ambapo wamechangia kiasi cha  shilingi 1,000,000  kwa ajili  ya kuchukua fomu ya kugombea Urais kwa Mhe.Rais na shilingi 577,000 kwa ajili ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini,Mhe.Vuma Olle  kuchukua fomu ya kugombea ubunge.  

 Akizungumza leo katika kikao cha robo ya tatu cha Baraza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Mhe. Eliya Kgoma,amesema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa Rais Samia amefanya kazi kubwa ya maendeleo wilayani humo.

Kwa upande wake ,Mkurugenzi Mtendaji wa halmsahuri hiyo, Dkt.Semistatus H. Mashimba akizungumza kwa niaba ya watendaji wa Halmashauri,amesema kuwa wanaungana na Baraza hilo katika kumpongeza Rais Samia kutokana na fedha nyingi alizoleta kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ambazo zimewanufaisha wananchi.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kasulu,Jennifer Chinguile,amepokea mchango huo kwa niaba ya chama na kuahidi kuuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM,Balozi Emmanuel Nchimbi kabla ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika badae mwezi huu.

Kwa upande wake,Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini, Simon Nzibuje ametoa shukrani kwa mchango huo na kuhaidi kuufikisha kwa mhusika.

Akitoa salamu za serkali, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,Mhe. Kanali Isaac Mwakisu amewataka wananchi kuwa na taadhari na kuhakikisha wanatunza chakula kutokana na hali isiyoridhisha ya usalama wa chakula kwa sasa.

Friday, May 16, 2025

SIRI YA WATOTO NJITI KANDA YA ZIWA JEH 'NI UGONJWA, MAZINGIRA AU LISHE?'

 NA ALBERT GSENGO/MWANZA

"Katika Jiji la Mwanza, sauti ya furaha ya kuzaliwa kwa mtoto imeanza kuchanganyika na hofu—hofu ya changamoto zinazowakumba wakinamama wanaojifungua watoto njiti. Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, hospitali za jijini hapa Hospitali ya Mkoa ya Sekoutore na Hospitali ya Rufaa ya Bugando zimeshuhudia ongezeko la visa vya watoto kuzaliwa kabla ya wakati yaani majuma 36, hali inayozua maswali kuhusu afya ya mama, mazingira, na mifumo ya huduma za afya. Wito umetolewa kwa serikali kufanya utafiti ili kubaini sababu za hali hiyo.

WIZI WA BIMA WAFUMULIWA, SERIKALI YAPANGA MASHAMBULIZI.

 


Serikali imepiga kengele ya tahadhari kufuatia ongezeko la madai feki ya bima yanayodaiwa kuisababishia nchi hasara ya mabilioni, huku ikiweka wazi kuwa asilimia 10 hadi 15 ya madai hayo duniani yana chembechembe za udanganyifu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Sada Mkuya, amesema hali hiyo imeifanya sekta ya bima kupoteza uaminifu wa umma na kuathiri utoaji wa huduma kwa wateja wa kweli wanaohitaji msaada halali.
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, wakati wa mkutano wa wataalamu wa udhibiti wa udanganyifu wa bima (IASIU), Dk. Sada alisema baadhi ya maofisa wa bima wanashirikiana na wateja kudanganya kwa malipo hewa, jambo alilolieleza kuwa ni uhujumu uchumi.

“Fedha zinazopotea kwa njia ya hila hizi zingetumika kuboresha huduma kwa wananchi Serikali haiwezi kufumbia macho wizi huu unaotendeka kwa hila ya taaluma,” alisema na kupendekeza kuanzishwa kwa mahakama au kitengo maalum kitakachoshughulikia uhalifu wa bima kwa haraka na kwa haki.
Kamishna wa Bima nchini, Dk. Baghayo Saqware, alisema serikali tayari imeanzisha kitengo maalum cha kuchunguza udanganyifu wa bima, huku ikiimarisha miongozo na weledi wa wafanyakazi katika kampuni husika.

Amesema licha ya juhudi za kutoa elimu kwa umma, wahusika wa udanganyifu nao wameendelea kubuni mbinu mpya kila kukicha, hivyo mashirikiano ya kitaifa na kimataifa ni muhimu zaidi sasa kuliko wakati wowote.

Rais wa IASIU Tanzania, Mjabwa Hanzuruni, aliitaka sekta binafsi kushirikiana na serikali kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na kuripoti madai yenye mashaka, akisema hatua hiyo itajenga uaminifu mpya katika soko la bima.

Thursday, May 15, 2025

Benki ya CRDB yawakaribisha Wanahisa kwenye Mkutano Mkuu wa 30

 

Arusha 14 Mei 2025 - Benki ya CRDB imewataka wanahisa wake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa, unaotarajiwa kufanyika Jumamosi, tarehe 17 Mei 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya mafanikio tangu kuanzishwa kwa benki hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye hoteli ya Gran Meliá, jijini Arusha, ambapo Benki ya CRDB pia ilizindua Ripoti yake ya Mwaka 2024, inayoonyesha maendeleo makubwa ya kifedha, kiutendaji na kijamii yaliyopatikana katika kipindi hicho.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay, amesema kuwa Mkutano Mkuu wa mwaka huu utakuwa wa kipekee kwani utatanguliwa na semina maalum kwa wanahisa na umma, itakayofanyika Ijumaa, tarehe 16 Mei 2025, katika ukumbi wa Simba, AICC. “Semina hii ya kihistoria itakuwa chini ya kaulimbiu yetu ya mwaka huu: ‘Miaka 30 ya Ukuaji wa Pamoja,’ na itafunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango. Ni fursa muhimu ya kutafakari mafanikio yetu ya pamoja, changamoto tulizozishinda, na mwelekeo wetu wa miaka ijayo,” amesema Dkt. Laay.

Ajenda mbalimbali zitajadiliwa katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB ni pamoja na uchaguzi wa wajumbe wa bodi, kuteua wakaguzi wa hesabu, kujadili mapendekezo ya maboresho ya Katiba ya Benki, kujadili na kupokea Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi, na Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa, pamoja na gawio kwa mwaka 2024 ambapo pendekezo la gawio la Sh 65 kwa hisa litawasilishwa sawa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa yamekamilika kwa asilimia 100. Nsekela amesema mkutano huo utafanyika kwa njia mseto “Hybrid Meeting” ili kutoa fursa kwa wanahisa wengi zaidi kushiriki moja kwa moja na kwa njia ya kidijitali. “Tumeweka muongozo wa jinsi ya kushiriki mkutano mkuu kwa njia ya mtandao kupitia tovuti yetu ya www.crdbbank.co.tz, mitandao yetu ya kijamii, lakini pia maelekezo yametumwa kwa ujumbe mfupi kwa Wanahisa,” amesema Nsekela huku akiwahakikishia kuwa Benki hiyo vizuri katika kuhakikisha wanashiriki bila chanagamoto yoyote.
Nsekela amewahamasisha wanahisa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Mkutano Mkuu huo wa kihistoria, akisisitiza kuwa uwepo wao ni muhimu kwa ajili ya kushuhudia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka 30. “Tumejenga taasisi imara inayotoa huduma bora, tumeongeza thamani kwa wanahisa, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa letu. Hii ni fursa adhimu kwa kila mwanahisa kujivunia sehemu yake katika mafanikio haya na kushiriki kuamua mustakabali wa benki yetu katika miaka ijayo,” amesisistiza.

GUGU MAJI JIPYA LACHOCHEA TAHADHARI MPYA ZIWA VICTORIA

NA ALBERT G.SENGO/MWANZA Hatimaye Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria imezindua rasmi jarida maalum linaloangazia jitihada endelevu za kudhibiti uoto vamizi wa gugumaji katika Ziwa Victoria. Uzinduzi huo umefanyika Mei 13/2025 katika viwanja vya Ofisi za Bonde vilizopo kata ya Igogo wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wahudumu na wafanyakazi wa shughuli za bonde kutoka serikalini, mashirika ya mazingira, na jamii zinazozunguka ziwa Victoria. Licha ya kuipongeza Bodi kwa hatua hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameiagiza kuhakikisha Jarida waliloliandaa kuhusu kukabiliana na uvamizi wa Gugumaji jipya aina ya Salvinia Molesta, linawekwa katika mifumo mbalimbali ili jamii iweze kuona, kusoma na kusikiliza ili kupata elimu tosha.

Wednesday, May 14, 2025

WAHIFADHI TFS SAO HILL WAKAGUA UKARABATI WA MIONDOMBINU YA BARABARATARAFA YA NNE YA SHAMBA MGOLOLO

 

Wahifadhi tfs sao hill wakagua ukarabati wa miondombinu ya barabaratarafa ya nne ya shamba mgololo akiwa katika eneo la ukaguzi wa barabaraWahifadhi tfs sao hill wakagua ukarabati wa miondombinu ya barabaratarafa ya nne ya shamba mgololo akiwa katika eneo la ukaguzi wa barabara

Na Fredy Mgunda,Mufindi.

Ukaguzi huo umefanyika ikiwa ni hatua ya kuhakikisha kuwa mawasiliano ya barabara zilizopo ndani ya msitu yanaendelea  kuwepo ili kuhakikisha  shughuli za shamba na zile za watumiaji wa barabara hizo ambao ni wavunaji wa miti wanaosafirisha malighafi za miti wanapita katika barabara hizo bila vikwazo vyovyote.


TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill imeendelea kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza ili kuhakikisha wadau wanaovuna malighafi katika Shamba wanafanya shughuli hiyo kwa wakati na hivyo kupekelekea uvunaji na usafirisha wa malighafi unafanyika bila vikwazo, na kupelekea wadau hao kufanya shughuli zao kwa wakati za kujipatia kipato kwa kuvuna malighafi ya miti na pia serikali kukusanya mapato yake kwa wakati uliopangwa.


Shughuli mbalimbali zinaendele hapa TFS - Shamba la miti Sao Hii katika Tarafa zote nne (4) za shamba ikiwa ni pamoja na maandalizi ya bustani ya miche ya miti kwaajili ya msimu ujao wa upandaji na uvunaji wa malighafi ya miti katika kipindi hiki ambacho mvua katika baadhi ya maeneo zinaendelea kunyesha.


ZAIDI YA BILIONI 17 KUSAMBAZA UMEME VITONGOJINI SINGIDA


MKURUGENZI wa Umeme Vijijini kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu, akitoa maelezo Mei 14, 2025 kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego (kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dk.Fatuma Mganga, wakati wa kumtambulisha Mkandarasi Kampuni ya M/s Transpower Limited na Whitecity International Contractor Ltd JV ambaye atasambaza umeme katika vitongoji 120 vya Mkoa wa Singida.



MKURUGENZI wa Umeme Vijijini kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu, (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego mkataba wa utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji 120 vya Mkoa wa Singida Mei 14, 2025. Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi wa Kampuni ya M/s Transpower Limited na Whitecity International Contractor Ltd JV ambaye ndiye ameshinda zabuni.

ZAIDI YA BILIONI 17 KUSAMBAZA UMEME VITONGOJINI SINGIDA

 

📌Kunufaisha Kaya 3,960 kutoka katika Vitongoji 120 ndani ya Wilaya Tano

 

📌Vitongoji 15 katika kila Jimbo la uchaguzi kunufaika

 

📌RC Dendego amshukuru Rais Samia na aipongeza REA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha vitongoji vyote vilivyosalia vinapatiwa umeme

 

Na Mohamed Saif- Singida

SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 17.39 wa kusambaza umeme katika vitongoji 120 utakaonufaisha Kaya 3,960 Mkoani Singida.

Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amebainisha hayo Mei 14, 2025 Mkoani Singida wakati wa kumtambulisha Mkandarasi aliyeshinda zabuni ya kutekeleza mradi huo Kampuni ya M/s Transpower Limited na Whitecity International Contractor Ltd JV kwa Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego.

“Tunamshukuru Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kiasi cha shilingi 17,394,214,690.85 kitumike kusambaza umeme katika vitongoji 120 Mkoani hapa, leo hii tumefika hapa kumtambulisha Mkandarasi na maandalizi ya awali ya kutekeleza mradi yameanza,” alisema Mhandisi Olotu.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego alimshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya kufikisha huduma ya umeme kwa wananchi mkoani humo hasa ikizingatiwa kuwa umeme ni miongoni mwa mahitaji muhimu kwa maendeleo ya jamii.

“Ninayo furaha kubwa leo hii kumpokea mkandarasi huyu kwani kama mtakumbuka Serikali iliahidi ifikapo 2025 itakuwa imekamilisha kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania Bara na sasa tumeshuhudia kabla hata ya 2025 vijiji vyote vilikuwa vimefikiwa na umeme na sasa tunatekeleza vitongojini,” alisema Mhe. Dendego.

Mhe. Dendego aliipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza miradi yake kwa ufanisi na uwazi na pia alimpongeza mkandarasi kwa ahadi yake aliyoitoa ya kukamilisha mradi huo kwa miezi 12 badala ya 24 kama ilivyo katika mkataba wake.

“Nimefarijika, tumepata mkandarasi mzuri kwani ametuahidi hapa atakamilisha kazi ndani ya miezi 12 nasi tutampatia ushirikiano na tutamsimamia ipasavyo ili ahadi hii ikamilike kwa kupata mradi bora,” alisema.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi wa kufikisha umeme katika vitongoji Mkoani humo, Mhandisi Olotu alisema kati ya vitongoji 2,289 vilivyopo mkoani humo, vitongoji 1,052 vimefikishiwa umeme na kwamba vitongoji 120 vitakavyopata umeme awamu hii vitaongeza idadi ya vitongoji vitakavyokuwa na umeme Mkoani humo.

Alisema mradi unatekelezwa katika vitongoji vya Wilaya za Singida DC, Ikungi, Manyoni, Mkalama na Iramba na kwamba vitongoji vitakavyobaki vitaendelea kusambaziwa umeme kulingana na upatikanaji wa fedha.

“Kwa mujibu wa mkataba, mradi huu unapaswa kutekelezwa ndani ya miezi 24 lakini mkandarasi ametuahidi na kutuhakikishia kuwa ndani ya kipindi cha miezi 12 atakuwa amekamilisha mradi,” alibainisha Mhandisi Olotu.


Kwa upande wake Meneja Usimamizi wa Miradi kutoka REA, Mhandisi Romanus Lwena alisisitiza kuwa umeme ni hitaji la muhimu na kwa kutambua hilo Serikali imewekeza fedha nyingi kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa.

“Serikali imetoa fedha nyingi kutekeleza miradi ya kusambaza umeme kote nchini, wito wetu kwa wananchi ni kuwapa ushirikiano wakandarasi na kuwa walinzi wa miundombinu hii,” alisisitiza Mhandisi Lwena.


Kwa upande wake mwakilishi wa Mkandarasi ambaye ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Transpower Ltd, Mhandisi Jackline Mushi aliahidi kufanya kazi kwa weledi na kukamilisha mradi kwa muda mfupi na kwa ubora unaopaswa.