ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 19, 2024

SHIRIKA LA GIZ LATOA MSAADA WA VIFAA VYA TEHAMA HOSPITALI YA KOROGWE MJI


Kaimu Meneja wa Mradi wa Afya wa GIZ Tanzania Erick Msoffe kulia akikabidhi vifaa vya Tehama wa kwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Mark Tanda akifuatiwa na Mratibu wa GIZ Apolinary Primus 


Na Oscar Assenga, KOROGWE.

Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) limetoa msaada wa vifaa vya tehama katika Hospitali ya Mji wa Korogwe ya Manundu na kuweka miundombinu ya Intaneti,Ufugaji wa Mfumo wa kieletroniki ambao ni mfumo wa taarifa za usimamizi wa Hospitali za Serikali ya Tanzania (GoTHOMIS) pamoja na kufanya mafunzo endelevu kwa watumishi.

 Ambapo hadi sasa zaidi ya wafanyakazi 150 katika hospitali ya Korogwe tayari wamefundishwa jinsi ya kutumia mfumo wa GoTHOMIS ambapo uwekezaji wake wa awali umegharimu Milioni 200,000,000 uliofanywa na GIZ hadi sasa na msaada zaidi ya kuifundi umepangwa ili kuhakikisha lengo linafikiwa ifikapo mwaka 2025.

 Akizungumza wvakati wa makabidhiano rasmi ya vifaa vya Tehama, Kaimu Meneja wa Mradi wa Afya wa GIZ Tanzania Erick Msoffe amesema kuwa mpango huo unalenga kubadilisha taratibu za kiutawala na kiafya katika hospitali hii kwa kuondoa matumizi ya kumbukumbu za karatasi, kuboresha uhifadhi na upatikanaji wa takwimu za wagonjwa, kuongeza hospitali ufanisi na kupunguza makosa katika takwimu.

Alisema kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani ambao ni wafadhili wao lakini pia wameshirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya pamoja na  Ofisi ya Rais Tamisemi wamekuwa wadau kwa mkoa wa Tanga kwa miaka tisa kwa awamu ya miaka mitatu mitatu.

Msoffe alisema kuwa mara nying wamekuwa kwenye awamu uliyoanza mwaka 2023 na itakwenda mpaka 2026 kwa mkoa wa Tanga na wana jumla ya Hospoitali 18 wanazozisaidia lakini katika eneo la Tehama pamoja na kwamba huyko nyumba wamefanya kazi na Hospitali nne kwenye eneo hilo lakioni watawasapoto kuweka miunbdombi na kuwafanya mafunzo watumishi waweze kuutumia.

 “Kwanini tupo Korogwe kuhakikisha sisi kama wadau na Serikali ikiwemo Hospitali wanaweza kufanya juhudi za kipekee kuona ni gharama gani zinahitajika ili kuitoa Hospitali ya wilaya kutoka kwenye matumiz ya mifumo ya katarasi na kwenda katika asilimia 100 ya matumizi ya Kiletroniki”Alisema


Sehemu ya Vifaa hivyo

 Alisema katika mafanikio yatakayopatikana katika hospitali ya Korogwe, yatatumiwa na serikali ya Tanzania kuongeza mageuzi haya ya kidijitali kwa hospitali nyingine chini Tanzania.

“GIZ inaipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya kisera na kutoa msaada wa kitaalamu katika kuboresha huduma za afya chini Tanzania”Alisema.

Alisema maboresho hayo yanayoendelea katika mifumo ya kidigitali na hasa mfumo wa GOTHOMIS ambao ni moja ya mifano tosha ya dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kusaidia vituo vya afya kuboresha huduma za afya kupitia teknolojia ya kidijitali.

 Hatua hiyo ni moja ya mambo ya msingi ya kuongeza ufanisi Hospitali ya Mji wa Korogwe inatangaza kwa fahari uamuzi wake wa kuachana na mifumo inayotumia makaratasi kabisa. Hospitali hiyo inakumbatia manufaa ya teknolojia katika kuimarisha huduma za afya na kurahisisha shughuli mbali mbali.

 Uamuzi huo umekuja baada ya ongozi na wafanyakazi kutambua changamoto zinazoendelea kukabili mfumo wetu wa huduma za afya zikiwemo uhaba wa watumishi, kazi kubwa inayowakabili watumishi kwa kujaza karatasi nyingi, takwim duni lakini pia muda mrefu ambao wagonjwa hukaa hospitalini kupata huduma.

Kwa hiyo hospitali ya Korogwe imejitolea kutumia maendeleo ya kidijitali ili kutoa huduma ya hali ya juu kwa wateja wake. Kuachana na matumizi ya makaratasi na kuharnia mifumo ya kidigitali ni tatua muhim katika kufikia lengo hili.

 Deutsche Gesellschaft fur Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH kupitia mpango wake wa afya wa Kuboresha Huduma ya Afya Tanzania (ICP) ni mshirika wa muda mrefu na wamekuwa wakisaidia mkoa wa Tanga na haswa hospitali ya Korogwe kutekeleza afua za afya za kidijitali ambazo zinalenga kuongeza fanisi na ubora wa huduma za afya.

Awali akizungumza Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mji wa Korogwe Dkt Heri Kilwale alisema kuwa kubadilika kutoka matumizi ya karatasi na kutumia mifumo ya kidijitali itawasaidia watoa huduma za afya kuweza kupata taarifa za mgonjwa kwa wakati na salama.

Alisema pia kutapunguza muda ambao wafanyakazi hutumia kufanya kazi za kujaza makaratasi mengi na hivyo wataalamu wa afya wataelekeza zaidi muda katika kutoa huduma kwa wagonjwa na hivyo kupelekea kuongezeka kwa ubora wa huduma zinazotolewa.

Korogwe ni miongoni mwa hospitali chache ambazo zimeanza kutumia toleo jipya la GoTHOMIS na kva msaada wa mara kwa mara kutoka kwa serikali, ongozi wa hospitali na washirika wa maendeleo, inatarajiwa kuwa hospitali ya Korogwe itafanikiwa katika dhamira yake ya mabadiliko kutoka matumizi ya karatasi Kwenda katika mifumo ya huduma za kidijitali na kwamba. Serikali itapanua msaada huo kwa hospitali zingine baada ya hapo.


Wednesday, January 17, 2024

JNHPP YAWA KIVUTIO ZANZIBAR

  








Wajiuliza mradi umefanikiwa vipi
Wakusanyika kupiga picha kwenye Bango


Watu wengi Mjini Unguja,Zanzibar wamejitokeza kutembelea Banda la TANESCO katika viwanja vya Fumba ambapo Maonesho ya 10 ya kimatafa ya Biashara yanafanyika .


Maonesho hayo yaliyoanzaTarehe 7 January 2024, yameleta Taswira mpya ya wadau wa Umeme juu ya jitihada ambazo Serikali inazifanya kwenye uwekezaji wa Sekta ya Nishati Nchini.


Mmoja ya wadau aliyetembelea Banda hilo ni Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari Mhe. Selestine Kakele ambae ameonekana kuvutiwa na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) na hasa mradi wa JNHPP ambao umefikia asilimia 95.83


Naye Bw. Mwangulumba Mtumishi katika Bodi ya Taifa ya Pamba,Tanzania amesema kuwa mradi wa JNHPP ni tumaini Jipya kwa Tanzania na kuwa utekelezaji wake umekua wa kipekee sana kwani ni mradi uliopitia changamoto nyingi sana hasa kutoka katika Mataifa makubwa yaliyoendelea lakini Tanzania imeonesha uthubutu.


“ najiuliza tumewezaje kulifanya hili, huu mradi wa kipekee , maono ya waasisi wetu yalikua makubwa sasa hata wale ma Giant wanatushangaa, hili tumeliweza”


Naye Bw.Issa Waziri mkazi wa Pemba, amesema kuwa mradi wa JNHPP si tu utatupatia umeme wa kutosha lakini umekua kivutio kwa namna unavyoonekana


“Mradi huu ni mzuri sana, kwanza unavutia, umeshawahi kufika (akiongea na mwandishi)natamani sana kufika hapo”


Shamra shamra za Maonesho haya zimekua za kihistoria kwa TANESCO na hasa kwa baadhi ya watu kuja na kupiga picha katika moja ya bango la Mradi

Monday, January 15, 2024

MLIPUKO WA KIPINDUPINDU KATIBU TAWALA ATINGA SOKO LENYE PILIKA NYINGI MWANZA KUTOA ELIMU & MAKATAZO

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Thomas Salala:- - "Inafika wakati tuchukuwe hatua kwaajili ya maslahi mapana ya watu wetu" - "Kipindupindu kinazuilika, tusipochukuwa tahadhari za usafi huu ugonjwa tutakaa nao kwa muda na makatazo yatakuwa mengi na hii itakuwa hasara kwenu, tusioneane aibu kwenye mabo ya msingi" Afisa wa Mazingira Mkoa wa Mwanza:- - "Kama tulivyofanya kipindi cha COVID kila mwananchi ahakikishe kwenye eneo lake ana chombo cha maji ya kunawa na sabuni pamoja na chombo cha kutupia taka" - Katazo limeshatoka kwa wafanyabiashara wanaotembeza maembe, karanga na ndizi huku wakipanga chini, tukikunasa jela miezi 6 inakuhusu na hakuna kutozwa faini" #kipindupindu #mwanza #samiasuluhuhassan

TAARIFA KWA UMMA


MUMANGI CONSTRUCTION CO LTD
P.C BOX 699
MWANZA.


- KATIKA SIKU ZA HIVI KARIBUNI, BAADHI YA MITANDAO YA KIJAMII IMEKUWA IKITOA TAARIFA KUHUSU KIJANA AITWAE OBBY AU MAMANGI ZIKIMTUHUMU JIHUSISHA NA VITENDO VYA UTAPELI

- KAMPUNI YA MUMANGI CONSTRUCTION INAPENDA KUUJULISHA UMMA KUWA HAINA MTUMISHI AU NDUGU ANAYEITWA OBBY AU MUMANGI, HIVYO KAMPUNI  HAIHUSIKI NA JAMBO LOLOTE LINALOFANYWA NA HUYO MTU ANAYEJITAMBULISHA KAMA 'OBBY'

- KAMPUNI YA MUMANGI INATOA TAHADHALI KWA WATU AU KIKUNDI WANAOTOA TAARIFA ZA KUICHAFUA KAMPUNI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUACHA MARA MOJA

- TAYARI KAMPUNI YA MUMANGI IMEMWELEKEZA MWANASHERIA WAKE KUCHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA ZA KUFUNGUA KESI MAHAKAMAN KUDAI, FIDIA.

TOA TAARIFA PINDI UNAPOKUTANA NA KADHIA TAJWA HAPO JUU.

IMETOLEWA NA UONG02I WA 

MUMANGI CONSTRUCTION CO. LTD

Sunday, January 14, 2024

RC PWANI AZINDUA RASMI MRADI MKUBWA WA KILIMO CHA PAMBA RUFIJI

 VICTOR MASANGU PWANI 

 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge  amezindua  Mradi wa kilimo cha Pamba Wilayani  Rufiji utakaotekelezwa na Kampuni ya Rufiji Cotton Ltd ambapo uzinduzi huo umeambatana na kupokea matrekta na pikipiki zitazotumika kwenye mradi huo.

Akizungumza na Wanachi wa Rufiji wakati wa hafla hiyo, Mhe Kunenge amewapongeza wawekezaji  hao kutoka India kwa uwekezaji huo amesema hana shaka na mwekezaji  huyo kwa sababu ni mzoefu kwenye sekta ya Pamba.



Kunenge amesema  kuwa  kwenye historia Pamba ilianza kulimwa Nchini  kwa mara ya kwanza wilayani Rufiji mwaka 1964 Amesema kuwa  Serikali ipo tayari kuumpa ushirikiano  mwekezaji na  kimtaka mwekezaji Afanye  yote aliyoahidi.

 Ameeleza Kupitia uwekezaji huo vijana watapata ajira, Kodi kwa serikali na ujuzi. Ameeleza kuwa  kwenye kipaumbele chake kwa Mkoa wa Pwani Kilimo ni kipaumbele na bado hakijafanya vizuri. 

Pia amepongeza wilaya ya Rufiji kwa  kuendelea  kuwapokea wawekezaji kwa sasa wilaya hiyo ina wawekezaji wakubwa wa Kilimo cha Sukari, na Kilimo cha Pamba. Kunenge amewataka wakazi wa Rufiji kutumia fursa hizi walizopata. Amewapongeza  wakazi wa chumbi kwa kuwezesha uwekezaji huo.
Naye Mkurugenzi  Mkuu wa Bodi ya Pamba  Bw. Wille Mtunga  ameeleza kuwa ziara ya India ya Mhe Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan imezaa matunda na leo tunazindua mradi wa Pamba Rufiji.  

 Alisema  kuwa  ili kuwa na kilimo bora wameleta timu ya  ushindi ambao ni maafisa ugani 24  watakao hudumu kwenye vijiji hivyo  24. ameeleza kuwa  Mpaka sasa wamesajili wakulima wenye jumla ya  Hekari 3012 wilayani Rufiji.

Naye Balozi wa  zao la Pamba  Nchini Mhe Aggrey Mwanri, ametuma Salaam kwa Mhe Rais  Dkt Samia za pongezi kwa kuvutia uwekezaji katika sekta ya Pamba. 

Ameeleza kuwa kazi yake  kama balozi ni kufanya pamba ipendeke kwa wananchi wote. Ameeleza wamechukua takwimu za wananchi wote wa Rufiji waliotayari kulima Pamba. 

Ameeleza kuwa Kilo zinazozalishwa  wilayani Rufiji ni laki moja na kiwanda  kitakacho jengwa kitahitahi kilo laki tano. Ameeleza  kuwa Halmshauri hiyo ikilima pamba vizur itapata ruzuku amehamasisha vijana wote kulima pamba na wale maafisa ugan 24 walioajiriwa kuhakikisha wanafanya kazi iliyokusudiwa.

Naye Mkurugenzi  Mkuu wa Kiwanda cha Rufiji Cotton Ltd  Bw Hassan Kinje   ameeleza  kuwa wamekuja kuwekeza Rufiji kwa sababu ya Mazingira mazuri ya uwekezaji, ameeleza kuwa wamekuja kulima Rufiji na si Kununua Pamba. Ameeleza kuwa kampuni hiyo itatoa uwezeshaji wa huduma bure ya  matrekta kwa ajili ya kilimo. 
Aidha wameajiri maafisa ugani 24  na kutoa pikipiki ambazo zitatumika kutoa  elimu kwa wakulima. Ameeleza kuwa  wanategemea kujenga kiwanda cha kuchambua Pamba, kiwanda vya nguo. Wamepongeza ushirikiano mkubwa walioupata kutoka katika uongozi  wa Mkoa katika kufanikisha uwekezaji huo.