ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 25, 2025

UWASHWAJI WA MWENGE WA UHURU KITAIFA PWANI MAMBO KUCHELE MAANDALIZI TAFIKIA ASILIMIA 96

 NA VICTOR MASANGU/PWANI 

Serikali Mkoani Pwani imesema kwamba maandalizi kwa ajili ya tukio kubwa la sherehe za uwashwaji wa Mwenge wa uhuru kitaifa yanakwenda vizuri na kwamba yamefikia kiwango cha asilimia 96 na kwamba unatarajiwa kuwashwa  rasmi April 2 mwaka huu katika viwanja  vya shirika la Elimu Kibaha.  
 

WAKAGUZI WA NDANI WALIA 'MABOSI' KUPUUZA USHAURI WAO

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Tabia ya baadhi ya wakuu wa taasisi na mashirika ya Serikali kupuuza mapendekezo ya wakaguzi wa ndani (Internal Auditors) imetajwa kuwa chanzo cha taasisi nyingi za Serikali kupata hati chafu kwenye Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kila mwaka. Tabia hiyo imebainishwa jana Jumatatu Machi 24, 2025 na rais wa Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani ya Kimataifa nchini Tanzania (IIA), Dk Zelia Njeza wakati wa uzinduzi wa mkutano wa wakaguzi wa ndani unaofanyika kwa siku tano kuanzia Marchi 24 hadi Machi 28, 2025. Dk Njeza ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania, amesema wakaguzi wa ndani wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, hata hivyo wamekuwa wakikumbana na vikwazo vya wakuu wa taasisi ama mashirika kutozingatia mapendekezo na ushauri.

MAAJIBU YA MASWALI MUHIMU KUIJUA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI ZIKIWEMO ADHABU KWA WATAKAO KAIDI

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) inaendeleza mkakati wake wa kutoa elimu kwa Umma kuhusu Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini kwa kuzungumza na waandishi wa habari waliopo jijini Mwanza. Akifungua semina ya siku moja ya waandishi wa habari jijini Mwanza Jumamosi, Machi 22, 2025 Mkurugenzi Mkuu wa PDPC, Dkt. Emmanuel Mkilia amewapa Waandishi wa Habari mbinu bora za kuzingatia ili wafanye kazi kwenye Maadili na Misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini. Pia Dkt. Mkilia amejibu baadhi ya maswali muhimu yaliyoulizwa na waandishi wa habari ili yatumike kama msaada wa utoaji wa elimu kwa jamii. MASWALI 1. Jeh ni taasisi ngapi nchini Tanzania zinapaswa kujisajili, mpaka sasa taasisi ngapi zimejitokeza na hali iko vipi kwa mkoa wa Mwanza? 2. Mwisho wa kujisajili ni lini? 3. Kwanini watanzania wanapaswa kuwa na matumaini na Tume hii? 4. Jeh taasisi kubwa ni zipi na taasisi ndogo ni zipi? 5. Kwa ambao hawatakuwa wamejisajili baada ya muda wa usajili kupita ni adhabu gani watakazokutana nazo? 6. Tunaelekea katika duru za Uchaguzi Mkuu wa 2025 hapa nchini, nini rai yako kwa waandishi wa habari na wanasiasa katika kutimiza wajibu wao? 7. Jeh taasisi zinajisajili wapi na vipi? Mhandisi Stephen Wangwe ni Mkurugenzi wa usajili na uzingatiaji PDPC anatoa majibu. ........................................................................................................................ “Ili kuhakikisha kuwa mnazingatia maadili na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni muhimu kuzingatia mbinu bora zikowemo kujiridhisha na vyanzo vya habari kabla ya kuchapisha taarifa inayohusu mtu binafsi, hakikisheni kuwa chanzo ni sahihi na kinazingatia Sheria. Pia tumieni mifumo salama ya kuhifadhi na kusambaza taarifa ili kuhakikisha kuwa taarifa za watu hazivuji” amesema Dkt. Mkilia Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi nchini, ilianzishwa rasmi tarehe 01 Mei, 2023 kufuatia kupitishwa kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Na. 11, 2022.

MSIGWA AKANUSHA TAARIFA ZA KURUDI CHADEMA.

 

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Peter Msigwa amekanusha vikali taarifa zilizosambaa mitandaoni zikidai kuwa amerejea katika chama chake cha zamani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). 

Uvumi huo umeenea kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii, lakini baadaye Mbunge huyo wa zamani wa Iringa Mjini, alizikanusha rasmi.

KUPITIA AKAUNTI YAKE YA X ALIANDIKA:-

"Puuzeni uvumi wowote unaotengenezwa na kuenezwa dhidi yangu kuhusu mustakabali wangu wa kisiasa. Hakuna mtu niliyemteua kuwa msemaji wangu kwa mambo ya kisiasa. Msijibebeshe majukumu ya kunisemea huku mkijua ninao uwezo wa kujisemea mwenyewe. Ni kijani, kijani, I’m here to stay."

Akizungumza na Nipashe Digital kwa njia ya simu, Msigwa amesisitiza kuwa hana mpango wa kurudi CHADEMA, na kudai kuwa taarifa hizo ni njama za wapinzani wake wa kisiasa wanaotaka kumchafua ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Niliondoka nikiwa na akili yangu timamu, siwezi kurudi CHADEMA kamwe. Kile kilichosambazwa mitandaoni ni uzushi wa kutengeneza. Wanataka kuniharibia huku niliko," amesema Msigwa.

Alipoulizwa kama amewahi kuombwa kurejea CHADEMA, alikiri kupokea maombi kutoka kwa wanachama wa chama hicho, lakini akaweka wazi kuwa hatarudi.

"Ni kweli wanachama wa CHADEMA wananiomba sana nirejee, lakini siwezi kamwe kurudi tena huko," amesisitiza.

Hata hivyo, Msigwa amebainisha kuwa urafiki wake na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, utaendelea, lakini hilo halimaanishi kwamba atarejea kwenye chama hicho.

Mchungaji Msigwa alihama kutoka CHADEMA na kujiunga na CCM mwezi Juni mwaka jana.



Monday, March 24, 2025

SERIKALI YAJA NA MBINU KUWABANA MATAPELI WANAOTUMIA MAJINA YAWATU & TAARIFA ZAO BINAFSI KUJINUFAISHA

 NA ALBERT GSENGO/MWANZA

"Kupitia 'Jamii Portal' kila mwananchi anakuwa na urahisi wa kujuwa taarifa zake zimetumika wapi" "Jamii Portal ni application itakayo mruhusu kila mtu kuangalia taarifa zake zilitumika wapi, kwanini na jeh aliridhia au hakuridhia na kama taarifa zilitumika sehemu na hakuridhia basi atawasiliana na tume kutoa taarifa na hatua za kisheria kufuatwa ikiwa ni pamoja na uwajibishwaji" Dkt. Emmanuel Mkilia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Tanzania (PDPC) ameyasema hayo wakati akifungua mkutano na semina ya Waandishi wa Habari jijini Mwanza ambapo tume hiyo imewaandalia ili kuwajengea uwezo juu ya majukumu ya tume hiyo nyeti.

WANAHABARI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA KURIPOTI TAARIFA BINAFSI

 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Tanzania (PDPC) Dkt. Emmanuel Mkilia amewataka waandishi wa habari kuzingatia sheria ya Tume hiyo katika kutoa taarifa binafsi za wananchi ili kulinda utu na faragha.

Dkt. Mkilia ametoa rai hiyo Jumamosi ya Machi 22, 2025 wakati akifungua mkutano na semina ya Waandishi wa Habari ambao tume hiyo imewaandalia ili kuwajengea uwezo juu ya majukumu ya tume hiyo nyeti.


Amesema, kuna madhara ya kijamii na hata kiuchumi endapo faragha za mtu zitazagaa bila ya ruhusa yake hivyo ni wasaa mzuri sasa wanahabari kufahamu sheria iliyoanzisha Tume hiyo na kuzingatia.

Ameongeza kuwa, pamoja na changamoto za kidigitali ambazo zinakuja kwa kasi Duniani kote bado wanahabari na wananchi wote wana wajibu wa kulinda siri za mtu ili kulinda utu wake pasipo kuathiri biashara ya kimtandao.


“Tumekuja Mwanza pamoja na mambo mengine tumekuja kuwajengea uwezo taasisi mbalimbali ili wapate uelewa wa sheria iliyoanzisha tume hii mwaka 2022 kwa sheria namba 11 na ikaanza kazi rasmi Mei 01, 2023 pamoja na uelewa wa ujumla wa ulinzi wa taarifa binafsi.” Dkt. Mkilia.


Akiwasilisha mada ya asili ya tume hiyo, Mhandisi Stephen Wangwe amebainisha kuwa Mkoa wa Mwanza upo chini kwa taasisi zake kujisajili kwenye mfumo wa tume hiyo na kwamba hali hiyo inatoa kiashairia kwamba Taarifa za watu bado haziko salama.

Semina hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza huku ikilenga kutoa fursa kujifunza na kujengeana ulewa wa kina jinsi ya kulinda faragha za watu katika kazi za habari.

Sunday, March 23, 2025

TETE FOUNDATION YAGAWA MAHITAJI /VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI WALIOPO KATA YA MIONO,CHALINZE -PWANI KWA MWAKA 2025

 

TETE FOUNDATION kupitia mradi wake wa “TUNAAMINI KATIKA WEWE” wamekuwa wakigawa mahitaji/vifaa vya shule kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wenye uhitaji maalumu kwa kuhakikisha mtoto hakosi shule mwaka mzima kwa sababu ya kutokuwa na mahitaji ya shule (Sare za shule, madaftari, Begi, viatu n.k)......


Mradi huu wa “Tunaamini katika wewe” unao  dhaminiwa na Kampuni ya Reliance Insurance kwa takribani miaka mitatu sasa, umeongeza ufaulu wa watoto mashule na kupunguza utoro mashuleni 

Zoezi hili la ugawaji wa mahitaji ya shule ulienda sambamba na Bonanza la Michezo lililojumuisha shule za msingi na Sekondari zilizopo katika kata ya Miono lililokuwa na dhumuni la kuwaleta watoto pamoja ili kuweza kutambuana na kushirikiana kwenye masomo ili kukuza ufaulu mashuleni

Imetolewa na Afisa Habari