ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 27, 2025

GENERATION SAMIA, PPRA WASHIRIKIANA KUTOA ‘KONEKSHENI’ YA TENDA ZA SERIKALI MWANZA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Generation Samia kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) watafanya Kongamano la Wazi la Fursa za Uchumi, litakalobeba ujumbe wa ‘Mgao wa 30% za Samia Kupitia Mfumo wa NeST’, likalofanyika Machi 29, 2025, Kwa Tunza Beach, jijini Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Msemaji wa Generation Samia, Bi. Sonnatah Nduka amesema lengo la kuandaa kongamano hilo linalotajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wakaazi wa Mwanza ni kuwafikishia ujumbe wananchi kuhusu uwepo wa fursa za tenda za Serikali zilizotengwa kwa ajili ya makundi maalum ambayo ni Wanawake, Wazee, Vijana na Watu Wenye Ulemavu zinazopatikana kupitia Mfumo wa NeST. Akizungumzia sababu ya kuita ‘Mgao wa 30% ZA Samia Kupitia Mfumo wa NeST, amesema hatua hiyo inatokana na ukweli kuwa katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ndipo Mfumo wa NeST ulijengwa na Sheria mpya ya ununuzi wa umma ilitungwa ikitoa fursa kwa makundi maalum kwa haki na usawa. “Watanzania ambao hawawezi kuwa na makampuni wamepewa nafasi ya kupata tenda kwa kuunda vikundi na kujisajili kwenye Mfumo wa NeST. Asilimia 30 ya bajeti ya ununuzi wa Serikali imetengwa kwa ajili ya makundi haya maalum. Naye Meneja wa PPRA Kanda ya Ziwa, Mhadisi Juma Mkobya alisema taasisi hiyo itawaeleza kwa kina watanzania kwenye jukwaa hilo jinsi ya kupata tenda za Serikali na itatoa huduma za usajili kwenye Mfumo wa NeST kwa washiriki watakohitaji na watakaokidhi vigezo. Kongamano hilo litahudhuriwa na Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, na wananchi kutoka makundi mbalimbali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.