ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 12, 2017

BREAKING NEWS: KARIA RASMI RAIS WA TFF

Wallace Karia amewabwaga wapinzani wake na kushinda nafasi ya rais wa TFF ambapo baada ya uchaguzi huo aliapishwa. 

  Michael Wambura ameshinda nafasi ya makamu rais wa TFF na hapa ni wakati akiapishwa.
 
Rais mpya wa TFF Wallace Karia (kulia) akiwa na wandishi wetu Jembe Fm Radio kipindi cha Sports Ripoti Juma Ayoo (kushoto).


SAFU KAMILI:- 
President: Wallace Karia 
Vice President: Michael Wambura 
Zone 1: Saloum Chama 
Zone 2: Vedastus Lufano 
Zone 3: Mbasha Matutu 
Zone 4: Sarah Chao 
Zone 5: Issa Bukuku 
Zone 6: Kenneth Pesambili 
Zone 7: Elias Mwanjala 
Zone 8: James Mhagama 
Zone 9: Dunstan Mkundi 
Zone 10: Mohamed Aden 
Zone 11: Francis Ndulane 
Zone 12: Khalid Abdallah 
Zone 13: Lameck Nyambaya

SEKTA YA UREMBO JIJINI MWANZA YAPATA MWEKEZAJI WA NGUVU NI ROSLY BEAUTY STUDIO.

MGENI rasmi Mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula akikata utepe kuashiria uzinduzi wa studio mpya ya kisasa kwaajili ya kunakshi katika masuala ya urembo kwa viwango vya juu kwa akinamama na akinadada katika hafla iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza, pembeni ni mkurugenzi wa Rosly Beauty Studio Bi. Alphoncina. Salon hiyo ya kisasa inapatikana barabara ya Hesawa, Jengo la Afya Radio, pande za Capri Point Nyamagana jijini humo. 

Katika hotuba ya ufunguzi aliyoitoa Mhe. Mabula amesema taifa linapo sisitiza wananchi wake kuchangamkia fursa hivi ndivyo inavyo maanishwa, ajira moja kubwa inaweza kuzalisha ajira kwa vijana wengine ..... "Ili kupata mafanikio vijana hatuna budi kushikana mikono na sote tukatembea pamoja, Alphoncina lazima tumsapoti, tusipomsapoti hatoendelea, biashara itasimama na ikisimama, hatutokuwa na kitu cha kujivunia" ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA ALICHOSEMA
Mkurugenzi wa Rosly Beauty Studio Bi. Alphoncina amesema kuwa moja ya sababu za uwekezaji wake ni kutaka kuupaisha mkoa wa Mwanza kwenye level zinazo hitajika kitaifa na kimataifa, saloon nyingi zimekuwa za viwango vya chini nazo huduma zikitolewa bila weredi wa fani, ameona uhitaji wa wakazi wa Kanda ya Ziwa ni makubwa hivyo akaamua kuja na kitu kipya chenye viwango na unafuu katika bei.
Kabla ya uzinduzi wa Rosly Beauty Studio, Saloon ya kisasa inapatikana eneo la Capri Point Nyamagana jijini Mwanza.
Kabla ya uzinduzi wa Rosly Beauty Studio, Saloon ya kisasa inayopatikana eneo la Capri Point Nyamagana jijini Mwanza.
Msimamizi katika ujenzi Kabula Kazi alifunguka juu ya changamoto za mafundi wakati wa ujenzi wa Rosly Beauty Studio, Saloon ya kisasa iyonapatikana eneo la Capri Point Nyamagana jijini Mwanza.
Rose Lulangwa ni mmoja wa wanawake wawekezaji katika sekta ya upambaji jijini Mwanza akitoa uzoefu wake jinsi alivyo pambana kwenye ujasiliamali hata hii leo akiwa ni shuhuda wa kazinzuri ya mdogo wake katika kazi mwekezaji mpya wa Rosly Beauty Studio, Saloon ya kisasa iyonapatikana eneo la Capri Point Nyamagana jijini Mwanza.
Pale sisters wanapokutana what do you expect....?
 Mwanabure ambaye ni sasa ni mwekezaji mkubwa wa sekta ya uokaji vitafunwa jijini Mwanza akifunguka juu ya uzoefu wake.
Sisters ndani ya hafla.
Mvinyo nao ulihusishwa kunakshi furaha za wadau waliohudhuria uzinduzi wa Rosly Beauty Studio.
The area.
Flowers.
Mgeni rasmi Mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula akisaini kitabu cha uzinduzi mara baada ya kukamilisha zoezi hilo eneo la Capri Point Nyamagana jijini humo.
Muonekano wa ndani wa Rosly Beauty Studio. Salon ya kisasa inayopatikana Capri Point Nyamagana jijini Mwanza.
"Karibu tukuhudumie"
"Wewe ni mtu muhimu sana kwetu"
Huduma nadhifu ziko hapa iwe kwa maharusi, wadau kawaida au kwa mitoko ya usiku basi hakuna tena shida.
Mambo ya massage.
Bango linasema na wewe.
Hafla ilipendeza nao waalikwa wali-enjoy vya kutosha.

Tufuate kupitia instagram @makeupbyrosly_mwanza

About Rosly Beauty Studio


The Beauty Studio is set inside Afya Radio department in Capri Point Nyamagana Mwanza.

Bi. Alphoncina established the business 4th of this August 2017 and her highly skilled team. They pride themselves on their strong local reputation for luxury professional treatments in a friendly, relaxing setting. They only use the latest techniques and products.


The Rosly Beauty Studio team are dedicated to providing you with professional services to help you look and feel amazing whether it is a new set of acrylic nails or a relaxing massage.
KARIBU SANA.

MBUNGE RIDHIWAN KIKWETE ATINGA KWENYE SOKA.

 
MBUNGE wa Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete juzi aligawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo la chalinze zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya bagamoyo. 

Sherehe hizo zilizofanyika kimange zilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Madiwani wote wa Jimbo la Chalinze na watendaji wao wa kata ambao walipokea jezi kwa niaba ya timu zao. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye muandaaji mkuu wa mashindano hayo akishirikiana na wabunge wa majimbo yote

Pamoja na kugawa jezi , mbunge wa chalinze aliahidi kumpatia zawadi mshindi wa pili wa mashindano hayo ya kombe la Mazingira,  pilkipiki ya Miguu miwili, na jezi kwa timu zote 3 za juu kufuatia mkuu wa wilaya ya Chalinze, kutoa zawadi ya mshindi wa kwanza pikipiki aina ya Toyo ya miguu mitatu ili itumike kwa shughuli za kipato na ujasiliamali kwa vijana.

ZIFUATAZO NI PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO HILO.





 



"Tangu utotoni nimejifunza mengi katika soka la mchangani, ni soka lenye asili ya mpira, huku tunashuhudia vipaji jicho kwa jicho yaani ana kwa ana, tunaona ufundi wa kiushindani wa mtu mmoja mmoja na timu kwa ujumla" Alisema Ridhiwan 

Kisha akaongeza kwa kusema "Kupitia soka la mchangani napata faraja na burudani kushuhudia vijana wakiweka ushindani wa dhati, nimeziona changamoto nami nimeona sina budi kuingia mfukoni na kuwasogeza japo mahala ili watimize ndoto zao, na kweli faraja yangu imetimia"  

UHURU AREJEA IKULU YA KENYA, RELI NYINGINE YA KISASA KUJENGWA, KIBANO CHA MAKINIKIA KUTUA TANZANITE.

Uhuru arejea Ikulu ya Kenya, Reli nyingine ya kisasa kujengwa, Kibano cha makinikia kutua Tanzanite.
 
Wachimbaji waishitaki Tanazanite One Bungeni, Maalim ala mweleka tena, Kilichomgharimu Odinga uchaguzi 2017, Rostam Matatani. Habarika na dondoo hizi za magazeti ya leo hapa;

HII NDIYO MIKAKATI YA KIWANDA CHA KUCHAMBUA MBEGU ZA PAMBA CHA QUTON KUMWEZESHA MKULIMA KUMKWAMUA MKULIMA ILI KUPATA TIJA KUPITIA ZAO LA PAMBA.

Mkurugenzi wa bodi ya pamba Kanda ya Magharibi Jones Bwahama akionesha mfuko wa ujazo wa kilo 6 wenye mbegu mpya aina ya UKM 08 toka kampuni ya Quton, mbegu hii tayari imefanyiwa majaribio na kuwa na sifa ya kuota bila kubahatisha nayo imekuja sokoni sasa kwaajili ya kuiondosha ile ya zamani iliyojulikana kama UKM 91.
Mbegu mpya aina ya UKM 08 toka kampuni ya Quton, ikiwa kwenye sahani ya maonesho, mbegu hii tayari imefanyiwa majaribio na kuwa na sifa ya kuota bila kubahatisha nayo imekuja sokoni sasa kwaajili ya kuiondosha ile ya zamani iliyojulikana kama UKM 91 pamoja na ile ya manyoya.
Tanzania imekuwa ikipoteza mbegu nyingi sana wakati wa upandaji kutokana na matumizi ya mbegu hizi za manyoya ambazo hazijachambuliwa kubaini yapi ni makapi lakini sasa kuna mikakati ya kuziondosha mbegu hizi zisizochambuliwa na kuziingiza zile za uhakika.
Mbegu iliyochambuliwa aina ya UKM 08 ambayo haijawekwa dawa toka kampuni ya Quton,  mbegu hii tayari imefanyiwa majaribio na kuwa na sifa ya kuota bila kubahatisha nayo imekuja sokoni sasa kwaajili ya kuiondosha ile ya zamani iliyojulikana kama UKM 91 pamoja na ile ya manyoya.
Meneja wa uzalishaji mbegu mpya toka kampuni ya Quton, Phineas Chikaura akitoa maelezo kwenye moja ya shamba darasa, ambalo ndilo wanalofanyia majaribio katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Waandishi wa habari wakichukuwa taswira za ukuaji wa mbegu zilizopandwa kwenye moja ya shamba darasa, ambalo ndilo wanalofanyia majaribio katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mtaalamu wa mbegu kiwanda cha Quton, Upendo Matulanya akitoa maelezo mbele ya waandishi wa habari juu ya uotaji na ukuaji wa mbegu mpya aina ya UKM 08 kwenye moja ya shamba darasa, ambalo ndilo wanalofanyia majaribio katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Hivi ndivyo mbegu aina ya UKM 08 inavyochipua katika shamba la majaribio.
Katika shamba hili mbegu aina mbalimbali zimepandwa kwaajili ya majaribio, kuanzia zile zenye manyoya, zile ambazo hazijapakwa dawa na mbegu mpya aina ya UKM 08.
Ndani ya chumba maalum cha kupandia mbegu toka kampuni ya Quton, na hapa ni majaribio ya uotaji wa mbegu aina ya UKM 08 ndani ya eneo la kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mtaalamu wa mbegu kiwanda cha Quton, Upendo Matulanya akitoa maelezo ndani ya chumba maalum cha kupandia mbegu toka kampuni ya Quton, juu ya majaribio ya uotaji wa mbegu aina ya UKM 08 ndani ya chumba hicho kilicho ndani ya eneo la kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mara baada ya kupata elimu ya shamba darasa safari ya waandishi wa habari ilielekea kwenye kiwanda cha uzalishaji pamba.
Meneja wa uzalishaji mbegu mpya toka kampuni ya Quton, Phineas Chikaura akitoa maelezo kwenye moja ya maghala ya kuhifadhi na kuchambua mbegu za pamba katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Wanahabari ndani ya katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Muonekano wa ndani kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Mratibu mkuu wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea kiwanda cha uzalishaji mbegu toka kampuni ya Quton, Bw. Kyaruzi akiwa ndani ya katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Pamoja na uzalishaji wa mbegu za pamba zilizonyunyizwa dawa pia Kampuni ya Quton huzalisha mbegu zisizo na dawa kutokana na haki za kimazingira.
Mifuko ya mbegu za pamba katika kiwanda cha Quton Tanzania Limited kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Kiwanda cha Quton Tanzania Limited kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Msimamizi mkuu wa Kampuni ya uchambuzi wa mbegu za pamba Quton Tanzania Limited, Pradyumanshinh Chauhan, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho kinachohusika na uchambuzi na usindikaji mbegu za pamba kilichopo Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
NA: ALBERT G. SENGO
SIMIYU 
SERIKALI  inatarajia kuondoa mbegu ya pamba aina ya UK 91 isiendelee kutumika katika uzalishaji wa zao la pamba kutokana na mbegu hiyo kushindwa kuzalisha pamba nyingi na yenye ubora.

Mkurugenzi wa bodi ya pamba Kanda ya Ziwa Jones Bwahama ametoa kauli hiyo wakati waandishi wa habari walipotembelea kiwanda cha kuzalisha mbegu ya pamba cha Quton wilayani Bariadi mkoani Simiyu.


Amesema kuwa hivi sasa bodi ya pamba kwa kushirikiana na wadau wa zao hilo wanajipanga kuongeza uzalishaji wa mbegu ya sasa inayofanya vyema kwenye kilimo aina ya UKM 08  ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2019 mbegu aina ya UK 91 iwe imeshaondoka kwenye mzunguko wa matumizi kwa wakulima. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
 



Bwahama ameongeza kuwa mkakati wa bodi ya pamba ni kuhakikisha kuwa uzalishaji wa zao la pamba unaongezeka ikiwa ni sambamba na kasi ya kilimo cha mkataba. 

BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
 


 

Phiniazi Kaula ni meneja wa mashamba ba ubora wa mbegu kutoka kampuni ya
QUTON anazungumzia hatua ambazo zinazochukuliwa kwaajili ya kuongeza uzalishaji wa mbegu aina ya UKM 08.
BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.


 

Mbegu iliyopo kwaajili ya uzalishaji wa zao la pamba imezalishwa mwaka 1990 na mbegu hiyo imekuwa haizalishi  vya kutosha na kutoa pamba sawia kama vile inavyotakikana, jambo ambalo limechangia kudidimiza uzalishaji wa zao hilo na kuwafanya baadhi ya wakulima kukata tamaa ya kuzalisha zao hilo.