MBUNGE wa Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete juzi aligawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo la chalinze zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya bagamoyo.
Sherehe hizo zilizofanyika kimange zilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Madiwani wote wa Jimbo la Chalinze na watendaji wao wa kata ambao walipokea jezi kwa niaba ya timu zao. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye muandaaji mkuu wa mashindano hayo akishirikiana na wabunge wa majimbo yote
Pamoja na kugawa jezi , mbunge wa chalinze aliahidi kumpatia zawadi mshindi wa pili wa mashindano hayo ya kombe la Mazingira, pilkipiki ya Miguu miwili, na jezi kwa timu zote 3 za juu kufuatia mkuu wa wilaya ya Chalinze, kutoa zawadi ya mshindi wa kwanza pikipiki aina ya Toyo ya miguu mitatu ili itumike kwa shughuli za kipato na ujasiliamali kwa vijana.
ZIFUATAZO NI PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO HILO.
"Tangu utotoni nimejifunza mengi katika soka la mchangani, ni soka lenye asili ya mpira, huku tunashuhudia vipaji jicho kwa jicho yaani ana kwa ana, tunaona ufundi wa kiushindani wa mtu mmoja mmoja na timu kwa ujumla" Alisema Ridhiwan
Kisha akaongeza kwa kusema "Kupitia soka la mchangani napata faraja na burudani kushuhudia vijana wakiweka ushindani wa dhati, nimeziona changamoto nami nimeona sina budi kuingia mfukoni na kuwasogeza japo mahala ili watimize ndoto zao, na kweli faraja yangu imetimia"
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.