ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 4, 2023

HOSPITALI YA BUGANDO YAELEMEWA NA WAGONJWA WA NJE, YAJA NA MWAROBAINI WA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA YANUNUA MABASI MAWILI YA KISASA

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA "Wazo la kuanzisha klinini ya Madaktari Bingwa Bugando lilianza baada ya bodi ya uendeshaji ya hospitali kwa kushirikiana na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kufanya maboresho makubwa ya huduma za matibabu na kupelekea kuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa, hasa wagonjwa wa nje. Ambapo kwa sasa tunapokea takribani wagonjwa wa nje 810 kwa siku sawa na wagonjwa 24,000 kwa mwezi na lengo letu la mbeleni ni kupokea zaidi ya wagonjwa wa nje 30,000 kwa mwezi" amesema Dr. Fabian Massaga, Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Bugando, kisha akaongeza..... "Ongezeko hili la wagonjwa lilisababisha bodi ya uendeshaji wa Hospitali kupata wazo la kuanza kufungua matawi mbalimbali ili kupunguza msongamano wa wagonjwa ndani ya hospitali mama Bugando, ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa huduma za afya na kuzisogeza kwa ukaribu zaidi ili kuwafikia wananchi wote"

Muonekano wa jengo la kliniki ya 'Bugando Specialized Polyclinic' iliyopo Nera jijini Mwanza.

Ukarabati, ununuzi wa mashine za kisasa, dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na uwekezaji mzima uliofanyika katika kliniki hiyo mpya ya 'Bugando Specialized Polyclinic' imegharimu takriban shilingi bilioni 2.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi akizindua moja ya mabasi mawili yaliyonunuliwa na Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwaajili ya wafanyakazi wake, hii ni mara baada ya kuzindua jengo la kliniki ya 'Bugando Specialized Polyclinic' iliyopo Nera jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Dr. Fabian Massaga 'akipiga gia' kwa moja ya mabasi mawili yaliyonunuliwa na Hospitali hiyo kwaajili ya wafanyakazi wake, hii ni mara baada ya kuzindua jengo la kliniki ya 'Bugando Specialized Polyclinic' iliyopo Nera jijini Mwanza.

Pozi la Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi mara baada ya kuzindua mabasi mawili yaliyonunuliwa na Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwaajili ya wafanyakazi wake, hii ni mara baada ya kuzindua jengo la kliniki ya 'Bugando Specialized Polyclinic' iliyopo Nera jijini Mwanza.

Wawakilishi wafanyakazi Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando.

Mabasi mawili yaliyonunuliwa na Hospitali ya Rufaa ya Bugando , yaliyozinduliwa hii leo sanjari na kuzindua jengo la kliniki ya 'Bugando Specialized Polyclinic' iliyopo Nera jijini Mwanza.


WATU 18 MBARONI WAKIWEMO WAALIMU KWA TUHUMA ZA KUIBA TSH 273 KWA MTANDAO.


Jumamosi, Machi 04, 2023


Jeshi la polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu 18 kwa tuhuma mbalimbali wakiwemo walimu wanane wa shule za msingi wanaodaiwa kuiba zaidi ya Sh273 milioni kutoka Benki ya Walimu (MCB) kwa njia ya mtandao Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amewaambia waandishi jijini Mwanza ijumaa Machi 3, 2023 kuwa walimu hao wanaotoka shule tofauti wanadaiwa kufanya wizi huo Februari 20, mwaka huu kwa kujihamishia fedha kwenye akaonti zao baada ya kuingilia mawasiliano na mfumo wa benki.

Amewataja wanaoshikiliwa na shule wanazotoka kwenye mabano kuwa ni Gasper Maganga (shule ya msingi Kilabela) Wilaya ya Sengerema, Marwa Mwita (shule ya msingi Nyitundu Sengerema), Masaba Mnanka (Shule ya Msingi Kilabela), Harold Madia (Bugumbikiswa), Clever Banda (Sekondari ya Nyamatongo Sengerema), Justin Ndiege (Shule ya Msingi Ishishangolo), Fredrick Ndiege (Pamba C) na Steven Sambali anayetoka shule ya msingi Nyangongwa.

SERIKALI YASEMA KILA MTOTO ANAYEZALIWA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO KUPIMWA USIKIVU WA MASIKIO BURE

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

1. Jeh ni magonjwa gani yanayojirudia kwa wagonjwa wengi wanaofika hospitalini hapo? 2. Hivi wajua kutoa nta kwenye masikio ni moja ya makosa tunayoyafanya bila kujua kuwa si salama kiafya na si sawa? 3. Licha ya wengine kuzaliwa na u-kiziwi na wengine kuupata ukubwani kutokana na mitindo ya maisha ikiwamo matumizi ya dawa bila kuwaona wataalamu, Jeh wajua kuwa unaweza kupata u-kiziwi kwa kurithi? ........................................................................................ ........................................................................................ HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO imeweka mkakati wa kukabiliana na tatizo la usikivu kwa kufanya upimaji kwa kila mtoto atakae zaliwa hospitalini hapo (New born hearing Screening), hivyo basi kila mtoto atakaezaliwa hospitalini hapa atapimwa uwezo wake wa kusikia kuanzia mwaka huu. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makiragi aliyemwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika hotuba yake aliyoisoma hii leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usikivu Duniani. TAKWIMU
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa mwaka 2020 ilipokea wagonjwa wenye changamoto ya usikivu 1635, kati yao asilimia 49.06% ni watu wazima (Kuazia miaka 18), asilimia 50.94% ni watoto. Kwa mwaka 2021 jumla ya wagonjwa walikua 856 kati yao asilimia 68.97% ni watu wazima, asilimia 31.03% ni watoto. Kwa mwaka 2022 jumla ya wagonjwa ni 970 kati yao asilimia 68.77% ni watu wazima na watoto ni asilimia 31.23 %. Takwimu zinaonesha ukubwa wa tatizo la usikivu wa masikio katika kanda na hata kitaifa. Juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanya na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ili kupambana na tatizo hilo, ikiwemo kuanzisha kitengo cha usikivu (Audiology Unit) hospitalini hapo mnamo mwaka 2016, na kuwapa matibabu ya kibingwa na kibingwa bobezi wagonjwa wanaofika.

Friday, March 3, 2023

DKT MSOWOYA AIKUMBUSHA JAMII KUHUSU MALEZI YA WATOTO


Mkurugenzi wa Msowoya Foundation akizungumza kuhusu malezi ya watoto
Mkurugenzi wa Msowoya Foundation akizungumza kuhusu malezi ya watoto
Mkurugenzi wa Msowoya Foundation akizungumza kuhusu malezi ya watoto

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mkurugenzi wa Msowoya Foundation, "Dkt Tumaini Msowoya"ameikumbusha jamii kuhusu malezi ya watoto.

Amesema mmomonyoko mkubwa wa maadili unatokana na malezi hafifu ya baadhi ya wazazi na walezi kutokana na ubize wa kazi bila kukumbuka watoto wao.

Akizungumza na wananchi wa baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Kilolo, Dkt Msowoya amesema watoto wanaweza kuwa salama ikiwa watalindwa na kufundishwa maadili mema.

"Kuna haja gani kwako kuwa bize wakati mtoto wako anaharibika? anafanyiwa ukatili wala huna habari? ukirudi nyumbani hoi hata muda wa kuongea nae huna, tubadilike ndugu zangu. Tukienda shambani basi tukumbuke tuna watoto," amesema na kuongeza;

"Sisi Msowoya Foundation tutaendelea kutoa elimu kwa jamij yetu, malezi ya watoto ndio ambayo yanaijenga kesho yenye watu wastaarabu na wenye utu," amesema.

Dkt Msowoya ni mwanaharakati wa haki za watoto, mwimbaji wa muziki wa Injili, mwanahabari nguli na mwanasiasa akishika nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa.

MNEC QWIHAYA: NITAWEKA TAA KUONDOA GIZA STENDI YA MABASI YA MAFINGA

 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Leonard Mahenda Qwihaya akikabidhiwa cheti cha pongezi kwa ushindi alioupata kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego wakati wa sherehe za pongezi

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Leonard Mahenda Qwihaya amesema ataweka taa ili kuondoa giza kwenye Kituo Cha Mabasi cha Mji wa Mafinga, Wilayani Mufindi.


Qwihaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Makampuni  ya Qwihaya amesema kwa hadhi ya mji huo hautakiwi kuwa stendi yenye  giza.


"Kwa Tanzania, mji wa Mafinga unaweza kuwa wa kwanza au wa pili kwa mapato kwa hiyo ni aibu kukosa taa za babarani kwa hiyo nitaweka  taa kwenye  stendi yote,"  amesema Qwihaya.


Qwihaya alitoa ahadi hiyo katika hafla ya pongezi iliyokuwa imeandaliwa na wananchi wa Mufindi kwa lengo la kuwapongeza viongozi wa CCM wa ngazi ya Mkoa na Taifa walio chaguliwa kutoka katika Wilaya hiyo.

Thursday, March 2, 2023

CCM YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA MADAKTARI HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO.

 

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani kulia akieleza jambo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhaman wakati wa  ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Tanga kutembelea Kambi ya Matibabu ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma walioweka kambi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo katikati aliyevaa koti la bluu ni Katibu wa Hospitali hiyo Abdiely Makange
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhaman akisikiliza maelezo kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani ambaye  hayupo pichani wakati wa  ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Tanga kutembelea Kambi ya Matibabu ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma walioweka kambi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Suleiman Mzee na kulia aliyesimama ni Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Abdiely Makange 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhaman akimsikiliza kwa umakini Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani  kulia aliyevaa koti jeupe na wa pili kushoto aliyevaa koti la bluu ni Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Abdiely Makange
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhaman akizingumza mara baada ya kutembelea kambi ya madaktari bingwa kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhamani akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhani akizungumza mara\ baada ya ziara hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajabu Abdurhamani
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa ya Jijini Dodoma Dkt Henry Humba ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu 



Na Mwandishi Wetu,Tanga.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimesema kwamba kinaridhishwa na utendaji mzuri wa madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa kuliko ilivyo kuwa miaka ya nyuma.

Akizungumza leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Tanga kutembelea Kambi ya Matibabu ya Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma walioweka kambi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Comred Rajab Abdurhaman alisema kwa sasa huduma zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa.

Alisema kwamba hivi sasa madaktari walikuwa wakijituma na kufanya kazi kwa ueledi mkubwa katika kuhakikisha wana wahudumia wagonjwa ambao wanakwenda kupata huduma hatua ambayo imepunguza kwa asilimia kubwa malalamiko.

"Nikiri Hospital ya Bombo sio ile tulioku tunaifikia zamani sasa hivi imebadilika sana kwa huduma maana yale malalamiko kwa wananchi yamepungua kwa asilimia kubwa na hata huduma zinazotewa wanaridhika nazo kwa kiasi kikubwa na madaktari wamekuwa msaada mkubwa kwao "Alisema Mwenyekiti huyo

Mwenyekiti huyo alisema kwamba wanamshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuboresha huduma katika Hospitali hiyo ikiwemo ununuzi vifaa vya kisasa vilivyopo kwa ajili ya uchunguzi ikiwemo Cstan ambavyo zamani havikuwep

Alisema kwamba ametembelea kambi hiyo na kujionea namna madaktari wanavyo wahudumia wagonjwa na hivyo kulazimika kutoa pongezi kwao na wale waliopo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.

Sambamba na hayo lakini amewapongeza madaktari bingwa waliotoka Hospitali ya Benjamini Mkapa kuja kuungana na madaktari bingwa waliopo kwenye Hospitali hiyo kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi

Aidha alisema wao kama watu waTanga wanawapongeza sana kwa maana kazi ya daktari na muuguzi ni wito hivyo mwenyezi Mungu atawalipa kwa yale yote mema mnayoendele kuwatendea watu wa Mkoa huo

"Tunampongeza Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu kwa sababu yeye ni sehemu ya kuchangia jambo hilo kwa asilimia kubwa madkatri wafika hapo kutoa huduma za za afya kwa wananchi wa Mkoa na mungu ambariki sana kwa juhudi zake hizi" Alisema

Hata hivyo alisema pia wanamshukuru Rais Samia Suluhu ruhusa yake alitoa baada ya Mbunge Ummy kumuomba na kumruhusi jambo hilo kuendelea.

Tagosine yafanya kweli kwa vitendo yamfagilia Rais Samia kukuza utalii wa ndani.



Na Victor Masangu,Pande 


Sekta ya utalii wa ndani hapa nchini Tanzania inazidi kukua kwa kasi kutokana na juhudi ambazo zinafanywa na Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu na mazingira ya kuwavutia watalii wa ndani na nje ya nchi.

Katika kuunga mkono jitihada hizo kwa vitendo Taasisi ya wasanii na waigizaji mbali mbali Tanzania (TAGOSINE) wameamua kufanya ziara maalumu kwa ajili ya kutembelea hifadhi ya pori la akiba la pande lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza na kujionea vivutio mbali mbali vilivyopo.

Wasanii hao Jafari Makatu na Cecilia Sengerema wakizingumza kwa nyakati tofauti walisema kwamba ziara hiyo imeweza kuwafumbua macho kutokana na kupata fursa mbali mbali kwa ajili ya kujionea vivutio vya aina yake vilivyomo katika hifadhi hiyo ya pande.

"Kwa kweli tunamshukuru Mwenyekiti weti David Msuya kwa kuona umuhimu wa kutukutanisha kwa pamoja na kuja katika ziara hii ambayo sisi kwetu tutàkuwa ni mabalozi wazuri katika kuitangaza hifadhi hii ya pande maana kumbe kuna Mambo mazuri katika utalii wa ndani.

Aidha Zainabu Yusuph ambaye ni mwanachama wa Tagosine alisema katika ziara hiyo wamejifunza Mambo mbali mbali ambayo watakwenda kuyafanyia kazi kupitia Sanaa zao ikiwa pamoja na kuendelea kumuunga Rais wa awamu ya sita katika kukuza utalii wa ndani.

Kwa Upande Afisa utalii wa hifadhi ya pori la akiba Mustafa Buyogera alibainisha kwamba kwa Sasa wamefanya maboresho makubwa kutokana na kupatiwa fedha na Rais Samia zaidi ya milioni 200  ambazo zimesaidia kujenga miundombinu ya majengo na kuboresha hifadhi hiyo ili kuwavutia watalii wa ndani.


Naye Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Tagosine amesema lengo kubwa la kufanya ziara hiyo ni kwenda kujifunza vitu vipya katika hifadhi hiyo ikiwa pamoja na kuweka mipango ya kuandaa filamu ambayo itaelezea utalii wa ndani lengo ikiwa ni kumpa sapoti Rais.

Pia Msuya alifafanua kuwa wameamua kuungana kwa pamoja kwa lengo la kuunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza na kuboresha utalii wa ndani.

Kufanyika kwa ziara hiyo na Taasisi ya Tagosine katika hifadhi ya pori la akiba la Pande ina lengo kubwa la kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita pamoja na kuwahimiza Watanzania kupenda vivutio vya kwao na kutembelea utalii wa ndani.

Wednesday, March 1, 2023

TMDA YAPIGA MSASA KWA WATOA HUDUMA MKOA WA IRINGA.

 

Felix zelote afisa usajili wa dawa na vifaa tiba ameelezea namna ya kufikisha matukio

Afisa wa mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba Elizabeth Mollel akitolea ufafanuzi kwa wataalamu wa afya kuhusu namna ya kuripoti kupitia fomu na namba ya simu ya bure pindi inapotokea madhara wakati wa utumiaji wa vifaa tiba.



Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mamlaka ya dawa na vifaa tiba [TMDA] Imetoa elimu ya kuhamasisha watumiaji wa vifaa tiba mkoa wa iringa ili kudhibiti madhara yatokanayo na vifaa tiba kupitia fomu na namba itakayotumika kutoa taarifa endapo kuna madhara yatajitokeza

Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo afisa usajili wa dawa na vifaa tiba Bw. Felix Nzelote amesema kuwa wanatoa elimu hiyo ili kudhibiti athari zinazojitokeza kutokana na vifaa tiba huku akibainisha mahali mgonjwa atakapotoa taarifa ndapo atapata madhara 

“Lengo ni kufikia wananchi au watumiaji wa vifaa tiba hapa nchini njia kubwa ni uhamasishaji katika vituo vyot vya kutola huduma na njia za kutoa taarifa kuna fomu zimeandaliwa ambayo ni ya orange ambayo tunakusanyia taarifa na namba ya free ambayo mtu atatumia ni 0800 110 084 pia USSD CODE ambayo ni *152*00#  ambayo utaselect pale itakuja afya unachagua TMDA utaingia utaweka taarifa ya kifaa kilicholeta changamoto mgonjwa anapopata madhara no la kutoa huduma anatoa taarifa alafu muhudumu anamsaidia kujaza" alisema 

Nzelote Godfrey mbangali ni mganga mkuu manispaa ya iringa na james joseph ni mratibu wa zoezi la utoaji wa elimu kimkoa walisema kuwa elimu hiyo itasaidia kutoa huduma iliyobora huku sababu ya athari za vifaa tiba visivyobora  ikiwa ni sababu ya kuanzisha kufikisha limu hiyo

“Hii inatusaidia tuweze kutoa huma bora na wito kwa watoa huduma wote tuto taarifa kweny vituo vya iringa wakitoa hizi taarifa inatusaidia sisi kuwapa taarifa tmda na kuwza kudhibiti hivi vifaa tiba ili hivi vifaa viwe bora na tutatoa huduma bora vitndanishi vikiwa havina ubora tunawza kupata majibu ambayo sio sahihi mwanzo hakukuwa na sehemu maalumu ya kuripotia vil vitu vipo au huwa vinakuwepo lakini kwa kukosa sehemu ambayo tunaweza kutoa taarifa ndiyo ilisababisha watu wakaingia katika mgogoro wa namna ile wa wauguzi kukwazana na hii itatusaidia watoa huduma za afya itasaidia sana kwa wateja hata wanapowkewa vitu kwenda navyo nyumbani wanatambua ubora wake"alisema Mbangali  

Kwa upande wake Mohammed Mang’una mganga mkuu Hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa alisema kuwa elimu hiyo iwe msaada wa kutambua muda wa matumizi ya vifaa tiba huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari pale vitakapopatikana vifaa tiba vilivyokwisha muda wake.

“Vile vifaa tiba huwa vinakuwa na muda wa kutumia na muda huo ukishafikia basi vinatakiwa kutafutiwa njia ya kuhifadhiwa ili visitumike tena sasamadhara yake kama tutakuwa tunandelea kuvitumia au hatujaviwka utaratibu mzuri basi vinaweza kuleta madhara kwa maana kuwa hatarishi kwa watumiaji either wagonjwa au hata wale wanao tumia kwa ajili ya wagonjwa wito wetu kwanza tuwe tayari kuupoka huu ujumbe pia tuwez kutoa ushirikiano pal ambapo tutakuwa tumepata vifaa tiba mbalimbali ambavyo tayari muda wake umkwisha wa kutumia na tukisma hivi sio vya kutumia wananchi wasije wakaona sehemu yoyote wasiviguse vitatupatia madhara"Alisema mang’una 

Zoezi hilo linafanyika katika wilaya mbili za mkoa wa iringa manispaa ya iringa na mji wa mafinga  huku TMDA ikitembelea vituo 12 vya vya afya vya serikali na binafsi

KAMPENI YA SOMA NA MTI SAFARI YA UHAKIKA KUELEKEA TANZANIA YA KIJANI MWANZA.

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Shughuli nyingi zinazofanywa na binadamu kama uchomaji mkaa, uchomaji misitu, ukataji miti, uvunaji mbao usio na mpangilio vimechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira. Ni mwaka sasa tangu kuanzishwa kwa kampeni ya SOMA NA MTI iliyozinduliwa kitaifa jijini Dodoma mnamo Tarehe 20 mwezi January Mwaka jana 2022 chini ya mwasisi wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Selemani Said Jafo ikiwalenga wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo kote nchini kusimamia utunzaji wa mazingira, huku kila mwanafunzi akijivunia utunzaji na ukuzaji wa mti wake, lengo na Madhumuni ni kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kuifanya Tanzania kuwa ya kijani. Baada ya kampeni hiyo kupita mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Dodoma sasa kampeni hiyo imeingia jijini Mwanza ikianzia Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agustino almaarufu SAUTI ambapo wanafunzi wa chuo hicho wameungana na wanafunzi wa vyuo vingine kupanda miti kwenye mazingira ya chuoni hapo. Mhe. Hamisi Mamza Hamisi Chilo ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika tukio hilo. "Hapa nchini kuna takriban wanafunzi milioni 14.1 ambao kila mmoja akipanda mti wake itasaidia katika kukabiliana na changamoto hizo za kimazingira ikiwemo ukame na uhaba wa maji" alisema Mr Tree Vyuo vingine vilivyoshiriki zoezi hili ni pamoja na Bugando, City College, Tandabui, CBE, TTC Butimba, Mipango, BOT, IFM, VETA, TIA na kuchagizwa kwa njia ya elimu kupitia kituo cha redio Jembe Fm Mwanza.

DC MOYO AMEAMURU KUVUNJWA MADARASA SHULE YA MSINGI MAJOGO

 

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo wa kwanza kulia akitembelea shule ya msingi Majogo kujionea hali halisi ya Madarasa ya shule hiyo yalivyochakaa
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwa na viongozi mbalimbali wametoka kujionea hali halisi ya Madarasa ya shule ya msingi Majogo yalivyo


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.


MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ameamuru kuvunjwa kwa baadhi ya Madarasa ya shule ya msingi Majogo katika Kijiji cha Litula kata ya Marambo kutokana na uchakavu wa majengo ya shule hiyo ambayo yanahatarisha maisha ya wanafunzi na walimu.

Akiwa katika ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo "ulipo nipo toa kero yako sema kweli sio majungu",mkuu wa wilaya huyo alifanikiwa kufika katika shule ya msingi Majogo na kuikuta shule hiyo ikiwa katika hali ya uchakavu mkubwa wa majengo ambayo yanahatarisha maisha ya wanafunzi.

Moyo alisema kuwa haiwezekani wanafunzi wakaendelea kusoma kwenye madarasa ambayo yamejawa na nyufa kila kona hivyo madarasa hayo yabomorewe haraka iwezekanavyo.

Alimtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kujenga upya madarasa hayo ili wanafunzi wa Kijiji cha Majogo waendelee kupata elimu inavyotakiwa kwa faida ya Taifa.

"Uchakavu mkubwa wa miundombini,kuhatarisha maisha ya wanafunzi na walimu, siwezi kukubali hali ya shule ya msingi Majogo waendelee kusoma katika shule yenye majengo hatarishi"alisema Moyo

Moyo pia alimuagiza mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kumalizia ujenzi wa vyoo vya shule ya msingi Majogo ili kuwalinda wanafunzi na walimu kiafya.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi walisema jengo la shule litaua wanafunzi,waomba libomolewe haraka haraka kwa kuwa wameshajenga jengo jipya la vyumba vya madarasa lakini havijamalizika.

Akijibu hoja hizo mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Injinia Chionda Kawawa alisema kuwa wameshatenga kiasi cha shilingi millioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa matundu mapya ya vyoo na wamelichukua suala la  kumalizia ujenzi wa vyoo ya shule ya msingi Majogo.

Kawawa alisema kuwa suala la umaliziaji wa jengo la shule ya msingi Majogo wamelichukua na watalifanyia kazi haraka sana ili kunusuru maisha ya wanafunzi na walimu wa shule hiyo.

MANISPAA YA IRINGA WAWAPONGEZA TARURA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINI

 

Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahimu Ngwanda akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kwa kutoa maelekezo ya maazimio ya Baraza hilo juu ya kuwapongeza TARURA

 

Na Fredy Mgunda, Iringa.

WAKALA wa barabara mijini na vijijini (TARURA) Manispaa ya Iringa wamepongezwa kwa utendaji mzuri wa kazi na uboreshaji wa miundombinu katika sehemu mbalimbali 

Wakitoa pongezi hizo madiwani wa kata za manispaa ya Iringa wamesema kuwa TARURA wamekuwa na wakati mzuri kutokana na kufanya kazi kwa bidii katika maeneo mbalimbali.

Awali akizungumza naibu meya manispaa ya Iringa Jully Sawani alisema kuwa TARURA wamekuwa wakifanya kazi nzuri hususani katika kata yake ya kihesa kwa kufanya marekebisho katika kipande Cha barabara kilichukuwa korofi Cha kihesa sokoni 

"mi nataka niwapongeze TARURA kwa kweli niwape pongezi wamefanya kazi nzuri Kama tunavyowasikia madiwani hapa kweli mmetenda kazi nzuri mi nilikuwa naangalia utekelezaji wake pale kihesa sokoni kiukweli mmefanya vizuri Sana ushauri tuu mnisaidie kurekebisha kale kakipande kengine kalikobakia maana Kuna makorongo yanayoweza sababisha ajali kutokana na madereva kuyakwepa matuta Yale " alisema

Naye diwani wa kata ya Kitwiru Mh. Muhehe alisema kuwa pamoja na utendaji wa kazi mzuri unaofanywa na wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA Manispaa ya Iringa kwa kuanza uboreshaji daraja la Kitwiru - Isakalilo huku akiiomba TARURA kuweka taa za barabarani ili kudhibiti vitendo vya ukatili na wizi ambao umekuwa ukifanyika katika maeneo yaliyo giza 

" Mnafanya kazi nzuri Sana niungane na madiwani wenzangu kuwapongeza lakini pia niwaombe TARURA mtusaidie Kule kata ya ilala hatuna taa za barabarani watoto wanaofanyiwa ubakaji kutokana na giza niwaombe mtusaidie pia katika hili " alisema Muhehe 

kwa upande wake Carlos Lunyili kaimu meneja wa TARURA Manispaa ya Iringa alisema kuwa pamoja na mafanikio waliyopata wamekuwa na changamoto ya uifinyu wa bajeti ,upungufu wa watenda kazi pamoja na wananchi kujenga katika miliki za barabara hali inayopelekea kupata changamoto wanapofanya kazi zao 

" Mheshimiwa mwenyekiti tumekuwa tukipata changamoto mbalimbali wakati wa kutemda majukumu yetu ufinyu wa bajeti umekuwa ukipelekea kushinda kufanya baadhi ya majukumu kwa wakati ,pia upungufu wa watenda kazi ,pia Kuna wananchi wanaojenga katika Hifadhi za barabara,pia TARURA kutokupewa ofisi " alisema lunyili

Ibrahim Ngwada ni  meya wa manispaa ya Iringa alisema kuwa changamoto hizo wamezipokea hivyo wanaahidi kutendea kazi huku akiwataka wananchi kuweka taa nje ya nyumba zao ili kuondoa matendo ya ukatili na wizi licha ya kuwepo kwa changamoto ya kutokuwepo kwa taa za barabarani

" nawapongeza TARURA kwa ufanyaji kazi mzuri Kama walivyosema waheshimiwa  Madiwani wenzangu hongereni pia kwa kuanza ujenzi na kuweka kwenye bajeti daraja la Kitwiru - Isakalilo lakini pia nimesikia changamoto ya taa za barabarani kazi hii niwape pia watendaji Kama ilivyo Sheria ya ukitaka kujenga lazima upande miti basi hata kuweka taa uwe hivyo kwa sababu tukiwa wabahili matukio hata hayawezi kuisha niwaombe wananchi waweke taa nje ya nyumba zao mpaka pale serikali itakapofanikiwa kuweka taa katika barabara zetu " alisema Ngwada.

Tuesday, February 28, 2023

SHULE YA SEKONDARI COASTAL YA JIJINI TANGA KUANZA KUNUFAIKA NA MKONGE

 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akizungumza wakati wa maafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Coastal High School ya Jijini Tanga yaliyofanyika kwenye Hotel ya CBA Jijini Tanga


Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Coastal High School ya Jijini Tanga kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Coastal High School Andrew Gasper akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,Lulu George


Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) ,Saad Kambona akimkabidhi cheti mmoja wa wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Coastal High School ya Jijini Tanga kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Coastal High School Andrew Gasper akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,Lulu George


Na Oscar Assenga,Tanga.

Shule ya Sekondari Coastal ya jijini Tanga,itaanza kunufaika na uwekezaji wa sekta ya mkonge baada ya Bodi ya Mkonge Tanzani (TSB) kuahidi kuiingiza katika majaribio ya klabu za vijana watakaoendelezwa.

Pia shule hiyo imeahidiwa kupewa ekari 100 kwa ajili ya kilimo cha mkonge ikiwa ni sehemu ya kuiongezea kipato .

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mko n ge nchini,Saad Kambona alitoa ahadi hiyo wakati wa mahafali ya kuwaaga wahitimu wa kidato cha sita walioanza mtihani ya kitaifa.

Alisema bodi hiyo imeandaa programu maalumu itakayowawezesha vijana kujiinua kiuchumi kuptia kilimo cha mkonge na bidhaa zitoakanazo na zao hilo.

Alisema kama inavyofahamika Bodi ya Mkonge ni taasisi ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ni kama imekufa sasa imeshafungua rasmi ofisi katika jengo lake na kuwezesha kuinua sekta ya mkonge kwa ujumla wake.

“Lakini tunategemea tunapokwenda mbele vijana wengi sana kutoka kwenye shule za Tanga ndiyo wahusike kwenye mpango mzima wa kuleta mapinduzi kwenye zao la mkonge kwani sasa hivi tunapozungumzia mkonge tunazungumzia bidhaa moja tu ya nyuzi za mkonge zitengeneze vikapu, makapeti, magunia, kamba na bidhaa nyingine zitokanazo na zao hilo ,lakini kuna bidhaa nyingti zinahitajika kama sukari,mbolea mvinyo na hata vyakula vya kunenepesha mifugo” alisema Kambona

Mkuu wa shule hiyo,Joseph Gaspar alisema ilianza rasmi mwaka 2000 na kwamba kwa miaka mitatu mfululizo imekuwa ikitoa ufaulu wa daraja la kwanza A na pili kwa wanafunzi wote wa kidato cha sita wote katik a mitihani ya kitaifa ya mchepuo wa sayansi.

“Hadi sasa shule hii imetimiza miaka 22 lakini kwa kipindi cha miaka miatatu mfululizo i mekuwa ikitoa wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza na la pili katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha sita...tunatarajia mitihani hii ufaulu utakuwa wajuu zaidi”alisema Gasper.

Makamu mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo,Lulu George alisema kuwa miongoni mwa mambo yanayotiliwa mkazo ni masomo ya sayansi wakiamini kuwa jukumu lao ni kupata wataalamu watakaoiendeleza nchi katika sekta ya uhandisi,udaktari na utafiti mbalimbali ikiwamo sekta ya kilimo na ufugaji.

SERIKALI YAKEMEA UKIUKAJI HAKI ZA BINADAMU

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Wakati wimbi la kuwanyima haki za kibinadamu kwa kuwaficha ndani watu wenye mahitaji maalum hasa watoto likitajwa kushamili katika jamii, Serikali imewataka wazazi kutojishusisha na vitendo hivyo, kwa kuwa ni ukiukwaji wa kisheria wa haki za binadamu. Katika makabidiano ya msaada wa fimbo kwa watu wenye uono hafifu na baiskeli za viti mwendo 70 kwa wenye mahitaji maalum, mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima, amesema yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

DC MOYO AANZA ZIARA NA MAAGIZO MAZITO

 

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo wakati wa uzinduzi wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo toa kero yako sio majungu
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo wakati wa uzinduzi wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo toa kero yako sio majungu
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo wakati wa uzinduzi wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo toa kero yako sio majungu.


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka viongozi wa serikali kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wanatakiwa kuwatumikia wananchi wa Nachingwea.

Akizungumza wakati wa ziara ya kijiji kwa kijiji yenye kauli mbiu isemayo ulipo nipo sema kweli sio majungu ya ,Moyo alisema kuwa hataki kusikia habari za mchakato kwenye utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo ya serikali.

Moyo aliwataka viongozi kutatua changamoto na kero za wananchi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi wilaya hivyo kama kutakuwa na kiongozi hataendana na kasi ya serikali ya awamu ya sita basi akae pembeni awapishe wengine wenye uwezo wa kufanya kazi kwa kasi ya serikali ya awamu ya sita.

Akiongea na wananchi wa kata ya Mbondo alitoa siku saba kwa uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kuhakikisha wanawapa wazee kadi za matibabu kama ambavyo serikali ya awamu ya sita inavyotaka.

Moyo aliwataka viongozi wa TARURA kuwasimamia vilivyo wakandarasi wote ambao wamepewe kazi ya ujenzi wa barabara katika wilaya hiyo ili zijengwe kwa kiwango kinachotakiwa.

Aidha Moyo alimtaka Injinia wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kuhakikisha miradi yote inajengwa kulingana na thamani ya fedha ambazo zimetolewa na serikali kuu pamoja na Halmashauri kwa faida ya Taifa na Wananchi wote.

Moyo alimazia kwa kuwataka wananchi wa wilaya hiyo kuwa walinzi wa amani ili kuondoa vurugu na migogoro mbalimbali ambayo imekuwa inahatarisha amani Taifa 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Injinia Chionda Kawawa alisema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa wilaya ya Nachingwea na watayafanyia kazi kwa faida ya wananchi wa wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla.

MAAFISA ARDHI NACHINGWEA WATAKIWA KUTOA HATI MILIKI MAENEO YA SERIKALI

 

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea juu ya umuhimu wa maeneo yote ya serikali kuwa na hati miliki ili kuondoa migogoro baina ya wananchi na serikali
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua maeneo ya kituo cha afya cha Mbondo na kuwaagiza ofisi ya ardhi kupima maeneo hayo
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua maeneo ya kituo cha afya cha Mbondo na kuwaagiza ofisi ya ardhi kupima maeneo hayo


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.


MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ameagiza idara ya ardhi kuhakikisha wanapima na kutoa hati miliki kwenye viwanja vyote vya serikali ili kuondoa migogoro ya ardhi kwa wananchi na serikali.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa kituo cha Afya cha Mbondo,Moyo alisema kuwa kumekuwa na migogoro mingi baina ya wananchi na serikali kutokana na tatizo la mipaka.

Moyo alisema kuwa zikitolewa hati miliki kwenye maeneo yote ya serikali kutatua na kuondoa kabisa migogoro ya ardhi na kuwaacha wananchi wakiendelea kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kiuchumi.

Aliagiza kwa maafisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kupeleka ofisini kwake taarifa ya utekelezaji wa agizo la kupima ardhi na maeneo yote ya serikali.

Moyo alisema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua changamoto za wananchi kwa kutatua migogoro mingi ya ardhi.

Kwa upande wake afisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Kantu Juma alisema kuwa wameyapokea maagizo ya mkuu wa wilaya hiyo ya kwenda kupima maeneo ya serikali na kutoa hati miliki ili kuondoa migogoro baina ya wananchi na serikali.

Monday, February 27, 2023

MATUNDA YA UWEKEZAJI BANDARI YA TANGA YAIWEZESHA MELI KUBWA YA MZIGO KUTOKA NCHINI URUSI KUTIA NANGA GATINI

 

.

 


 Meli kubwa ya Mzigo kutoka nchini Urusi yenye urefu wa mita 150 ikiwa imetia nanga katika Bandari ya Tanga mapema leo

 Meli kubwa ya Mzigo kutoka nchini Urusi yenye urefu wa mita 150 ikiwa imetia nanga katika Bandari ya Tanga mapema leo

Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha akizungumza na waandishi wa habari leo
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Bandari ya Tanga Rose Tandiko akizungumza 




Na Oscar Assenga,TANGA.

Matunda ya uwekezaji wa Bandari ya Tanga yameanza kuonekana mara baada ya Meli kubwa ya Mzigo kutoka nchini Urusi yenye urefu wa mita 150 kutia nanga gatini katika Bandari hiyo

Hatua hiyo ni baada ya kukamilika kwa gati lenye urefu wa mita 300 ambao umeiwezesha meli hiyo kuweza kutia nanga gatini na kuandika historia kwa mara ya kwanza kupokea meli kubwa mpaka gatini na hivyo kuandika historia ya kipekee baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali.

Akizungumza leo wakati wa mapokezi ya meli hiyo ambayo ilikuwa imebaba shehena ya Mbolea kwa ajili ya viwanda ,Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha alisema ujio wa meli hiyo ni matunda makubwa ya uwekezaji ambao umefanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kwenye Bandari hiyo.

Alisema kwamba meli hiyo ilikuwa imebeba mzigo wa tani 6909 unaokwenda nchini Kongo ambapo utapakuliwa kwa muda wa siku mbili kuanzia leo Jumatatu.

Aidha Meneja huyo aliwataka wafanyabiashara kwamba Bandari ya Tanga imeanza kufunguka kutokana na maboresho makubwa hali ambayo imepelekea huduma kuimarika zaidi.

Awali akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Bandari ya Tanga Rose Tandiko alisema kwamba matunda ya ujio wa meli hiyo ni kutokana na uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na Rais Samia Suluhu.

Alisema uwekezaji huo umewezesha kuandika histoiria katika Bandari hiyo kwa kuanza kuhudumia meli ya kichele gatini jambo ambalo awali lilikuwa halifanyiki.

Hata hivyo alisema kwamba wanamshukuru Rais Samia Suluhu kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika katika Bandari hiyo na matokeo yake yameanza kuonekana .