Na Victor Masangu,Pande
Sekta ya utalii wa ndani hapa nchini Tanzania inazidi kukua kwa kasi kutokana na juhudi ambazo zinafanywa na Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu na mazingira ya kuwavutia watalii wa ndani na nje ya nchi.
Katika kuunga mkono jitihada hizo kwa vitendo Taasisi ya wasanii na waigizaji mbali mbali Tanzania (TAGOSINE) wameamua kufanya ziara maalumu kwa ajili ya kutembelea hifadhi ya pori la akiba la pande lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza na kujionea vivutio mbali mbali vilivyopo.
Wasanii hao Jafari Makatu na Cecilia Sengerema wakizingumza kwa nyakati tofauti walisema kwamba ziara hiyo imeweza kuwafumbua macho kutokana na kupata fursa mbali mbali kwa ajili ya kujionea vivutio vya aina yake vilivyomo katika hifadhi hiyo ya pande.
"Kwa kweli tunamshukuru Mwenyekiti weti David Msuya kwa kuona umuhimu wa kutukutanisha kwa pamoja na kuja katika ziara hii ambayo sisi kwetu tutàkuwa ni mabalozi wazuri katika kuitangaza hifadhi hii ya pande maana kumbe kuna Mambo mazuri katika utalii wa ndani.
Aidha Zainabu Yusuph ambaye ni mwanachama wa Tagosine alisema katika ziara hiyo wamejifunza Mambo mbali mbali ambayo watakwenda kuyafanyia kazi kupitia Sanaa zao ikiwa pamoja na kuendelea kumuunga Rais wa awamu ya sita katika kukuza utalii wa ndani.
Kwa Upande Afisa utalii wa hifadhi ya pori la akiba Mustafa Buyogera alibainisha kwamba kwa Sasa wamefanya maboresho makubwa kutokana na kupatiwa fedha na Rais Samia zaidi ya milioni 200 ambazo zimesaidia kujenga miundombinu ya majengo na kuboresha hifadhi hiyo ili kuwavutia watalii wa ndani.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Tagosine amesema lengo kubwa la kufanya ziara hiyo ni kwenda kujifunza vitu vipya katika hifadhi hiyo ikiwa pamoja na kuweka mipango ya kuandaa filamu ambayo itaelezea utalii wa ndani lengo ikiwa ni kumpa sapoti Rais.
Pia Msuya alifafanua kuwa wameamua kuungana kwa pamoja kwa lengo la kuunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza na kuboresha utalii wa ndani.
Kufanyika kwa ziara hiyo na Taasisi ya Tagosine katika hifadhi ya pori la akiba la Pande ina lengo kubwa la kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita pamoja na kuwahimiza Watanzania kupenda vivutio vya kwao na kutembelea utalii wa ndani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.