ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 9, 2016

WAZIRI NAPE NNAUYE AKUTANA NA WAYHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI LEO JIJINI DAR

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari  mapema leo,alipokutana nao na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabiri tasnia hiyo,mkutano huo umefanyika kwenye moja ya ukumbi ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari 

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano uliohusu kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda na kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa . 
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano ulioitishwa na Waziri Nape kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kati ni Waziri Mh.Nape pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akitoa muongozo kwa Wahariri wa Vyombo vya habari (hawapo nchini) kuhusina na mkutano wao ulioitishwa na Waziri Nape kujadili mambo mbalimbali na changamoto zinazoikabiri tasnia hiyo kwa ujumla.
 Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo.
 Mmoja wa Wahariri Kurwa Kaledia kutoka New Habari Hause akiomba ufafanuzi wa jambo kwa Mh Waziri Nape huku baadhi ya wahariri wakifuatilia kwa makini.
 Mmoja wa Wahariri Grace Hoka akifafanua jambo kwenye mkutano huo
 Baadhi ya Wahariri wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
 Baadhi ya Wahariri juu pichani wakishiriki kuchangia mambo mbalimbali kwenye mkutano huo.
 Mmoja wa Wahariri akifafanua jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya Wadau wakubwa wa habari pia walikuwepo kwenye mkutano huo .PICHA NA MICHUZI JR

TAJATI YAFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA VIWANDANI JIJINI MBEYA NA KUSHUHUDIA MAGOFU NA MITAMBO ILIYOTELEKEZWA


Baadhi ya mitambo iliyotelekezwa kwenye Kiwanda cha kutengenezea Zana za Kilimo ZZK
Mitambo ambayo ilikuwa ikitumika kutengenezea Zana za Kilimo katika kiwanda cha ZZK Iyunga jijini Mbeya ikiwa imetelekezwa
Niranjan Bandi, aliyejitambulisha kuwa ndiye Mkurugenzi mkuu wa shughuli zinazoendelea katika kiwanda cha ZZK  chini ya kampuni ya CMG akiwapa maelezo waandishi wa habari.
Waandishi wakitoka katika kiwanda cha ZZK huku wakijiuliza maswali mbali mbali kutokana na walichokikuta ndani ya kiwanda hicho
Baadhi ya waandishi wakichungulia ndani ya majengo ya kilichokuwa kiwanda cha kutengeneza sabuni HISOAP Kushuhudia kama kuna kilichosalia.
Huu ndiyo muonekano wa ndani ya majengo ya kilichokuwa kiwanda cha kutengenezea sabuni HISOAP kukiwa hakuna kitu licha ya kuwepo Mlinzi.
Muonekano wa Jengo la kiwanda cha HISOAP lililotelekezwa ili hali serikali ya awamu ya tano ikisisitiza kuwa serikali ya Viwanda

CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) katika kutekeleza majukumu yake kimefanya ziara katika viwanda vine vilivyopo Iyunga jijini Mbeya na kushuhudia baadhi vikiwa vimetelekezwa.

Waandishi hao  15 kutoka vyombo mbali mbali ambao ni wanachama wa TAJATI, walifanya ziara hiyo iliyoanzia katika majengo yaliyokuwa ya Kiwanda cha kutengenezea sabuni kilichokuwa kikijulikana kwa jina la HISOAP kilichopo Iyunga jijini Mbeya na kukutana na majengo hayo yakiwa yametelekezwa.

Mbali na kutelekezwa kwa majengo hayo,pamoja na  kuwepo kwa mlinzi ambaye alikiri kulinda majengo ambayo ndani yake hajui kilichomo kwa kupitia matundu ya mlangoni,wanahabari hao walishuhudia ndani kukiwa hakuna hata mtambo mmoja ulichosalia na na matanki makubwa yanayoendelea kuoza nje.

“Mimi nalinda hapa kwa maagizo ya bosi wangu lakini huko ndani hakuna shughulli yoyote inayofanyika kwani hata hizo mboga zilizolimwa ni mali ya walinzi wenzetu ndiyo wamelima,sijui humo ndani kama kuna mitambo sijawahi kuona milango ikifunguliwa hata mwenye funguo simjui” alisema Mlinzi ambaye alitaka jina lake lihifadhiwe kwa usalama wake.

Aidha katika ziara hiyo timu ya waandishi ilifika katika majengo ya kilichokuwa kiwanda cha serikali, Kiwanda cha kutengenezea zana za kilimo maarufu kwa jina la ZZK ambapo timu hiyo ilipokelewa na raia mmoja wa kigeni mwenye asili ya kiasia,  Niranjan Bandi, aliyejitambulisha kuwa ndiye Mkurugenzi mkuu wa shughuli zinazoendelea hapo chini ya kampuni ya CMG.

Katika maelezo yake kwa waandishi wa habari Bandi alisema ndani ya kiwanda hicho kuna shughuli za kutengeneza vipuri vya magari, uunganishaji wa matrekta madogo ya kilimo(powertiller ) kutoka China na kwamba zana za kilimo wameshindwa kutengeneza kutokana uchakavu wa mitambo iliyopo na imepitwa na teknolojia.

Aliongeza kuwa ifikapo januari 15 mwaka huu wanatarajia kuanza kutengeneza mabati baada ya kupata mtambo kutoka China ambao hivi sasa unafanyiwa marekebisho kabla ya kuanza kazi sambamba na uanzishwaji wa kiwanda cha kuzalisha bia cha Serengeti.

Wakati mwekezaji huyo akijieleza na kuonyesha mashaka makubwa ya uzalishaji kuwa ni changa la macho,Waandishi wa habari  walishuhudia mitambo iliyokuwa ya kutengenezea zana za kilimo ikiwa imetekelezwa bila kufanya kazi ndani ya majengo hayo ambapo Mkurugenzi huyo alisema hawana uwezo wa kuiendesha.

Baada ya kukamilisha mahojiano na Mkurugenzi huyo waandishi hao walielekea moja kwa moja katika kiwanda cha Malumalu cha Marmo Granito ambapo walitembelea mitambo ya kuchonga na kukata mawe na bidhaa mbali mbali zinazotokana na  miamba ya asili.

Mkurugenzi wa Marmo,Salim Jessa alisema tangu walipoanza uwekezaji katika Mkoa wa Mbeya wameanza kupata masoko nje ya nchi ikiwemo India,Italia na kutafuta masoko mengine nchini  China ambako watakuwa wakiuza malighafi zilizoongezwa thamani kwa ajili ya matumizi mengine.

Alisema changamoto kubwa ni ushindani wa soko baada ya kampuni zingine kujitokeza na kuanza kutengeneza bidhaa zinazotokana na mawe ya asili kama wao sambamba na uingizaji wa bidhaa zilizochakachuliwa kutoka nje kwa lengo la kuharibu soko.

Ziara hiyo ya TAJATI ilihitimishwa katika kiwanda cha Bia cha TBL ambapo waandishi walitembezwa kiwandani hapo na kisha kupata muda wa kuuliza maswali kutoka kwa wahusika.

Akizungumza na wanachama hao, Meneja wa Kiwanda cha Bia Mbeya, Waziri Jemedari alisema licha ya mafanikio waliyoyapata katika uzalishaji wanakabiliwa na changamoto kubwa ambazo ni miundombinu mibovu, gharama kubwa za maji na umeme sambamba na mlundikano wa vinywaji kutoka nje ya nchi vinavyoharibu bei ya vinywaji vinavyozalishwa nchini.

Jemedari alisema bia nyingi zinaingizwa nchini kutoka nje zinauzwa bei ya chini hivyo kupelekea wateja wengi kukimbilia na kuua soko la vinywaji vya ndani.


Na Mbeya yetu

AKILI MKICHWA.

Mwalimu mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia ''Kesho kila mwanafunzi aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, Yaani kama unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya mbili hivyo hivyo"
Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea madaftari na vitu vingine vya shule ''Wanafunzi wakakubali afu kesho yake wanafunzi wakazibeba zile nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na wengine nyingi sana.
Kama mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu ambao wanafunzi wanawachukia.
Baada ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu akawaambia kila mwanafunzi azirudishie nyanya zake kwenye begi lake afu aziache humo humo ndani ya begi kila siku awe anakuja nazo shuleni na kurudi nazo.
Baada ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa wale waliobeba nyanya nyingi kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu mbaya na zinaharibu vitu vyao vizuri walivyoweka kwenye mabegi. Mwalimu akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu moyoni usiowapenda. 

Kama mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya kwenye begi vipi kuhusu madhara ambayo moyo unayapata kwa kuubebesha mzigo wa chuki dhidi ya watu.? Moyo unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa chuki kila wakati kila siku moyo unakuwa na chuki na hapo ndipo unaharibika na kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri vilivyokuwa moyoni. Moyo ni kama lile begi la kubebea madaftari unahitaji kubeba vitu vizuri.
Safisha moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe mana ni moja ya virutubisho vya moyo wako. Hata Mungu anasema wasamehe wale waliokukosea ili upate amani na baraka moyoni mwako. Nawatakia siku njema.

CHEREKO LA HARUSI YA JONAS NA BENITHA LILIYOFANYIKA JIJINI MWANZA.

 Bwana Jonas Songora na Bi. Benitha Tebuka wakiwa katika red carpet kwenye ukumbi wa sherehe Gold Crest Mwanza, baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la AICT Makongoro jijini humo. 
Wakivalishana pete kuwa mwili mmoja...
Vyeti vya ndoa.....!!
WapambeZ...!
Bi harusi Benita Tebuka katika pozi na dadaz kabla ya sherehe.
Zwanga photo na Selfie...
Mke ni pambo.....
Who is next?
Jonas & Benitha.


Siku ya Furaha yenye historia.
Mr & Mrs David Simba ndiyo waliopata dhamana ya kusimamia harusi hiyo.
Jonas & Benitha take one.
Jonas & Benitha take two.
Wow...that's good muonekano.
Men in Black.
Matayarisho kuelekea sherehe ya harusi...
Taswira adimu.
Ninyweshe nikunyweshe....Furahia utamu wake.
The cake.
Hatariiiiii...
Engo adimu.
Furaha wacha itawale.
PICHA NA ABC STUDIO MWANZA.
ILI KUPENDEZESHA HARUSI YAKO BASI TUWASILIANE.

LUHAGA MPINA ATUPA RUNGU NEMC

Naibu wa waziri wa ofisi ya makamo wa rais mazingira Luhanga Mpina ametoa siku 7 kwa NEMC Mbeya kuhakikisha wanapima maji machafu yanayotoka katika kiwanda cha Songwe. 

MAGAZETI YA LEO:- AFUKUZWA KWA KUHALALISHA HEKALU LA MCHUNGAJI LWAKATARE.

Wahamiaji haramu 79 watiwa mbaroni. Bomoa bomoa ipo palepale. Afukuzwa kwa kuhalalisha hekalu la mchungaji Lwakatare;  Wasiopeleka watoto shule kutozwa faini mil.5. Wawili wafariki, mmoja apooza kwa mshtuko wa bomoa bomoa.
Magufuli ampa tano Samatta. Yanga haishikiki Mapinduzi Cup. Wafaransa wamfuata Samatta Dar, avuliwa uraia.

HII HAPA SIMULIZI YA HISTORIA YA MBWANA ALLY SAMATA.

Hivi ulishawahi kujiuliza Mshindi wa Tuzo ya mchezaji bora wa Africa kwa ligi za ndani 2015 - 2016 Mbwana Samata anapokuwa Congo katika klabu yake ya TP Mazembe, anapohojiwa na vituo vya televisheni na radio vya kule je hutumia lugha gani? **SPORTS RIPOTI** ya JEMBE FM 93.7 inayosikika kila siku saa Tatu kamili hadi 4 imekupa jibu BOFYA PLAY KUSIKILIZA.WADAU WAKO WANAOKUUNGANISHA NI:- @elikanamathias @jumaayoo @gsengo Tupate popote ulimwenguni kupitia Google play store kwa kusachi JEMBE Fm kisha sikiliza LIVE kupitia simu yako ya mkononi @jembenijembe @samagoals @bobwhite_pamba @mzairebokilo_93.7 @mrekebishatabia @meddymtabora @abog_a_plus_b

Friday, January 8, 2016

WAHAMIAJI HARAMU 12 RAIA WA BURUNDI WATIWA MBARONI SHINYANGA.


Idara ya Uhamiaji Shinyanga imewakamata vijana 12 ambao ni wahamiaji haramu toka nchini Burundi wakijishughulisha na biashara ya Boda boda.

ANT LATIFA MASASI HATOA HUDUMA ZA AFYA KWA WATOTO YATIMA WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA DARUl-ARQAM CHLDRENS HOME


Muhudumu wa Afya ya baba mama na mtoto wa kituo cha alafa kilichopo wilaya ta Temeke Bi, Latifa Masasi kushoto akichukuwa vipimo vya damu ya mtoto Raban Mansur wakati alipotembelea kituo cha watoto yatima cha Darul-Arqam Childrens Home kilichopo tandika magorofani kwa ajili ya kuwapima afya watoto wanao lelewa katika kituo hicho
Muhudumu wa Afya ya baba mama na mtoto wa kituo cha alafa kilichopo wilaya ta Temeke Bi, Latifa Masasi kushoto akichukuwa vipimo vya damu kwa mtoto Abdulatif Said kwa ajili ya kujua afya yake kushoto ni Hamis Rajabu wakati alipotembelea kituo cha watoto yatima cha Darul-Arqam Childrens Home kilichopo tandika magorofani kwa ajili ya kuwapima afya watoto wanao lelewa katika kituo hicho

Muhudumu wa Afya ya baba mama na mtoto wa kituo cha alafa kilichopo wilaya ta Temeke Bi, Latifa Masasi kushoto akichukuwa vipimo



 Muhudumu wa Afya ya baba mama na mtoto wa kituo cha alafa kilichopo wilaya ta Temeke Bi, Latifa Masasi kushoto akichukuwa vipimo vya damu kwa mtoto Aman Ramadhani kwa ajili ya vipimo wakati alipotembelea kituo cha watoto yatima cha Darul-Arqam Childrens Home kilichopo tandika magorofani kwa ajili ya kuwapima afya watoto wanao lelewa katika kituo hicho.

WAHAMIAJI 435 WAKAMATWA MKOANI MARA.

Idara ya uhamiaji mkoani Mara yaeleza kukamata wahamiaji haramu 435 kwa mwaka 2015

NI ZAMU YA MBWANA SAMATA KUING'ARISHA TANZANIA ANGA ZA KIMATAIFA.

@samagoals - Nachukua nafasi hii kwanza kumshukuru Mungu kwa kila lililotokea. Pia Baba yangu pamoja na familia kiujumla, ndugu, jamaa na marafiki. Pia kwa dhati kabisa nawashukuru Watanzania wenzangu bila kujali wadhifa, kwani dua zenu za pamoja na sapoti yenu kwangu ndio imeleta hii tuzo nyumbani Tanzania. Nawashukuru sana, sina cha kuwalipa. Kila mmoja wenu Mwenyezi Mungu amuongezee katika sehemu yake. Asanteni sana TANZANIA. Na leo ndo nalala hivyo, atakayeniamsha tutapigana Walahi tena, mniache mpaka niamke mwenyewe.