ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 12, 2019

WAISLAMU MKOA WA MWANZA WAUNGANA NA SHEIKH MKUU VITA DHIDI YA MUZIKI MOTO


BAADA ya Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi kutangaza kupiga marufuku dufu na kaswida maarufu kama ”mziki moto” akizitaja kuwa, zinaaibisha na kuchafua sura ya Uislamu huku zikitoka nje ya utamaduni na maadili ya dini tukufu ya Kiislamu. Mkoani Mwanza Sheikh wa Mkoa huo, Hassan Kabeke naye ameapa kupambana na hilo ili kuhakikisha maadili ya Uislamu yanalindwa.

RAIS MAGUFULI ATANGAZA KUACHIWA KWA NDEGE YA TANZANIA ILIYOKAMATWA CANADA


Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imakamatwa nchini Canada imeachiwa na wananchi watatangaziwa siku ya kuwasili ili waipokee jijini Mwanza.
 
Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa amesema hayo wakati anafungua Semina ya Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Inayofanyika Jijini Mwanza.

“Kwa taarifa tu, Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa siku ya kuipokea na itapokelewa hapa Mwanza,” amesema.


Wednesday, December 11, 2019

HIFADHI YA TAIFA KUPEWA KIPAUMBELE,SHUGHULI NYINGINE KUSITISHWA.

Kamishna wa hifadhi tanapa dactar ALLAN  KIJAZI  amesema kuwa wadau mbalimbali hapa nchini wanatakiwa kuona namna  bora wanaweza  kusimamia hifadhi  mpya ya TAIFA  YA NYERERE kwani ni  hifadhi muhimu KITAIFA ambayo ilikuwa ni sehemu ya pori la akiba lililipo chini ya mamlaka ya  usimamizi wa wanyama pori TAWA ambapo ilitangazwa rasmi na raisi  DK, JOHN  POMBE MAGUFURI baada ya bunge la jamuhuli ya muungano wa TANZANIA  kuridhia azimio kupandishwa hadhi hifadhi hiyo.

BAADA YA SUNGUSUNGU KUSISIMUA MAADHIMISHO YA UHURU 2019 RAIS MAGUFULI AWAZAWADIWA NG'OMBE 10



“TUNAJUA vikundi hivi vikiimarishwa kitaaluma na kiuwezo vinakuwa na nafasi kubwa ya luketa mabadiliko katika mfumo wa maboresho ya ulinzi katika jamii yetu. Nimalize kwa kunena Sungusungu ni muhimu sana katika jamii yetu kwa sababu ni walinzi wetu wanaoishi katika eneo letu na wanawajua vibaka wetu mitaani na namna ya kupambana nao. Pia hao ni msaada wa karibu kwa polisi walioko katika doria ndani ya maeneo yao” Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, wakati akikabidhi zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Joseph Magufuli kwa vikosi 13 vya Sungusungu mkoani Mwanza baada ya kutia for a katika maonesho ya Sherehe za Uhuru wa Tanganyika miaka 58 na 57 ya Jamhuri, makabidhiano yakifanyika Ng’ungumalwa wilayani Kwimba mkoani humo.

MWANZO MWISHO WALIVYOACHIWA WAFUNGWA GEREZA LA BUTIMBA MWANZA KWA MSAMAHA WA RAIS MAGUFULI



 Siku moja baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kuwasamehe wafungwa 5,533 katika maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, wafungwa 79 kati ya hao waliokuwa wamefungwa katika gereza la Butimba Mkoa wa Mwanza wameachiwa Jumanne Desemba 10, 2019.

Rais Magufuli alitangaza msamaha huo katika maadhimisho hayo, akibainisha kuwa idadi hiyo ni kubwa kuwahi kutokea kuliko wakati mwingine wowote na kutaka walengwa ndio waachiwe.

Katika mkoa wa Mwanza wafungwa watakaopata msamaha huo ni 190.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amefika katika gereza la Butimba kwa ajili ya kushuhudia utekelezaji wa agizo la Magufuli huku mkuu wa gereza hilo, Hamza Hamza akitaja idadi ya watakaoachiwa.

MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI NOVEMBA WAONGEZEKA.


Mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwaka ulioishia Mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi  asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 kwa Mwaka ulioishia Mwezi Octoba 2019.

Hayo yameelezwa hii leo Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu  za Jamii,Ruth Minja wakati akizungumza na waandishi wa habari hii leo na kuongeza kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba  2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Octoba 2019.

Minja ameongeza kuwa baadhi ya bidhaa zisizo za Vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi Novemba 2019,zikilinganishwa na bei za mwezi Novemba 2018, ni pamoja na Mavazi kwa asilimia 2.7,Mkaa kwa asilimia 4.4,Samani kwa asilimia 3.1,huduma ya malazi kwenye nyumba za wageni kwa asilimia 5.0 na Mazulia kwa asilimia 6 3 huku pia akibainisha kuongezeka kwa Mfumuko wa bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019


"Mfumuko wa bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 5.1 kwa mwaka ulioishia mwezi Octoba 2019"Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ruth Minja

Katika nchi ya Kenya Minja amesema kuwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.56 kutoka asilimia 4.95 kwa mwaka ulioiehia mwezi Novemba 2019 na kwa upande wa Uganda,Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 2.5 kwa mwaka ulioishia mwezi Octoba 2019.

Monday, December 9, 2019

RAIS MAGUFULI AHIMIZA AMANI, USHIRIKIANO NA KUJITEGEMEA 'SHEREHE ZA UHURU'

 Amani, mshikamano, kufanya kazi kwa bidii na kujitegemea ni kati ya mambo yaliyosisitizwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli katika hotuba yake ya maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika mjini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba leo Jumatatu Desemba 9, 2019, kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema Serikali imejipanga na itafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kulinda amani na utulivu.

“Tumefanya mengi ya kujiletea maendeleo katika awamu zote kwa miaka 58 ya Uhuru lakini msingi mkuu wa mafanikio yote ni amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.”

“Serikali inawahakikishia wananchi kuendelea kulinda na kudumisha amani hiyo,” amesema Rais Magufuli.

Huku akitaja baadhi ya maeneo ambayo Taifa limepiga hatua ikiwemo kusomesha na kupata wataalam wa fani mbalimbali, kuboresha na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji, Rais Magufuli amesema amani, mshikamano na umoja wa Kitaifa ni nyenzo ya kufanikiwa zaidi.

“Kazi ya kuendeleza Taifa sio lelemama. Viongozi na waasisi wa Taifa hili wamefanya mengi kwa mafanikio makubwa licha ya changamoto nyingi.”


“Ni jukumu letu kizazi cha sasa kuendeleza na kulinda yote mema yaliyoasisiwa na kusimamiwa na waasisi wetu,” amesema Rais Magufuli.

Ameongeza, “amani na usalama, umoja, mshikamano wa kitaifa, moyo wa kujitolewa na kujitegemea ni miongoni mwa nyenzo muhimu ya kutufikisha katika lengo la kuwa na Taifa lenye maendeleo endelevu.”

Mkuu huyo wa nchi ametumia fursa hiyo kujivunia mafanikio yaliyopatikana katika miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, akitaja ujenzi wa viwanda zaidi ya 4,000, vita dhidi ya ufisadi, kudhibiti uvuvi haramu na ulinzi wa rasilimali za Taifa.

Magufuli ametaja maeneo mengine kuwa ni kuboresha usafirishaji kwa njia ya barabara, reli, maji na anga kwa kujenga miundombinu, kukarabati na kununua vyombo vya usafirishaji ikiwemo ndege, meli na mitambo.

MAKAMU WA RAIS APIGILIA MSUMARI ISHU YA BIMA YA AFYA


 Kutoka Hospitali ya wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kuelekea Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru miaka 58, Makamu wa Rais Samia Suluhu ......

AAAA

PICHA:- RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA MELI NA CHELEZO PAMOJA NA UKARABATI MKUBWA MELI 2 ZIWA VICTORIA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wakimsikiliza Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria Meja Abel Gwanafyo akitoa maelezo kuhusu miradi hiyo kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Meli mpya ya M.V Mwanza (Hapa kazi Tu) wakati wakimsikiliza Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria Meja Abel Gwanafyo akitoa maelezo kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia katika Sherehe za Uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuashiria uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria katika sherehe zilizofanyika eneo la
Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwachangia Kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza walipokuwa wakiimba kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019

Kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza walipokuwa wakiimba kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu),
Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019. 



Muonekano wa Chelezo inayojengwa katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019. 



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai pamoja na viongozi wengine wakiinua mikono juu kwa umoja na furaha mara baada ya uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria katika sherehe zilizofanyika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba
08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkandarasi wa Ujenzi wa Meli mpya ya M.V Mwanza Bw. Dowan Kim kutoka kampuni ya STX Engine mara baada ya sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Desemba, 2019 ameweka jiwe la msingi katika miradi ya ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Chelezo na ukarabati wa meli za MV Victoria na MV Butiama katika Ziwa Victoria.

Sherehe za uwekaji jiwe la msingi katika miradi hiyo zimefanyika katika Bandari ya Mwanza Kusini Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Wabunge, viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, viongozi wa taasisi mbalimbali, viongozi wa Dini na viongozi wa vyama vya siasa.

Ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu utakamilika Januari 2021 kwa gharama ya shilingi Bilioni 89.764 ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 43.74 na unatekelezwa na kampuni za ukandarasi za Gas Entec Company Limited na Kangnam Corporation za Jamhuri ya Korea kwa kushirikiana na Suma JKT. Kampuni hizi zimeshalipwa shilingi Bilioni 39.249.

MV Mwanza Hapa Kazi Tu itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari makubwa 3 na magari madogo 20, inatarajiwa kufanya kazi kati ya bandari za Mwanza, Kemondo, Bukoba na Musoma pamoja na kwenda nchi jirani za Kenya na Uganda na hivyo kukabiliana na adha ya usafiri kwa wananchi na mizigo katika Kanda ya Ziwa baada ya MV Bukoba kupata ajali ya kuzama majini mwaka 1996 na meli nyingine 4 kuharibika.

Ujenzi wa chelezo unafanywa na kampuni za STX Engine Company Ltd na Saekyung Construction Company Ltd, zote za Jamhuri ya Korea kwa gharama ya shilingi Bilioni 36.4 ambapo mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 68 na wakandarasi hao wameshalipwa shilingi Bilioni 32.85 sawa na asilimia 90 ya fedha zote.

Ukarabati mkubwa wa meli za MV Victoria na MV Butiama unafanywa na kampuni za KTMI Co. Ltd ya Jamhuri ya Korea na kampuni ya Yuko’s Enterprises (EA) Co. Ltd ya Tanzania kwa gharama ya shilingi Bilioni 27.71 ambapo mpaka sasa shilingi Bilioni 11.57 zimeshalipwa na kazi imefikia asilimia 65 na 60 mtawalia. 

MV Victoria ina uwezo wa kuchukua abiria 1,200 na mizigo tani 200 wakati MV Butiama ina uwezo wa kuchukua abiria 200 na mizigo tani 100. Meli hizi zitakuwa zinafanya safari kati ya Bandari za Mwanza, Kemondo, Musoma, Bukoba na Nansio-Ukerewe. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Bw. Eric Benedict Hamissi amesema ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli hizo ambao unafanywa kwa kiwango cha kuzirudisha kuwa meli mpya kabisa unatarajiwa kukamilika Machi 2020.

Bw. Hamissi amempongeza na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa Serikali kufanya uwekezaji mkubwa wa mara moja ambao haujawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru, ambapo katika kipindi kifupi cha miaka minne imewekeza shilingi Bilioni 152 katika usafiri kwa njia ya maji, na ameahidi kuwa MSCL itafanya kazi kwa juhudi na maarifa kuhakikisha uchukuzi kwa njia ya maji unaboreshwa ukiwemo mpango mkakati wake wa kuanzisha huduma za usafirishaji mizigo katika Bahari ya Hindi kati ya Dar es Salaam, Comoro, Madagascar, Shelisheli na maeneo mengine.

Mhe. Rais Magufuli amempongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa MSCL Bw. Hamissi kwa mageuzi makubwa anayoyasimamia ambayo yameonesha mwelekeo mzuri wa kampuni hiyo ya Serikali ambayo kwa kipindi kifupi imefufua meli nne kati ya 14 zilizoachwa na Hayati Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na amewapongeza wananchi wa Kanda ya Ziwa kwa kupata matumaini mapya ya kurejeshewa huduma za uhakika za usafiri kama alivyowaahidi wakati akiomba kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Amewapongeza Watanzania wote kwa kuchapa kazi na kulipa kodi zinazotumika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, na amesisitiza kuwa kutekelezwa kwa miradi hiyo ni uthibitisho kuwa Watanzania wanaweza hata bila kukopa au kupata ufadhili unaokuja na masharti magumu.

Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa kwa kutumia fedha za Watanzania wenyewe ikiwemo mpango wa karibuni wa kujenga reli ya Mwanza – Isaka kwa kiwango cha kisasa (standard gauge), kukarabati meli nyingine 5 na ameahidi kuwa Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kununua meli mpya itakayofanyakazi katika Bahari ya Hindi kuanzia bajeti ijayo.

Amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Aloyce Kamwelwe kwa kazi nzuri zinazofanywa na wizara hiyo zikiwemo ujenzi wa meli 3 katika Ziwa Nyasa, ukarabati wa MV Liemba utakaofanyika hizi karibuni, uanzishaji wa Wakala wa Huduma za Bandari (TASAC) na upanuzi wa Bandari za Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Kemondo, Bukoba na Nyamilembe.

Kesho tarehe 09 Desemba, 2019 Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatakayofanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Mwanza
08 Desemba, 2019

Sunday, December 8, 2019

LIVE: HAFLA YA UWEKAJI JIWE LA MSINGI UJENZI WA MELI MPYA , CHELEZO NA UKARABATI WA MV VICTORIA NA BUTIAMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anaweka Jiwe la Msingi miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya , Chelezo na Ukarabati wa M.V Victoria na M.V Butiama katika Ziwa Victoria Jijini Mwanza. Sherehe zinazofanyika Katika Bandari ya Igogo Jijini Mwanza.

Bondia Anthony Joshua kutoka nchini Uingereza ameshinda kwa pointi akimgaragaza Andy Ruiz Jr. kutoka Mexico, katika pambano la marudiano uzani wa juu lililomalizika usiku huu, Saudi Arabia Ushindi wa Joshua ni kisasi kwa Ruiz kufutia kupoteza kwa TKO katika pambano la kwanza lililofanyika mwezi Juni mwaka huu.

KWA MARA YA KWANZA WAZEE WA MILA WAKUTANA NA KUUNGANA KWENYE VITA DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI



 Wazee wa mila kutoka mikoa tisa nchini yenye kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia wamekubaliana kutumia ushawishi walio nao ili kwenye mapambano dhidi ya vitendo hivyo ikiwemo ukeketaji, kutakasa wanawake, mimba na ndoa za utotoni.

Wazee hao wamefikia maazimio hayo Disemba 05, 2019 jijini Mwanza kwenye mkutano ulioshirikisha viongozi wa mila zaidi ya 200 kutoka makabila mbalimbali ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita, Kagera, Simiyu, Tabora, Katavi na Manyara ulioandaliwa na shirika la UN Women.

Hata hivyo mmoja wa wazee hao, Chifu Mfungo Charles kutoka mkoani Geita amesema changamoto waliyonayo ni kukosa nguvu kisheria na hivyo kuomba Serikali kuwarejeshea mamlaka waliyokuwa nayo hatua itawaongezea nguvu ya kupambana na yeyote atayekumbatia mila zinazochochea ukatili wa kijinsia.

Kwa upande Mkuu wa kitengo cha kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike kutoka shirika la UN Women, Lucy Tesha amesema wazee wa mila ni wadau muhimu katika kutokomeza mila na desturi zinazorudisha nyuma maendeleo ya wanawake hivyo kuwashirikisha kwenye mapambano hayo kutasaidia kuleta mabadiliko katika jamii zao ikiwemo kuwashirikisha wanawake katika shughuli za kiuchumi.

Itakumbukwa mikoa yenye kiwango kikubwa cha ukatili nchini ni Mara asilimia 78, Shinyanga asilimia 78, Tabora asilimia 71, Kagera asilimia 67, Geita asilimia 63, Simiyu asilimia 62, Kigoma asilimia 61, Mwanza asilimia 60, Njombe asilimia 53, Dodoma asilimia 50 na Katavi asilimia 50.




  Wazee wa mila kutoka mikoa tisa nchini yenye kiwango kikubwa cha ukatili wa kijinsia wakifuatilia mkutano huo.
 Wazee wa Mila kutoka mikoa tisa nchini yenye kiwango kikubwa cha vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa kwenye mkutano wa kujengeana uwezo na kuweka mikakati ya kutokomeza vitendo hivyo.

WARATIBU ELIMU WAZEMBE KUCHUKULIWA HATUA KALI MKOANI SONGWE

 Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akizungumza na Waratibu Elimu kata na Wasimamizi wa Sekta ya Elimu Mkoa wa Songwe ambapo amesema atawachukulia hatua kali za kinidhamu waratibu wazembe.
 Waratibu Elimu kata na Wasimamizi wa Sekta ya Elimu Mkoa wa Songwe wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila (Hayupo pichani) wakati wa kikao cha kutathmini Maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa mwaka 2019 na kupanga mikakati ya kuboresha elimu kwa mwaka 2020.

Waratibu Elimu kata na Wasimamizi wa Sekta ya Elimu Mkoa wa Songwe waliobainishwa katika ripoti ya uchunguzi wa hali ya sekta ya Elimu kuwa ni wazembe katika kusimamia maendeleo ya elimu watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amesema hayo jana wakati wa kikao na Waratibu Elimu Kata na Maafisa Elimu ili kutathmini maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa mwaka 2019 na kupanga mikakati ya kuboresha elimu kwa mwaka 2020.
“Tuliwapa kazi wadhibiti ubora ya kufanya uchunguzi kwanini Mkoa wetu haufanyi vizuri kielimu na ripoti yao imebainisha uwepo wa uzembe wa waratibu elimu Kata katika usimamizi, sasa nitachukua hatua kali kwa waratibu elimu wote wazembe.”, amesema Kafulila.
Kafulila amesema Waratibu Elimu kata wote walisaini Mkataba ambao uliwataka kusimamia Sekta ya elimu na kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda lakini pia serikali imewawezesha posho na usafiri lakini wapo baadhi yao ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao.
“Serikali imewapa posho na Waratibu Elimu Kata lakini baadhi yao wamebainishwa katika ripoti kuwa wanafanya kazi kwa kuogopana na kuendekeza urafiki, hawawachukulii hatua walimu na wakuu wa shule ambao hawatimizi majukumu yao, hao hatuwezi kuwavumilia.”, amesisitiza Kafulila.
Naye Mwenyekiti wa Wadhibiti Ubora wa Elimu Mkoa wa Songwe Mwalimu Jackson Lwafu amesema walitathmini kwanini baadhi ya shule katika Mkoa wa Songwe zimeshuka kielimu na walibaini kuwa usimamizi dhaifu umechangia kwa kiasi kikubwa.
Lwafu amesema endapo wasimamizi wa Elimu Mkoa wa Songwe watatambua majukumu yao na kuyasimamia, maendeleo ya sekta ya Elimu Mkoa wa Songwe yatakuwa mazuri.
Mratibu Elimu Kata ya Mkukwe Wilayani Songwe Mwalimu Judith Mwasoke amesema taarifa ya wathibiti ubora inasikitisha kwakuwa ili kuwe na mafanikio lazima taratibu zifuatwe hivyo suala la kuoneana aibu na kuogopana halifai na waratibu Elimu Kata wenye tabia hiyo waache.
Afisa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mtafya Wilson amesema kwa mwaka 2020 watahakikisha walimu wanafundisha vipindi vyote pamoja na kuwasimamia Waratibu Elimu Kata wanatimiza wajibu wao.
Afisa Elimu Mkoa wa Songwe Juma Japhet Kaponda amesema Matokeo ya darasa la saba mwaka 2019 hali haikuwa nzuri kwakuwa Mkoa ulipanda ufaulu kwa asilimia 1.65 kwa kuwa na ufaulu wa asilimia 75 na Mkoa ukishika nafasi ya 21 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2018 wa asilimia 73 na nafasi ya Mkoa wa Songwe ilikuwa 17.