ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 11, 2019

MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI NOVEMBA WAONGEZEKA.


Mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwaka ulioishia Mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi  asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 kwa Mwaka ulioishia Mwezi Octoba 2019.

Hayo yameelezwa hii leo Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu  za Jamii,Ruth Minja wakati akizungumza na waandishi wa habari hii leo na kuongeza kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba  2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Octoba 2019.

Minja ameongeza kuwa baadhi ya bidhaa zisizo za Vyakula zilizoongezeka bei kwa mwezi Novemba 2019,zikilinganishwa na bei za mwezi Novemba 2018, ni pamoja na Mavazi kwa asilimia 2.7,Mkaa kwa asilimia 4.4,Samani kwa asilimia 3.1,huduma ya malazi kwenye nyumba za wageni kwa asilimia 5.0 na Mazulia kwa asilimia 6 3 huku pia akibainisha kuongezeka kwa Mfumuko wa bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019


"Mfumuko wa bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 5.1 kwa mwaka ulioishia mwezi Octoba 2019"Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ruth Minja

Katika nchi ya Kenya Minja amesema kuwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.56 kutoka asilimia 4.95 kwa mwaka ulioiehia mwezi Novemba 2019 na kwa upande wa Uganda,Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 2.5 kwa mwaka ulioishia mwezi Octoba 2019.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.