ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 31, 2012

SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI








Picha ya wadau wa mazingira pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Mwanza.

KAMPENI ZA KIRUMBA ZAMALIZIKA LEO CHADEMA WACHOMA BENDERA NA KADI ZA CCM

Mh. Sitta na mgombea udiwani kata ya Kirumba Jackson Robert 'Masamaki'

Sehemu ya wananchi wa Kirumba.

"Mate ya mzee hayaanguki chini ovyo" Waziri wa ushirikiano nchi za afrika mashariki Samwel Sitta.

"Kupitia uchaguzi wa Kirumba imedhihirika kwa umma kwamba Chama cha mapinduzi kinaumoja" Waziri wa Nishati na Madini, Mbunge wa Sengerema Wiliam Ngeleja.

Diwani wa kata ya mkolani Mabula akizungumza na wananchi katika kampeni za mwisho leo kumnadi swahiba wake Jackson 'Masamaki'.

Kaborow naye alikuwepo.

Manjonjo..

Madiwani walioingia kwenye kinyang'anyiro na hatimaye Jackson kuwashinda wakimnadi mwenzao.

Sehemu ya Wananchi waliojitokeza.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe akimwaga sera za CHADEMA kumnadi mgombea wa udiwani kata ya Kirumba.

Harakati zikiendelea jukwaa kuu.

Manjonjo.

Wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa mwisho kumnadi mgombea udiwani kata ya Kirumba kwa Tiketi ya CHADEMA Bahati Kahungu.

Kampeni za Chadema kumnadi mgombea wake Kahungu zilimalizika kwa kuchoma bendera na kadi za CCM kitendo kilichofanyika jukwaani wazi wazi.

Kampeni rasmi zimeisha hii leo navyo vituo tayari vimeandaliwa kilichobaki ni kupiga kura kumchagua diwani hapo kesho tarehe 01/04/2012.

DIAMOND KUKAMUA LEO GOLD CREST MWANZA

Ze bango.

Stoper wa The Big Top Ten na Diaamond.

Diamond na we' ndani ya Mwanza.

Friday, March 30, 2012

FLORA MBASHA KUTUMBUIZA TAREHE 1 APRIL NCHINI MAREKANI

Mwimbaji maarufu Afrika Mashariki katika medani ya Muziki wa Injili Flora Mbasha yuko ziarani kwa mwezi sasa nchini marekani kwaajili ya huduma ya tar1 april hapa ni mchanganyiko wa wanamuziki mbalimbali maarufu wa nyimbo za injili katika mazoezi ya nyimbo zitakazoimbwa.

Hapa Flora alikuwa akielezea jinsi ya kuitikia nyimbo zake zote atakazoimba, baada ya ziara nchini Marekani mwimbaji huyo anategemea kuelekea nchini Canada kwa wiki moja kisha Uingereza kwa wiki 1 tena na kurudi nyumbani Tanzania.

Vionjo vikipikwa..

Kushoto ni mpiga piano maarufu sana na ndiye mwalimu wa sauti na anasimamia music ni music dirrector pia ndiye mwandaaji wa marathon hapa Boston kwa wale wanaojua kukimbia Tanzania fursa ipo pembeni aliyesimama ni mpiga Bass maarufu sana ni mkali mno anapiga Bass utasema ni mashine inapiga kumbe ni vidole tu.

Hapa kitu kinapikwa..

Aaaah mwana wa kwetu..

Chagua pozi kali Pozi namba 1.

Au Pozi namba 2.

Nani kaona mboga?

Meneja ambaye vilevile ni mume wa Mwanamuziki wa injili Flora Mbasha, Emanuel Mbasha akiwa na wenyeji wake.

Flash ya pamoja.

TANZANIA INAONGOZA KUWA NAVIZUIZI VISIVYOFAA JUMUIYA YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI: MBUNGE MASHA

Tanzania inatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kuwa na vizuizi ving visivyofaa mipakani na katika sheria zake kuliko nchi nyingine zote Afrika Mashariki ambavyo vinasababisha watu wake kuzikosa fursa zilizopo ndani ya jumuiya hiyo, hayo yamebainishwa na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Dr.F.Lwanyantika Masha alipotembelea ofisi ya Chama Cha Waandishi wa Habari Mwanza (MPC).

Pia mbunge huyo amesema kuwa watanzania wengi hawajapewa habari vya kutosha kuhusu fursa zilizopo ndani ya soko la nchi za Afrika Mashariki ili kuzichangamkia fursa zilizopo.

Dr.Masha ameshauri na kutia msisitizo kuwa badala ya kunung'unika Tanzania yapaswa kujiandaa na changamoto za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili wadau wake wasipwaye katika soko.


Makamu Mwenyekiti wa MPC Frola Magabe akisoma risala mbele ya Mh. Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Dr.F.Lwanyantika Masha alipotembelea ofisi ya Chama hicho chenye wanachama 130 jijini Mwanza anayefuata ni katibu wake E. Soko.

Ndani ya Mwezi April 2012, Dr.F.Lwanyantika Masha anategemea kuzindua vitabu vyake viwili MAJUKUMU YA MBUNGE na AZIMIO LA ARUSHA (alichokishika).

Picha ya pamoja.
Kuhusu MUUNGANO WA KISIASA Masha amesema kuwa moja kati ya makubaliano ya Shirikisho la Jumuiya ya Afrika mashariki ni kwamba hatimaye mara baada ya kuondoa Ushuru wa forodha, kuwa na Common Market, kuwa na Sarafu moja pamoja na mfumo wa fedha hatua itakayofuata ni kuwa na Shirikisho la kisiasa (POLITICAL FEDERATION) nayo mazungumzo tayari yamekwishaanza.

ANGETILE OSIAH AREJEA TOKA INDIA KWA MATIBABU

Katibu mkuu wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah amerejea akiwa mzima wa afya baada ya operesheni ya kichwa nchini India. (picha juu ni kichwa chake baada ya kufanyiwa upasuaji)

Angetile Osiah ambaye hapo awali alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wodi ya taasisi ya Mifupa (MOI) alipelkwa Nchini India kwa matibabu zaidi mara baada ya vipimo kufanyika na ushauri wa jopo la madaktari nchini kutolewa.
Mungu ashukuriwe.

Thursday, March 29, 2012

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA KUANZA MAANDALIZI YA BONANZA LA MEDIA DAY

Chama cha Waandishi wa Habari jijini Mwanza wameanza mchakato wa maandalizi ya Bonanza (Media day Spots gala bonanza) kwa ajili ya kuadhimisha sikukuu ya habari (Media Day) inayotarajiwa kufanyika tarehe 15 April mwaka huu. Tamko limetolewa rasmi leo katika ofisi ya Club hiyo (MPC) na mratibu wa Bonanza hilo Bw. Edwin Soko. Mratibu wa Bonanza la Wandishi wa habari, Bw. Edwin Soko akisoma tamko rasmi la kuanza kwa maandalizi hayo mbele ya wandishi wa habari

Bw. Soko ameeleza kuwa Bonanza hilo lina lengo la kuwaunganisha waandishi wa habari wote wa mkoa wa Mwanza na wadau wa habari ili kufurahia pamoja huku ikizingatiwa kuwa Tanzania inaadhimisha miaka hamsini ya uhuru ikiwamo na uhru wa waadnish wa habari. Bw. Soko anasema kuwa Bonanza hilo litakuwa la kukata na shoka na ambalo halijawahi kutokea nchini Tanzania toka kupatikana kwa uhuru wa nchi yetu.

Ili kufanikisha Bonanza hilo, Bw. Soko amewaomba wadau mbalimbali kuweza kujitokeza ili kuunga mkono maandalizi hayo kwa kudhamini Bonanza hilo. Wadau mbalimbali walioombwa kujitokeza ni pamoja na wamiliki wa Mahotel, Taasisi za fedha kama mabenki, makampuni ya vinywaji, shule na vyuo mbalimbali, kampuni za simu, mifuko ya akiba ya jamii, kampuni za usafirishaji na wadau wengine mbalimbali wenye nia njema na tasnia ya habari.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini mratibu wa bonanza hilo Bw. Soko

Mratibu huyo amesema wadau hao wataweza kujitangaza vyema kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa jijini na hivyo kuongeza wateja na uzalishaji wa bidhaa na huduma zao. Amesema pia waandishi wa habari watakuwa na nafasi nzuri ya kujenga mahusiano na kufikiwa na jamii kwa huduma wanazotoa na kuboresha uimara wa tasnia ya habari hapa jijini Mwanza na tanzania kwa ujumla.

Bw. Soko alimalizia kwa kuwaomba wadau wajitokeze ili kudhamini Bonanza hilo na kutangaza biashara zao kupitia vyombo vya habari vya jijini Mwanza.
wadau wakibadilishana mawazo mara baada ya Bw. Soko kumaliza kusoka tamko hilo.

Hapa ni picha ya pamoja ya waandishi wa habari, akiwemo shani Saidi (wa kutoka kushoto), Edwin Soko, Jane Kajoki, Bw. Marcus na wengine waliojitokeza ofisini hapo.
PICHA/HABARI NA ALLAN KISOI

SAFARI NDEFU YA SOKA LA BONGO.

Niko uwanja wa mkwakwani kuangalia ligi ya mkoa kati ya Manguli wa zamani African sports na Prison Tanga. Kilicho nisikitisha ni utaratibu mbovu wa kuingia uwanjani na baiskeli, tena kibaya zaidi zikiwekwa kwenye njia na majukwaa ya kukalia.

Angalia kwenye kiambatanisho.
From "Mohamedi Mtoi"