ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 29, 2012

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA KUANZA MAANDALIZI YA BONANZA LA MEDIA DAY

Chama cha Waandishi wa Habari jijini Mwanza wameanza mchakato wa maandalizi ya Bonanza (Media day Spots gala bonanza) kwa ajili ya kuadhimisha sikukuu ya habari (Media Day) inayotarajiwa kufanyika tarehe 15 April mwaka huu. Tamko limetolewa rasmi leo katika ofisi ya Club hiyo (MPC) na mratibu wa Bonanza hilo Bw. Edwin Soko. Mratibu wa Bonanza la Wandishi wa habari, Bw. Edwin Soko akisoma tamko rasmi la kuanza kwa maandalizi hayo mbele ya wandishi wa habari

Bw. Soko ameeleza kuwa Bonanza hilo lina lengo la kuwaunganisha waandishi wa habari wote wa mkoa wa Mwanza na wadau wa habari ili kufurahia pamoja huku ikizingatiwa kuwa Tanzania inaadhimisha miaka hamsini ya uhuru ikiwamo na uhru wa waadnish wa habari. Bw. Soko anasema kuwa Bonanza hilo litakuwa la kukata na shoka na ambalo halijawahi kutokea nchini Tanzania toka kupatikana kwa uhuru wa nchi yetu.

Ili kufanikisha Bonanza hilo, Bw. Soko amewaomba wadau mbalimbali kuweza kujitokeza ili kuunga mkono maandalizi hayo kwa kudhamini Bonanza hilo. Wadau mbalimbali walioombwa kujitokeza ni pamoja na wamiliki wa Mahotel, Taasisi za fedha kama mabenki, makampuni ya vinywaji, shule na vyuo mbalimbali, kampuni za simu, mifuko ya akiba ya jamii, kampuni za usafirishaji na wadau wengine mbalimbali wenye nia njema na tasnia ya habari.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini mratibu wa bonanza hilo Bw. Soko

Mratibu huyo amesema wadau hao wataweza kujitangaza vyema kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa jijini na hivyo kuongeza wateja na uzalishaji wa bidhaa na huduma zao. Amesema pia waandishi wa habari watakuwa na nafasi nzuri ya kujenga mahusiano na kufikiwa na jamii kwa huduma wanazotoa na kuboresha uimara wa tasnia ya habari hapa jijini Mwanza na tanzania kwa ujumla.

Bw. Soko alimalizia kwa kuwaomba wadau wajitokeze ili kudhamini Bonanza hilo na kutangaza biashara zao kupitia vyombo vya habari vya jijini Mwanza.
wadau wakibadilishana mawazo mara baada ya Bw. Soko kumaliza kusoka tamko hilo.

Hapa ni picha ya pamoja ya waandishi wa habari, akiwemo shani Saidi (wa kutoka kushoto), Edwin Soko, Jane Kajoki, Bw. Marcus na wengine waliojitokeza ofisini hapo.
PICHA/HABARI NA ALLAN KISOI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.