ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 25, 2009

FLASH BACK PICTURE NA MIE WIKI HII


UTOTONI NILIKUWA NAAMINI KUWA WAKATI UKIPIGA PICHA HURUHUSIWI KUVUTA PUMZI NI MWENDO KUGANDA. HAPA NI NDANI YA PHOTO ME STUDIO ARUSHA waliosimama kuanzia kushoto MY Bro ADAM SENGO, young father KEREBU & my young mom ELIZABETH CHARLES.
walioketi kutoka kushoto G.SENGO, my late young mom LYDIA CHARLES, sis LEAH SENGO (aliyepakatwa) & my sis RODHA SENGO. NAKUMBUKA MARA BAADA YA PICHA HII KUPIGWA NIKASEMA "MAMDOGO KIDOGO NIHEME" (lafudhi ya kichaga) TEHE! UNACHEKA NINI......?

TUMETOKA MBALI AISEE! NI MIAKA YA 80 MITAA YA KATIKATI YA JIJI JAMAA WAMEPIGA PICHA WAKILA MAHINDI. HEBU MDAU VUTA PICHA JAMAA HAWA KABLA YA PICHA WAKATI WAKILITAFUTA POZI WALIMWAMBIAJE MPIGA PICHA? AU KULIKUWA NA UBISHANI :-OOH TUPIGE TUMEYASHIKILIA, OOH TUPIGE TUKIWA TUKIWA TUNAKULA, NG'ATENI KABISA WATAJUAJE NI YETU WATASEMA TUMETUMWA AU TUMEYAAZIMA KWA MAMA MUUZA KUPIGIA PICHA. TEHE!

MUZIKI WA KIROHO

MUZIKI WA INJILI KATIKA MIAKA YA SASA UMEJIPATIA UMAARUFU MKUBWA IKIWA NI PAMOJA NA KUVUTIA WASANII WENGI KUSHIRIKI WAKE KWA WAUME. KANDA YA ZIWA INAJIVUNIA KUWA NA KWAYA NYINGI MPYA MPYA NA ZA ZAMANI ZENYE HISTORIA KTK UIMBAJI. VILE VILE KUNA WASANII SOLO WANAO HUSIKA NA MUZIKI WA INJILI AMBAO WAMEKUWA WAKIJIUNGA KWA WINGI TENA KWA VIWANGO JAMBO AMBALO NI LA KUJIVUNIA KATIKA UKUAJI WA MUZIKI HUO. HAPINESS G. MUNISI MUIMBAJI SOLO ALIANZA KUIMBA KITAMBO NA HATIMAYE 2008 ALBUM YAKE "NI MUNGU" YENYE NYIMBO 8 IKAKAMILIKA NOW ANAJIANDAA NA VOL 2. KAMATA COPY YAKO.

Wednesday, September 23, 2009

VIVA AFRIKA MAWIO NA MACHWEO YA MUZIKI WA AFRIKA


HABARI NZURI ZA UHAKIKA BILA KOROMBWEE HABARI ZA WASANII UWAPENDAO NA MUZIKI WA AFRIKA TEMBELEA www.vivaafrika.blogspot.com RUBANI WAKO AGAPE MSUMARI AMBAYE NI MTANGAZAJI, MWANAHABARI KAKAMILIKA NA ANAUFAHAMU MKUBWA WA HISTORIA YA MUZIKI HATA KUIMBA GEJI INASOMA NI ILE ILE "FULL ARIFU". picha kwa hisani ya vivaafrika.

SIKINDE MMESIKIA HII?


EH BANA VIJEMBE VISHAANZA MSONDO WANASEMA KUWA KWENYE MPAMBANO WAO WA NANI ZAIDI KATI YAO NA SIKINDE UTAKAOFANYIKA MWANZA USIKU WA TAREHE 3 OCTOBER WATAMPIGA MTU GOLI TATU. LA UTANGULIZI LITACHANWA NAYE SAID MABELA. KIMTINDO GANI?, STYLE GANI?, NDANI YA JEZI GANI? KAMA WE BARUTI BASI LIPUKA NAMI TWENDE TWENDEEEE! mabe-mabe-mabe-mabela!!!!

AJALI KAMA KAWA


TUKIWA BADO NA ZOEZI KUBWA LA KUKAGUA UBORA WA VYOMBO VYA USAFIRI BARABARANI SAMBAMBA NA UBORA WA MADEREVA KILA KUKICHA SIMULIZI ZA AJALI IMEKUWA SIYO HABARI MPYA TENA (ni suala la kuzoeleka) LEO ASUBUHI SAA 3:45 ENEO LA PEPSI JIJINI MWANZA MWENDESHA BAISKELI AKIWA ANA OVATEKI DALADALA MBELE AKAKUTANA NA PIKIPIKI KUIKWEPA KULIA ZAIDI IKAMFATA ZIKAPEANA. JAMAA WA BAISKELI ENEO LA KULIA KICHWANI KAPATA MAJERAHA MAKUBWA NA DAMU ZINATIRIRIKA KINOMA NA ALIKUWA KABEBA CHEREHANI NYANG'ANYANG'A. MWENYE PIKIPIKI MTARONI AZUNGUMZI VIZURI KAUMIA TAYA. INGAWA BAADAE ALITOROSHWA NA WENZIE.

MWENDESHA BAISKELI AKITAFAKARI MAUMIVU MARA BAADA YA KUPATA AJALI ENEO LA PEPSI BARABARA YA KENYATA KIUKWELI KAUMIA VIBAYA SANA.

JAMAA ALIYELAMBANA NA MWENDESHA BAISKELI AKIONDOSHWA KIMYAKIMYA NA WAENDESHA PIKIPIKI WENZAKE MARA BAADA YA KUONA WATU WA USALAMA KWA MBALI WAKIKARIBIA ENEO LA AJALI. YAWEZEKANA KABISA HANA SIFA ZA KUFANYA BIASHARA YA KUBEBA ABIRIA NDO MANA AKAAMUA KUTIMUA.

Tuesday, September 22, 2009

NAPIGA ''MOJA - MBILI - TATU''


TANGU ENZI ZA PHOTO ME STUDIO ARUSHA, AMITHA PHOTO STUDIO NA ONE WAY SHINYANGA BILA KUSAHAU MAMBO KAHAMA, LONG TIME MZAZI NIMEYAMIS MASUALA YA KUPIGA PICHA STUDIO. SO THIS TIME WACHA NIJIKUMBUSHEEEE.. KATIKA MAMBO YETU YALEE YA FLASH BACK PICTURE IJUMAA ITAKUWA ZAMU YANGU@ g.sengo

NI MSONDO AU SIKINDE?


MIAKA IMEENDA MIAKA IMERUDI, KILA MMOJA AMEKUWA AKIMTAMBISHIA MWENZIE :- OOH MIMI MKALI, OOH HAWATUWEZI, OOH WAMEKWISHA WALE, OOH SIJUI NINI NINI... YOTE TISA, KUMI WAKATI UMEWADIA KUTAMBUA UPI MCHELE ZIPI PUMBA. HUKU SIKINDE HUKU MSONDO NI LIVE BILA CHENGA NDANI YA JIJI LA MWANZA SIKU HIYO GITAA ZITALIA, SAUTI ZITASEMA

MAHALI:- CCM KIRUMBA MWANZA
TAREHE:- 3/10/ 2009
KUANZIA SAA 1:30 USIKU
MPAKA MSHINDI APATIKANE
KIINGILIO TSH 5000/=
MSONDO Vs SIKINDE NANI ZAIDI?
HATOKI MTU MZIMA