ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 17, 2022

NAIBU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA AWAASA VIJANA KUWA WAAMINIFU.



 Naibu Katibu mkuu wa Uvccm Tanzania bara Mussa Mwakitinya aliyevalia suti ya bluu akizungumza na wanafunzi wa chuo Cha Furahika katika mahafali hayo ya kumi.


 Mkuu wa Chuo Cha Furahika Devid Msuya aliyevalia shati la kijana akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho.

Na Victor Masangu


Naibu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (Uvccm) Tanzania bara Mussa Mwakitinya amewaasa vijana kuwa na maadili na uaminifu pamoja na kujiunga katika vikundi ili waweze kupata fursa za mikopo inayotolewa na halmashauri.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mahafali ya kumi ya wanafunzi wa chuo Cha Furahika Education College kilichopo Wilaya Ilala Jijini Dar es Salaam na kuwataka kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ili kuweza kutimiza malengo yao.

Alisema kwamba  serikali imetenga asilimia kumi ambazo zinatoka kwa halmashauri kwa lengo la kuwasaidia vijana,wanawake na walemavu hivyo hiyo ni fursa ya kipekee ambayo itawasaidia kuwakomboa vijana ambao tayari wamejiunga katika vikundi.

"Kitu kikubwa ambacho ninawaasa vijana ambao mmeweza kumaliza katika chuo hiki ni lazima kuwa na uaminifu pamoja na maadili na kuachana kabisa na vitendo vya wizi pindi unapopewa dhamana ya kazi ya mtu sio unaamua kuiba vifaa hii sio sahihi,"alisema Mussa

Aidha aliongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngazi za chini hadi juu hivyo kuwataka mafunzo ambayo wameyapata wakayatumie vizuri ili waweze kufika mbali na kutimiza ndoto zao.

Katika hatua nyingine alisema atahakikisha anashirikiana na wawazi na walezi katika maeneo mbali mbali ambao watoto wao wameshindwa kujiendeleza zaidi katika suala la elimu ili waweze kwenda kujiunga na chuo hicho ambacho kitawasaidia kupata ujuzi wa fani mbali mbali.

"Ninaahidi kuyafanyia kazi yale yote ambayo yamesemwa katika risala yenu na kwamba nimeambia chuo hiki cha Furahika kinatoa elimu bure kabisa hii programu itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwakomboa vijana wetu ambao wameshindwa kujiendeleza,"alisema Naibu huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Devid Msuya alisema lengo la kuanzisha chuo hicho ni kuunga mkono  juhudi za serikali ya awamu ya sita katika suala zima la kuwasaidia vijana kwenye mambo ya elimu.


Msuya alibainisha kuwa baada ya kuanzishwa kwa chuo hicho kimeweza kuwapa fursa ya vijana zaidi ya 500 kupata ajira pamoja na wengine zaidi ya mia 200 kujiajiri wao wenyewe katika shughuli zao mbali mbali kutoka na fani ambazo wamezisomea.

Aidha alisema katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 36 wameweza kuhitimu katika kozi mbali mbali ikiwemo ya udereva,ufundi wa kusho,uselemana,ufundi nyumba,ufundi wa kompyuta pamoja na fani nyinginezo.


"Chuo chetu hiki cha Furahika wanafunzi wote wanasoma bure lakini mzazi au mlezi anatakiwa kumuwezesha mtoto wake baadhi ya vitendea kazi lakini lengo letu kubwa ni kuwasaidia vijana ambao wameshindwa kujiendeleza katika suala zima la masomo,"alisema Msuya.


Pia Msuya alisema lengo lao lingine ni kufikia vijana wapatao 300 kwa kila mwaka kutoka Tanzania bara na visiwani ili kuweza kuwapa ujuzi wa fani mbali mbali ambazo zitawasaidia kupata ajira kutoka maeneo tofauti na wengine kujiajiri wenyewe.

Friday, September 16, 2022

BENKI YA CRDB YAPATA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 130 KWA AJILI YA KUWEZESHA SEKTA YA BIASHARA NCHINI

 


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Mkuu wa Masuluhisho ya Mikopo kwa Afrika kutoka Investec Bank, Rowan King (wapili kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Mikopo ya Pamoja wa Benki ya Intesa Sanpaolo, Gustaaf Eerenstein (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Benki Kimataifa wa Bank One, Carl Chirwa (wapili kushoto) pamoja na Meneja Mikopo Maalum Benki ya Biashara ya Mauritius,Hans Dallo wakiweka mikono pamoja ikiwa ni ishara ya kuonyesha ushirikiano baada ya kusaini mikataba ya makubaliano waliyosaini inayoiwezesha Benki ya CRDB kupata kiasi cha dola za kimarekani milioni 130 kwa ajili ya kukopesha sekta za biashara na wajasiriamali nchini.
---
Benki ya CRDB Mnamo tarehe 15 September 2022 imeingia mkataba wa makubaliano na Benki ya kimataifa ya Intesa Sanapaolo ya nchini Italia, na Investec Bank ya nchini Afrika Kusini unaoiwezesha benki hiyo kupata kiasi cha dola za kimarekani milioni 130 kwa ajili ya kukopesha sekta za biashara na wajasiriamali nchini.

Mapema mwaka huu, Benki ya CRDB iliingia mkataba wa awali na benki hizo za kimataifa kusaidia kupatikana fedha katika masoko ya kimataifa kwa ajili ya kuimarisha mtaji wa benki hiyo na kukuza uwezo wa kutoa mikopo.

“Tunafurahia sana kufanikisha makubaliano haya. Fedha hizi zilizopatikana kutoka masoko ya kimataifa zitasaidia kuimarisha mtaji wa Benki yetu na kukuza uwezo wetu wa kutoa mikopo kwa wateja wakubwa na wadogo hapa Tanzania na Burundi. Kipekee niwashukuru Investec Bank na Intesa Sanpaolo kwa ushirikiano waliotupa,” alisema Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB.

Benki ya CRDB inakuwa benki ya kwanza nchini kupata fedha za uwekezaji kutoka masoko ya kimataifa. Kwa mujibu wa Nsekela, lengo lilikuwa ni kukusanya dola milioni 50, lakini viwango bora na ufanisi mkubwa wa benki hiyo ulivutia wawekezaji wengi wa kimataifa, na kupelekea kupatikana kwa dola milioni 130.

Benki ya CRDB ni moja ya benki kumi zilizoorodheshwa kama benki bora na salama zaidi kuwekeza barani Afrika na Moody`s Investors Services na kupewa daraja la ‘B1 Outlook” ambalo ni daraja la juu zaidi kwa taasisi za fedha katika ukanda wa jangwa la Sahara. Mwaka huu Benki hiyo pia imetajwa kuwa ’Benki Bora Tanzania’ na jarida maarufu la nchini Uingereza.

“Kama Benki inayoongoza nchini Tanzania, Benki ya CRDB inaendelea kutazama fursa za biashara katika sekta za kimkakati ili kukuza uchumi wa nchi. Fedha hizi zitatusaidia kuimarisha shughuli zetu za utoaji mikopo hususani mikopo ya wanawake na vijana na kuimarisha zaidi nafasi yetu katika soko kama benki inayoongoza kwa kufadhili sekta za uchumi,” aliongeza.

Rowan King, Mkuu wa Masuluhisho ya Mikopo kwa Afrika kutoka Investec Bank, alisema kupatikana kwa fedha hizo katika masoko ya kimataifa kunaonyesha ni imani ya taasisi za fedha duniani kwa Benki ya CRDB na uchumi wa Tanzania.

"Tanzania imeonekana kuwa sehemu muhimu ya hadithi ya ukuaji wa Afrika katika miaka michache iliyopita. Bidhaa nyingi muhimu zinazozalishwa Afrika Mashariki, zinasafirishwa nje ya nchi kupitia bandari za Tanzania. Tanzania ina jukumu muhimu katika biashara katika kuimarisha biashara baina ya nchi za Afrika,” alisema.

Dola milioni 130 zilizopatikana ni mara mbili na nusu ya kiasi kilichokusudiwa, anasema Gustaaf Eerenstein, Mkurugenzi wa Huduma za Mikopo ya Pamoja Investec Bank. "Hii inaonyesha kiwango cha juu cha imani ambayo wawekezaji wanayo kwa Benki ya CRDB," alisema Eerenstein.

Ushirikiano huu na Benki ya CRDB na benki za Intesa Sanpaolo na Investec unaendelea kuimarisha uwezo wa benki hiyo katika kutoa mikopo, ambapo mwaka huu pekee imeweza kuingia makubaliano ya zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 300 na mashirika kama IFC, AFDB, AGF, PROPARCO, USAID na DFC kwa ajili ya uwezeshaji wa biashara ndogo na za kati (SME), na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na sekta zisizo rasmi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Mkuu wa Masuluhisho ya Mikopo kwa Afrika kutoka Investec Bank, Rowan King (wapili kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Mikopo ya Pamoja wa Benki ya Intesa Sanpaolo, Gustaaf Eerenstein (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Benki Kimataifa wa Bank One, Carl Chirwa (wapili kushoto), na Meneja Mikopo Maalum Benki ya Biashara ya Mauritius,Hans Dallo wakionyesha mikataba ya makubaliano waliyosaini inayoiwezesha Benki ya CRDB kupata kiasi cha dola za kimarekani milioni 130 kwa ajili ya kukopesha sekta za biashara na wajasiriamali nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto), Mkuu wa Masuluhisho ya Mikopo kwa Afrika kutoka Investec Bank, Rowan King (wapili kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Mikopo ya Pamoja wa Benki ya Intesa Sanpaolo, Gustaaf Eerenstein (wapili kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Benki Kimataifa wa Bank One, Carl Chirwa wakisaini mkataba wa makubaliano unaoiwezesha Benki ya CRDB kupata kiasi cha dola za kimarekani milioni 130 kwa ajili ya kukopesha sekta za biashara kwa wajasiriamali nchini katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB, jijini Dar es Salaam leo tarehe 15 Septemba 2022.

RC MGUMBA WANAOWEKA FEDHA KWENYE MAGODORO WAMEPUNGUA

 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza wakati akifungua tawi la Benki hiyo eneo la Ngamiani Jijini Tanga
Afisa Mkuu na Wateja wakubwa wa Benki ya NMB Alfred Shayo akizungumza wakati wa halfa hiyo
MENEJA wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Dismas Prosper akizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Uchumi na Takwimu wa Benki Kuu ya Tanzania BOT Tawi la Arusha Ernest Ndunguru akizungumza wakati wa halfa hiyo
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa halfa hiyo
MENEJA wa Benki ya NMB tawi la Ngamiani Elizaberth Chawinga akizungumza wakati wa halfa hiyo

Na Oscar Assenga,TANGA

SERIKALI mkoani Tanga imesema kwamba kusogezwa karibu kwa huduma za kibenki kumesaidia kupunguza wananchi waliokuwa wakihifadhi fedha zao kwenye magodoro jambo ambalo ilikuwa ni athari kubwa ikitokea wizi inakuwa rahisi kuweza kuibiwa au kupotea lakini pia zimekuwa salama na hivyo kuepukana na matumizi yasiyokuwa ya lazima.


Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba wakati akifungua tawi jipya la Benki ya NMB Ngamiani lililopo barabara ya 20 Jijini hapa katika halfa iliyokwenda sambamba na utoaji wa mabati 250 kwa shule ya msingi Masiwani.


Alisema uwepo wa tawi hilo utawawezesha wananchi kupata sehemu ambayo yataweza kuhifadhi fedha zao walizozitolea jasho na kuondoa changamoto ya uhifadhi kwenye vyungu vya maji au kulalia kwenye magodoro ambapo ikitokea moto au wizi kuiba kwake inakuwa ni rahisi lakini pia fedha zina vishawishi ukiziweka ndani matumizi yake yanakiwa ni makubwa sana.


Mkuu huyo wa mkoa alisema lakini ikiziweka benki unaweza kuokoa matumizi yasiyokuwa yalazima na unaweza kutumia hapo baadae kwenye matumizi muhimu katika mahitaji na maisha yenu.



Alisema Serikali imeweka mazingira mazuri kuhakikisha jamii ya kitanzania inapata huduma Bora sa kibenki na nafuu huku akiishukuru benki hiyo ambayo imekuwa ikiunga mkono juhudi za Serikali na hivi karibuni mlitenga zaidi ya Bilioni 200 ya mikopo kwenye sekta ya kilimo kwa riba ya asilimia 9.


"Niwapongeze Benki ya NMB kwa kuendelea kubuni huduma mpya kwa kufungua matawi mapya na zaidi ya hapo kuwajali na kuwathamini wateja bila kujali kipato pia serikali inatambua juhudi zenu za kuwawezesha wananchi kupitia mikopo ya wafanyakazi,wakulima na wafanyabiashara wakubwa na wadogo" Alisema Mkuu huyo wa Mkoa

Alisema dunia kwa sasa inakwenda kasi hususani kwa upande wa teknolojia ambazo zimerahisisha huduma za kibenki kutokutegemea matawi rasmi ingawa haiondoi ukweli kwamba kufungua matawi mapya ni kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi ambao hauwezi kupata nje ya tawi la benki.


Mkuu huyo wa mkoa alisema pamoja na mafanikio yaliyoyapata katika kubuni huduma bora na nafuu na za haraka ikiwemo huduma mpya ya Teleza Kidigitali ambayo kwa mara ya kwanza benki inatoa mikopo midogo midogo bila kufika kwenye tawi la benki bila kuwa na dhamana unakopa mwenyewe kupitia simu ya mkononi.


Alisema mikopo hiyo itaondoa adha kwa mama mntilie,babalishe na watu wengine wenye biashara ndogondogo ambao mitaji yao haizidi laki tano hiyo inafaida kubwa ya matumizi ya teknolojia kwani wananchi wengi hususani wafanyabiashara wadogo wadogo huduma hiyo itawanufaisha sana.


Aidha alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu imaweka mikakati mizuri ya kupunguza umaskini kwa wananchi wake hivyo nitoe changamoto kwa ajili ya kuwasaidia na kukuza ajira kwa wananchi kuendelea kutoa mikopo kwa wakazi wa vitongoji vyote vya mkoa wa Tanga mijini na vijijini.


Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo,Afisa Mkuu na Wateja wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB Alfred Shayo alisema kwamba benki hiyo imekuwa ikiendeshwa kwa waledi na ufanisi na ndio maana wameweza kufikia hatua kubwa ya kimaendeleo hapa nchini


Alisema tokea Benki hiyo ilipoanzishwa mwaka 1997 imepiga hatua kubwa kwani awali ilikuwa na matawi 97 lakini sasa matawi yamefikia 227 na uzinduzi wa tawi hilo unaongezeka na kufikia 228 ni hatua kubwa imefanya ili kuweza kuwafikia wateja wake kwa karibu zaidi ambapo usogezaji karibu huduma kwa wananchi hatujaaachwa nyuma kidigitali.


" Benki ilipoanzishwa ilikuwa haina wakala wala ATM lakini kwa sasa ina na atm 762 na mawakala zaidi ya 15000 hii inaonyesha namna mnavyoishi ndoto zenu Benki ua NMB karibu yako na kujipanua kwenye mtandao na tunafanya kazi karibu na Serikali pamoja na wateja wetu kuhakikisha tunaboresha huduma na kutoa masuluhisho kwa wateja wetu"Alisema.


Alisema kwa mwaka jana wametoa trilioni 4.3 za mikopo kwa wateja wadogo wadogo kwa kilimo, biashara ndogondogo na wateja binafsi hiyo imetokana na ushirikiano mzuri walionayo kati yao na Serikali na wateja wao


"Kwa Tanga Benki wetu ya NMB ina matawi 10 kanda ya kaskazini tuna matawi 40 hii inaonyesha namna gani tupo karibu na serikali huku wananchi wanapata masuluhisho ya kuwasaidia kuendeleza shughuli za kuweza kujikwamua kiuchumi"Alisema


Alisema kwa upande wa Kilimo kama walivyosikia serikali ilitoa trilioni 1 kwa ajili ya kukopesha sekta ya kilimo kwa riba ambayo ni ya chini ya asilimia 10 huku akieleza kwamba hawakwenda kuchukua hela benki kuu Tanzania (BOT) hivyo walitenga fedha zao Bilioni 100 kwa ajili ya kukopesha kwa asilimia 10 ilipoisha na wakatenga nyengine bilioni 100 ambayo wanapokesha wakulima wadogo wadogo kwa riba ya asilimia 9.


Naye kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Prosper kwa niaba ya Benki alisema kwamba wamefarijika sana kuona mwitikio kutoka kwa wananchi waliojumuika katika shughuli hiyo muhimu ya uzinduzi wa tawi hilo ambapo ni utekelezaji wa azma yao ya kusogeza huduma karibu na wana chi.


Naye kwa upande wake Meneja wa Uchumi na Takwimu Benki kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Arusha Ernest Ndunguru alisema baadhi ya Benki zimekuwa na tabia ya kutokuweka fedha kwenye ATM mashine hususani nyakati za sikukuu na wikiendi jambo ambalo zimekuwa kero kwa wananchi wengi.


"Mimi ni moja ya wateja wa Benki hapa nchini lakini changamoto kubwa ambazo umekuwa tukikutana nazo ni kukosekana kwa fedha kwenye ATM Mashine hususani nyakati za sikukuu na wikiendi hili tatizo tunaomba lishughulikiwe "Alisema

Thursday, September 15, 2022

WIZARA YABARIKI TFS SAO HILL KUANZISHA UTALII MBIO ZA MAGARI

 

 

 NA ALBERT G. SENGO/ IRINGA
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania ((Tanzania Forest Services (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lilopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamefanikisha mashindano ya magari ya mbio fupi ya Sao Hill Auto Cross ambayo yalikuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa waliofika katika eneo ambalo mashindano yalifanyikia Akizungumza baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mashindano hayo katika Shamba la Miti Sao Hill linalomikiliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Mhifadhi Mkuu wa Shamba hilo Lucas Sabida amesema ndio mara ya kwanza kwa Wakala huo kuandaa mashindano hayo ikiwa ni utalii mpya ambao wameutambulisha kwenye sekta ya utalii nchini.

WANANCHI WA ISUPILO WAMKATAA MWEKEZAJI OVERLAND

 

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kijiji cha Isupilo namna ambavyo watatua mgogoro huo wa ardhi
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Isupilo wakimsikiliza 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakati wa kutafuta njia ya kutatua mgogoro wa ardhi katika kijiji hicho
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa kijiji cha Isupilo namna ambavyo watatua mgogoro huo wa ardhi


Na Fredy Mgunda, Iringa.

Wananchi wa Kijiji cha Isupilo wilaya ya Iringa wamesema kuwa viongozi wa Kijiji hicho wamekuwa chanzo cha migogoro ya ardhi baina ya wananchi na wawekezaji.


Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo walisema kuwa kumekuwa na mgogoro ambao umedumu miaka mingi.


Walisema kuwa kutokana na kutokuwa na uongozi imara kumesababisha familia ya Mzee Kivike kuuza ardhi ambayo imekuwa inakariwa na kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na wananchi kwa zaidi ya miaka kumi na tano.


Waliongeza kuwa mwekezaji Overland aliponunua shamba kwenye familia ya Mzee Kivike amejiongezea eneo la mipaka la hekari zaidi ya 250 ambayo kwa sasa ndio ambalo linaleta mgogoro na wananchi.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa atamwita mwekezaji Overland, viongozi wa ardhi na viongozi wa Kijiji ili kuhakikisha wanatatua mgogoro huo.

 

Moyo alisema kuwa mgogoro huo wa ardhi utatuliwa kwa njia ya amani kwa kuhakikisha kila mtu anapata haki yake kwa mujibu wa sheria za ardhi zinavyosema .


Juliasi Mgeni ni mmoja ya wananchi wa Kijiji cha Isupilo alisema kuwa mwenyekiti wa Kijiji hicho Joakimu kisinini ndio chanzo cha migogoro ya ardhi.


Mgeni alisema kuwa mwenyekiti huyo amejimilikisha ardhi ya wananchi kwa kutumia madaraka aliyokuwa nayo.


Alisema kuwa watu wa ardhi wanachochea mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na mwekezaji kwa kutoa taarifa tofauti tofauti kila mara.


Mgeni alisema kuwa hawaridhishwi na maamuzi ya ofisi ya ardhi ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa hivyo mkuu wa wilaya anaombwa kutatua mgogoro huo.


alimalizia kwa kusema shamba la muwekezaji kampuni ya Overland linahekari 1262 huku hekari 953 hazina mgogoro wowote na hekari 296 ndio zinamgogoro ambao kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha tuhuma hizo

 

ALICHOSEMA MBUNGE WA NYAMAGANA MBELE YA MAKAMU WA RAIS

 NA ALBERT G SNGO/ MWANZA

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Jijini Mwanza Stanslaus Mabula haya ndiyo aliyoyawasilisha jana Tarehe 14 September 2022 mbele ya Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, akihitimisha ziara yake kwa kuweka jiwe la msingi Mradi wa Maji Butimba, Mwanza. Mahitaji ya maji kwa sasa kwa jiji la Mwanza ni lita milioni 160 lakini uwezo wa kuzalisha maji wa chanzo cha maji Capripoint ni lita 98 tu, hivyo baada ya mradi huu kukamilika ifikapo mwezi Disemba 2022 (kama ahadi ya kuharakisha) utaongeza lita milioni 48 na kuwa suluhu ya uhakika kwa changamoto ya upatikanaji wa maji hadi mwaka 2040.







TANZANIA NA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO ZASAINI MAKUBALIANO YA KUBORESHA SEKTA YA ULINZI

 

Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrsai ya Kongo(DR CONGO) zimetiliana saini ya makubaliano katika ushirikiano wa kuboresha sekta ya ulinzi ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mahusiano mema yaliyopo baina ya Mataifa hayo.

Akizungumza jana  baada ya zoezi la kusaini hati ya makubaliano Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nchini Tanzania *Stergomena Tax* amesema kwamba zoezi la makubaliano limeanza baada mazungumzo ya kamati ya ushirikiano sekta ya ulinzi *JPC* ambapo kamati hiyo ikafikia makubaliano hayo.

Aidha amesema kwamba makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano wa kuimarisha sekta ya ulinzi ya Tanzania na DR Congo ili kuwa na mwambata wa wanajeshi yaani Tanzania kupokea wanajeshi kutoka DR Congo huku DR Congo ikipokea wanajeshi kutoka Tanzania kwa ajili yakukabiliana na vitendo vya uhalifu.

“Makubaliano haya yamelenga kuboresha maeneo mbalimbali katika sekta ya ulinzi ikiwemo kubadilishana taarifa za kiintelejensia,kufanya kwa pamoja mafunzo na mazoezi ya kijeshi na kitaalamu, kutembeleana ‘ kushirikiana katika masuala  ya maafa,pia kushirikiana katika tiba wakati wa oparesheni mbalimbali” amesema Waziri Stergomena


Aidha ameongeza kuwa hakuna maendeleo bila amani hivyo Tanzania na DR Congo zinahitaji kuimarisha Biashara na vichocheo vingine akitolea mfano miundombinu ya barabara pamoja na bandari huku akisihi DR Congo kuwa sehemu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi wa DR Congo *Gilbert  Kabanda Kurhenga* amesisitiza kuendeleza mahusiano mazuri kati ya Taifa lake na Tanzania huku akiwa na imani kuwa kupitia makubaliano hayo ya kuboresha sekta ya ulinzi itasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

” Leo ni siku ya furaha kukutana katika mkutano huu wa kusaini hati ya makubaliano ya kuimarisha sekta ya ulinzi kwa mataifa yetu ambayo yamekua kama ndugu kufuatia ushirikiano wetu wa muda mrefu, hivyo naimani tutaendeleza uhusiano wetu na tutaboresha sekta ya ulinzi pamoja na mambo mengine muhimu kwa mataifa yetu ” amesema Kurhenga

CHANZO: FULL SHANGWE BLOG

Wednesday, September 14, 2022

UHABA WA MAJI BUSWELU, NYAKATO NA KISESA MAKAMU WA RAIS ATOA AGIZO KWA WAZIRI AWESO KUKAMILISHA MRADI WA MAJI KABLA YA KRISMASI LA SIVYO...

 

NA ALBERT G. SENGO / MWANZA

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ameiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha mradi wa maji Butimba unakamilika Desemba mwaka huu. Dk Mpango ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 14, 2022 wakati akiweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa chanzo na kituo cha tiba ya maji Butimba kilichopo jijini Mwanza.
Makamu wa Rais amesisitiza kwa kusema kuwa suala hilo siyo utani na endapo ataona mradi huo unasuasua atakuja kula Krisimasi hapa jijini Mwanza.

Mahitaji ya maji kwa sasa kwa jiji la Mwanza ni lita milioni 160 lakini uwezo wa kuzalisha maji wa chanzo cha maji Capripoint ni lita 98 tu, hivyo baada ya mradi huu kukamilika ifikapo mwezi Disemba 2022 (kama ahadi ya kuharakisha) utaongeza lita milioni 48 na kuwa suluhu ya uhakika ya tatizo la upatikanaji wa maji hadi mwaka 2040.

MAKAMU WA RAIS KULA KRISIMASI JIJINI MWANZA ILI KUHAKIKI KUKAMILIKA KWA MRADI WA MAJI.

 

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango akiweka jiwe la msingi katika mradi wa chanzo na kituo cha kutibu maji cha Butimba jijini Mwanza.


Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ameiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha mradi wa maji Butimba unakamilika Desemba mwaka huu.

Dk Mpango ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 14, 2022 wakati akiweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa chanzo na kituo cha tiba ya maji Butimba kilichopo jijini Mwanza.mpango pic

Kwa mujibu wa Mkataba, mradi huo ulianza Januari 2021 na kutakiwa kukamilika Februari 2023, kutokana na changamoto ya maji jijini humo lakini Dk Mpango alimtaka Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kuhakikisha mradi huo unaisha Desema mwaka huu.

“Nawaagiza Waziri wa Maji (Jumaa Aweso) na timu yake, wakae na mkandarasi, wafanye kazi usiku na mchana, waongeze watu katika kutekeleza mradi huu,” amesema na kuongeza

“Narudia tena mbele ya wananchi hawa wa Mwanza, muongeze uzalishaji wa maji kwenye chanzo hiki ili kumaliza kabisa kero ya maji katika jiji la Mwanza,”

Amesema haiwezekani wananchi wa mkoa huo wawe wanalia kukosa maji ya uhakika wakati wamezungukwa na Ziwa Victoria.


“Muhakikishe wananchi hawa wa Mwanza wanapata zawadi ya Mama Samia Suluhu Hassan (Rais wa Tanzania) zawadi ya Chrismas maji ya uhakika,”

“Na nikiona mnasuasua nitaamua kuja kulia Chrismass hapa na mimi sifanyi utani, kwahiyo Waziri na team yako msinizingue maana mkinizingua mimi kabla sijaenda kwa mama mtakuwa mmeshapata habari yenu," amesema Dk Mpango

Amesema hatokubali kutoa ahadi ya uongo mbele ya wananchi huku akiwataka kuhakikisha wananchi waliopo karibu na mradi huo wanakuwa wakwanza kupata maji.

Dk Mpango pia ametaka wananchi kuonganishiwa maji ndani ya siku saba huku akionya ubambikizaji ankara za maji kwa wananchi.

Awali Waziri wa Maji, Juma Aweso aliahidi mradi huo utakamilika kama maelekezo ya Dk Mpango.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Anthony Sanga amesema mradi huo utakaozalisha lita milioni 48 za maji utagharimu zaidi ya Sh 69 bilioni na kunufaisha zaidi ya wakazi 450,000.



Tuesday, September 13, 2022

WAFUASI WA RUTO WAPATA AJALI WAKIELEKEA UWANJANI KUSHUHUDIA UAPISHO.

 

Wafuasi wa Rais Mteule William Ruto kutoka kijijini Sugoi wamepata mkosi walipokuwa wakielekea Kasarani kushuhudia mtoto wao akiapishwa.

Tukio Hilo lilitokea mapema leo kabla ya uapisho baada ya basi la shule walilokuwa wakitumia kuhusika katika jali eneo la Sachagwan barabara ya Eldoret- Nakuru. 

Taarifa zinaarifu kuwa abiria 31 walipata majeraha mabaya wakati wa kisa hicho. 

Na kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa basi hilo lilipoteza mwelekeo na ndipo likaingia kwenye mtaro na kubingirika mara kadhaa. 

Waliojeruhiwa walikimbizwa hospitali ya kaunti ya Molo kwa matibabu huku safari yao ya kushuhudia Ruto akiapishwa ikaishia hapo.

RIGATHI GACHAGUA AMPONDA UHURU KENYATTA KASARANI. "TUNARITHI NCHI ILIYODORORA"


Baada ya kula kiapo katika uga wa Kasarani, Naibu Rais Rigathi Gachagua alipanda jukwaani kutoa hotuba yake ya kuapishwa. 

Katika hotuba yake, Gachagua alichukua muda huo kumrushia makombora yasiyo ya moja kwa moja rais mstaafu Uhuru Kenyatta. 

Bila kumung'unya maneno, naibu rais alimshutumu Uhuru kwa kuzorotesha uchumi wa nchi, ambao serikali mpya itakuwa na kibarua kigumu kuujenga. "Ukweli wa mambo ni kwamba tumerithi uchumi duni ambao unakaribibia kufifia. 

Tuna kazi kubwa ya kuikomboa nchi hii na kuirejesha pale ambapo Kibaki aliiacha," alisema Gachagua.  "Tunarithi Uchumu Uliooza" Alisema serikali ya Kenya Kwanza itajitahidi kurudisha uchumi wa nchi katika mkondo alioacha marehemu rais Mwai Kibaki.

 "Ninataka kuwaambia Wakenya kwamba mko huru hatimaye. 

Hamfai kuzungumza na kila mmoja wenu kupitia Whatsapp kwa kuogopa kurekodiwa na kuteswa na mashirika ya serikali," aliongeza. Wakati uo huo, Gachagua alimkumbusha Rais William Ruto kwamba safari iliyo mbele yake si rahisi. 

Katika hotuba yake ya kwanza kama naibu wa rais, Gachagua alitoa wito kwa Wakenya kuombea utawala mpya huku ukijitahidi kurudisha uchumi katika mwelekeo wake. 

Gachagua alibainisha kwamba kwao kuwa mamlakani ni kazi ya Mungu na maombi kutoka kwa Wakenya. "Haikuwezekana sisi kushinda uchaguzi huu ni kwa mkono wa Mungu leo ​​mtoto kutoka familia maskini ameapishwa kuwa rais wa Kenya. 

WAZIRI CHANA AIPONGEZA TFS MBIO ZA MAGARI SAO HILL

 

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule akimkabidhi kombe bingwa wa Mashindano  Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania  The Royal Tour
Moja ya magari ambayo yalishiriki katika 
Mashindano  Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania  The Royal Tour
Moja ya magari ambayo yalishiriki katika Mashindano  Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania The Royal Tour
Hizi na zawadi ambao washindi wa Moja ya magari ambayo yalishiriki katika Mashindano  Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania  The Royal Tour walipewa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dk Pindi Chana amevutiwa na ubunifu na mawazo  mazuri yaliofanywa na Shamba la Serikali Sao hili kwa kuandaa Mashindano ya mbio za Magari katika msitu huo kwani ni fursa kubwa ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo kwenye Shamba hilo.


Balozi Dk Chana ameyasema Hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu katika Mashindano  Sao Hill Misitu auto Cross Tanzania the Royal Tour kwa kushirikiana Iringa Motorsports club Tanzania kwa ubunifu huo kwani unaumuhimu mkubwa katika masuala mazima ya kutangaza utalii.


" Haya nimaelekezo ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ambaye alituelekeza kuendelea kubuni vyanzo mbalimbali vya utalii kwani ndio chanzo kimoja wapi katika masuala mazima ya utalii wa aina hiyo wa mashindano ya mbio za mahari au Rally katika misitu yetu ambavyo tunaihifadhi mwenye maeneo yetu ." Alisema dk  Balozi Chana


Aidha alieleza Mkakati wa wizara ni kunatukio masuala ya michezo mbalimbali  ambayo utafanyika  katika maeneo ya hifadhi za Serikali ikiwemo msitu katika eneo la Sao hill.


" Ni jambo zuri na tuendelee kuratibu ili liweze kufanyika mara kwa mara  kadiri Kamati ya maandalizi tutakavyo amua I'll kupata washiriki wengi zaidi." Alisema Waziri huyo


Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Sao hill Lucas Sabida alisema wameandaa mashindano mafupi ya mbio za mahari lakini wanampango wa kuandaa mashindano makubwa zaidi.


Alisema lengo la mashindano Hayo ni kuendelea kujitangaza kama Shamba la TFS kwa ajili  kutangaza utalii wa ikolojia na nyuki kupitia utalii wa michezo wa mbio za Magari kutokana na mwitikio kuwa mkubwa kwao Wananchi.


Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa wilaya hiyo inamisitu Msingi ambapo wanaziadi ya hekta 100,000 ambayo inatumiwa kwa ajili ya uzalishaji wa mbao pamoja na bidhaa zingine kama Marine boad, Mirunda  na nguzo za umeme.


Alisema mazao Hayo wamekuwa wakiyatumia na kuwasaidia kwa uchumi na mapato kwa mustakabali wa jamii  lakini kupitia Program ambayo ilianzishwa na Rais wa Jamhuria ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  The Royal Tour.

Monday, September 12, 2022

MWANAMUME AREJEA NYUMBANI NA PANGA BAADA YA KUTOWEKA KWA MIAKA 53

Mwanamume mmoja amerejea nyumbani kwao katika kijiji cha Gachiongo katika Kaunti ya Tharaka Nithu baada ya kutoweka kwa zaidi ya miaka 50. 

Familia yake imejawa na furaha baada ya jamaa wao kurejea nyumbani wakisema kuwa alitoweka mwaka 1969. 

Kwa mujibu wa familia yake, Njeru Mwiru ambaye amerejea akiwa na umri wa miaka 70, alitoweka akuwa kijana. Mwiru amefichua kuwa kwa miaka 53 ambayo hajakuwa nyumbani kwao amekuwa akiishi katika Kaunti ya Kitui. 

Familia yake ilikuwa na furaha kubwa kumuona, ndugu zake wakisema kuwa hawakuwa wamechoka kumtafuta.

Mmoja wa ndugu zake wadogo alisema kuwa alikuwa amemtafuta eneo la Ukambani kufuatia ripoti kuwa Mwiru alikuwa anaishi eneo hilo. Katika muda wa miaka 53 ambao amekuwa ametoweka, Mwiru hakuoa wala kupata watoto. 

Familia yake inasema kuwa alirejea nyumbani akiwema amebeba nguo zake katika gunia na upanga ambao alinunua akiwa mafichoni. 

DAX FT CHI BROWN