ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 14, 2022

MAKAMU WA RAIS KULA KRISIMASI JIJINI MWANZA ILI KUHAKIKI KUKAMILIKA KWA MRADI WA MAJI.

 

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango akiweka jiwe la msingi katika mradi wa chanzo na kituo cha kutibu maji cha Butimba jijini Mwanza.


Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ameiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha mradi wa maji Butimba unakamilika Desemba mwaka huu.

Dk Mpango ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 14, 2022 wakati akiweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa chanzo na kituo cha tiba ya maji Butimba kilichopo jijini Mwanza.mpango pic

Kwa mujibu wa Mkataba, mradi huo ulianza Januari 2021 na kutakiwa kukamilika Februari 2023, kutokana na changamoto ya maji jijini humo lakini Dk Mpango alimtaka Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kuhakikisha mradi huo unaisha Desema mwaka huu.

“Nawaagiza Waziri wa Maji (Jumaa Aweso) na timu yake, wakae na mkandarasi, wafanye kazi usiku na mchana, waongeze watu katika kutekeleza mradi huu,” amesema na kuongeza

“Narudia tena mbele ya wananchi hawa wa Mwanza, muongeze uzalishaji wa maji kwenye chanzo hiki ili kumaliza kabisa kero ya maji katika jiji la Mwanza,”

Amesema haiwezekani wananchi wa mkoa huo wawe wanalia kukosa maji ya uhakika wakati wamezungukwa na Ziwa Victoria.


“Muhakikishe wananchi hawa wa Mwanza wanapata zawadi ya Mama Samia Suluhu Hassan (Rais wa Tanzania) zawadi ya Chrismas maji ya uhakika,”

“Na nikiona mnasuasua nitaamua kuja kulia Chrismass hapa na mimi sifanyi utani, kwahiyo Waziri na team yako msinizingue maana mkinizingua mimi kabla sijaenda kwa mama mtakuwa mmeshapata habari yenu," amesema Dk Mpango

Amesema hatokubali kutoa ahadi ya uongo mbele ya wananchi huku akiwataka kuhakikisha wananchi waliopo karibu na mradi huo wanakuwa wakwanza kupata maji.

Dk Mpango pia ametaka wananchi kuonganishiwa maji ndani ya siku saba huku akionya ubambikizaji ankara za maji kwa wananchi.

Awali Waziri wa Maji, Juma Aweso aliahidi mradi huo utakamilika kama maelekezo ya Dk Mpango.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Anthony Sanga amesema mradi huo utakaozalisha lita milioni 48 za maji utagharimu zaidi ya Sh 69 bilioni na kunufaisha zaidi ya wakazi 450,000.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.