Shirika la Afya Duniani WHO
limesema limesikitishwa na taarifa ya vifo vya watoto 15 katika kijiji
cha Nachodokopele Mashariki mwa Kapwete nchini Sudan Kusini,
vinavyohusiana na kampeni ya chanjo ya surua ya tarehe 10 hadi 14 Mei
kwenda mrama.
Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja
iliyotolewa Alhamisi na WHO, Shirika la Kuhudumia watoto UNICEF na
Wizara ya Afya ya Sudan Kusini ,baada ya uchunguzi wa kina wa vifo hivyo
imebainika kwamba kampeni hiyo ya chanjo ilihusika na vifo vya watoto
hao. Tariki Jasarevic msemaji wa WHO amebaini kuwa makosa ya kibinadamu
yamechangia vifo hivyo.
Mtoto akichanjwa. |
Amesema sababu kuu vifo hivyo ni
kutumiwa wahudumu wasio na ujuzi ambao hawakupata mafunzo ya jinsi ya
kutoa chanjo kwa viwango vinavyotakiwa na kutofuatiliwa na kusimamiwa
ipasavyo utoaji chanjo hiyo.
Ameongeza kuwa bomba moja la sindano
lilitumika kutoa chanjo kwa siku zote nne badala ya kutupwa baada ya
kutumika mara moja jambo ambalo ni kinyume na viwango vya afya na
usalama vya WHO, na kusababisha dawa ya chanjo kuchanganyika na vitu
visivyotakiwa na kuwadhuru watoto hao.