Na Abog: JEMBE FM
Mashabiki na viongozi wa klabu ya Simba leo wameungana na
wanafamilia wa aliyekuwa shabiki kindakindaki wa klabu hiyo Shose Fidelis
Masao, kuuaga mwili wake kwenye Ibada iliyofanyika majira ya Saba hadi saa Tisa
mchana, kwenye kanisa la Roman Catholic Magomeni jijini Dar es salaam.
Shose alifariki kwa ajali ya gari Mei 29, eneo la
Dumira mkoani Morogoro alipokuwa akitokea Dodoma kuishabikia klabu hiyo kwenye
mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho. Katika gari hilo alikuwa na kiungo na
nahodha wa Simba Jonas Mkude ambaye alinusurika pamoja na wengine wawili.
Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema klabu
itamuenzi shabiki huyo na watamkumbuka daima kwani msiba wake umewagusa
wanasimba wote pamoja na jamii ya wapenda soka wote Tanzania.
Marehemu Shose alizaliwa 1988, Ilala, Dar es salaam
na mwili wake utasafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Bwana ametoa
na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.