Kamanda mkuu wa jeshi la Somalia,
Jenerali Ahmed Mohamed Tredishe amesema mwanachama huyo wa al-Shabaab
anayejulikana kwa jina Bishar Mumin Afrah amejisalimisha kwa jeshi hilo
katika mji Buloburte eneo la Hiran, yapata kilomita 200 kaskazini mwa
Mogadishu, mji mkuu wa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Inaarifiwa kuwa, kamanda huyo mwandamizi
wa genge la kigaidi la al-Shabaab amejisalimisha kwa vyombo vya usalama
sambamba na kukabidhi bunduki mbili aina ya AK47 na shehena ya risasi.
Hivi karibuni Rais wa Somalia, Mohamed
Abdullahi Farmajo alitoa msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo wa al-Shabaab
ambao wataweka silaha chini na kujisalimisha kwa serikali.
Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia. |
Mapema mwezi uliopita wa Mei, Wizara ya
Habari ya Somalia ilisema kuwa, Moalim Osman Abdi Badil, kamanda wa
ngazi za juu wa al-Shabaab pamoja na wanamgambo wengine watatu wa genge
hilo waliuawa katika mapigano na jeshi la Somalia kwenye eneo
la Shabelle ya Chini.
Katika hatua nyingine, walimu wawili wa
Kenya wameripotiwa kutekwa nyara na wanamgambo wa al-Shabaab katika mji
wa Fafi kaunti ya Garissa usiku wa kumkia leo baada ya magaidi hao
kuteketeza moto shule moja katika eneo hilo la kaskazini mashariki.
Kadhalika magaidi hao wameng'oa na kuiba mlingoti wa mawasiliano ya simu
ya mkononi (rununu) katika eneo hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.