Kwa mujibu wa ripoti
iliyochapishwa leo na wizara hiyo kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya
Kuwalinda Watoto ambayo huadhimishwa Juni Mosi kila mwaka kote duniani,
mbali na watoto elfu tatu kuuawa, wengine zaidi ya 13 elfu wamejeruhiwa
na wanajeshi hao.
Ripoti hiyo imebainisha kuwa, watoto
wasiopungua 72 wameuliwa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel
tangu mwezi Oktoba 2015, wakati ilipoanza Intifadha ya Tatu ya Quds.
Wizara ya Habari ya Palestina imefichua
kuwa, mtoto mdogo zaidi aliyeuliwa shahidi na wanajeshi wa Israel
ni Ramadan Mohammad Faisal Thawabta, aliyekuwa na miezi minane tu,
ambaye alifariki dunia Oktoba 30, 2015 baada ya kuvuta gesi ya kutoa
machozi iliyofyatuliwa na wanajeshi Wazayuni katika maandamano
yaliyofanyika mjini Beitul Fajjar, kusini mwa Beitul Lahm.
Watoto wa Kipalestina katika jela za Israel.
Watoto wa Kipalestina katika jela za Israel.
Kadhalika ripoti hiyo ya Wizara ya
Habari ya Palestina imebainisha kuwa, watoto zaidi ya 12 elfu wa
Kipalestina wametekwa nyara na askari wa Israel na kuzuiliwa chini ya
mazingira magumu, katika kipindi cha miaka 17 iliyopita.
Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za
wafungwa wa Palestina la Addameer, wanajeshi katili wa Israel
wamewahukumu vifungo jela watoto 300 wa Kipalestina tangu mwezi Aprili
mwaka huu hadi sasa, vikiwemo vifungo vya hadi miaka 20 jela.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.