Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura
amesema kuwa marehemu Mzee Francis Kanyasu hakuwa mbunifu wa nembo ya
taifa kama watu wanavyodhania bali alikuwa mchoraji.
Wambura amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa
viti maalumu (Chadema), Devotha Minja alilouliza juu ya serikali
kushindwa kumthamini pamoja na kumuhujumu Mzee Ngosha aliyechora nembo ya
taifa na hatimaye kufa masikini.
"Si kweli kwamba Mzee Ngosha serikali imemuhujumu, kimsingi Mhe.
Spika yapo majina mezani kama matatu hivi yanayohusiana na ubunifu wa
nembo ambayo tunaitumia, nembo ya taifa. Kwa hiyo mpaka sasa bado
haijajulikana nani hasa ambaye ni mbunifu wa nembo hii kwa sababu mfano
yupo marehemu ambaye alishatangulia mbele za haki muda mrefu ambaye
anaitwa Abdallah Farhani wa Zanzibar yeye vielelezo tayari vishakutwa
katika kumbukumbu zake jinsi alivyokuwa akibuni nembo yetu ya taifa,
nembo ya Kenya pamoja na hata nembo ya OAU kipindi hicho alipokuwa
anasoma Makerere University. Kwa hiyo yapo majina ambayo yanadaiwa
kwamba yalishiriki katika kutengeneza nembo hii" alisema Wambura.
Pamoja na hayo Naibu Waziri amewaomba wataalamu kufuatilia kiundani kabisa juu ya suala hili ili waweze kutambua ukweli wake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.