Friday, May 30, 2025
SAMIA: TUSIGWAJIMANISED CHAMA CHETU, MAGWAJIMA TUYAACHE NJE.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wajumbe wa chama hicho kuhakikisha mchujo wa wagombea unafanyika kwa haki na weledi ili kulinda hadhi ya chama, akisisitiza kuwa ni muhimu kuepuka kuwapitisha watu wasiostahili.
Akihitimisha Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa leo Ijumaa, Mei 30, 2025, jijini Dodoma, Samia amesema chama kisiruhusu kuathiriwa na tabia za baadhi ya watu waliopoteza mwelekeo wa kisiasa.
“Tukitoa mwanya ndugu zangu, tukapitisha wanaotafuta tu, na mie niwemo, ndiyo tunapata wale wanaokwenda huko - chama kinakuwa Gwajimanised,” amesema Rais Samia na kuongeza, “Kwa vyovyote vile tusigwajimanised chama chetu, Magwajima tuyaache nje,”
Amesisitiza umuhimu wa kuwapima wagombea kwa sifa, maadili na uwezo wao, siyo kwa mapenzi binafsi, hofu au mahusiano ya karibu. Aidha, ameonya kuwa mtu ambaye hana uhusiano wa kweli na chama hawezi kusaidia, bali atakivuruga.
“Mcheza ngoma si yake lazima ataharibu... Ukicheza ngoma si yako utaharibu na utajulikana tu,” amesema kwa mafumbo ya kinadharia yaliyolenga kuhimiza uaminifu na ushirikiano wa kweli ndani ya chama.
KUHUSU KATIBA MPYA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kuhuisha na kukamilisha mchakato wa Katiba mpya kabla ya mwaka 2030, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2025–2030.
Akizungumza jijini Dodoma leo katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, Mwenyekiti wa Kamati ya Ilani ya CCM, Profesa Kitila Mkumbo amesema hatua hiyo inalenga kudumisha demokrasia, utawala bora na mshikamano wa kitaifa.
Amesema CCM inaamini kuwa misingi ya utawala wa sheria, haki za binadamu na demokrasia ni msingi muhimu kwa maendeleo endelevu ya Taifa, na kwamba chama hicho kitaielekeza serikali kuweka mfumo wa kisheria wa kutekeleza falsafa ya uongozi ya 4R.
Wednesday, May 28, 2025
NIC YATIKISA MIRADI MIKUBWA NCHINI TANZANIA SASA YABISHA HODI MV MWANZA
NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Kutoka kwenye SGR inayopita kwa kasi, kuelekea kukamilika hadi kwenye daraja la JPM linalounganisha Kigongo na Busisi... na kutoka kwenye nguvu ya maji ya Bwawa la Nyerere hadi kwenye mawimbi ya Ziwa Victoria – NIC haichezi mbali! Sasa, Mfuko wa Bima wa Taifa (NIC) watingisha tena – safari hii wakitua kwa kishindo kwenye meli ya kisasa MV Mwanza! Hiki ni kielelezo cha namna NIC inavyobadilisha si tu taswira ya bima nchini, bali pia maendeleo ya taifa. Hebu tusikie, hatua kwa hatua, jinsi walivyofanikisha yote haya!.Tuesday, May 27, 2025
'UDHAMINI WENYE TIJA! PAMBA JIJI FC YAVUNA FAIDA KUTOKA NIC'
NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
"Ushirikiano kati ya NIC Insurance na Pamba Jiji FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, haukuwa tu juu ya udhamini wa jina au kuonekana kwa chapa yetu. Licha ya kupata nafasi kubwa ya kuonekana (visibility) na kueneza brand ya NIC kwa wapenzi wa soka, pia tumeshuhudia matokeo ya moja kwa moja ya kiuchumi. Kupitia uwekezaji wetu kwa timu ya Pamba, tumeweza kuzalisha faida inayokaribia mara tatu ya kile tulichowekeza — hii ni zaidi ya asilimia 300 ya mapato dhidi ya gharama" "Ushirikiano huu unaonyesha jinsi michezo inaweza kuwa jukwaa dhabiti la kibiashara na kijamii." Kauli ya Karim Mesharck Mkurugenzi wa Masoko na mawasiliano NIC InsuranceAZIZ KI KAZINI LEO OFISI MPYA WYDAD IKIMENYANA NA SEVILLA YA HISPANIA
NYOTA mpya wa Wydad Athletic, Stephane Aziz Ki aliyesajiliwa kutoka Yanga ya Tanzania mwishoni mwa wiki leo anawea kuwa sehemu kikosi cha timu yake mpya kitakachomenyana na Sevilla FC ya Hispania katika mechi ya kirafiki leo kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Mohammed V mjini Casablanca.Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Wydad kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA 2025 inayotarajiwa kufanyika nchini Marekani kuanzia Juni 15 hadi Julai 13.
Taarifa zaidi zinasema kwamba pamoja na mechi dhidi ya Sevilla ambao waliwasili jana Casablanca – Wydad pia watacheza na FC Porto ya Ureno Jumapili kukamilisha mbili za kirafiki kabla ya Klabu Bingwa ya Dunia.
Wydad imeachana na aliyekuwa Kocha wake, Rhulani Mokwena wa Afrika Kusini baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Morocco maarufu kama Botola Pro ikiwa na pointi 54, nyuma ya FAR Rabat iliyomaliza pointi 57 na mabingwa RSB Berkane waliomaliza na pointi 70 baada ya mechi 30 za msimu.
Wydad Athletic ambao sasa wapo chini ya Kocha wa nyumbani, Mohamed Amine Benhachem wamepangwa Kundi G katika Klabu Bingwa ya Dunia pamoja na Manchester City, wababe wa Italia Juventus, na Al Ain ya Falme za Kiarabu (UAE).
Mbali na Aziz Ki Wydad imeimarisha kikosi chake kuwa kuwasajili winga mkongwe, Nourredine Amrabat kutoka Hull City ya England na mshambuliaji Hamza Hanouri kutoka FUS Rabat.
MBOGGO ACHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA TANGA KUPITIA ACT- WAZALENDO HUKU AKIHAIDI KUIREJESHA TANGA YA VIWANDA
Katibu wa Chama cha ACT -Wazalendo Wa Jimbo la Tanga Mohamed Salim Ponda (kushoto) akimkabidhi fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge Jimbo la Tanga mwanachama wao John Charles Mboggo (katikati) kulia ni Mwenyekiti wa Wazee Jimbo la Tanga (ACT Wazalendo) Zaharan Mohamed
Na Oscar Assenga, Tanga.
KADA wa Chama Cha ACT –Wazalendo Mkoani Tanga John Charles Mboggo amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania Ubunge katika Jimbo la Tanga kupitia chama hicho huku akihaidi kuirejesha Tanga ya Viwanda ambayo ni ndoto kubwa ya wananchi wa mkoa huo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo alisema lenbgo la kuchukua fomu ya kuwania Ubunge ni kutaka kuhakikisha anatoa mchango wake katika kurejesha viwanda vya Tanga ambavyo wananchi wamekuwa na kiu navyo.
Alisema kwamba kwa sababu viwanda ni ajira na nguvu kazi ya Tanga wanaongelea kuna vijana asilimia 68 ya vijana wakitumika kwenye viwanda watakuwa na uchumi kwenye Jimbo hilo na Mkoa kwa Ujumla.
“Tanga tunaamini sisi ni watu tunaamini watu wa kuleta maendeleo na ndio maana tunawahamasisha wananchi wenye sifa za kupiga kura kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi la kura kwa lengo la kuwachaguoa viongozi watakaowaongoza”Alisema
Awali akizungumza Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Jimbo la Tanga Anasi Mohamed Rweymamu alisema kwamba wanaendelea kuwakaribisha wagombe na kura zao wa maoni ndani ya chama ndizo zitakazoamua nani anaweza kupeperusha tiketi ya chama hicho kwenye nafasi ya Ubunge.
Alisema kwamba ACT Wazalendo ndio chama pekee ambacho kinaweza kupeperusha vyema B
Naye kwa upande Katibu wa ACT WaaJimbo la Tanga Mohamed Salim Ponda alisema kwamba wapo kwenye maandalizi ya uchaguzi kama chama hicho Taifa kilipotangaza kwamba zoezi la kuchukua fomu kutoka Aprili 18 mwaka huu mpaka 31 mwezi Mei katika nafasi za Ubunge na Udiwani.
Alisema kwamba katika uchaguzi huo wamejipanga kwamba wagombea watakao wapitisha katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo hilo watakuwa imara kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera hiyo.
KOKA KUCHELE AFUNGUKA MAZITO ALIVYOPAMBANA KUSAIDIA KUBORESHA NS KUINUA SEKTA YA ELIMU JIMBONI
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA