IDARA ya Uhamiaji
Mkoani Mwanza imeendelea kuwanasa Wahamiaji haramu wanaoingia nchini kwa njia
za panya baada ya hivi karibuni kuwakamata vijana watatu raia wa Burundi.
Akizungumza ofisini
kwake leo Naibu Kamishina Msaidizi na Kaimu Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Mwanza Bi. Anamaria Yondani alisema kwamba hii inatokana na Idara hiyo
kuendelea kupokea taarifa kutoka kwa wananchi na kuzifanyia kazi, huku pia
uhamiaji ikiendelea kutekeleza mradi wa Shirika la Kimataifa ambalo linahusika
na shughuli za Kiuhamiaji (OIM) kupitia mradi wa Capacity Buiding in Migration
Management (CBMM-II)
Bi Yondani aliwataja
vijana hao waliokamatwa kuwa ni Akizmana Adamu (15), Gerlad Michael (17) na Boaz
Ernest (15) wote wakazi wa Ruingi raia
wa nchi yaBurundi walioingia nchini kwa njia za Panya kupitia Mkoani Kigoma
kabla ya kunaswa Mkoani Mwanza wakiwa kwenye harakati za kutafuta kazi ili
kuwasaidia kuishi nchini kinyume cha taratibu na sheria za nchi.
Kaimu Mkuu huyo wa
Uhamiaji Mkoa alisema tatizo la
wahamiaji haramu limekuwa ni Janga la Kitaifa na Mkoa wa Mwanza ni Kitovu cha
Mawasiliano, Biashara ,Elimu na Usafiri kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nchi za
Maziwa Makuu na wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akitoa taarifa ya
Mkutano wa Kamati ya National
Immigration Inter-regional Steering Committee (NIISC) uliofanyika Mjini
Sumbawanga Mkoani Rukwa Machi 11 hadi 12 mwaka kwa lengo la kuendeleza mradi wa
CBMM-II, kuongeza Mikoa wanachama wa NIISC na Namna ya kushirikiana na IOM
katika kuendeleza mradi wa huo ambayo yalijadiliwa katika mkutano huo.
“Mradi huu wa NIISC awali ulianzisha na Mikoa ya
Mwanza, Mara, Kagera na Kigoma mwaka 2012 na kasha kuongeza Mkoa wa Rukwaa hii
ikumbukwe ipo katika Kanda ya Ziwa ambapo kuna vivutio kadhaa vinavyosababisha wahamiaji haramu
kuingia na kujipenyeza katika sekta za i Uvuvi, Kilimo, Ufugaji, Madini,
Biashara, Elimu na Usafiri hali ambayo
Uhamiaji imekuwa ikizifanyia
doriawavutia ”alisema
Aidha katika mkutano huo uliweza kuongeza wanachama wapya katika
Kamati ya NIISC ambayo ni Mikoa ya Geita, Shinyanga ,Tabora na Katavi ili
kuongeza ushirikiano katika kubadilishana taarifa na uzoefu wa utekelezaji wa
majukumu ndaji ya kila siku katika kupambana na wimbi kubwa la wahamiaji
haramu.
“Tunatambua wahamiaji haramu bado wanaendelea
kupitia nchini mwetu kwa ajili ya
kuelekea nchini Afrika ya Kusini ambapo
awali walikuwa wakipita Mpaka wa Sirali kutokea nchi ya Kenya kuingia Wilaya ya
Tarime,Musoma kisha Mkoani Mwanza na kuelekea Mikoa ya Kati hadi Mkoani Mbeya
kabula ya kuanza safari kuelekea nchi za kusini hadi Afrika Kusini ili kuwa
lahisishia kwenda nchi za Ulaya”alisema.
Bi Yondani alisema kwamba baada ya kutekelezwa kwa
mradi wa CBMM-II wahamiaji haramu
waliamua kubadili njia pengine kupita mawakala ambao ni raia wa Tanzani
wanaowasaidia kuwaingiza kwa njia haramu na sasa kupitia Mikoa ya Kaskazini ya
Kilimanjaro,Arusha,Manyara na Tanga na kuelekea mikoa ya Kati kwa ajili nya
kuelekea Mkoani Mbeya na kuvuka kuelekea Malawi na Zambia.
“Lengo kuu la wahamiaji haramu ni kwenda Afrika
Kusini ni kutafuta maisha bora na kuwa njia lahisi ya kwenda Mataifa ya Bara la
Ulaya na Marekani huku wahamiaji wengi wanaoingia kinyume na utaratibu wa
kisheria wengi ni kutoka nchi za Ethiopia,Eritrea na Somaliaambao wamekuwa
wakinyanyaswa, kuteswa na kufariki wanapokuwa safarini kwenye maroli ya mizigo
na watu wanaowasaidia”alisema
“Wanatumia njia za panya kusafiri kupita mipaka
isiyo rasimi na husaidiwa na
mawakala (Maajenti) wao ambao wengine ni
watanzania wasio na uzalendo na wamekuwa wakiwapakiza katika maroli ya
mizigo,magari ya makontena na hata
wengine kupitishwa kwenye Hifadhi za wanyama wakali na baadhi yao kupitia Ziwa
Victoria kwa mitumbwi na kuvuka mito yenye wanyama wakali wakati wa
usiku”alieleza
Bi.Yondani ametoa wito kwa wananchi kurejesha
uzalendo wa Taifa na kushirikiana na maafisa uhamiaji na polisi kutoa taarifa
kwa watu ambao wanawahisi kuwa siyo raia na watu ambao wameingia kwa njia za
panya katika maeneo mbalimbali ya Mikoa yao na wanaotafuta kujipenyeza kufanya
kazi ambazo zitawasaidia kuonekana kuwa ni raia wakati huu taifa linaelekea
kutoa vitambulisho vya uraia .
“Wananchi sasa warudishe uzalendo wao na kuacha
kuwasaidia wageni na wahamiaji haramu walioingia nchini kinyume cha taratibu na
kuvunja sheria za nchi kwa kuwatolea taarifa kwa ofisi za uhamiaji na vituo vya
jeshi la polisi kwa lengo la kupambana na janga hili la kitaifa la kupambanana
wahamiaji haramu wanaoingia nchini kila siku kwa kusaidiwa na mawakala na
kuhifadhiwa na watu wasiokuwa na uzalendo”alisisitiza
Amevipongeza vyombo vya habari kwa kushirikiana na
Idara hiyo kutoa taarifa kwa wananchi ikiwemo Elimu kwa kueleza bayana athari
za kuwa na wahamiaji haramu ambao wengi wao wamekuwa wakifanya uhalifu na
kuwapora mali na kufanya mauaji kwa wananchi na sasa wananchi katika maeneo yao
ya mitaa na kata kuwa kuwatolea watu ambao si raia ili kuwabaini kabla ya
kutolewa vitambulisho vya uraia kitaifa.