Lile pambanolililokuwa linasubiriwana mashabiki wengi wa ngumi
katika jiji la Accra nchini Ghana kati ya bondia kijana anayechipukia Frederick
Lawson na mkongwe Isaac Sowah limemalizika muda wa sekunde ya 43 katika raundi
ya tatu baada ya referii Shedrack Aquaye kuingilia kati kumwokoa Isaac Sowah
asiendelee kupokea mkong’oto kutoka kwa kijana Frederick Lawson.
Wawili hao walikutana kwenye uwanja wa mpira wa Accra katika
mpambano ambalo ulirushwa live na Super Sport pamoja na mitandao ya televisheni
nyingi duniani. Mpambano mkubwa usiku wa leo ulimshughudia mbabe Joseph Agbeko
wa Ghana akimshinda kwa taabu na kuchukua ubingwa wa dunia dhidi ya bondia
kutoka nchini Columbia Luis Melendez.
Kwa sasa bondia Frederick Lawson anangojea mapambano mengine ya
kuinua kipaji chake na anga ndiyyo tu itakuwa kilele chake katika juhudi zake
za kuchanja mbuga kwenye ngumi!
Pambano la wawili hao lilisimamiwa na Rais wa IBF katika bara la
Africa, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi ambaye
yuko katika jiji la Accra akitokea Windhoek, Namibia!
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.