ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 23, 2013

MAANDAMANO YA KUMTAKA WAZIRI WA ELIMU AJIUZURU JESHI LA POLISI MWANZA LAIPIGA STOP CHADEMA.

Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limepiga marufuku maandamano ya CHADEMA yaliyopangwa kufanyika siku ya jumatatu kumshinikiza Waziri wa Elimu ajiuzuru kufuatia matokeo mabaya ya kidato cha nne kwa mwaka 2012.

Akitoa taarifa leo asubuhi katika ofisi za jeshi hilo mkoani Mwanza Kamanda wa polisi mkoa Ernest Mangu amesema kuwa jeshi lake limeyazuia maandamano hayo kwa sababu za kimsingi za usalama. (Bofya play kumsikiliza)

Akizitaja sababu hizo kamanda Mangu amesema kuwa suala la matokeo ya kidato cha nne kuwa mabaya serikali tayari imeliundia tume ambayo bado inaendelea kukusanya maoni kwa wananchi hivyo haoni sababu za CHADEMA kufanya maandamano na kuwataka viongozi wake kuwasilisha hoja zao wanazodai kuwa za msingi kwenye tume husika na si kufanya maandamano yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. 

Kwa mkoa wa Mwanza CHADEMA ilitoa taarifa za kufanya maandamano katika wilaya za Sengerema, Misungwi na Magu.

Mangu ameongeza kuwa jumatatu ni moja kati ya siku za kazi na shughuli mbalimbali za biashara hivyo kufanya maandamano kwenye viunga mahali kokote ni chanzo cha kuzuia shughuli za uzalishaji na biashara kufanyika kwa ufanisi kwani wadau watafunga shughuli zao wakihofia uporaji na usalama wa mali zao.

Tayari jeshi la polisi Mwanza limepokea taarifa ya makundi mbalimbali kuibuka na kudai kuyapinga maandamano hayo wakiwemo wafanyabiashara walioko katikati ya jiji wakisema kuwa yatasababisha huduma zao kusimama.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. hawa chadema sasa huko siko mnakoelekea,
    kwa style hii mie binafsi sikupi kura yangu
    kuiongoza nchi. mshiiindweeee.
    waziri ajiuzuru yeye ndie aliewatuma madent
    kujaza utumbo kwenye final pepa? yeye ndie aliwaambia wamchore messy? mbona mnakurupuka na maamuzi yenu?
    hii inaonesha wazi mmeishiwaaaa,,,kakaeni mjipange upya na jipya zaidi sio kukurupuka.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.