ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 24, 2013

AMSHA AMSHA NA PASAKA YASHIKA KASI NDANI YA METRO FM

Mkurugenzi wa COSU Entertainment Fabian Fanuel akifafanua jambo ndani ya kipindi cha muziki wa injili radio Metro Fm  kuhusu Kusanyiko la Muziki wa Injili lijulikanalo kama Pasaka Gospel Festival linalotarajiwa kufanyika tarehe 31 siku ya pasaka ya 2013 CCM kirumba jiijini humo. 

Mtangazaji wa Metro Fm kipindi cha Gospel Songs Delphina Kiharusi akiendesha mpango mzima asubuhi ya leo, ndiye alikuwa mwenyeji wetu  aliyefanya mahijiano nasi kuhusu Kusanyiko la Muziki wa Injili lijulikanalo kama Pasaka Gospel Festival linalotarajiwa kufanyika tarehe 31 siku ya pasaka ya mwaka 2013 CCM kirumba jiijini  Mwanza. 

Meneja Uendeshaji wa COSU Entertainment Albert G. Sengo amewaalika wananchi wote wa jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha lililoandaliwa kwa ufundi likichagizwa na ubora wa waimbaji, pia wategemee kuzunguka ndani ya bwana kupitia wema wake na mwimbaji Enock Jonas, wakijipa raha ndani ya Yesu kupitia mwimbaji mahiri Afrika Mashariki na kati Neema Mwaipopo 

Waimbaji wengine ni Nesta Sanga (JIANDAENI), Danni Safari, John Shahban, Jeska Julius, Isaya Msangi (SHETANI IMEKULA KWAKO), Danny Sanga kutoka Iringa, Tumaini Mbembela  kutoka Mbeya na mkoa wa Arusha utawakilishwa na Neema Munisi.

Kwaya za mkoa wa Mwanza ni nyingi za kutosha Anglican Vijana kwaya, EAGT City Centre kiufupi kwa zote zitaweka kambi kwenye shughuli yetu ya Uzinduzi Pasaka hii.

Jumatatu ya pasaka tutakuwa Geita uwanja wa CCM Katoro
Kiingilio kwa maeneo yote kitakuwa ni shilingi. 2000/= tu
Hivyo tunawakaribisha wote kwenye uzinduzi huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.