ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 14, 2023

MAGOLI YOTE | Singida Big Stars 1-2 Mlandege FC | Fainali Mapinduzi Cup 2023 - 13/01/2023

Tazama magoli yote matatu yaliyofungwa kwenye fainali ya #MapinduziCup2023 katika dimba la Amaan Zanzibar Mlandege ni mabingwa kwa ushindi wa mabao 1-2 Wafungaji ni Bashima Saite, Abdulnassir Mohamed kwa upande wa Mlandege na Francy Kazadi kwa upande wa Singida Big Stars

Friday, January 13, 2023

KILIVYONOGA KIJORA CHA SEGA 'LAZIMA UDATE'

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Asubuhi ya Ijumaa ya leo Tarehe 13 January 2023 kipindi cha Sega la Leo kutoka hapa Jembe Fm kimeruka live kikiwa na vihusishi vyake, askwambie mtu humo ndani ilikuwa full burudani #kijorachasega2023 live na Mashabiki wa 93.7 JEMBE FM katika viwanja vya Sega . . Powered by @the_cask_bar_grill @fredycatering @fay_printing @mtn_cakes_mwanza @cecytotoshop @mamanyimbodeco MUA 💄@johainakimaromakeup . . #JembeFm2023Kimewaka

Thursday, January 12, 2023

WA NEC WA MKOA WA MWANZA WATIA NENO MIKUTANO YA HADHARA, MAPOKEZI YAO YASIMAMISHA JIJI.

 NA ALBERT G SENGO/MWANZA

Wajumbe wa halmashauri shauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa kutoka Mkoa wa Mwanza Mh.Dkt Angelina Mabuba na Hellen Bogohe wamesema kuwa wapo tayari kwa mikutano ya hadhara ambayo imeridhiwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hivi karibuni. Wajumbe hao wametoa kauli hiyo wakati wa mapokezi yao Mkoani Mwanza ambapo wakisema kuwa wapo tayari kuzinadi kazi nzuri zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na Rais wa awamu ya sita Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ilichukuwa dakika kadhaa Jiji la Mwanza kusimama kutokana na Wajumbe hao kupata mapokezi ya kishindo yaliyo ambatana na maandamano ya msafara wa magari na watembeao kwa miguu kuanzia viwanja vya Furahisha hadi makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi yaliyopo katikati ya jiji hilo.

MWANZA SASA KAMA ZANZIBAR KULIMA ZAO HILI LENYE 'MKWANJA MREFU' VIJANA WAITWA KUCHANGAMKIA FURSA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

UNAAMBIWA SASA MWANZA KUWA KAMA ZANZIBAR - KIVIPI? Karibu kwenye mafunzo ya zao lenye kuzalisha mkwanja mrefu duniani, Kipato Chap Chap! Soko lipo! Wanunuzi wapo!! Ni zao la Vanilla, ambalo tayari wenzetu visiwani Zanzibar wameanza kulima na kunufaika nalo, sasa limejaribiwa kwenye ardhi ya mkoa wa Mwanza na limekubali kupita maelezo. VANILLA kiungo muhimu na ghali duniani, kinachotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile Chocolate, Kutia nakshi ya ladha kwenye keki na vyakula mbalimbali na hata hutumika kutengeneza marashi na perfume mbalimbali ulimwenguni. Kwa sasa soko la Vanilla lipo hapa nchini, nalo soko kuu likiwa nchi za Falme za kiarabu. VUTA PICHA Tofauti na mazao mengine na vile unavyodhani hauhitaji kuwa na shamba kubwa ili upate faida, Vanilla haihitaji palizi na haina gharama kubwa kuihudumia, Mkulima ukivuna tutanunua kutoka kwako KILO MOJA YA VANILLA KWA SHILINGI MILIONI MOJA. Ewe kijna uliyesaka ajira kwa kipindi kirefu au umefanya ujasiliamali wa kila aina na haukutoboa, unangoja nini? Karibu kwenye semina ya BURE bila malipo yoyote, upate mafunzo jinsi ya kulima zao hilo na pia tukutambulishe kwa wadau wa soko la Vanilla hapa nchini. Ni Jumamosi hii ya Tarehe 14/ 01/2023 Katika ukumbi wa GOLD CREST HOTEL jijini Mwanza Muda ni kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa alasili.
WATU WOTE MNAKARIBISHWA.

Licha ya kuhamasisha wakulima mkoani Mwanza na kote nchini kuchangamkia fursa hiyo kampuni ya Vanilla International, itatoa elimu bure kwa wale watao kuwa tayari kujikita katika zao hilo huku wakiwahakikishia upatikanaji wa soko kwa asilimia 99.9.

“Zao la Vanilla ni zao la fedha nyingi na kilo moja imeweza kufika mpaka zaidi ya milioni moja niwaombe sana wakulima kuwasiliana na sisi ili tuweze kuwasaidia katika kilimo”alisema Simon Mukondya mkurugenzi wa Vanilla International Ltd

Vanilla huchukua muda wa miezi mitatu tu tangu kupandwa hadi mavuno na gharama yake kila kilo moja inatajwa kufikia sh.laki 9 hadi mil.1 kwa sasa.

Zao la Vanilla lililoanza kulimwa kwa sasa mkoani Njombe kutokana na kuendelea kuhamasishwa ili kulima kilimo hicho kutoka na thamani yake.
Mmea wa zao la Vanilla.
Mmea wa zao la Vanilla.
Simon Mukondya mkurugenzi wa Vanilla International Ltd wakati akifafanua faida na matumizi ya zao hilo huku akiwasihi vijana walio kwenye ajira, wanaosaka ajira na wakulima wanaopenda kujihusisha na kilimo hicho kuweza kufika kwenye Semina hiyo kujizolea elimu bila malipo. 

Aidha kampuni hiyo imekuwa ikifanya shughuli zote za kilimo na kumkabidhi mkulima shamba likiwa tayari kwa kuendelea kulitunza.

Tuesday, January 10, 2023

WANAKIJIJI WAUWA FISI NANE WALIOUWA MTOTO.

 

NA ALBERT G. SENGO

Siku chache baada ya @jembefmTz kuripoti Habari ya mtoto Emmanuel Nyangela kufariki dunia baada ya kuliwa na fisi, wakazi wa kijiji cha Mwangika kata ya Mwabomba wilayani Kwimba mkoani Mwanza kwa kushirikiana na kundi maalum la kuuwa fisi wamefanikiwa kuwauwa fisi nane. Mtendaji wa Kijiji cha Mwangika, George Ernest amesema baada ya tukio hilo kutokea tarehe 27 mwezi wa 12 mwaka jana askari wa wanyapori walifika katika Kijiji hicho na kusaka fisi hao bila mafanikio hadi lilipofika kundi maalum la kuuwa fisi wakiwa wameambata na mbwa zaidi ya themanini ndipo wakafanikiwa kuwauwa fisi hao nane. "Na baada ya wao kushindwa kuuwa fisi sisi kama viongozi wa Kijiji tulikaa tukaweza kuwatafuta wawindaji wa kienyeji kutoka wilaya ya Misungwi wakaja watu kama 76 pamoja na mbwa wao wawindaji wa kienyeji ni watu ambao wanawinda kwa njia za asili kwa kutumia dawa za kienyeji na walitumia siku nne na wakauwa fisi wanane" amesema Mtendaji huyo wa kijiji cha Mwangika, George Ernest.
#DriveMix . . . . #2023Kimewaka

KABLA MJINI HAPAJAPOA HARMONIZE AFYATUA NYINGINE KALI.

 Harmonize Ft. Alice Kella - Best Friend (Official Music Video)

Harmonize - Made For Us Album

Stream/Download: https://smartklix.com/MadeForUsbyHarm... Subscribe for more official content from Harmonize: https://www.youtube.com/c/Harmonize255/ Follow Harmonize Instagram: https://www.instagram.com/harmonize_tz/ Twitter: https://twitter.com/harmonize_tz Facebook: https://web.facebook.com/Harmonize255 TikTok: https://vm.tiktok.com/JYFv7PN/ Listen to Harmonize YouTube: https://www.youtube.com/c/Harmonize255/ Audiomack: https://audiomack.com/harmonize Apple Music : https://music.apple.com/tz/artist/har... Spotify : https://open.spotify.com/artist/1eCae... Boomplay: https://www.boomplaymusic.com/share/a... The official YouTube channel of Harmonize. Subscribe for the latest music videos, performances, and more. For Bookings & More Email: Harmonizemanagement@gmail.com Call: +255 652 892 317, +255 658 135 762 #Harmonize #BestFriend #MadeForUsAlbum

UJAZWAJI MAJI BWAWA LA JULIUS NYERERE WAFIKIA MITA 108


 Ujazo wa maji katika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) linalotarajiwa kujaa ndani ya miezi 18 hadi jana ulifika mita 108.31 kutoka usawa wa bahari.


Ujazaji maji katika bwawa hilo linalotarajiwa kuzalisha megawati 2,115 za umeme likiwa na uwezo wa kuhifadhi lita bilioni 32 ulianza Desemba 22 mwaka jana.


Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Wadau wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Elihuruma Ngowi alisema bwawa linaendelea kujaa kwa kasi kwa sababu yamejikusanya kwenye eneo dogo.


“Muda wa kujaa bado ni uleule yaani misimu miwili ya mvua. Mita zinaonekana ziko juu kwa sababu maji yamejaa sehemu moja, lakini yakianza kusambaa maeneo mengi, zitakuwa zinakwenda taratibu,” alisema Ngowi.


Wakati maji ya masika ya mwaka na mwakani yakiendelea kujaa, alisema shughuli nyingine za ujenzi zinaendelea.


“Ujenzi hautosimama, mwenendo wa bwawa kujaa maji ni mzuri,” alisema Ngowi.


Siku ya ujazwaji maji, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Maharage Chande alisema wamejenga tuta lenye urefu wa mita 131 kwenda juu huku bwawa lenyewe likiwa na urefu wa kilomita 100 sawa na kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze.


Ujenzi wa njia za kuporomosha maji alisema umekamilika kwa asilimia 96 na mahandaki matatu yenye mashine zitakazotumika kuzalisha megawati 235 kila moja, yana urefu tofauti, moja likiwa na urefu wa mita 390, jingine 440 na 520.


“Maji yanayopita katika njia moja ya mashine hizo ni lita 200 kwa sekunde, ni mradi mkubwa sana,” alibainisha.

MWENYEKITI WA CCM TANGA AMPONGEZA RAIS DKT SAMIA SULUHU KWA KUIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Tanga wakati akitoa tamko la kumpongeza na kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt Samia Suluhu

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza 

Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo

Na Oscar Assenga, TANGA

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM) kimetoa pongezi kwa Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimarisha demokrasia nchini huku wakitoa wito kwa wana CCM  kujielekeza katika kufanya siasa zenye hoja,tija na majawabu kwa watanzania wa rika zote na ambaye atakwenda kinyume chake chama kitahangaika naye.

Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman wakati akizungumza na waandishi wa habari akitoa tamko la wana CCM Mkoa wa Tanga la kumpongeza na kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha na kuishaurisha demokrasi Nchini.

Ambapo alisema kufuatia Rais Samia kuridhia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ni vyema kila chama cha siasa kuheshimu taratibu na sheria zilizopo ili kufanya siasa zenye utashi na ustawi wa maendeleo huku akitaka vyama vya siasa kutumia nafasi walioipata kuheshimu taratibu zilizopo ili kufanya siasa za kistaarabu.

"Ndugu zangu waandishi nimewaita leo hii ili kuongea na wana CCM na watanzania kwa ujumla kuongea juu ya mambo makubwa mawili ambayo mwenyekiti wa ccm Taifa na Rais dkt Samia Suluhu Hassan kayapanga kwa upendo mkubwa kwa watanzania na vyama vyote nchini moja kukubali maridhiano ya mazungumzo baina ya serikali ya ccm chama cha mapinduzi na vyama vingine vya siasa vipavyo 18,"

Alisema kwamba baada ya kuruhusiwa kufanyika kwa mikutano ya siasa hawata mvumilia au kuona mwanasiasa yeyote ambaye atakuwa na nia ovu ndani ya ccm na nje ya ccm ya kuvuruga mikutano ya vyama vya siasa ambalo ni tamko lililoruhusiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Kuridhia na kukubali yeye binafsi na chama cha mapinduzi juu ya kuruhusu kazi ya kuimarisha siasa ya vyama vyote nchini kuendelea kufanya siasa bila upendeleo kwa kuruhusu mikitano ya hadhara hivi karibuni alipokutana na vyama vyote hivyo kama Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na kwaniaba ya wana CCM na wananchi wote wa Mkoa wa Tanga tunatoa pongezi nyingi kwa hatua hii ambayo imeonyesha kuwa Rais ni mtu mwenye hofu ya Mungu na amejua na kuelewa kwa busara za hali ya juu kuliongoza Taifa letu na wananchi wake, "Alisema Mwenyekiti Rajab.


Mwenyekiti Rajab alisema mchakato huo ulianza kwa mazugumzo ambayo yalipelekea kuunda kikosi kazi kitakachofanya kazi kwa weledi na ustadi zaidi ili kutoa maoni na ushauri namna ya kufanya siasa baina ya vyama vyote nchini ambapo kazi hiyo haikuwa rahisi kama wanavyofikiria.

Alisema jambo hilo lilihitaji uongozi makini na wenye busara za kiungozi ili kupokea na kufanya maamuzi juu ya kuridhia kuanza siasa kwa usawa wa vyama vyote hivyo kutokana na hilo wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

"Maono ya Mwenyekiti wetu wa ccm na Rais yamejikita katika mawazo ya (4R) maridhiano na ustahamilivu katika mabadiliko ya kujenga umoja na mshikamano baina yetu sisi kama watanzania na wanaccm tunapaswa kumpa ushirikiano mkubwa kufanya jambo hili kuwa na ukweli wa wazi ili kila mmoja wetu afaidi matunda ya mawazo yake, "alisisitiza Rajab.

"Kwa muktaza huo wanaccm na wananchi wa Mkoa mzima wa Tanga nimesimama mbele yenu kuelezea furafa yetu katika jambo hili muhimu lenye tija kwa maendeleo ya watanzania wote wapenda amani pia tunaelekeza mawazo yetu na nguvu zetu katika kulisimamia na kuliishi tanko hili ambalo ni dira maendeleo ya siasa, "

Aidha amewataka viongozi na watendaji wa serikali kusimamia maelekezo ya Rais kwa vitemdo bila kusahau kuimarisha ulinzi na usalama kwa kila mtanzania.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Salim Mohamed Ratco wakati huu serikali imefungua pazia la mikutano ya hadhara ni vyema vyama vyote vizingatie sheria na kanuni zinavyoeleza wakati wakitekeleza wajibu wao.

"Kila kitu kina mipaka yake ukikengeuka ukasema mambo yasiyofaa sheria itachukua mkondo wake ni vyema kila mwanasiasa akafuata taratibu sheria na kanuni za mikutano zinavyotaka, "alisema Ratco.

Alisema jambo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la kuruhusu mikutano ya hadhara lengo ni kupana wigo wa siasa nchini ikiwemo kurekebishana, kutoa maoni na kushauriana ili isaidie kuchochea maendeleo.

Monday, January 9, 2023

MBRAZIL WA SIMBA AMEANZA TAMBO.

 

KOCHA Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera raia wa Brazil ameweka wazi kuwa kwa namna ambavyo ameanza kazi na wachezaji wa timu hiyo amefurahishwa na uwezo wao.

Kocha huyo raia wa Brazil amepewa mikoba ya Zoran Maki aliyevunja mkataba na timu hiyo mwanzoni mwa msimu wa 2022/23.

Nchini Dubai Simba imeweka kambi yake ambayo itachukua siku saba tayari wameanza mazoezi kwa ajili ya kuandaa kikosi hicho kilichotoka kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Kocha huyo amesema:”Nimeona wachezaji wakijituma na inaonyesha kabisa wana vipaji kwenye uchezaji pamoja na kutimiza majukumu yao hivyo nina amini tutakuwa imara kwenye mbinu,”.

Sunday, January 8, 2023

MWANAHARAKATI WA MAPENZI YA JINSIA MOJA KENYA AKIRI KUUA.


Mshukiwa wa mauaji Jactone Odhiambo amekiri kuwa alimtoa uhai aliyekuwa rafikiye Edwin Kiptoo maarufu kama Chiloba. actone Odhiamboamekiri kumtoa uhai Edwin Chiloba. Chanzo: Twitter 

Odhiambo amewaambia polisi hakuna haja ya kupoteza muda wakichunguza kifo hicho kwani yeye ndiye alitekeleza mauaji. 

Amesema sababu ya kuamua kumuua Chiloba ni machungu ya kusalitiwa kimapenzi kwani walikuwa na uhusiano wa mapanzi. 

Polisi wanasema mshukiwa huyo alisema alitekeleza mauaji hayo Januari mosi saa chache tu baada ya kuukaribisha mwaka moja wakiwa pamoja katika klabu moja maarufu mjini Eldoret. 

Makachero wanaochunguza kisa hicho wamesema kuna washukiwa wengine wawili ambao walisaida Otieno kutekeleza unyama huo. 

OCPD wa Langas alisema Odhiambo aliambia polisi kuwa ugomvi ulizuka kuhusu CHiloba kuwa na mpenzi mwingine. 

Wawili hao wamekuwa wakiishi kwenye chumba kimoja mjini Eldoret eneo la Chepkoelel ambapo majirani walisema hawakuwahi skia ugomvi. 

Aidha inaarifiwa kuwa hata baada ya Chiloba kuuawa, Odhiambo aliendelea kutumia simu yake na hivyo wengi hawakushuku kuna lolote limefanyika. 

Kwa wakati mmoja, majirani waliskia uvundo ukitoka nyumba ya awali hao na walipouliza, mshukiwa akawaambia kulikuwa na panya amefia ndani. 

WANAHABARI 6 WAKAMATWA KWA KUVUJA VIDEO INAYOMUONESHA RAIS AKIJIKOJOLEA.

 


Waandishi sita wa habari nchini Sudan Kusini wamekamatwa kwa kusambaza picha na video zinazomuonyesha Rais Salva Kiir akijikojolea. Katika video hiyo iliyosambaa mitandaoni, Rais Salva Kiir anaonyeshwa akijikojolea huku wimbo wa taifa ukipigwa.


  Katika video hiyo iliyosambaa mitandaoni mnamo Disemba 2022, Rais Kiir anaonyeshwa akijiendea haja ndogo huku wimbo wa taifa ukipigwa kwenye hafla. 

Kufuatia tukio hilo mashirika ya kutetea haki za vyombo vya habari yanasema kuwa wafanyakazi sita kutoka shirika la utangazaji la serikali walikamatwa wiki hii, BBC inaripoti. Hata hivyo, Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC) linasema video hiyo haikuonyeshwa kwenye kituo hicho. 


 Kulingana na Patrick Oyet ambaye ni rais wa Muungano wa Waandishi wa Habari wa Sudan Kusini, aliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba waandishi hao wanashukiwa kufahamu namna video hiyo ilivujwa.


 Waziri wa Habari wa Sudan Kusini Michael Makuei naye aliiambia Sauti ya Amerika kuwa watu wanapaswa kusubiri kujua sababu ya wanahabari hao kukamatwa. 


Sudan Kusini nchi mpya zaidi barani Afrika - mnamo 2011. Lakini nchi hiyo imekumbwa na mizozo mingi tangu wakati huo, ikivumilia migogoro ya kikatili, machafuko ya kisiasa, majanga ya asili na njaa. 

UCHAPAKAZI UNALIPA MBEYA YETU WAZOA TUZO KATIKA 'TJA'

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye usiku wa Januari 7, 2023 alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo za umahiri wa Uandishi wa Habari (Tulia Trust Journalism Awards) 2022/23 iliyofanyika katika ukumbi wa Tughimbe Jijini Mbeya.

Katika hafla hiyo ambayo lengo lake kuu ni kuchochea hamasa ya vyombo vya Habari pamoja na Wanahabari kufanya kazi zao katika weledi, ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, vyama vya siasa pamoja na Wananchi kutoka maeneo tofauti ambapo jumla ya shilingi milioni 22 zilitumika katika maandalizi ikiwemo zawadi.


Joseph Mwaisango – Tuzo ya mshindi wa jumla (Online TV)

Baadhi ya Washindi walioibuka kidedea katika tuzo hizo kwa vipengele mbalimbali ni pamoja na ;-

i. Ezekiel Kamanga- Tuzo ya Uandishi wa Habari za madini na gesi (Online TV)

ii. Rashid Mkwinda- Tuzo ya Uandishi wa Habari za kilimo, mifugo na uvuvi (Online TV)

iii. Enock Simon – Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watoto (Online TV)

iv. Joseph Mwaisango – Tuzo ya mpiga picha bora (Online TV)

v. Joseph Mwaisango -Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Maliasili (Online TV)

vi. Kakuru Msimu – Tuzo ya Uandishi wa habari za utamaduni na michezo 

vii. Joseph Mwaisango – Tuzo ya mshindi wa jumla (Online TV)

Kwa upande wa vituo vya redio

i. Washindi wa tuzo ya Uandishi wa Habari za afya ni Samwel Mussa, Pascal Ndambo na Fredrick Gumusu

ii. Washindi wa tuzo ya Uandishi wa Habari za mazingira ni Esther Lekasio na Joshua Sengo

iii. Washindi wa Habari za Michezo Jirani Mtembezi na Samwel Mussa

iv. Mshindi wa Habari za uchumi na biashara Prince Fungo

v. Mshindi wa tuzo ya Uandishi wa habari za unyanyasaji wa kijinsia ni Anitha Mahenge

vi. Mshindi wa Habari za Watoto ni Isakwisa Mbyale na Joshua Sengo


Wakati huohuo taasisi ya Tulia Trust ikiongozwa na Mkurugenzi wake Dkt. Tulia Ackson ilitoa mchango wa Shilingi milioni 15 kwa Umoja wa Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya (Mbeya Press Club Vikoba) kama sehemu ya kuwaongezea mtaji wa kukopeshana kwenye mfuko wao.