NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
UNAAMBIWA SASA MWANZA KUWA KAMA ZANZIBAR - KIVIPI? Karibu kwenye mafunzo ya zao lenye kuzalisha mkwanja mrefu duniani, Kipato Chap Chap! Soko lipo! Wanunuzi wapo!! Ni zao la Vanilla, ambalo tayari wenzetu visiwani Zanzibar wameanza kulima na kunufaika nalo, sasa limejaribiwa kwenye ardhi ya mkoa wa Mwanza na limekubali kupita maelezo. VANILLA kiungo muhimu na ghali duniani, kinachotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile Chocolate, Kutia nakshi ya ladha kwenye keki na vyakula mbalimbali na hata hutumika kutengeneza marashi na perfume mbalimbali ulimwenguni. Kwa sasa soko la Vanilla lipo hapa nchini, nalo soko kuu likiwa nchi za Falme za kiarabu. VUTA PICHA Tofauti na mazao mengine na vile unavyodhani hauhitaji kuwa na shamba kubwa ili upate faida, Vanilla haihitaji palizi na haina gharama kubwa kuihudumia, Mkulima ukivuna tutanunua kutoka kwako KILO MOJA YA VANILLA KWA SHILINGI MILIONI MOJA. Ewe kijna uliyesaka ajira kwa kipindi kirefu au umefanya ujasiliamali wa kila aina na haukutoboa, unangoja nini? Karibu kwenye semina ya BURE bila malipo yoyote, upate mafunzo jinsi ya kulima zao hilo na pia tukutambulishe kwa wadau wa soko la Vanilla hapa nchini. Ni Jumamosi hii ya Tarehe 14/ 01/2023 Katika ukumbi wa GOLD CREST HOTEL jijini Mwanza Muda ni kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa alasili.WATU WOTE MNAKARIBISHWA.
Licha ya kuhamasisha wakulima mkoani Mwanza na kote nchini kuchangamkia fursa hiyo kampuni ya Vanilla International, itatoa elimu bure kwa wale watao kuwa tayari kujikita katika zao hilo huku wakiwahakikishia upatikanaji wa soko kwa asilimia 99.9.
“Zao la Vanilla ni zao la fedha nyingi na kilo moja imeweza kufika mpaka zaidi ya milioni moja niwaombe sana wakulima kuwasiliana na sisi ili tuweze kuwasaidia katika kilimo”alisema Simon Mukondya mkurugenzi wa Vanilla International Ltd
Vanilla huchukua muda wa miezi mitatu tu tangu kupandwa hadi mavuno na gharama yake kila kilo moja inatajwa kufikia sh.laki 9 hadi mil.1 kwa sasa.
Zao la Vanilla lililoanza kulimwa kwa sasa mkoani Njombe kutokana na kuendelea kuhamasishwa ili kulima kilimo hicho kutoka na thamani yake.Mmea wa zao la Vanilla.Mmea wa zao la Vanilla.
Simon Mukondya mkurugenzi wa Vanilla International Ltd wakati akifafanua faida na matumizi ya zao hilo huku akiwasihi vijana walio kwenye ajira, wanaosaka ajira na wakulima wanaopenda kujihusisha na kilimo hicho kuweza kufika kwenye Semina hiyo kujizolea elimu bila malipo.
Aidha kampuni hiyo imekuwa ikifanya shughuli zote za kilimo na kumkabidhi mkulima shamba likiwa tayari kwa kuendelea kulitunza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.